Lissu ambana Mbowe: Aelezea Historia yake, adai hajawahi omba kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, "Nimekijenga chama kwa jasho na nguvu zangu"

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,925
10,479
Ningependa niweke wazi na Watanzania wakielewe, sijawahi kuomba kuwa mwenyekiti kwa mtu yeyote, mwaka 2004 nilikuwa Mwenyekiti baada ya wajumbe wa kamati kuu na wazee wa Chadema kunipendekeza kutokana na historia na commitment yangu ya chama.

Nilianza harakati za kuijenga Chadema baada ya kuona kinasinzia mwaka 2000, nikiwa na Dk. Wilbrod Slaa na wengine watatu, tulitoa magari yetu tukatembea nchi nzima kufanya mikutano. Nikaenda vyuo vikuu kutafuta wanafunzi walioonesha mwelekeo wa kuwa viongozi.==========

Mahojiano kati ya Tundu Lissu na Freeman Mbowe yaliyofanyika katika kipindi cha Speaking out with Tundu Lissu.

Lissu:
Habari za popote ulipo, tuambie uko wapi?

Mbowe: Asante sana nakushukuru Tundu Nakushuru sana, mimi kwa sasa hivi nipo nje ya nchi nipo nje ya Tanzania na sasa hivi napozungumza na nazungumzia kutoka Nairobi Kenya nimekua nje ya Tanzania kwa mda mrefu kama nilivyokuwa nikisema.

Lissu: Asante sasa, habari za Nairobi?

Mbowe: Nairobi ni kwema na namshurukuru Mungu ni kwema sana.

Lissu: Freeman Aikael Mbowe ni jina kubwa sana katika siasa za ukanda huu wa Afrika, Wengi wanakuona wengi wanakufahamu ukiwa bungeni ukiwa jukwaani ukiwa katika mahali pengi leo tunataka tuanze kabisa kuzungumza na Freeman Aikael Mbowe akiwa mtoto, akiwa kijana tunataka tuzungumze maisha yako yote, hebu tuambie una umri wa miaka mingapi? Ulizaliwa mwaka gani? Na wapi?

Mbowe: Kwanza ndugu yangu Tundu sidhani kama masaa mawili yanatosha kueleza historia ya maisha yangu lakini nitajitahidi kufupisha kadri niwezavyo, lakini mimi nilizaliwa mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Hai, Machame kutoka katika wazazi wawili baba Aikael Alfayo Mbowe na mama aliitwa Aishai Ephraimu Shuma hawa ndio walikuwa wazazi wangu nikizaliwa mtoto wa kumi kwa baba yangu na mtoto wa tisa kwa mama yangu kwa hiyo mimi nikiwa kitinda mimba kwa wakubwa wangu kwa maana nikiwa mtoto wa mwisho kwa baba na mama.

Lissu: Oooo kwa hiyo wewe ni mtoto wa mama na mtoto wa baba hongera sana. Hujatwambia mwaka iliozaliwa, tarehe.

Mbowe: Nilizaliwa mwaka 1961 mwaka ambao nchi yetu ilipata uhuru na nikazaliwa tarehe 14/9/1961 na nikabatizwa siku ya 9/12/1961 siku bendera ya mwingereza yaani (Union Jack) inashushwa na mimi nikabatizwa siku ya uhuru kwa maana 1961nikapewa maji ya uzima ya ubatizo na ndio sababu nikapewa jina la Freeman ikiwa na maana mtu huru kwa sababu nilibatizwa siku ya uhuru baada ya kuzaliwa mwaka wa Uhuru.

Lissu: Kwa hiyo hii Freeman sio tu kwamba iliokotwa ni mtoto wa uhuru.

Mbowe: Kabisa niipewa jina hilo maalum kabisa na wazazi wangu siku ambayo nilibatizwa siku ambayo Taifa yetu ilipa uhuru.

Lissu: Hawa wazazi ambao wanampa mtoto majina haya ya uhuru ni wazazi wa aina aina gani, Uhuru Kenyatta na Freeman Mbowe ni watoto wa uhur hawa ni wazazi wa aina gani ambao walikuwa na tashwishwi waswahili wanasema ya kumpa mtoto wao jina la Freeman jina la mtu huru hebu tuambuie kidogo juu ya mzee na mama Mbowe.

Mbowe: Mzee wangu marehemu baba Aikael Alfayo Mbowe alizaliwa mwaka 1922 January tarehe 5 mwaka uleule ambao Mwalimu Julias Nyerere alizaliwa na mama yangu yeye alizaliwa mwaka 1931 Septemba 11 baba alikuwa ni mfanyabiashara katika ahatua za awali kabisa akiwa anashughulika na biashara na ukulima na ufugaji akianza biashara mapema hata kabla ya uhuru na mama yangu alikuwa ni mwalimu na baadae akawa mama maendeleo lakini alikuwa ni mwalimu akiwa anafundisha shule kadha wa kadha kule Kilimanjaro na wazazi wangu hawa wenye historia ya Ualimu na ukulima na ufugaji walikuwa wanafanya shughuli ambazo watu wa kijijini wanafanya. Walianza biashara mapema kabisa hata kabla ya uhuru.

Wakati wanaanza biashara hata kabla ya uhuru watoto wengine tisa walikuwa wameshazaliwa wakati nazaliwa mimi mwaka 1961 familia yetu ilikuwa kwenye biashara miaka nyingi sana.

