Wanaharakati: Ziachieni simu za VodaCom!

Wanaharakati: Ziachieni simu za VodaCom!

Nafikiri kuhama mtandao wa voda siyo ubaguzi wa aina yeyote ile ila ni kupambana na mafisadi mpaka wasalimu amri! waiache Tanzania istawi kama ilivyobarikiwa kuwa na rasilimali tele! wewe kama kweli unataka kupambana na mafisadi huna budi kuacha kutumia bidha zao zote! mwenye kujua bidha za mafisadi azitaje ili tusinunue. Kwa kweli inauma sana na ni aibu kwa nchi yenye kila rasilimali halafu wananchi wake wamechoka mbaya! huduma za jamii aibu tupu!

Je niki kuambia kampuni zote za simu Tanzania zina dalili za ufisadi utaacha kutumia huduma za simu moja kwa moja? Upo tayari kukaa bila simu mkuu? Ujue kuwa haya mambo ya kususia bidhaa ni kama kuna alternative bora. Kuna vitu nina uhakika kabisa kama haona alternative nyingine hata uonyeshwe ushahidi wa ufisadi wake ni uta tumia tu. Mfano rahisi ni kama upo sehemu ambapo hakuna mtandao mwingine una kamata zaidi ya Vodacom hata katika hali hiyo utaacha kutumia hudumza zao? Telling people to boycott Vodacom na huduma zake siyo solution kwa sababu kuna watu wana faidika na huduma zake directly or indirectly. Kama huduma za Vodacom zina kubalika bado watu wataendelea kui tumia tu kwa sababu watu wengi hawajali nani ana miliki nini bali wana angalia ubora wa huduma. Kuna sehemu hakuna mtandao unashika zaidi ya Vodacom, watu wa huko hawata acha kuitumia hata kama ina milikiwa na Vodacom. Kuna watu gharama zao za simu wana lipiwa na ofisi ndiyo inaamua mtandao gani uta tumika, hawa nao hata uwaambieje hawata acha kutumia Vodacom. Kuna waajiriwa wa Vodacom ambao kuwepo kwa Vodacom ndiyo kuwepo ajira yao hawa nao hawa jali Vodacom ina milikiwa na nani hawata acha kui tumia. Na kuna mifano mingi zaidi kama hii siwezi kuitaja zote. In short kama hauta kuja na sababu za maana na za msingi hamna mtu ataacha kutumia kitu simply because someone said so. Kama wewe umeweza kuacha kutumia Vodacom sawa ila situations zina tofautiana mtu hadi mtu. Kilicho nafuu kwako siyo nafuu kwa wengine. Bado tunam subiria muanzisha mada aje kutoa maelezo zaidi.
 
siku hizi; ni soko huria; hutakiwi kumchagulia mtu aende wapi katika swal la biasha; kama tatizo ni bei; he/she will run sio achuguliwe mahala pa kwenda; tatizo siku hizi watu wan simu si kwa manufaa bali kwa ubishoo na kujionyehsa kuwa unaongea; unaongea nini? no water in; quality saves cost; sasa huoi msemo inabidi wengine kwenda shule tena; Mwanakijiji hii post imekaa kimajungu ya kibiashara; hata kenya waliposeama kususia they had a MAN BASE; itafikia mahala post hizi zitakuwa hazina maji kama tutakuwa tunakurupuka; is not about kutetea mafisadi but about making sure you fight the right way
 
Je na vyombo vya habari kama Vya IPP,Mwanahalisi nk wanapokea matangazo ya Vodacom vipi nao wasusie matangazo hayo????

Wala hau hitaji kwenda mbali kote huko. We waulize jhao wanao taka kuisusia Vodacom je wakiwa wako kwenye situation where they have no other alternative but Vodacom bado wataendelea na mgomo wao baridi katika hali hiyo? Tukumbuke kuwa kila mtandao ina maeneo yake inapo kamata vizuri zaidi ya mitandao mingine.
 
As a matter of fact, hamia "kwingine" within the next 72 hours (beginning Monday). Do it or be ready to live with the consequences.

Nilikuwepo.

M.M.
Heshima mbele MMKJJ, kwanza nakushukuru kwa angalizo, ila hukutoa sababu ya angalizo hili. Mimi naamini issue sio gharama wala umiliki wa mafisadi.
ila sio tuu umetoa ushauri, bali pia umetoa tahadhari "Do it or be ready to live with the consequences". hii ikimaanisha yakishapita hayo masaa 72, yatatufika yakutufika.

