Wanaume acheni kudhalilisha miili ya wanawake

Wanaume acheni kudhalilisha miili ya wanawake

Nahisi kusisimka jamani uwiii,
Kilichonifanya nilete huu uzi nilikua napiga story na polisi kituoni ghafla linaletwa janaume limembaka mtoto wake mwenyewe wa miaka miwili tena wamelifumaniwa red-handed imagine!!!

Kuna mwingine alimbaka mtoto wake pia wa mwaka na nusu, akamnyonga na kumtupia kwenye mfereji wa maji.
Sasa hapa ndo utaona akili za wanaume wanaotetea ubakaji eti chanzo ni mwanamke au msichana kuwa ni mafwalaa...
Sasa hapo huyo mtoto anabakwa na baba ake ni kuwa alitembea na kimini? Au huyo baba ni kichaa kinamsumbua yani mwanaume ambae hawezi kuresist hisia zake na utupu wa mwanamke achilia mbali mtoto huyo hawezi kuwa baba wala sio mwanaume wa kawaida...
 
Bado wale wamama wanaoamka alfajiri kuwahi masokoni au kuchota maji wanabakwa, huko Kigoma kuna majamaa yalijiita teleza yanajipaka mafuta mengi yanaingia kwenye nyumba wanazolala wanawake peke yao na kuwabaka sijui na wao walivaa vimini,
Kuwatetea nyie watu ni kazi sana
Ni mtu tuu anaona kila kitu abishe awe mwamba...kuna vitu mpaka aibu hata kubisha unajiita great thinker....😅😅
 
Ndo mfanye kikao cha wanaume muulizane vizuri...
Mbona zamani wazazi wetu walivaa nguo fupi..sie watoto nakumbuka mpk miaka 5 sijui sita tunavaa vi nguo vya kitoto vya kutuacha wazi kabisa mbona hayo mambo hayakuwepo??
Mavazi ya zamani na ya sasa hivi ni tofauti, pia wadada wa siku hizi sijui wanakula nini, wanajaa na kuvutia haraka sana.
Wa zamani walikuwa wakijipaka mafuta ya ng'ombe na kupunguza ushawishi, ila wa sasa wanajipaka mafuta ya kunukia yanayoshawishi uendelee zaidi kumsogelea.​
 
Nikienda uhamiaji na kimini changu nitabakwa? nikienda msikitini au kanisani au ofisi za serikani na kimini changu nitabakwa? nilikua nakuona zimo zimo kidogo kumbe ni wale wale,

Kwanini umnyime mwanamke uhuru wake kwa ajili tu mwanaume ana tamaa, hizo tamaa zake kwanini asioe akatulia na familia yake au kwanini asiende kwa wanaouza akanunua badala yake akabaka,

Na yule mtoto mdogo au mzee anayebakwa kosa lake ni nini?
Jadili mada usijadili mtu. Zimo zimo ndio nini?

Anyway hapa hatuongelei watoto wala wazee.

Tunaongelea wanawake waliopevuka na kujielewa na wala sio chizi.

Yes ukienda uhamiaji hutaingia watakufukuza kama mwizi kwa kuwa unaenda pale kutega watu na sio kupata huduma. Ukienda msikitini hata hatua hutasogelea. Ukienda kanisani utaishia mlangoni na chupi yako nje....

Pia usome kuelewa sio unasoma ili ujibu. Nimekuambia vaa kutokana na mazingira na wakati sio unajivalia tu mipaja nje sehemu yoyote.

HAta hao mnaowaiga ulaya na marekani ushawahi ona kwenye function za serikali wamevaa kihuni kihuni? Au unaamini maisha ya Tv ndio ya halisia?

Level up.
 
Kwa hiyo nikionesha mapaja nje ndio nibakwe? au hujaelewa mada? mifano uliyoitoa ipo mbali mbali na mada, mada ni kubaka na kudhalilisha wanawake kwa uanamke wao, wewe unaleta mambo ya kimini na misikitini, wale wanawake wa kule Kigoma waliokua wanavamiwa usiku wanabakwa wakiwa wamelala na watoto zao walimvalia nani kimini? huko Taliban na Iraq kwenye mavita wanawake wanabakwa walimvalia nani kimini?