Lissu: Mimi nilisoma Ilboru miaka ya mwanzo ya 80 Arusha ukienda Moshi ukifika maeneo yale ya Kakafu kakafu magari yalikuwa yanasiamama muda mrefu sana ukiuliza unaambiwa mzee Mbowe yupo na benzi lake kule mbele na wakati ule unaambiwa kuna benzi mbili tu nchi hii moja la mwalimu na jingine la mzee Mbowe. Hebu tuambie Mzee Mbowe alikuwa na connection gani na Mwalimu Nyerere au na mabo ya kisiasa siasa za TANU au za CCM na kadhalika.

Mbowe:Kwa kweli nikiri tu kwamba wakati mzaa anaanza kufanya mabo ya siasa a kina mwalimu na wazee wenzake mimi nilikuwa bado ni mtoto mdogo sana lakini historia nimeikuta simulizi nimezipata maandiko nimeyakuta, mzee alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mwaliku Nyerere na mahusiano yao yalianzia kwenye harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Mzee Mbowe alikuwa ni mzee ambae alikuwa na umashuhuri mkubwa katika Tanganyika kanda ya Kaskazini kwa maana ya Arusha na Kiliamanjaro na Manyara na alikuwa na mahusiano na wale watawala wote wa kiasili ma Mangi wote wale ma Mangi wa Kichaga kuanzia Mangi Maliale na maluma wa Rombo Mangi Shangali wa Machame baba alikuwa ni mtu wao wa karibu sana kwa sababu alikuwa mfanyabiashara mashuhuri kabla hata ya uhuru.

Katika mazingira kama hayo baba alikubaliana na wenzake kadhaa kuhamasisha harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika katika kada ya Kaskazini kwa kuwa watawalawa jadi walikuwa na nguvu sana na walihitaji mtu ambae alikuwa na ushawishi mkubwa sana na waliweza kuingiza TANU kanda ya kaskazini hasa sehem ya Kilimanjaro na hapo ndio mahusiano ya familia ya Mwalimu ilipoingia kwenye familia yetu na alikuwa na ukaribu hata na Oscar Kambona na wazee wengine kadha wa kadha ambao walishiriki katika harakati za uhuru wa nchi kwa hiyo historia ya mwalimu na baba yalikuwa hivyo kwa hiyo hayo mambo ya magari tuyaache tu wazazi wangu walikuwa na magari muda mrefu tu na si benzi tu walikuwa na magari mengine pia.

Lissu: Kwenye hilo hilo la mahusiano la Mbowe na Mwalimu nataka kujua kama umbea niliousikia ulikuwa ni kweli, eti wakati unataka kununua gari yako ya kwanza ulipata kibali kutoka nyumbani kwa mwalimu?

Mbowe: Wakati ule miaka ya 70, 80 kuingiza gari nchini ilikuwa ni kazi kubwa kidogo na ilikuwa ni lazima upate kibali cha state motor cooperation na wakati ule mimi wakati naanza biashara nikataka kuingiza gari yangu ya kwanza mimi kuingiza nchini ilikuwa ni BMW 528 I na kwa sababu mimi nilikuwa nataka kuingiza gari basi baba yangu akamfata mwalimu kuwa mtoto wangu anataka kuingiza gari na mwalimu akasema hebu mpeni Mbowe kibali basi nikapewa kibali na nikaingiza gari. Ila kilikuwa kitu cha kawaida kwa kuwa wengi walikuwa wanapewa kama ambavyo mzee wangu alipewa.

Lissu: Hebu fikiria ni watu wangapi wanajua kuwa Mzee Mbowe alishirikiana na mwalimu katika kutafuta uhuru na mtoto wake ni kiongozi wa chama cha upinzani mkubwa kabisa kwa Tanzania nafikiri ni vitu muhimu kabisa kwa watu kuvifahamu.

Lissu: Mimi ni mwanasheria na nimekuwa nikishughulika na kesi nyingi za uchaguzi. Kesi iiyoweka misingi ya sheria za uchaguzi ni kesi ya Eliafo vs Mbowe, hawa ni kina nani?

Mbowe: Hawa nawafahamu kwa kuwa ni wazee wetu na zamani kulikuwa hakuna jimbo la Hai kulikuwa na Jimbo la Kilimanjaro ambako mbunge wa Kilimanjaro alikuwa anaongoza jimbo kubwa maana moka wa Kilimanjaro ulikuwa una majimbo mawili Same na Kilimanjaro, walikuwa wanagombea jimbo La Kilimanjaro katika uchaguzi wa kwanza kabisa wa mwaka 1965.

Mzee Mbowe na Mzee Alufoo kwanza ni marafiki wa karibu na wameoleana na wametoka Mchame wote ni marehemu Yaani mimi shangazi yangu alikuwa ameolewa na kaka yake na Alufoo na walijikuta ndugu, marafiki wameingia kwenye uchaguzi na Alufoo alishinda uchaguzi huo kwa mujibu wa uchaguzi na wkapelekana mahakamani.

Lissu: Nafikiri ni vyema ukafahamu na watanzania wakafahamamu kuwa mahakama iliamua kuwa kulikuwa na uchakachuaji kwenye kesi ile kwani kura zilikuwa nyingi kuliko wapiga kura. Na mahakama ikaamua ikitokoea kura ni nyingi kuliko wapiga kura basi matokeo yanatanguliwa hivyo mambo haya yalianza siku nyingi.

Lissu: Nataka tuzungumzie historia yako ya elimu ujana wako kikazi na mabo yanayohusiana na hayo.

