Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,743
Jana dunia imeshuhudia hukumu ya haki iliyotolewa na mahakama dhidi ya kada mwandamizi wa CCM Lengai Ole Sabaya ambaye amehudumu nafasi mbalimbali ndani ya chama (UVCCM), na hata kuteuliwa na JPM kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.
Hukumu ya Mahakama imeenda kuhitimisha kesi iliyomkabili Sabaya ambapo alitiwa hatiani kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha.
Sitaki kuingia undani wa kesi kwa sababu wachambuzi mbalimbali wameshaweka mabandiko humu wakielezea kwa kina na kwa vipengele vya kisheria na hata wengine waliweka bettings za kumtoa au kumtia Sabaya hatiani.
Hapa najikita kwenye eneo la Siasa.
Sabaya ametenda makosa yake akiwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya. Hakuwahi kuonywa wala kupewa angalizo dhidi ya mwenendo wake huo. Ikumbukwe katika moja ya matukio aliyoyafanya aliwahi kusifiwa na mteuzi wake, waziri wa fedha (sasa Makamo wa Rais), Gavana wa Benki Kuu na hata TRA waliwahi kutia neno la kumuunga mkono.
Hitimisho la.kesi hii, hata kama Sabaya atakata rufaa na kushinda limeiweka CCM kwenye kona mbaya sana ya kukosa uaminifu wa kisiasa. Sabaya kama Mkuu wa Wilaya, anashika nafasi ya 4 kwenye Kamati ya Siasa ya Wilaya. Anaingia vikao vyote vya maamuzi ya CHAMA ngazi ya Wilaya. Pia ikumbukwe yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mahakimu wikayani. Hivi vyeo vyote vilipaswa kumfanya awe makini na tahadhari kuwa kwenye wajibu wake.
Ushiriki wake kwenye siasa kama kamisaa wa Chama Wilayani umeleta tafsiri mpya sasa, tafsiri yake ni kwamba hawa viongozi wanaoteuliwa na Rais wamekuwa wanajiona wana kinga ya kutoshtakiwa wakati Katiba ya JMT inatoa kinga kwa rais pekee. Wanaweza wakafanya lolote kwa yeyote na wasifanywe chochote.
Sabaya alifanikisha mradi wa CCM kuwaminya Wapinzani Wilaya ya Hai. Ikumbukwe namna alivyofanikisha ushindi wa kibabe kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 2020 ambapo Mbowe alikosa ushindi kwa kuporwa kura zake huku mshindani kutoka CCM akishinda isivyo halali.
Kufungwa miaka 30 jela kwa kosa la ujambazi, na kosa lenyewe lilifanyika akiwa Mteule wa Rais ambapo anaongoza vyombo vya Ulinzi na Usalama Wilaya ni DOA kubwa sana kwa medani za kisiasa. Doa hili halimuachi salama mteuzi. Doa hili haliiachi salama CCM.
Kutumia madaraka yako kufanya ujambazi tena wa silaha dhidi ya watu ambao umeapa kuwalinda na kuwahakikishia ustawi wao kijamiii na kiuchumi ni jambo linaloleta ukakasi mkubwa kwa wadadisi wa kisiasa.
Inawezekana Sabaya ameangukiwa na jani la vunjagenge lakini wapo wengine ambao hawajaguswa na kiujambazi ni wabaya kuliko Sabaya.
Wapinzani wakiacha siasa zao za OyaOya na kujikita kimkakati, huu ndiyo wakati wa kuielezea CCM kwa Umma namna ambavyo inakumbatia na kulinda wahalifu kwa kigezo cha HUYU NI MWENZETU. Hukumu ya Sabaya iwafungue macho kuifahamu CCM halisi na siyo hii ambayo inajitabainisha kuwa ina viongozi safi na wenye falsafa.
Wananchi wameshaanza kuichoka CCM tangu kale, na kinachoisaidia ni ndoa yake ya mitala na vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo vimeapa kufanya lolote hata ikibidi kuua nusu ya Watanzania ili CCM iendelee kutawala.
Ukishatishia maslahi ya CCM, fahamu kuwa umetishia maslahi ya Nchi. Ifike mahala tuyaone haya mambo kwa jicho la udadisi na utafiti.
Nyerere aliwahi kusema Tanzania na Watanzania Kwanza kisha mengine yanafuatia. Pia aliwahi kusema kuwa CCM siyo baba wala mama yake.
Ni wakati sasa wa walio wasafi ndani ya CCM kujiepusha na chama hiki ili kuleta mwanzo mpya wa siasa na uongozi wa nchi yetu.
Kesi hii ya Sabaya imezua mijadala mitaani kuhusu hatima ya CCM kwenye chaguzi zijazo.
Mungu isaidie na kuibariki Tanzania