Kwanini unawatoa Wazee na Watoto? kua wao wanastahili zaidi kubakwa? au kipi unachokificha hapo,

Ni mshenzi na mpumbavu pekee anayehalalisha mwanamke abakwe kisa kavaa sketi fupi, wewe hulijui paja? kwanini usimtongoze kama umemtaka hadi umparamie?

Man up, hata manyani na masokwe hayabakani.
 
Guys, wallah leo nimechafukwa sana ukija hapa uje na akili timamu, nina kirungu changu ukileta uzwazwa nakubwenga cha utosi akili ikukae sawa,

Matukio ya ubakaji wanawake na watoto wa kike ni mengi hadi natetemeka lakini haya yote yanaletwa na wanaume wapumbavu wanaoangalia mwili wa mwanamke kama chombo cha starehe,

Hivi nyie wanaume miili ya wanawake ina tofauti gani na yenu? ile kujazia jazia hata nyie mmejazia, wembamba hata nyie kuna wembamba, manyonyo hata nyie kuna wenye nayo, nini shida jamani mbona mnatukosesha amani wanawake?

Mwanamke akivaa kiguo chake kifupi atembee kwa raha zake inakua gumzo lakini mwanaume akivaa kiguo kifupi husikii kabakwa au kadhalilishwa, miili mbona ni ile ile tu,

Mbona watu wa zamani walikua wanaishi uchi na hakukua na matukio ya ubakaji wala udhalilishwaji, hiki nini mnafanya nahisi hadi kichefu chefu,

Ifike mahala sasa tutaichukua heshima yetu kwa nguvu, haiwezekani kila siku nyinyi tu, kuna wengine humu humu hizo tabia chafu mnazo, unajisikiaje kushika titi la mwanamke bila ridhaa yake au kushika tako la mwanamke ambaye huna mahusiano nae?,

Hakuna mwili unaohalalisha ubakaji,
Hakuna vazi linalohalalisha ubakaji,
Hakuna tabia inayompa mtu haki ya kuvuka mipaka ya mwingine,

Tujenge jamii inayohehimu wanawake bila kufanya miili yao kua sababu ya lawama au udhalilishaji,

Nikisema hii gender ifutwe naitwa feminist.
Alie waambia mtembee uchi ni nani?
 
Kwa hiyo nikionesha mapaja nje ndio nibakwe? au hujaelewa mada? mifano uliyoitoa ipo mbali mbali na mada, mada ni kubaka na kudhalilisha wanawake kwa uanamke wao, wewe unaleta mambo ya kimini na misikitini, wale wanawake wa kule Kigoma waliokua wanavamiwa usiku wanabakwa wakiwa wamelala na watoto zao walimvalia nani kimini? huko Taliban na Iraq kwenye mavita wanawake wanabakwa walimvalia nani kimini?

Kwanini unawatoa Wazee na Watoto? kua wao wanastahili zaidi kubakwa? au kipi unachokificha hapo,

Ni mshenzi na mpumbavu pekee anayehalalisha mwanamke abakwe kisa kavaa sketi fupi, wewe hulijui paja? kwanini usimtongoze kama umemtaka hadi umparamie?

Man up, hata manyani na masokwe hayabakani.
I think tupo page tofauti. Pole.

Hakuna anayestahili kubakwa kwa namna yoyote. Hilo lipo wazi.

Samahani kwa kutonielewa.
 
I think tupo page tofauti. Pole.

Hakuna anayestahili kubakwa kwa namna yoyote. Hilo lipo wazi.

Samahani kwa kutonielewa.
Mnawahi kukurupuka kutetea ujinga hata mada hukuisoma, watu tunaongelea ubakaji wa wanawake, watoto na wazee wewe unaleta mambo ya kutokupewa huduma kwenye ofisi za serikali kisa mini sketi,

Badala muwakanye wanaume wenzenu nyie mnawatetea wait siku mbakaji akiingia kwenye familia yako ndio utamwambia mkeo au binti yako kua alivaa kimini ndio maana akabakwa
 
Tuliza munkari manka....
Mpunguze kutega wanaume pia kujiepusha na hayo mambo ili baadae uplay victim...
 
Back
Top Bottom