Mimi nimezaliwa kijijini na nimesoma kijijini nimesoma shule ya Lambo Machame kuanzia chekechea mpaka darasa la saba 1974 na nikaenda sekondari ya Kolila na 75 nikasoma sekondari kwa mwaka mmoja na form two nikaenda kusoma Kibaha shule ya Serikali nikasoma mpaka mwaka 1979 wakati huo vita ya Kagera vikiwa vinapamba moto na nikaenda shule ya sekondari Ihungo kidato cha Tano mama hakupenda ila baba akasema kama watoto wa wenzake wameenda Ihungo basi na yeye ataenda Ihungo kwa hiyo nikaenda sehemu ambapo vita vinapiganwa, Nilisoma HGE na kumaliza.

Na moja ya matukio ambayo mpaka leo nayakumbuka ni kwamba wakati wanajeshi wanarejea kutoka uwanja wa mapambano kule Bunazi sisi wanafunzi wote wa Shule kubwa tulitakiwa tutembee kwa mguu mpaka Mtukula kule Bunazi na tulitembea mchana na usiku na kuna wakati ndege zilipiga kwenye choo chetu cha shule. Nakumbuka wanajeshi walikuwa wanakaa kwenye mahandaki na hata sisis wanafunzi kuna wakati tulilazimika kukaa kwenye mahandaki. Nilimaliza na kupata alama za kwenda chuo kikuu.

Lakini kipindi kile kabla ya kwenda chuo kikuu ilikuwa ni lazima uende jeshini kwa hiyo nikaenda jeshini kambi ya Ruvu katika operation ya imarisha. Baada ya operation ushindi ilifata operation imarisha, na nilikaa pale mpaka nikamaliza mafunzo ya Ukuruta na baadae nikaenda kambi ya Lugalo na hapo nikaa nikamaliza mafunzo kwa mujibu wa sheria na nikawa natakiwa kwenda kazini.

Kipindi kile kabla ya kwenda chuo kikuu ilikuwa ni lazima ufanye kazi kulikuwa na azimio la Musoma yaani huwezi kwenda chuo mpaka ufanye kazi miaka miwili kisha uende chuo ukiwa kazini.

Mimi nililetewa fomu nikajaza kwenda benki kuu na foreign affairs ( wakati ule ilikuwa unaletewa fomu ujaze unataka kwenda kufanya kazi wapi rahisis sana) nikapata chaguo langu la kwanza nikaenda bank kuu kama bank officer two.

Kuna mabo ambayo inabidi tujifunze kuhusu sera zetu kuhusu mifumo yetu ya kielimu na kiajira. Bado hatujachelewa.

Lissu: Kwa nini uliacha kazi Benki kuu si ungekuwa Gavana leo?

Mbowe: Kuna vitu vingine vinakuwa ni Coincidence kama unakumbuka aliekuwa Gavana wa benki kuu Mzee Mtei aliondoka benki kuu na nafasi yake akachukua mzee alikuja kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Alikuja kuwa katiba wa kwanza wa CHADEMA ni yule aliekuwa makamu wa Mtei benk kuu. Watu wengi hawatambui kuwa alienifukuza kazi mimi bank kuu alikuwa ni Bob Makani.

Sasa wakati nipo kidato cha sita mama yangu alifariki na sikupata nafasi ya kumhudumia mama yangu kama nilivyotamani. Sasa tukabaki na baba na baada ya mama kufariki ambaye alikuwa mkurugenzi mwenzake na baba hivyo baba akanichagua mimi kuwa mkurugenzi nikawa nafanya kazi bank kuu na wakati huo ni mfanyabiashara.

Ikawa nikiyoka lunch nakimbia kwenye biashara halafu narudi tena saa nane bank hivyo nikawa nimezidiwa sana, hata wakati ulipofika wa kwemda chuo sikuweza kwani nikawa nimezidiwa na majukumu.

Nikaamua niende kuomba likizo kwa Gavana Bank, likizo ya bila malipo, nikaenda kwa Mzee Makani nikitegemea ataniangalia kwa Jicho la tofauti kwa kuwa ni mtoto Wa mzee Mbowe ila alinambia unaona huo mlango nikigeuka nisikione sitaki kukuangalia.

Nikatoka mbio natoka jasho nikarudi kwa sekretary wake nahema na hiyo ndio ilikuwa siku yanmwisho kufanya kazi Bank kuu sikurui tena nikawa nimeenda tu kwenye biashara na baadae kusoma ila si kwa utaratibu ule.

Lissu: Nataka tuzungumzie Mbowe Mfanya biashara, kuna mahali nimewahi kusikia kuwa ulikuwa unafanya biashara ya uvuvi, kuuza matunda nje ya nchi nk hebu tuambie

Mbowe: Ni kweli mimi biashara zangu zilikuwa za aina mbili kuna biashar ambazo nilikuwa namsaidia baba na kuna biashara ambazo zilikuwa za kwangu mwenyewe nilifungua biashara na marafiki zangu kama mtu ambaye nilikuwa na wito wa kibiashara. Na kwa sababu nilikuwa nafanya kazi bank kuu upande wa fedha za kigeni uweze kupata kibali cha kununua dola, wakati ule kufanya biashara ilikuwa ni lazima kupata kibali bank kuu ili kupata fedha za kigeni hata ukitumiwa tiketi lazima ukaikatie kubali bank kuu na kurugenzi ambayo nilikuwa nafanya mimi kazi ndio ilikuwa inashughulika na vitu hivyo na hivyo nikajua mapema sana maswala ya kuimpot na kuexport biashara.

