Heshima mbele MMKJJ, kwanza nakushukuru kwa angalizo, ila hukutoa sababu ya angalizo hili. Mimi naamini issue sio gharama wala umiliki wa mafisadi.
ila sio tuu umetoa ushauri, bali pia umetoa tahadhari "Do it or be ready to live with the consequences". hii ikimaanisha yakishapita hayo masaa 72, yatatufika yakutufika.
Ushauri wangu ni kuwa naomba utusaidie kwanza sababu ambazo naamini ni za msingi, na pili sisi watu wa mazoea ambao hatuna mpango wowote wa kuhama voda, sio vibaya ukitujulisha yatakayo tukuta ili tuwe more prepared for the so called "be ready to live with the consequences".
Naomba na mimi niwape facts zangu,
1. Kama ni simu kusikilizwa kinyume cha sheria, mitandao yote iko monitored na wenye nchi, na sio hao tuu, bali mpaka mabwana wakubwa wa wenye nchi. Rule out sababu za kiusalama.
2. Naitumia sana voda hswa kwa mtandao, nakiri jamaa wako ghali sana, Zain wana 3.5 G wako faster, cheaper kuliko Voda, ila tatizo kwangu ni mazoea.
3.Nimesikia Zentel ndio the cheapest, hivyo kama kweli issue ni kuibiwa, watu washauriwe kujiunga Zentel.
Angalizo, wana JF lazima tuwe makini zaidi kwenye haya, tusijejikuta tunatumiwa bila sisi wenyewe kujijua katika vita vya biashara vya mafisadi, iwe ni mafisadi papa, nyangumi, ama hata visamaki vidogo mpaka vifisadi dagaa.