Tanzania , ni nchi ya ajabu sana ulimwenguni, na ndio maana inaongoza kichawi na kinajimu.
Baada ya Kawawa kufa Sheikh Yahaya anajitapa mitaani kuwa utabiri wake kuwa mwaka 2009 usingeisha bila kiongozi mkubwa kufa umetimia.
Sasa kama nchi iko hivyo mnataka Gavana aweje?
Naye huyu kutumia bilioni 3 kujenga nyumba wakati nchi inaenda kuomba msaada wa vyandarua na kupewa vyenye dhamani ya milioni 78 wanakuja na kuutangazia umma kuwa ni mafanikio ya JK .
Inatia uchungu sana, nilikuwa Tanga Jimbo la Handeni wakina mama wanachota maji kwenye mto , na tangu Augusti mwaka jana kata ya Kiva pekee imeshapoteza watu 248 kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, halafu gavana anajenga jumba ambalo , sijui la kazi gani.