Wakati nafanya kazi za baba ambazo zilikuwa ni mahotel nikapata wazo la kuanzisha biashara yangu nikaanzisha na rafiki ya Martin kampuni inaitwa Freemart yaani Freeman na Martin. Tukaanza kuvua samaki kamba, tukawa tunafanya hiyo biashara ngumu kweli kweli na wakati huo tukapa kazi ya kusafirisha matunda tukawa tunapeleka matunda kupitia ndege na tulifanya biashara hiyo na kulikuwa na watu wengi.

Mzee Mbowe alikuwa anafanya biashara kabla ya Uhuru katika maisha yake ya biashara mzee Mbowe hakuamini katika ujamaa. Na mwalim aliamua kuingia kwenye Ujamaa na hivyo hivyo Mzee Mbowe aliamua kuacha siasa kwa kuwa hakukubaliana na sera za Ujamaa za mwalimu hivyo akasema yeya anaamini kuwa kufanya biashara kwa haki na uhuru na si ujamaa.

Lissu: Katika hii miaka ya hawa marais watano unaweza kutuambia nini kuhusu maisha haya ya kibiashara kwa awamu zote tano za kibiashara mazingirayamekuwaje unawalinganishaje hawa marais watano?

Mbowe: Nianze na Mwalimu, kufanya kazi katika kipindi cha mwalimu ilikuwa ni ngumu sana na walioweza kumudu ni watu wenye mitaji midogo na ya kati tu kwa kwasababu wenye mitaji mikubwa walitaifishwa majumba walinyag'anywa mali zilitaifishwa na baada ya hapo Akaja waziri mkuu Molinge Sokoine na wale wafanabiashara waliokuwa wanaonesha bado wana vimitaji vidogovidogo wakafanyiwa crapdown mbaya sana na nchi ikawa na ufukara mkubwa na ikatungwa sera ya Uhujumu uchumi na mali zilitaifishwa na watu wakatupa mali watu walikufa walifungwa kuw ani wahujumu uchumi na watu walimwaga sukari kwenye mito.

Baada ya hapo akaja Rais Mwinyi baada ya mwalimu kuamua kutoka madarakani Mwinyi akaruhusu milango ya kibiashara kufunguliwa na hapakuwepo na watanzania wengi waliokuwa na uzoefu na biashara wakawepo watazania wachache waliofaya wakaanza kuagiza bidhaa nje na uchumi ukaanza kufunguka na zile shida ndogo zilizokuwa zinategemea serikali zikaanza kutatuliwa maana ilikuwa ukitaka sukari uende kwenye maduka ya ushirika na hapo ndipo neno ulanguzzi lilipoanza.

Ulanguzi ilikuwa ni ile mbinu ya kupata kibali kijanja ukanunue vitu kwenye maduka ya ushirika na ukaviuze kwa bei ya mara mbili na unapata pesa nyingi tu na hapo ndio ulanguzi na magendo yalipoingia kwa hiyo Mzee mwinyi aliturahisishia mambo mengi tu hata nguo tulikuwa haturuhusiwi kuingiza nguo Tanzania hata mitumba tulikuwa hatuna tulikuwa tunategemea viwanda vya ndani tu kama MWATEX, nk.

Mzee Mwinyi akawa mzee wa RUKSA na hatukuwa na sera za tunataka uchumi wa aina gani kukawa na mvutano kati ya mwalimu na Mwinyi mwalimu anaona ujamaa wake unazikwa na Mwinyi anaona reforms ni sawa na timu yake wakawa wanavutana sana na kuelewana mwisho ikafika zamu ya mzee Mkapa.

Mzee Mkapa akaingia kwenye madaraka 1995 mzee Mkapa alipokuja alirekebisha udhaifu kwenye maeneo ambayo yalikuwa na udhaifu wakati wa Mwinyi na yeye akaingia kwenye sera ya ubinafsishaji akabinafsisha mashirika ya umma ambayo kimssingi yalikuwa yamekuwa mzigo kwa serikali. Mkapa aliamua kufanya reforms na kuingia kwenye maswala ya globlelization na dunia yote ilikuwa imeingia huko na watu wakawa wanamuona kama anachukua sera za magharibi ila alijaribu kuleta mifumo ya kiuchumi. Mzee mkapa alikuwa mwana diplomasia. Alijaribu kuleta mifumo rasmi ya kiuchumi.Na viongozi wengi walichaguliwa kwa misingi ya kidemokrasia na si kurithi.

Lakini bahati mbaya sana yote yalikuwa yanatokea awamu baada ya awamu na hayakuweza kuwasaidia sana wazawa na hatimae akaingia mzee Kikwete na yeye hakukuta mashirika mengi sana alikuta mashirka machache sana na yeye akaendelea kuyamalizia malizia.

Akaendelea kusisistiza katika uwekezaji kutoka nchi za nje na watu wengi walikuja kwa maswala ya mafuta na gesi na mifuko ya jamii ikashirikishwa katika kuwekeza kwenye kuchagia uchumi wakaanza kujenga majengo makubwa na internrt ikaingi na makampuni ya mawasiliano nayo yakaingia. Na utawala wa Kikwete ukawa umefika ukomo na utawaala wa Magufuli ukaingia.