Ushauri wangu ni kuwa naomba utusaidie kwanza sababu ambazo naamini ni za msingi, na pili sisi watu wa mazoea ambao hatuna mpango wowote wa kuhama voda, sio vibaya ukitujulisha yatakayo tukuta ili tuwe more prepared for the so called "be ready to live with the consequences".
Naomba na mimi niwape facts zangu,
1. Kama ni simu kusikilizwa kinyume cha sheria, mitandao yote iko monitored na wenye nchi, na sio hao tuu, bali mpaka mabwana wakubwa wa wenye nchi. Rule out sababu za kiusalama.
2. Naitumia sana voda hswa kwa mtandao, nakiri jamaa wako ghali sana, Zain wana 3.5 G wako faster, cheaper kuliko Voda, ila tatizo kwangu ni mazoea.
3.Nimesikia Zentel ndio the cheapest, hivyo kama kweli issue ni kuibiwa, watu washauriwe kujiunga Zentel.
Angalizo, wana JF lazima tuwe makini zaidi kwenye haya, tusijejikuta tunatumiwa bila sisi wenyewe kujijua katika vita vya biashara vya mafisadi, iwe ni mafisadi papa, nyangumi, ama hata visamaki vidogo mpaka vifisadi dagaa.
 
kaka leo umechemsha sana,
nilikuona wa maana sana hapa juzi kati lakini kwa hili umenikera sana

Usihukumu nawe utahukumiwa bro.
We subili kama unanyolewa 72hrs bado sana endelea kusubili.
 
Tofauti na mawazo ya wengine mimi na "feel proud" kushutumiwa kuwa nina chuki binafsi na mafisadi - ndio nawachukia na nina kila sababu ya kufanya hivyo. Sasa kama kuwashikia bango mafisadi ni kuwa na chuki binafsi dhidi yao je, kwa nini kuwatetea kusitafsiriwe kama kuwa kuwadi wao. Kwa nini kuna watu wanadai nina chuki binafsi kwa kumwita RA fisadi lakini wanakuja juu kwa mimi kudai wao kwa kumtetea RA wana mapenzi naye.
Huwezi kupiga vita ufisadi kwa kuwakumbatia mafisadi.
 
Masatu we! kama kawaida yako. Ama kweli wewe ni beki mstaarabu.

Huyu jamaa sasa ataanza kupoteza heshima au ndo ana zeeka vibaya?!

Muwe mnaelewa hoja kabla ya kukurupuka. Sometimes kukaa kimya inalipa zaidi kuliko kudisplay utupu
 
105d0k0.jpg

Biashara ngapi ziko connected na ufisadi? na hasa za kule mbeya? au basi tuu?
 
1. Kama ni simu kusikilizwa kinyume cha sheria, mitandao yote iko monitored na wenye nchi, na sio hao tuu, bali mpaka mabwana wakubwa wa wenye nchi. Rule out sababu za kiusalama.
.

Kwa jinsi angalizo lilivyokuja nalichukulia kama kuna watu wanataka kufyonza data illegally kwa kutumia huu mlango wa Voda. Kama ni kusikiza mazungumzo au kusoma texts fulani fulani za walengwa. Inawezekana ktk formal procedures dola inafanya, ila hatuwezi kuwa na uhakika kama mmiliki atakapokwenda kuitumia advantage ya umiliki wake ku-gain information ambazo hakustahili kupata, akishirikiana na baadhi ya wana-dola kwa kisingizio cha formal procedure. Hii ndio hoja.
 
Acha uongo wewe na dhihaka zako. Hilo bandiko lako tumeshaliona siku nyingi sana likiwa linasambazwa kwenye mtandao kwa nia mbaya ya ushindani wa kibiashara. Ingia kwenye website ya Vodacom http://www.vodacom.co.tz/docs/docredir.asp?docid=3389 ujue gharama halisi wanazolipisha usitufanye wajinga sisi wote hapa JF.

Mazingira,

Wewe ni mtumiaji wa Vodacom? Kama sio mteja wa Voda basi ilikuwa ufanye kwanza utafiti kidogo tu hata kwa kumuomba mteja wa voda yeyote atume sms then muone amekatwa bei gani!

