Walimu wadada mbona mmepinda sikuhizi?

Walimu wadada mbona mmepinda sikuhizi?

Walimu ni zao la jamii hivyo ukiona wameharibika ujuwe jamii iko hovyo zaidi kwani pamoja kufunzwa haiba wako hivyo walivyo
 
Naongelea waalimu wa shule za msingi na upili (baadhi sio wote) zamani enzi za mwalimu ukitaka kuoa waalimu ndio walikuwa ni candidate wa kupigiwa mifano kila mtu atakupongeza kwa kubahatika kupata jiko kama hilo la uhakika ndio maana unaweza kuona viongozi kibao serikalini walijitwalia wake huko na hawajawahi angushwa/jutia kupata wake huko wenye haiba na maadili yaliyotukuka.

Kwa miaka ya karibuni wamebadilika sana wengi micharuko kama huku mtaani tu kama wako wa kupigiwa mfano inabidi umulike na tochi hata ukipata wengine wanaona kila mtu ni kama mwanafunzi wake wa darasani/kila kitu anajua yeye!Mpaka kwenye sehemu zisizo na staha unakuta walimu pia wapo (mfano social network na magroup mbalimbali wako huko) utajenga vipi maadili ya wanafunzi na familia yako wakati wewe mwenyewe umepinda?

Nimeongelea walimu kwakuwa ni vioo kwa vijana wetu waliohuko mashuleni kwao na katika jamii.

Karibu kwa wenye hoja na mitizamo/uzoefu tofauti na waalimu wa kike, dada na wake zetu.
hivi waalimu wa kiume hatakiwa kuwa vioo vya jamii?
mbona wanaume wanawasakama wanawake?
je! wew mwanaume ndo unahaki kufanya kila uchafu na sio vibaya?
ikiwa wew kipanga huoni ni haki yako kupata mcharuko?
kwanini upande ulezi uvune mahindi?
 
Kwingine kooote umeongea point ila hapo ulipo gusa socia network ndo umeharibu ila imesaidia kujua wewe ni mtu aina gani aisee,sijui ulitaka walimu waandikiane barua na kutuma posta ili wasitumie social media?
 
mkuu mada ya leo ni wadada hiyo unayosema inaweza kuwa mada mpya.
 
mkuu wanatamaa! wanapenda maisha ya telemundo.
Kwa sababu uwezo wanao. Tatizo watu wanafikiri walimu ni watu wa dhiki asee.. Sasa hivi npo sehem flan na walimu wenzangu wawili tunapata kilaji kwa raha zetu.
 
Kwingine kooote umeongea point ila hapo ulipo gusa socia network ndo umeharibu ila imesaidia kujua wewe ni mtu aina gani aisee,sijui ulitaka walimu waandikiane barua na kutuma posta ili wasitumie social media?
nimefafanua kuhusu hilo.wapo waliouliza kuliko wewe umeshafanya conclusion
 
Kwa sababu uwezo wanao. Tatizo watu wanafikiri walimu ni watu wa dhiki asee.. Sasa hivi npo sehem flan na walimu wenzangu wawili tunapata kilaji kwa raha zetu.
mbona.wengi wanakauka midomo mpaka.wanataka msafiri bure kwa daladala?
 
Mshana nakuheshimu sana lakini kwa uzi kama huu heshima yako inaanza kupungua taratibu.. Kwamba na walimu wa kike wako social networks! Watajenga vipi maadili! Mshana umekosea sana
 
Zamani walimu wa diploma na wa cheti walikuwa wengi, na huko kwenye vyuo ualimu walikuwa wanafundishwa mambo ya malezi na haiba ya ualimu kwa ujumla. Sasa hivi walimu wengi wanatoka vyuo vikuu ambako mambo ya malezi na haiba hakuna anayeyaangalia.

Aliyesoma diploma halafu akaenda chuo kikuu ataungana na mimi katika hiki ninachosema. Na haiwezekani huko vyuoni ukaanza mambo ya malezi haiba kwa wanachuo ualimu tu wakati wanachuo wa kozi wengine wakijiachia...nyakati zimepita sasa, twende hivyo hivyo!
 
Kada pekee ambayo bado haina mushkeli ni wadada wa kazi tu....
Mkuu wewe unatania, kuna mdada wa kazi ana kijana wa ng'ombe, ana boda boda wa kijiwe cha mtaani, kijana wa kiume wa humo ndani, yani balaa
 
kwa hiyo mitoko vigumu kufanya hayo matayarisho! na ukizingatia shule zilivyonyingi wakaguzi wachache hawafiki kukagua madarasani walimu mnaishi kwa free style
Wanafunzi wenyewe kama hawa?
Screenshot_2016-03-09-21-14-39-1.png
 
Attachments

  • Screenshot_2016-03-09-21-14-39-1.png
    Screenshot_2016-03-09-21-14-39-1.png
    246.5 KB · Views: 38
Mkuu unaongelea walimu ambao wanatoka vyuo hivi vyenye skendo za uaji wa utoaji mimba au walimu wap?
 
Back
Top Bottom