Katika mazingira yote ya kibiashara iwe zangu au za familia wafanyabishara hawajawahi kupitia kipindi au mazingira magumu kabisa ya kibiashara kwa awamu zote. Nadhani alitamani biashara zote zifanywe na seriakli japo hakutamka, na hatukujua alisimamia sera ipi ya kibiashara na aliamini serikali inapaswa kusimamia mapato yote hata zile mamlaka za udhibiti zilizoundwa wakati wa Kikwete aliamini kama zilikuwa zinafanywa ulanguzi hivyo akarudisha mashirika baadhi na kuyapa kazi za kiserikali hata kazi za ulinzi tu alitaka zifanywe na JKT si viabaya kunywa na JKT lakini unaondoa taasisi binafsi ambazo zinalipa kodi unawapa Majeshi kufanya vitu. Hakuona umuhimu wa kuwezesha sekta binafsi ila aliona kama sekta binafsi zinainyima serikali mapato.

Akataka ujenzi wote mkubwa ni aidha unafanywa na makampuni ya wachina au unafanywa na wazawa wachache sana au unafanywa na mashirika ya kiserikali. Unajua Magufuli alitumia zaidi nguvu kuliko ujuzi wa kibiashara, biashara ni ACT huwezi kuchukua leo NSSSF ikaazishe kiwanda na ikaweza lazima itashindwa lakini sekta binafsi zinaweza mfano Bakressa amesoma kwenye chuo chochocte cha biashara lakini anaweza akaendesha bishara zake na zikawa kubwa. Wafanya biashara wengi wakubwa ni watu wenye vipaji tu si elemu biashra ni kipaji tu.

Huwezi kuwa na uchumi ambao serikali inataka kuendesha kila kitu na mbaya zaidi wanaopewa kuendesha wakawa hawajui kuendesha. Na kwa hakika katika kipindi hiki kwa mfanya biashara yoyote katika kipindi hiki ambaye atataka kuwa mkweli hawezi sema alifanya biashara katika kipindi hiki kwa amani lakini wengine wote wanalia labda amabo walikuwa wanfanya biashara kwa upendeleo wa mkono fulani na ahao huwezi sema kuwa ni wafanya biashara.

Nataka tuzungumze Mbowe Mwanasiasa

Lissu: Kwa nini siasa, kwa nini siasa za upinzani na kwa nini CHADEMA

Mbowe: Kama nilivyotangulia kusema kuwa mimi nimezaliwa kwenye familia ya kibiashara alikuwa na asili ya kisiasa vilevile na alipoona hii siasa hapana na Mzee mbowe hakutaka kuingia katika upinzani dhidi ya mwalimu na akaamua kubaki kwenye biashara na nikiri kuwa hata mwalimu hakumzonga mzee Mbowe sana hivyo haikumzua baba kufanya biashara.

Lissu: Nyie mali zenu hazikutaifishwa?

Mbowe: Mali zilitaifishwa, Lakini haikuzuia mzee kufanya biashara hata pale jengo la EXTELECOM lilipo leo ilikuwa ni hetel ya Marehemu baba ilibomolewa kwa hiyo tukipita pale tunakumbuka kulikuwa na property ya mzee pale mtaa wa Samora.

Lissu: Kwa hiyo hayo machungu ya kunyang'anywa mali katika wakati huu wa Magufuli yanakukumbusha mbali sana kwa kutaifishwa mali za mzee.

Mbowe: Kwanza nitoe ufafanuzi kidogo, mzee baada ya kutaifishwa ile hoteli yake ya pale mtaa wa Samora katika kumpa biashara mbadala ndio wakampa ile new Pares Hotel baadae akaigeuza ikawa Mbowe Hoteli baadae mimi nikaigeuza ili kuipanua na nikaingia ubia na NHC ubia na serikali kipindi hicho ilikuwa inaruhusiwa. Wakati huo walianza kuruhusu kuingia ubia majengo mengine ambayo yalikuwa ya serikali yakauzwa na katika watu ambao waliingia ubia na serikali mmoja wapo nilikuwa na mimi na nikaingia ubia na NHC na wao wakawa na asilimia 25 na mimi nikawa na 75 na mkataba upo mpaka leo na tukakubalina na NHC kuwa tutashea mapato yote kulingana na asilimia.

Baadae vyama vingi vikaanza na mimi ndio nikajitokeza kwenye siasa za upinzani, 1992. Why CHADEMA na kwa nini niliingia kwenye siasa, ugumu uliotokea kwenye mifumo ya ujamaa baada ya mwalimu kuondoka na hata leo bado kuna ulaibu wa ujamaa, kwa hiyo vuguvugu la kupenda maendeleo na watu kufanikiwa ndio likaanzisha vuguvugu la watu kuanzisha vyama vingi.

Ugumu uliotokea kwenye mifumo ya kisiasa yaani ideology ya ujamaa uliendelea kuwepo na hata leo hangover ya ujamaa kwenye nchi yetu na hata leo bado kuna hangover ya ujamaa kwa hiyo hulka ya kupenda maendeleo kuendeleza uhuru wa kibiashara ni watu wachache sana amabao walilikubali hilo.

Sasa wakati huo kukawa na vuguvugu la watu kutaka uhuru zaidi wa kibiashara watu wakaanza kufikiria kuanzisha vyama vingi 1992 kuna harakati za kina mzee Mapalala, kuna harakati vyuo vikuu kuna harakati za kina mzee Malando kuna harakati za kina mzee Fundikira wengi wana siasa wakaanza kujitokeza kipindi kile na sisi bado wadogo wadogo.