Kifupi hiyo link uliyoweka hapo juu, inakupa rates za zamani sana......kwa mfano sms wanasema ni 45 before VAT....hii si bei ya sasa...bei ya sasa ni 59 including kodi!...angalia table ya kwanza kny link yako!

Mimi ni mteja wa vodacom tangia mwaka 2002 na sijawahi badilisha line yangu.......nakiri vodacom ni expensive sana na kwamba hiyo bei kwenye table hapo juu si sahihi kabisa.....ni za zamani sana!

Kwa mfano jana asubuhi nilikuwa na balance ya 1,025 hivi kny simu yangu, nikampigia jamaa wa Celtel...nikashangaa napigiwa king'ora cha kuashiria hela imeisha before 2minitues kuisha....nilipoangalia salio ilikuwa 25 shs, nikaangalia call time...ikawa inaonesha 1.44 minutes....!

Hesabu ya kawaida hapo ni kwamba nilitumia shilingi (1,025-25)=1,000 kwa 1.44minutes which means kwa dakika moja ilinicost 1,000/1.44=694.44!

Kwahiyo nakubaliana na watu wote wanaosema Vodacom ni too expensive kwa kweli, ila tu sisi wengine tupo huko kwa sababu ya mazoea sana na kuofear shifting costs basi!

On the side of MMM na post yake, sinauhakika kama angalisho lake limebase kny costs za huduma zitolewazo na voda...perhaps more to do with security reasons na mambo ya privacy!

Cheers!
 
Makampuni ya simu Tanzania na ufisadi wake:

(a). VodaCom- Kuna RA (share holder 35 %), Somaiya (Shivacom -super dealer ), Lowasa - Alphatel (dealer)


Wana percentage gani hao?


(b). Zain (wameifisadi TTCL hadi ikabinafsishwa kwa bei chee na wameingia TZ kwa wizi na utapeli mkubwa)

Zain sio walioifilisi TTCL. TTCL ilinunuliwa na MSI/Detecon (kampuni mbili, za Amsterdam na Germany), na sasa imerudishwa serikalini.
MSI walibaki na license ya GSM network ambayo TTCL waliinunua kabla ya kubinafsishwa. Sasa,

Zain haimilikiwi na MSI kwakuwa iliuzwa kwa Zain International ya Bahrain.

Sioni utapeli wa Zain.

(c). Tigo (wamekuwa wakibadili majina kila baada ya miaka 5 kukwepa kodi: 2001 from Mobitel to Buzz, 2006 from Buzz to Tigo) na ukifuatilia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 ikishirikiana na shirika la posta na simu wakati huo mpaka sasa ime-undergo several dubious contracts na serikali. Mpaka sasa kampuni inamilikiwa na Millicom ya Luxemburg kwa asilimia 100 % kinyume na sheria za nchi

Mkuu hapa hauko sahihi kabisa
, aidha ni kwa kujua au kutokujua.

Tigo ni jina la kibiashara na wala sio jina la usajili wa kampuni. Jina halisi la la usajiliwa (ambalo pia hutumika katika mikataba na hati nyinginezo za kiofisi ni MIC Tanzania Limited (Kampuni hii inamilikiwa na MIC ya Luxenburg). MIC stands for Millcom International Cellular.

Mkuu, majina kama Mobitel, Buzz, Tigo sio majina ya usajili. Haya ni majina wanayotumia kuuzia product zao (brand names) tu. Walipoanza biashara walitumia Mobitel kwa kuwa ni jina lililokuwa rahisi kwa wateja wao (usajili wao ulibaki kuwa MIC Tanzania). Walianzisha Buzz walipoanza kutoa huduma ya prepaid (hivyo Buzz ilikuwa prepaid service ya MIC Tanzania. Waliamua kufuta branda names zao zote na kutumia Tigo badala yake.

Hivyo tigo ni brand name na sio jina la usajili. Kampuni bado inaitwa MIC Tanzania Limited, na hivyo sio rahisi kukwepa kodi au kukwepa majukumu oyote ya kiutawala, kisheria n.k.


(d). TTCL - hii nayo imebinafsishwa kwa Wa-Kanada kifisadi kupita kawaida na bila shaka mafisadi wana share huko. Kwahiyo tunatupa simu zote na kufunga landline zetu zote tuwasiliane kwa internet na barua.

Mkuu, inaelekea umeamua kutokufanya uchunguzi kabisa katika mambo haya.

