Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Ukishakuwa kuwa kiongozi wa Umma, mambo yako mengi ni lazima yajulikane kwa Umma.
Kama hamtaki, ondokeni kwenye ofisi za Umma muone kama tutataka kujua chochote juu yenu.
 
Sidhani hata kama wanajali hizi dukuduku za wananchi. Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli aliyesemekana kufariki lakini serikali ikaja kutoa taarifa baada ya wiki moja hivyo kusogeza mbele tarehe ya kifo chake.

Ngoja pia waendelee kuficha ugonjwa wa Mpango lakini kifo kitawaumbua kama kilipowaumbua kwa Magufuli. Wakati ukuta.
Aisee,watu wana Roho ngumu sana.
 
Akili za mleta mada ni ugoro kabisa. Awe Hai au amekufa ni nini?
Kwa hiyo serikali ikisema alipo kama ni wa kufa ndio hatakufaaa.
Upuuzi wa kiwango cha Gambosh huu.
 
Mtu akiwa haonekani tu, zinaanza kusambazwa taarifa zisizo na maana.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Kwa nini asionekane kama yupo.Haya ndiyo matokeo ya kukaa kwao kimya,they should be ready for it.Kwa Magufuli walikaa kimya,kilichotokea unakijua,sasa kwa nini tusiamini kwamba kilichotokea kwa Magufuli kitatokea kwa Mpango?It is commonsense.Ukiumwa na Nyoka hata ukiona unyasi unastuka.Mpango hayupo salama.
 
Akili za mleta mada ni ugoro kabisa. Awe Hai au amekufa ni nini?
Kwa hiyo serikali ikisema alipo kama ni wa kufa ndio hatakufaaa.
Upuuzi wa kiwango cha Gambosh huu.
Aisee,uliyoandika hapa ni utopolo kabisa,and only proves that Mpango is dead.And we know why they hate him:ni threat kwa kambi ya "Wahuni." Hawataki kuwa na the types of Magufuli again, ambao watazuia upigaji wao na uovu wao mwingine.
 
Hii ni kwa afrika tu kufichwa taarifa muhimu juu ya afya ya kiongozi wao kufichwa, ulaya na amerika hakuna mambo hayo utasikia he/she has hospitalized hata kama kama kapata mafua tu utajulishwa yuko kwenye bed rest anapatiwa matibabu
 
Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.
CCM wanajifanya wanamiliki hadi afya za watu wengine
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.

Rais ni wa Jamhuri ijulikane kuwa anamilikiwa na wananchi wote bila kujali itikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.

Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nao watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.

Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.

Serikali, imeendelea kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza uvumi (uliokuwa siyo uvumi) enzi Mwendazake wakati anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.

Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenya mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.

Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kusimama na wananchi wote na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wanafanya kila linalowezekana ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.

Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.

Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.

Naomba tujulishwe
Hata wewe ungekuwa uko serekaliNi sizadhni kma ungetangaza habr za kuumwa kwake kuumwa siyo Jambo la kutangaziwa watu

Mm Niko upande wa serekali kwenye hili Jambo ni kweli Ni kiongozi wetu ila sioni sababh ya kuuzua taaruki Kama kafa itajulikana tu Kama Yuko hai atajulikana tu hakuna kitaba imefunjwa hapo
 
Akili za mleta mada ni ugoro kabisa. Awe Hai au amekufa ni nini?
Kwa hiyo serikali ikisema alipo kama ni wa kufa ndio hatakufaaa.
Upuuzi wa kiwango cha Gambosh huu.
Mie ndo binadamu wa kwanza kuwa na akili za ugoro mkuu.
Je inakuumiza popote?:D
 
Hata wewe ungekuwa uko serekaliNi sizadhni kma ungetangaza habr za kuumwa kwake kuumwa siyo Jambo la kutangaziwa watu

Mm Niko upande wa serekali kwenye hili Jambo ni kweli Ni kiongozi wetu ila sioni sababh ya kuuzua taaruki Kama kafa itajulikana tu Kama Yuko hai atajulikana tu hakuna kitaba imefunjwa hapo
Kama hautaki kutangazwa basi zisitumike pesa zetu kukutibu.
tunaweza kutangaziwa kwamba anaumwa na si lazima waseme ugonjwa gani.

Nahisi sehemu kubwa ya waliomo serikalini ni zombiez kuliko sisi raia:D
 
Back
Top Bottom