Wakati huo Mzee Mtei alishatoka IMF , na akateuliwa na Mzee Mwinyi kuwa mwenyekiti wa tax reform commisionakawa anakaa Dar es Salaam akiwa ni mshauri wa serikali kama mwenyekiti wa tax reform na wakati huo akawa anadouble kama chairman wa TDFL wakati Mtei yupo kwenye tax reform ndio vuguvugu la mageuzi limeanza na pakatokea watu katika makundi matatu.

1. Kundi la kwanza ni watu waliokuwa wametumikia serikalini na wakaona siasa za ujamaa hazitupeleki popote hao ni kina Mtei. Kina Makani nk. Kwa sababu Mtei alishafanya kazi serikalini na alikuwa karibu na Mwalimu akawa anaonekana kuwa anaweza kuongoza mapambano.

2. Kundi la wafanya biashara walikuwa wanaamini kuwa kasi ya kukua kiuchumi wa biashara haiko sahihi sana katika uongozi wa chama cha Mapinduzi, kwa hiyo tukawa tunahitaji chama kingine ambacho kitaweza kuendesha uchumi wa kibiashara, na hapo ndipo tuakajikuta na sisi tumeingia.

3. Watu wasomi wazuri tu wengine wapo vyuoni wengine wapo kwenye mashirika ya umma lakini wakawa wanaamini katika siasa za mageuzi.

Kwa hiyo tukakubaliana kuwa Mtei ndie mtu anaefaa kuwa kiongozi wetu tukawa tunatafutana tunakutana na wakati huo tukaunda tume ya waasisi wa CHADEMA. Tulikuwa tuna waasisi wengi sana na wengi kwa bahati mbaya ni marehemu kwa wengi walikuwa ni watu wazima. Na wengi walikuwa ni watu waliojitosheleza na kujitegemea na misingi ya kujitegemea na kujitosheleza kwa CHADEMA iliaanza wakati huo.

Sisi tulikuwa kabisa hatutaki siasa za kijamaa, japo kuna vyama vingine vilianzishwa ila vilikuwa vina mlengo wa siasa za kijamaa kama CCM ila sisi tulikuwa hatutaki kabisa siasa za Kijamaa na mimi ndio nilikuwa mwanzilishi mdogo kabisa wa CHADEMA ila nilikuwa najitosheleza kwa kuwa nilianza biashara nikiwa mdogo sana miaka 29 tu nilikuwa nimeanza CHADEMA na nilikuwa najitoa sana.

Kipindi nimeanza CHADEMA nilikuwa mdogo kwa kuwa wengi waliokuwa chamani walikuwa washakuwa mawaziri mabalozi, magavana nk mimi nilikuwa mdogo na nilionekana kama kijana wa kutumwa na nilikuwa nikitumwa nakubali.

Lissu: Kuna hili pia nilisikia kuwa wewe ndie uliemleta aliekuja kuwa katibu mkuu na baadae makamu mwenyekiti wa CHADEMA Dk. Amani Kaburu

Mbowe: Ni kweli ila siwezi kusema kuwa ni mimi ndie nilimleta ila tulikuwa tunatafuta mtu wa kuja kugombea KIgoma baada ya aliekuwa mgombea wake kufariki na baadae tukasikia kuwa kuna kijana wa Kigoma anafundisha chuo cha Marekani, baadae Mtei akatakiwa aende kumtafuta Kaburu na kweli Mtei akaenda akazungumza nae na akakubali swala likaja ni nani atatoa fedha, Kwa sababu mimi nilikuwa na fedha za kigeni na nilikuwa na akaunti Lonon nilikuwa a kadi ya Wingereza ikabidi nilipe tiketi ya Kabaru kutoka Marekana na Kabulu akaja lakini hakuwa na pesa ya kuishi wala mradi ikabidi. Ndesamburu akajitolea kumpa nyumba ya kuishi ipo Sea View na Shinganya akasema atamlipa mshahara na mimi nikasema nitamlipa mshahara nusu na tulifanya hivyo ili aweze kuishi na mkewe hapa nchini, na tulifanya hivyo kwa watu wengi kwa kuwa tulikuwa tunakikuza chama.

Lissu: Ilikuwaje ukabakia kuwa mwenyekiti wa CHADEMA?

Mbowe: Kuna jambo moja napenda niliweke wazi, wakati tunaunda CHADEMA Lilian mke wangu hakuwa kwenye picha na hakuwa kabisa kwenye siasa za Mtei na hayuko kabisa kwenye siasa yeye yupo zaidi kwenye sayansi kuliko siasa. Mahusiano na lilian yalianza kabla hata hatujaunda CHADEMA. Familia yangu na Na familia yake ni familia zilizokuwa zinafahamiana muda mrefu.

Sisi tulikuwa tunakutana Regen clab Dar tuliuwa tunakutana pale kwa lengo la kufungua clab tulikuwatunakutana pale watu wengi kina Shangai, Makani Basically CHADEMA iliaasisiwa pale ch=lab.

Mimi nilikuwa kwenye CHADEMA kwanza kama mwasisi lakini pia kama kijana niliekuwa nasadia sana kwenye chama, kwanza nilikuwa mjumbe kwenye chama wa vijana na kitu ambacho hawajui watu mzee Mtei na Mzee Makani walihudumu kwa kipindi kimoja kimoja tu. Mtei sio mzee wa kuwekeza kwenye chadema ni miongoni mwa wanasiasa na watendaji wa serikali ambao wako safi, Mtei akifika mwisho wa mwaka hajapelekewa makadirio ya kodi anafanya mwenyewe na anakwenda TRA kuuliza kwa nini hamkuniletea makadirio, hajawahi kuomba wala kulipwa chochote na chadema wala kulipwa posho ila yeye ndio katoa vitu vingi sana ktika kuijenga chadema hasa katika miaka 10 ya kwanza.