TTCL inaongozwa na SaskTel ya Canada baada ya kushinda katika tender ya utafutaji wa kampuni ya kuindesha TTCL (uamuzi wa serikali). Uamuzi huu ulifikiwa baada ya TTCL kurudishwa serikalini kutoka kwa mbia mwenza MSI International (ambao waliinunua kwa asilimia 35).

Uongozi ulirudhishwa kwa TTCL na Kaimu MD alikuwa Marehemu Said Mkumba. taratibu uliotumika kuipa SaskTel management contract unaweza kufananishwa na ule waliokuwa wamepewa Net Group Solutions ama City Water n.k.

Hivyo muda wa mkataba ukiisha, watatakiwa kuomba tena ama serikali ikiamua kuendelea kuongoza yenyewe itafanya hivyo. Hivyo TTCL haijauzwa kwa yeyote. NI mali ya serikali.
 
It is too late now but not too late enough..

Ina maana tumeshaathirika tayari bila kujijua? Kivipi, hebu fafanua.

kama uko kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na hauko tayari kusalimu amri, nakushauri kuachilia namba za simu za Vodacom ASAP

Ni vipi watatulazimisha kusalimu amri kwa sababu tu ya kuwa na line ya vodacom? mimi nina line za mitandao yote, je nifanyeje? Au unakusudia kusema nisitumia line ya vodacom kwenye mapambano dhidi ya mafisadi?

As a matter of fact, hamia "kwingine" within the next 72 hours (beginning Monday)

Ni wapi mafisadi hawawezi kutia pua zao?

1) Zantel?(Serikali ya ccm ya znz ina hisa!), na ina uhusiano mkubwa tu na vodacom; soma hapa:

Zanzibar-based Zanzibar Telecommunication Company Ltd (ZANTEL) and Vodacom Tanzania have entered into an agreement of co-operation whereby Zantel will provide national coverage on the Mainland using Vodacom's infrastructure.

By simply using the Vodacom network, ZANTEL users will immediately be able to use their SIM cards on the mainland with ZANTEL products and tariffs.

2) TTCL - Almost dying kwa sababu ya mafisadi!

3) Zain - hawa si ndo wameiuwa TTCL (kwa kuifisadi). Kumbuka TTCL ilikuwa(bado?) kampuni ya umma.

4) TIGO - Walituibia sana hawa wakati wanaingia. Tulikuwa tunalipia simu hata kwa kupokea. Mambo yalibadilika baada ya kuingia kwa Vodacom kama sikosei!

5)Dovetel - Not yet reliable! Hatujui mafisadi wanamiliki kiasi gani.

6)HITS - Not yet reliable! Hatujui mafisadi wanamiliki kiasi gani.

Do it or be ready to live with the consequences.

Tafadhali hebu fafanua hapa! Do us some justice! In maana hatutaweza kutoka baada ya masaa hayo 72? Unanikumbusha ile nadharia ya 666 kwenye 'baibo'- hatutaweza kuuza wala kununua bila muhuri!
 
Last edited:
It is too late now but not too late enough.. kama uko kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na hauko tayari kusalimu amri, nakushauri kuachilia namba za simu za Vodacom ASAP. As a matter of fact, hamia "kwingine" within the next 72 hours (beginning Monday). Do it or be ready to live with the consequences.

Nilikuwepo.

M.M.

Hii topic tuliijadili hapa kwa kirefu mwaka jana.

Kwa wale walioanza kutumia mitandao jana jana na wale ndugu na marafiki wa wakina RA hawa hawajui machungu ya mitandao kama ya Voda.

Mimi nilishajitoa voda siku nyingi pamoja na kujidai kwamba wao ndio wako kila sehemu nchi hii. Hili lilikuwapo miaka mingi imepita. Sasa hivi mitandao yote imejizatiti huko vijijini. Ukweli na sim kadi mbili za voda nilizowahi kuzimiliki hata namba zake sizikumbuki maana waliniboa kwanza kwa rates kubwa kupita kiasi.

Niliamua kubaki na line ya tigo na zain tu. Wengine hao ni fisadis including Zain .Hizo zingine nilishaachana nazo zamani. Wanaoendelea kubaki nazo nawahurumia. Nawashangaa hata kwa utetezi wao usiokuwa na maana. Una maana kama ni sehemu ya ufisadi huo. Na kwa taarifa yao kugomea bidhaa ni silaha iliyowahi kufanikiwa duniani hapa dhidi ya madhalimu. VodaCom Afrika kusini ni moja ya walioonja joto hiyo.

