Wana CCM naomba mhalalishe picha hizi

I salute you Mzee Mwanakijiji. Nimechoka, sina la kusema. Yapo ya taabu nyingi zaidi ya shida hizi za afya, ukigusa elimu ndiyo usiseme, watoto wanakaa kwenye mavumbi, hakuna madarasa, hakuna vyoo, hakuna waalim, hakuna mlo shuleni hata majumbani, you name all.
 
Naku-support mkuu 100%, ni kweli kabisa, na nafikiri ukiacha ufisadi janga lingine linalopaswa kutibiwa haraka iwezekanavyo ni huko kuzaliana hovyo wakati uwezo wa kutunza haupo, sioni hatari tukichukuwa hatua kama china, tuweke limit ya idadi ya watoto (siyo lazima iwe mmoja kama china) ili wale wachache watakao zaliwa waweze kukua kwenye mazingira bora.
China na india zina ukubwa gani? zina watu kiasi gani? wametoka katika hali gani na wapo katika hali gani?

Wakina mama wakiaa Temeke, au mwananyamala ndo wamezaa hovyo? inakuwaje kama uchumi hautoshi kwenda AgaKhan? kama wilaya nziam ina hospitali moja? population ya Dar es Salaam ni watu wangapi?

Great thinker Indead!!!!
 
China na india zina ukubwa gani? zina watu kiasi gani? wametoka katika hali gani na wapo katika hali gani? !!!

Walikuwa na hali ngumu sana kuliko sisi leo hii wanatupa misaada wao sisi mweh! mchawi aliye tuloga alisha kufa tiba kuipata ni kazi bora arudi mwingereza tu aendelee kututawala mambo yatanyooka.
 
aaargh! hizi picha zinapandisha munkari! this iz veri tuu machi, hako kadada kamevaa jinzi kamependeza lakini.

beki to za topik. waziri ajiuzulu
 
Huyu Ndullu kabla ya kwenda kufanya kazi Washington alikuwa anafanya kazi World Bank office hapa Dar na alikuwa akiishi nyumbani kwake Mbezi Beach, kuna mtu anaweza kutupatia picha ya nyumba yake binafsi iliyoko Mbezi Beach tuone kama ilikuwa na swimming-pool? Kama alikuwa nayo then tutajua kua kwavile kwao Ifakara/ Mahenge alizoea kuogelea mitoni basi aliendeleza utamaduni huo hata hapa mjini; ama sivyo asingekuwa na sababu ya kudai swimming pool toka kwenye fedha yetu!!
 
Kuna sababu gani tena za kumrudisha Kikwete madarakani??? Hutu Ndullu ni fisadi pure kwanza ana tofauti gani na Balali??solution ni kufumua serikali yore...na hili linawezejana kabisa.
 
nilichojaribu kusema ni kuwa
watu wachukulie kuwa afya zao ni muhimu
kuliko kununua khanga au hereni za dhahabu...
zipo dispensary nyingi za binafsi za bei nafuu.....

sio lazima kila mtu akasuburi huduma
ya bure mwananyamala au amana.

mimi binafsi nawajua wamama kadhaa ambao
wana uwezoa kwenda kwenye dispensary
za binafsi za bei nafuu,but wanaenda
hospitali za serikali kwa kila tatizo lao.

wapo kweli masikini wasio na uwezo
but sio wote,wengine ni mazoea ya
huduma za dezo.


Kaka The boss post yako ya kwanza umeboa kwa kweli na ulipaswa kuomba radhi kwa wanajamvi naa hata hao uliowatukana maana wapo dad zetu pia kama si mama zetu, kumbuka unyanyapaa si kwa wagonjwa wa ukimwi tu hata hiyo post yako inanyanyapaa kwa namna moja au nyingine, kumbuka alichokifanya mwana kijiji ni kuonyesha hayo majumba ya bei mbaya ambayo yamejengwa kwa kodi zetu sasa why hospitali zinaosa facilities muhimu kama vitanda na net za kulalia mama na mtoto?? hiyo mihela ya nyumba moja vingepatikana vitanda vingapi?? a wodi ngazpi za uzazi zingepatikana?? Usiiwe mvivu wa kufikiria yaani kusoma hujui hata picha nazo huzioni?? HERI YA MWAKA MPYA KWAKO THE BOSS
 
Nchi inaendeshwa na watu wajinga sana , kwani kama wangekuwa werevu wasingekubali hata hili kutokea kwa kipindi hiki.

Aliyeteua Bodi ya BOT ndio mwenye matatizo zaidi kwani kama hiyo Bodi haiwezi kukataa ama kupinga kitu chochot basi bora isiwepo kabisa.
 