Lissu; Uenyekiti wako sasa.

Mbowe: Kitu pekee ambacho ningependa watu wafahamu, SIJAWAHI KUOMBA KUWA MENYEKITI WA CHADEMA katika kipindi chochote, ila nilipendekezwa mwaka 2004 na wajumbe wa kamati kuu na nilikubali kwa masharti matatu 1 Lazima DK Slaa awe katibu mkuu 2. Tufanye mabadiiko ya kimfumo ndani ya CHAMA, na hapo nilishakuwa mbunge na tukaona chama chetu kinadorora tukaanza harakati za kwenda vyuo vikuu kutafuta basi na nikwa mwenyekiti. wanafunzi na tulikuwa wanne tu. Walisema Mbowe sasa ameshakuwa kijana achukue hiki chama, na walinipendekeza kwa sabubu ya kujitoa kwangu kwenye chama historia yangu kwa kuwa nakijua chama na nikiamua kufanya jambo kwenye chama basi nalifanya kwa kujitoa hapo ndipo nilipokuwa mwenyekiti wa CHADEMA na Chama kilikuwa na wabunge wanne. Tulikuwa hatuna katiba hatuna kanuni kwa hiyo kukafanya reform .

Na baadae mwaka 2005 wakanipendekeza kuwa mgombea wa urais, nilikataa lakini wakasema lazima uwe mgombea wa Urais, chama kilikuw ahakina uwezo wa kuwa na mgimbea uraais ia wakasema ili chama chetu kikue lazima tuwe na mgombea urasi. Basi tukaangalia ni nani anaweza kuwa mgimbea wa urais na tukaona Pr. Balegu kuwa anafaa tukampendekeza, na Dk Balegu akaenda kuwaambia nyumbani kuwa nimependekzwa kugombea urais mkewe akasema ukiendelea na kazi hiyo tunaachana leo. Na sisi tulishawaita waandishi ili tumtambulishe kuwa mgombea wa urais ila akasema haiwezekani, sasa tukasema itakuwaje chama hakina mgombea urais. Basi wakasema ni lazima Mbowe usimame. Chama hakina fedha hakina gari hakina kila kitu nakumbuka nikuwa nimekwenda Makambako nakumbuka walikuja kina Mdee, Zotto nk wakasema mwenyekiti lazima ugombee urais.

Lissu: Ni kitu gani unajivunia kwenye chama na kitu gani unaona kama hukufanya vizuri katika uongozi wako kama mwenyekiti.

Mbowe: Nilichofanya vizuri nazungumzia ni kuwa na CHADEMA mpya ambapo tulitengeneza mifumo, Tulikuwa na ndoto na tuliwezakuikamirisha ndoto yetu, tulifanya mabadiliko makubwa ya kimfumo, tulitengeneza katiba ya chama, mabaraza ya chama, mifumo ya kitaasisi na wakati vyama vya upinzani vinasinyaa CHADEMA ilikuwa inashamiri kwa wakati huo na ndipo nikawaambia wenzangu kuwa inabidid tufungue milango tusione kuwa CHADEMA inajitosheleza bali tunahitaji watu wengine ambao tutawaleta pamoja na kufikiri pamoja na ndipo katika kipindi hicho tulikupata wewe.

Chama cha CHADEMA hakijawahi kunilipa mimi chochote, hakijawahi kulipa mshahara, hakijawahi kunilipa posho ila mimi ndio huwa nakigharamia kwa gharama zangu pale napokuw ana uwezo.

Sijawahi kutaka kuwa mwenyekiti na sijawahi kutaka kugombea urais ndio maana aligombea Slaa na baadae Lowasa na ukaja wewe Lissu na kama ningekuwa nataka kugombea urais ingekuwa rahisi tu kwa kuwa nafasi ya kwanza inaenda kwa mwenyekiti mojakwamoja lakini hiki kitu ni mimi ndio nimekibadilisha.

Sasa basi chama kimekuwa ila kwa bahati mbaya ile kasi ya kukua kwa CHADEMA baada ya kuingia kwenye uchaguzi na Magufuli uchafuzi uliofanyika ulitukwamisha japo hatuwezi kusema kuwa tulishindwa ila tulishinda sana sema uchaguzi ulikuwa wa kutumia nguvu na ulikuw wa kibabe na hii kwangu mimi naichukulia kama fursa amabapo watu wetu wajaribiwa na tumeweza kujua nani nani nani na nani ni mtu safi na nani hafai.

Lissu ni kutu gani ambacho unakijutia au unatamani kama kisingetokea au kisingefanyika.

Mbowe: Kwanza niseme sina chochote ninachokijutia ila kuna matukio ambayo yametukia ambayo yameumiza. Kwa sababu kuna viongozi ambao unakuwa unawaamini kwa kuw akwenye siasa ni lazima watu muaminiane, sasa kuna nguvu zinazotumiwa na CCM ili kuumiza vyama vya upinzani na kwa bahati mbaya hawatumia njia ambazo ni halali na si haramu wanatunga sheria Ila hili swala haliumizi upinzani tu bali linaumiza nchi kwa kuwa swala la watu kuondoka watu wanaondoka CHADEMA wanenda huko kusema umbea hii inaumiza na kuvunja sana moyo ila kuna wakati inatia nguvu kusema kuwa tunaweza kwenda mbele.