Jamani tugomee bidhaa zote zitokanazo na mafisadi.
 
Hizi ndio balaa tulizoletewa na Ami Mpungwe, sijui huko yeye ana asilimia ngapi kwenye pie.
 
Thread ya kuisusa VodaCom ilishaanzishwa humu siku za nyuma. Tukaijadili mpaka basi. Tusipande pia ndege za PrecisionAir, kuna akina Mramba humo. Mafisadi wamejenga hadi misikiti na makanisa, tusisali humo. Kuna mashule yamejengwa na mafisadi, tuwatoe watoto wetu huko. Rais tulienae kachangiwa sana na mafisadi kwenye kampeni zake 2005, tumkatae, tumwondoe, tumng'oe?
 
Ama katika hoja za kipuuzi hii ni moja wapo, yalimshinda Mmerekani na vikwazo vya biashara, utaweza wewe?

No no no. Hilo umechemsha kama kawaida yako, ni chuki za kibinafsi na agenda za siri zimekujaa (Mwanakijiji), sasa inaonesha unaposhindwa kisiasa unaanza mashambulizi kibiashara, wewe nadhani unaweza kuuwa kwa roho mbaya ulionayo!

Sio siku zote chuki binafsi ni mbaya inategemea unamchukia nani. sijui kama unamfahamu unayemtakia mema, ungemjua ungeungana kwenye kundi unalo liiita chuki binafsi
 
Nilikuwa Tunduma pale nilishangaa watu wanajiproud kwa kutumia Voda huku wakinishangaa mm nae tumia tiGo dah kwakweli watu akili zao hazifanyi kazi kabisaa wametekwa kama si kuzama kabisa.
Mtu anajiona ufahari kutumia pesa nyingi kwenye line ya voda na anasema huu ndo mtandao wa sisi wenye pesa maskini mtaendelea kutumia tigo.
Miafrika jamani bado sana.
 
Kumbe Mwanakijiji amewatahadharisha wale ambao wamejipambanua wazi kuwa wako kwenye mapambano dhidi ya ufisadi. Sio watu kama sisi ambao tunapambana kwa majina bandia na wala usafi wetu haufahamiki!
 
Machungu ya mtandao wa voda utayapata kama voda ndiyo namba yako hotline!!! Monthly budget yangu kwa voda ilikuwa kubwa sana. Na nilikiwa rigid pia. Baada ya ku-test tigo budget imepungua na mpaka customer service voda walinipigia siku moja maana wananifahamu na kuuliza vipi bosi siku hizi unataka kutukimbia??? Maana nafikiri natumia kama elfu kumi tu kwa voda kwa mwezi kufanya wasifunge line yangu, tofati na hapo nyuma ilikuwa natumia laki tatu mpaka tano kutegemea na shughuli za mawasiliano kwa mwezi huo. Sasa nimeshift to tigo na matumizi ya kazi zile zile hata na zaidi but gharama haifiki laki moja kwa mwezi . Taratibu nitaachana na voda, nitajaribu tena Zantel then I will conclude the two hotline numbers. Zain nilishaachana nayo long time, tangu ilijulikana kama Celtel.
 

Tusifanye mambo kwa kutaka kuridhisha nyoyo zetu bila ya kuangalia na kujali maslahi ya Taifa

Maslahi ya taifa shurti yawekwe kwenye mizani kwa kulinganisha idadi ya watanzania wanaofanyakazi kwenye kampuni ya mafisadi na idadi ya watanzania wanaoumia kutokana na ufisadi wa wamiliki wa kampuni hiyo, kweli umefika wakati wa kutangaza vita kali dhidi ya mafisadi hususan wageni kama RA wanaohujuma uchumi wa nchi hii kwa maslahi yao binafsi.

Ikumbukwe watanzania wataokosa kazi katika kampuni inayopigwa vita wana mtaji wa ujuzi kama hawajaingia kwa mlango wa nyuma, watapata kazi kwenye makampuni halali. Vita yoyote ile ina madhara lakini kama faidi ni kubwa na endelevu kuliko hasara hatunabudi kupigana. Tuwapige mafisadi kwa nguvu zetu zote kwani faida ni kubwa na endelevu kuiko hasara...
 
Back
Top Bottom