Ndugu zangu wapendwa,Mabibi na Mabwana,kila mmoja wenu kwa cheo na nafasi yake:
Natumai wakati wa kutamka rasmi bila kuogopa wala kuficha kuwa CCM na SEREKALI yake imeendelea KUTUKOSEA ADABU kwa muda mrefu sasa. miaka mitano ya mwisho ya Mkapa na minne hii ya Kikwete, tumejionea Maajabu ya Musa na Majuto ya Firauni. Hakuna yeyote anaeweza kuhalalisha au kutetea yanaonekana kwenye picha hizo na tafsiri yake. Siku zote inafahamika kuwa serekali hua haina Huruma, lakini mara zote inajaribu kuwa na ADABU na HESHIMA kwa Wananchi wake, Inasikitisha, Inaudhi, Inatiauchungu na Inaghadhibisha kuona serekali ya Tanzania chini ya CCM imeendelea kutudharau na kutudhalilisha kiasi hiki. Akina mama wajifungue na kulala sakafuni, Watoto wetu Shule chini ya miti, viti vyao mawe, maji watu wanachota kwenye vidimbwi vya ovyo ovyo, leo karine ya ihirini na moja, karibu miaka Hamsini toka kujikomboa, AIBU KIASI GANI??? Eti watu wachache, familia nne tu zinawekwa kwenye NYUMBA zilizogharimu BILIONS OF SHILLINGS!! KUNA WAALIMU wangapi na ASKARI POLISI wanaolala vibandani?? Wao na Gavana NDILU wana tofauti gani si wote tunakwenda Msalani?? Ndgu zangu tunaandika na kusema sana humu, lakini ndio ile hadithi yakumpigia Mbuzi gita. sasa kuna haja ya kutafuta suluhisho la matatizo yetu kivitendo na simaanishi Vurugu.
 
Askari ndio wanalinda jumba hilo la Ndullu na asubuhi wanaondoka na kuingia wengine waliotokea nyumba za mabati pale Kunduchi , na wao wanaona sawa tuu sasa kuna haja ya asikari wetu kutuonyesha njia walau wamtoe mmoja mfano ndio watu watajua kuwa haya mambo yanakasirisha na kuudhi.

Wewe unamlinda mtru na mke wake kwenye jumba kama hilo halafu ukienda kwako Kunduchi nyumba ni ya mabati fuul suti ,joto kibao halafu unaona kuwa ni sawa tuu,?
 
Wazungu wakitutukana sisi Manyani tusilalamike!Hawaamini kuwa tunaweza kusort out hili tatizo!Tuko tayari kununua Phd fake,kuendesha FWD ,na corruption./ufidadi etc!

Hata wakinamama Wabunge ndio hovyo kabisa.Mwanamke ana moyo,lakini no body cares plight ya wanawake wenzao hapa.CCM inanunua magari zaidi ya 200!
Hizi pesa zinaweza kununua vitanda,hata kujenga maternity wards !
Shame on me,shame on you ,i am sick to death watu wanalia crocodile tears kwa kifo cha Kawawa!
Niko tayari kutoa machozi kwa hawa akina mama watanzania wenzetu ambao hawana
uwezo!

Hivi hujui kuwa wa-TZ ni manyani, na akili zilishapiga kutu miaka mingi iliyopita? T-shirt, pilau na pombe za kienyeji zinatosha kabisa kutusahaulisha adha tulizonazo!! kama huamini subiri matokeo ya uchaguzi mwakani!!
 
Nilijoin JF long time enzi inaanza. Kati ya vitu vilivyofanya uchangiaji wangu upungue kasi ni hali ya plenty of talk and no action. As a girlfriend of mine puts it NATO (no action talk only). Hua napandwa na hasira, naweza andika au changia then I go about my daily activities. It's for the same reason I don't practice religion. Mchungaji au sheikh ana preach pale na unajua kabisa kuna dhambi unazitenda, unaumia yet ukitoka unaenda zifanya tena na kurudi kanisani/msikitini next time for the some routine.
IN SHORT I HAVE A PHOBIA OF BEING A HYPOCRIT.
Sasa basi, mimi naomba hivi: kuna mtu hapa katoa idea nzuri ya kuchapisha picha zinazoonyesha class differences ya viongozi na wananchi ktika nchi yetu, nami namuunga mkono (si mara ya kwanza mimi kuomba hivi).
I kindly ask mwanakijiji, his team and us jamiiforumites to create various educational leaflets to target various groups in our community.
For example a leaflet consisting of pictures and short statements to be effective to village people and maybe deeper dossiers like that of meremeta for the more educated people.
These leaflets are then made to be easily accessible to any body using jamiiforum and people are encouraged to print them and distribute them to any section of the society he or she is conviniently in touch with or can afford to be in touch with. We print make copies and one can anonymously drop a batch when goin shopping at kariakoo, leave a few kwenye daladala e.t.c.

WE TALK TOO MUCH!!! I think the above can be done by even the laziest and most passive among us!
 