Lissu: Ulikuwa mbunge kwenye Bunge la Pius Msekwa na ukawa mbunge kwenye Bunge la Mama Anna Makinda na baadae ukawa mbunge kwenye bunge la Job Ndugai unawazungumziaje hawa maspika wa bunge.

Mbowe: Bunge ni taasisis muhimu sana kwenye nchi yoyote kama hatuna bunge lenye meno nchi hiyo iko hatarini.

Msekwa hakuwa na utoto wala hakuwa na mambo ya kutaka kutesa wapinzania hata katika udogo wake, Msekwa alikuwa amekomaa, msomi msomi wa vitabu na hakuwa na uswahili.

Anne Makinda alikuwa mwanamke mwema anasikiliza japo alikuwa anapendelea chama chake cha Mapinduzi ila katika staha na alikuwa bunge lilikuwa na heshima bunge kuna wakati tunaweza tukaamua tuachane na mambo ya vyama tusaidiane katika hiyo ajenda kwa kuwa ni ajenda ya kitaifa.

Ndugai, Sitamani kumzungumzia kwa kuwa sina wa kumlinganisha nae kati ya uliotaja. Ndugai ana uwezo mdogo sana, la nimewahi kujiuliza kwa nini ana chuki na mimi hawezi kuongea bungeni bila kumtaja Mbowe bila kusema uwongo juu ya Mbowe nimewahi hata kumtumia meseji kumuuliza kwa nini hii imekuwa binafsi sana ila nikaja kujua kuwa tuna spika ambaye ana uwezo mdogo sana hafai hata kuwa mwenyekiti wa mtaa, hafai hata kumjadili kama hivi tunavyomjadili niseme tu ana uwezo mdogo sana.

Lissu: Katika safari ndefu ya kisiasa umeingia gharama sana hebu tueleze kuwa kiongozi wa chama cha upinzani kuna gharama gani?

Mbowe: kuna gharama kubwa sana si kwa fedha tu bali hata kifamilia, familia yangu imekumbwa na madhila kutokana na siasa zangu hata watoto wangu wananambia baba vipi nawaambia kuwa huu ni wito, tumepeata hasara kibiashara, watoto wangu na mke wangu hatuonanani wakati mwingine tunapishana tu Airpot. Tumekichangia chama na si mimi tu hata nyie mmekichangia sana chama leo hatuna luzuku hata shilingi moja wote tunachangia chama.
 
Ningependa niweke wazi na Watanzania wakielewe, sijawahi kuomba kuwa mwenyekiti kwa mtu yoyote, mwaka 2004 nilikuwa mwenyekiti baada ya wajumbe wa kamati kuu na wazee wa Chadema kunipendekeza kutokana na historia na commitment yangu ya chama.
Chama ni chako mkuu wewe endelea tu.

Hata Museven na Kagame wanachaguliwa na wananchi, sasa kama wananchi wenyewe wanawapenda wao ni nani wawakatalie?
 
Ningependa niweke wazi na Watanzania wakielewe, sijawahi kuomba kuwa mwenyekiti kwa mtu yeyote, mwaka 2004 nilikuwa Mwenyekiti baada ya wajumbe wa kamati kuu na wazee wa Chadema kunipendekeza kutokana na historia na commitment yangu ya chama.

Nilianza harakati za kuijenga Chadema baada ya kuona kinasinzia mwaka 2000, nikiwa na Dk. Wilbrod Slaa na wengine watatu, tulitoa magari yetu tukatembea nchi nzima kufanya mikutano. Nikaenda vyuo vikuu kutafuta wanafunzi walioonesha mwelekeo wa kuwa viongozi
je kwanini kila aonyeshaye nia ya kuuhitaji uenyekiti hutimuliwa?
 
Mwamba anaunguruma .
Mwenyekiti wangu mie huyo.โœŒ๐Ÿฝ
Yaani utabaki kuwa Mwenyekiti ili MaCCM yaendelee kuzima mmoja bada ya mwingine .. DADEKI..๐Ÿ’ƒ๐Ÿพ๐Ÿ•บ๐Ÿฝ๐Ÿ’ƒ๐Ÿพ๐Ÿ•บ๐Ÿฝ๐Ÿ’ƒ๐Ÿพ๐Ÿ•บ๐Ÿฝ๐Ÿ’ƒ๐Ÿพ

leo lumumba na Chamwino washapata kazi yakuwaingizia hela. Ni kumtukana Mzee Mbowe, mpaka vijasho vya kwapani viwatie fangasi. ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
MaCCM yanamuogopa sana Mbowe.
โœŒ๐ŸฝโœŒ๐ŸฝโœŒ๐ŸฝโœŒ๐ŸฝโœŒ๐ŸฝโœŒ๐ŸฝโœŒ๐ŸฝโœŒ๐Ÿฝ
 
Katika vetting bora Kuwai kufanyika Tanzania ni hii ya mbowe kuwa mwenyekiti

Other wise chadema ingekuwa tayari ni historia.

Kama ilivyo kwa CUF, NCCR, TADEA, UDP na ACT
Ndiyo maana wana cdm tunajivunia sana kuwa na mwenyekiti mwenye msimamo usiyo yumbishwa.

Ule usemi wa tulianza na Mungu wala hatukuuokota mitaani bali ulikuwa na chanzo chake na maana yake halisi.
 
Back
Top Bottom