Walimu wadada mbona mmepinda sikuhizi?

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Naongelea waalimu wa shule za msingi na upili (baadhi sio wote) zamani enzi za mwalimu ukitaka kuoa waalimu ndio walikuwa ni candidate wa kupigiwa mifano kila mtu atakupongeza kwa kubahatika kupata jiko kama hilo la uhakika ndio maana unaweza kuona viongozi kibao serikalini walijitwalia wake huko na hawajawahi angushwa/jutia kupata wake huko wenye haiba na maadili yaliyotukuka.

Kwa miaka ya karibuni wamebadilika sana wengi micharuko kama huku mtaani tu kama wako wa kupigiwa mfano inabidi umulike na tochi hata ukipata wengine wanaona kila mtu ni kama mwanafunzi wake wa darasani/kila kitu anajua yeye!Mpaka kwenye sehemu zisizo na staha unakuta walimu pia wapo (mfano social network na magroup mbalimbali wako huko) utajenga vipi maadili ya wanafunzi na familia yako wakati wewe mwenyewe umepinda?

Nimeongelea walimu kwakuwa ni vioo kwa vijana wetu waliohuko mashuleni kwao na katika jamii.

Karibu kwa wenye hoja na mitizamo/uzoefu tofauti na waalimu wa kike, dada na wake zetu.
 
Mkuu unataka mpaka leo waalimu wawe wanavaa gagulo la rangi ya jani la mgomba uku wamesuka twende kilioni au wamepaka zazuu kichwani na viatu vya Juma na Roza ndio uone kua sio micharuko,siku hazigandi kaka acha nao waende na wakati alafu imani kua waalimu ndio kisima cha kusaka wakuoa imepitwa na wakati
 
So unatushauri tufate kada gani mbadala wa walimu!??

Btw tabia ni mtu sio taaruma alionayo...
mkuu inawezekana huelewi kuwa waalimu wanafundishwa HAIBA ya ualimu na MAADILI katika masomo yao ni tofauti na fani zingine ambazo watu tunapuyanga kama kondoo asiyekuwa na mchungaji.kwenye mke sikushauri mkuu.usije ukarudi kwangu yakikushinda
 
Naona unajifanya mwinyi mpekuzi wa jarida la sani ... Lol... By the way mambo yanabadilika kwahyo usishangae hata na walimu nao wakibadilika
mkuu mitaala yao kule vyuoni walikofuzu haijabadilika.kwanini wabadilike huku mtaani?
 
Mkuu unataka mpaka leo waalimu wawe wanavaa gagulo la rangi ya jani la mgomba uku wamesuka twende kilioni au wamepaka zazuu kichwani na viatu vya Juma na Roza ndio uone kua sio micharuko,siku hazigandi kaka acha nao waende na wakati alafu imani kua waalimu ndio kisima cha kusaka wakuoa imepitwa na wakati
mkuu kuna mavazi ya waalimu tofauti.na customer care wa voda/Tigo.sio mbaya wabadilike lakini tusipoteze imani nao katika jamii.wao ni walezi na vioo vya jamii.
 
Mtoa mada umetumia staha sana kuongelea hawa baadhi ya walimu wengi wakike. Zamani ilikua hivyo walimu wa kike walikua ni mfano wa kuigwa lakini kwetu sisi sasa hivi wamekua ni mfano wa kuonyea. Maadili hawana kabisa, wazinzi sana( zamani ilikua ma askari lakini miaka hii walimu nao wapo sana ila hawavumi), walevi, tamaa, kibuli , ubishoo na usista duu NK. Miaka ya nyuma kama unahitaji kuoa mwl wa kike, tulikua tunaoa tu tena bila hata kuuliza tabia lakini sasa hivi kama huta chunguza vizuri utapata fisi maji aliye jifunika ngozi ya ualimu.
Mwisho nadhani ukosefu wa ajira huku mtaani na mikopo huko mavyuoni labda umefanya baadhi ya watu wengi kusomea fani ambazo sio zao ndio maana hii kada ya ualimu nayo ni muhanga.

NB: Nimesema sio walimu wa kike wote ila baadhi yao wengi wako na hizo matabia. Kwahiyo badilikieni.
 
wivu unakusumbua kada yako inadharaulika, tutapata wapi material uptodate tusipopekua kona mbalimbali unataka wanafunzi watuaibishe kwenye current issues??

mfano mwalimu wa civics daily majipu yanatumbuliwa mawaziri wapya, mifumo ya serikali ama unataka akaseme bado waziri mkuu ni Sumaye? tuache best hatutaki kupauka tena na siee
 
wivu unakusumbua kada yako inadharaulika, tutapata wapi material uptodate tusipopekua kona mbalimbali unataka wanafunzi watuaibishe kwenye current issues??

mfano mwalimu wa civics daily majipu yanatumbuliwa mawaziri wapya, mifumo ya serikali ama unataka akaseme bado waziri mkuu ni Sumaye? tuache best hatutaki kupauka tena na siee
madam hayo ni matumizi mazuri ndio maana hata serikali inampango wa kuwapa laptop.lakini kuwa muwazi wote mnatumia mitandao in a constructive way? ndio maana nimesema baadhi.
 
Kila mahali kuna akina dada walioharibika tabia. Kuoa si kutazama taaluma ya mtu. Ni kumtazama mtu mwenyewe.
sio kweli kuna maadili ya upolisi.kama hayafuatwi hatuwezi kusema ni jamii nzima.pia kwa waalimu kuna ethics wanafundishwa.sijakurupuka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom