Very special for mkuu
EMT... Much respect kwako kaka
Yuko wapi lakini?
Nipo Babu. Mihangaiko tuu ya hapa na pale. Sijui nianzie wapi maana niko kote kote. Pia sijui nimtaje nani na nimwache maana huwa nawasoma na ku-interact na watu wengi. Katika mwaka 2013 nimeendelea kujifunza mengi kutoka kwa WanaJF hasa kwenye threads/posts zao za kujifunza, kuhabarisha, kufurahisha na pia za kuhusunisha sana. Hivyo kujaribu kuwataja wote will be like fighting a loosing battle.
Hata hivyo, niwapongeze waendeshaji wa JF kwa kuendelea kuboresha jukwaa hili hasa katika kipindi hiki ambacho JF imepanuka kwa kuwa na members ambao siyo wapya tuu bali pia walio na mawazo tofauti. Niwapongeze moderators kwa kazi yao ngumu ya ku-moderate JF. Japokuwa baadhi yetu huwa tunawanaga kwenye posts zetu, we still value your your work. Ni vigumu sana ku-moderate social media ambayo information ina-flow horizontally.
Lakini pia nichukue nafasi hii kuwashukuru baadhi ya WanaJF ambao wameni-trust kiasi cha kuniomba ushauri katika masuala yao binafsi bila kuwashirikisha Members wengine au kwa kuwashirikisha Members wachache sana. I know we go through through life by putting our trust on others, lakini inapofikia mpaka mtu ambaye hakujui na humjui nje ya JF kuku-trust na kukuomba ushauri kwenye masuala yake binafsi huna budi ku-appeaciate na kushukuru. So, I thank all those JF Members who have put trust on me. For confidentiality reasons, sitawataja hapa.
Pamoja na faida binafsi ambazo tunazipata hapa MMU, nadhani kama wapenzi wa jukwaa hili bado tuna changamato kubwa. Tuna changamoto ya kuwakubali members wapya ambao wana mawazo tofauti na tuliyoyazoea huko nyuma. Tusiwanage sana bali tukubali kuwa JF inaelekea kwenye hatua nyingine. JF is no longer a club for certain type of people. JF inaanza ku-reflect maisha ya Watanzania kupitia kwenye michango ya members wake.
Lakini changamoto kubwa ambayo naiona mbele yetu ni jinsi ya kulifanya jukwaa hili kuwa na impact siyo tuu kwetu sisi individually kama JF Members, bali pia kwa jamii yetu nzima kwa ujumla. Mahusiano, mapenzi na urafiki ni mambo muhimu siyo tuu kwa mtu mmoja mmoja bali pia kwa jamii nzima. Kama kuna mahusiano, mapenzi na urafiki ndani ya jamii, basi jamii hiyo itachanua na kusaidia nyanja nyingine kuchanua pia.
If a person cannot live without love, then the society cannot also live without love. Tunajitaji mahusiano, mapenzi na urafiki kwenye jamii yetu. Lakini jamii yetu kwa sasa inaelekea kuendekeza ubinafsi kwa kutothamini maisha ya watu wengine. Ubinadamu unapungua kwa kasi kubwa sana kwenye jamii yetu.
Tumesoma na wengine tumeona yaliyotokea Mwanza. Kama alivyosema
Chakaza kwenye uzi wake, "
Marehemu ameuwawa katika eneo lake la uongozi ambalo mwaka 2010 alitajwa kuwa alishinda kwa kishindo na amekuwa mwakilishi wao katika baraza la madiwani la wilaya ya Magu toka wakati huo. Hii ni kuonyesha kuwa Raia hao alikuwa nao siku zote, wanamfahamu kama kiongozi wao, shida zao za kila siku wanampelekea yeye kama Diwani na mahusiano yapo ya kila mara kati yake na viongozi wa vitongoji vya kata hiyo ya Kisesa" lakini bado wakaamua kumwua. Wengi wamelichukulia hili suala kama ni la kisiasa, lakini linaweza pia kuwa suala la kijamii aka kukosekana kwa mahusiano, mapenzi na urafiki baina ya wahusika.
Jamii imefanya baadhi ya watu waamini kuwa wanaweza kuishi bila mahusiano, mapenzi na urafiki na ku-thrive. Watoto ambao hawatunzwi na kupendwa huwa wanafariki kutokana na kitu kinachoitwa "failure to thrive". Wale ambao wanafanikiwa kuishi kwenye jamii isiyokuwa na mahusiano, mapenzi na urafiki wanashia kuwa anti-social (kutokuwa na mahusiano, mapenzi na utafiki), wanakata tamaa na wanashindwa kuzalisha. Matokeo yake ni kuwa na jamii iliyo na wazalishaji wachache sana.
Hakuna jamii au mtu binafsi anaweza kushamiri bila kuwa na mahusiano, mapenzi na urafiki. Hivyo basi, wakati MMU ikitusaidia kuboresha mahusiano, mapenzi na urafiki baina yetu kama WanaJF, pia tutathmini jinsi MMU itakavyoweza kuimarisha na kuboresha masuala hayo nyeti kwenye jamii yetu kwa ujumla.