Ndugu zangu wapendwa,Mabibi na Mabwana,kila mmoja wenu kwa cheo na nafasi yake:
Natumai wakati wa kutamka rasmi bila kuogopa wala kuficha kuwa CCM na SEREKALI yake imeendelea KUTUKOSEA ADABU kwa muda mrefu sasa. miaka mitano ya mwisho ya Mkapa na minne hii ya Kikwete, tumejionea Maajabu ya Musa na Majuto ya Firauni. Hakuna yeyote anaeweza kuhalalisha au kutetea yanaonekana kwenye picha hizo na tafsiri yake. Siku zote inafahamika kuwa serekali hua haina Huruma, lakini mara zote inajaribu kuwa na ADABU na HESHIMA kwa Wananchi wake, Inasikitisha, Inaudhi, Inatiauchungu na Inaghadhibisha kuona serekali ya Tanzania chini ya CCM imeendelea kutudharau na kutudhalilisha kiasi hiki. Akina mama wajifungue na kulala sakafuni, Watoto wetu Shule chini ya miti, viti vyao mawe, maji watu wanachota kwenye vidimbwi vya ovyo ovyo, leo karine ya ihirini na moja, karibu miaka Hamsini toka kujikomboa, AIBU KIASI GANI??? Eti watu wachache, familia nne tu zinawekwa kwenye NYUMBA zilizogharimu BILIONS OF SHILLINGS!! KUNA WAALIMU wangapi na ASKARI POLISI wanaolala vibandani?? Wao na Gavana NDILU wana tofauti gani si wote tunakwenda Msalani?? Ndgu zangu tunaandika na kusema sana humu, lakini ndio ile hadithi yakumpigia Mbuzi gita. sasa kuna haja ya kutafuta suluhisho la matatizo yetu kivitendo na simaanishi Vurugu.