Hivi hujui kuwa wa-TZ ni manyani, na akili zilishapiga kutu miaka mingi iliyopita? T-shirt, pilau na pombe za kienyeji zinatosha kabisa kutusahaulisha adha tulizonazo!! kama huamini subiri matokeo ya uchaguzi mwakani!!

Kuwaita Watanzania ni manyani na akili zilishapiga kutu miaka mingi iliyopita ni matusi kwao na uonevu mkubwa kwao. Wananchi wanateseka, wanahangaikia maisha yao na ya watoto wao kwa kulima na kufanya shughuli mbalimbali kujitafutia kipato ili watoto wao wapate chakula, malazi, dawa etc etc. na wengi wao hawajui wao na watoto wao watakula nini kesho hawana kosa lolote la kustahili matusi hayo. Naamini kwa dhati kabisa hata ingelikuwa wewe uko kwenye position waliyonayo asilimia kubwa ya Watanzania ungelishawishika kupokea hizo t-shirt, pilau na pombe. Watukane wale wanaotoa hizo t-shirts n.k. kwa kutumia mateso waliyonayo wananchi kama mtaji wao wa kupatia nafasi za uongozi.
 
aaargh! hizi picha zinapandisha munkari! this iz veri tuu machi, hako kadada kamevaa jinzi kamependeza lakini.

beki to za topik. waziri ajiuzulu

The only solution to all this ni kumpata kiongozi ambaye atajitoa muhanga na kuwa dikteta na kufumbia macho sheria zote zilizowekwa makusudi kuhalalisha uozo mwingi tunaouona ukifanyika na ukifanywa na viongozi nchini mwetu kwa kisingizio kwamba kesi haziwezi kufunguliwa dhidi yao kwa "kukosekana ushahidi".
 
Nduli ni mwajiriwa wa Serikali, asingeweza kukataa haki yake ya kupewa nyumba. Angekuwa mwanasiasa anayetafuta umaarufu ningekuelewa. Pia, aliyepitisha ujenzi wa hekalu hilo si Ndulu. Ni Balali, na ukapata baraka za Bodi ya Wakurugenzi.

Usituletee hadithi za kusadikika! Ndulu kwa cheo chake alichonacho anaweza kabisa kubadilisha maamuzi yote yaliyofanywa na Balali na yakatelezwa to the letter hata bila ya kupeleka kwenye Bodi kama maamuzi yenyewe ni ya kunusuru na kuokoa fedha za umma. Bodi watakuwa 'wehu' iwapo watakataa kuidhinisha hatu hiyo ya kizalendo.
 
Mbaya zaidi hiyo ni hospitali ya wilaya DAR ES SALAAM.

Can U even imagine hospitali ya wilaya say LINDI, MTWARA hali ikoje???

Hivi sisi watanzania hata aibu hatuna kweli kununua mashangingi zaidi ya 1,000 kila mwaka ambayo nina uhakika pesa hizo zingeweza kabisa kuondoa tatizo la angalau vyumba vya dada zetu kuweza kujifungulia salama.

May God Bless Tanzania

Tatizo jingine ni watu kukimbilia mijini wakati uwiano wa kitanda kwa mgonjwa hauna kasi ya uhamiaji wa mijini.
 
Tatizo jingine ni watu kukimbilia mijini wakati uwiano wa kitanda kwa mgonjwa hauna kasi ya uhamiaji wa mijini.

Kama 'watu' wangelikuwa na akili nzuri wakaboresha maisha ya vijijini kama alivyodhamiria kufanya Mwalimu Nyerere katika sera ya Vijiji vya Ujamaa tusingelikuwa na matatizo haya ya watu especially vijana kukimbilia mijini kutafuta maisha.

Nina bahati ya kupata maelezo kutoka kwa watu waliokula chumvi nyingi jinsi ambavyo baadhi ya vijiji vya ujamaa viliweza kushamiri kwa kufuata maelekezo waliyokuwa wakipewa. Kuna vijiji vilianzisha viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza sabuni, kusindika sukari guru na sukari mchanga, kusindika mafuta ya alizeti n.k. n.k. Kwa maana nyingine vijiji hivi vilikuwa vikijitosheleza kwa basic requirements na wakati huo huo kuajiri vijana kuendesha shughuli hizi na kujipatia posho zilizowawezesha kutowaza kwenda mijini.

But alas! Kwa kuwa ndani ya binadamu kuna kitu 'ubinafsi' ni wachache walioweza kuelewa manufaa ya shughuli hizo na concept nzima ya vijiji vya aina hiyo. Ubinafsi ukasababisha baadhi ya watu wahujumu juhudi hizo na hatimaye kuua nia njema ya kuendeleza vijiji, vijana wakakimbilia mijini wakidhani kwamba kuna neema zaidi. Moja ya matokeo yake ni huo msongamano wa wazazi mawodini!
 
Back
Top Bottom