Kupanda cheo kwa walimu kwa kigezo cha PEPMIS

Kichaka12

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2018
Posts
317
Reaction score
287
Wasalaam ndugu zangu jukwaa la elimu

Kumekuwa na taarifa kuwa waalimu watakaopanda vyeo KIGEZO CHA asilimia za ujazaji wa e utendaji.

Hiki KIGEZO kitawanyima walimu wengi haki Yao ya msingi kwasababu zifuatazo.

1. Uelewa mdogo wa mfumo
Tangu serikali iunde mfumo huu ni watumishi wachache sana walipewa semina namna ya kutumia na wengi wao hawana uelewa wowote kuhusu mfumo huo.

2. Ugeni wa mfumo Kwa wakuu wa shule
Mfumo wa pepmis unahusisha pia mkuu kuweka performance indicator.. ambazo hizi sasa zitatengeneza total score. Kwa hiyo hizi zikisetiwa vibaya mwalimu hata upandishe vipi taarifa zako kwenye mfumo hiyo total score inakuwa ndogo.

3. Matatizo ya kimfumo
Wakati mwengine mfumo unasumbua hasa kwenye maeneo yenye shida ya kimtandao. Pia unaweza jaza asilimia mia ila report ya mfumo inaonesha asilimia chache kuliko zile ulizoweka. Nani wa kulaumiwa? Changamoto

4. Matatizo ya mtandao
Hapa Tanzania yapo maeneo network ni ya shida sana na walimu wapo huko

5. Uelewa mdogo wa maswala ya mtandao
Kwahakika hapa Tanzania Kuna watumishi ni paper based. Hivi vitu vya mfumo wanahitaji mazoezi ya muda mrefu sana.

6. Kutokujua athari kabla
Swala la kufikisha asilimia 75 za upande daraja walimu wengi wameona kwenye waraka wa mwaka huu. Ukijumlisha na ugeni wa mfumo kwakweli hurima inahitajija Kwa mwaka huu

7. Taarifa zq mfumo hazithibitishi utendaji
Ni kweli tunatakiwa kuripotia kwenye mfumo kila tunachofanya. Lakini wapo wengi wanajituma na kazi wabazofanya zinaonekana ila tu walisahau au walishindwa kuripotia. Huruma inahitajika

8. Mkuu kushindwa kuzifanyia kazi taarifa za mfumo
Kuna baadhi ya walimu wameripotia taarifa zao vizuri ila unakuta mkuu wake ndio ameshindwa kuzifanyia kazi ila inakula Kwa mwalimu

Changamoto ni nyingi siwezi andika zote.. naomba tu vyombo vya habari zipaze sauti walimu wahurumiwe.. MFUMO NI MPYA

NAWASILISHA
 
Pole , unadhani walioanzisha hawatambui hizo changamoto zote, Cha msingi timiza wajibu mkuu.
 
Huu mfumo sio walimu pekee yao bali ni wawatumishi wote wa umma
 
Acha lawama ndugu yangu ,kama ni mfumo unajza kila wiki siku moja , inakuwaje ukose 75% kwa mwaka nzima ? Labda itokee mkuu wako hajaaprove na kakufanyia roho mbaya.

Unazungumzia tu Pepmis sisi wengine mifumo mikubwa hata seminar ya siku moja hatujapewa zaidi ya kudownload Manual na kusoma ili kujua...Labda useme hamna vitendea kazi ila hata simu unaweza kujaza ... Kingine hata kusimamizi wako awe anajua kwamba leo iko hivi kwa sababu wengine ni wavivu labda chini yake kuna watu zaidi ya 10 anawasimamia so sio rahisi akuapprove kwa wote.
 
Mbona hoja kichangamoto zina mashiko sana ila wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi hamuwakilishi hizi changamoto miaka nenda rudi ajenda ni posho, hizi hoja ni za msingi sana hivi unawezaje furahia cheo au mshahara mzuri ,posho nzuri huku ukitaabika kwenye utendaji si kutengeneza presha na kufa tu pasipo kuja kufaidi pension
 
Sijalaumu,

Unajaza progressive report.. na unaweka percentage za performance, mkuu ana approve.. unaona progression zinapanda na tulijaza mpaka 100.

Ila mfumo umeweka 88 kama progressive percentage na 62 kama total score. Sasa ilitakiwa nifanye nini ambacho sijafanya?
 
  • Thanks
Reactions: K11
Acha lawama ndugu yangu ,kama ni mfumo unajza kila wiki siku moja , inakuwaje ukose 75% kwa mwaka nzima ? Labda itokee mkuu wako hajaaprove na kakufanyia roho mbaya.

Unazungumzia tu Pepmis sisi wengine mifumo mikubwa hata seminar ya siku moja hatujapewa zaidi ya kudownload Manual na kusoma ili kujua...Labda useme hamna vitendea kazi ila hata simu unaweza kujaza ... Kingine hata kusimamizi wako awe anajua kwamba leo iko hivi kwa sababu wengine ni wavivu labda chini yake kuna watu zaidi ya 10 anawasimamia so sio rahisi akuapprove kwa wote.
Sijalaumu,

Unajaza progressive report.. na unaweka percentage za performance, mkuu ana approve.. unaona progression zinapanda na tulijaza mpaka 100.

Ila mfumo umeweka 88 kama progressive percentage na 62 kama total score. Sasa ilitakiwa nifanye nini ambacho sijafanya?

Na pia elewa idadi ya walimu na level zao za uelewa., huwezi linganisha na kada zenye watu wachache wanaoweza kujifunza Kwa manual guide.

Hivi unayajua mazingira ya walimu wote tz.. nasemea wengi pia
 
Hiyo barua umeambiwa usiitume kwenye mitandao ya kijamii. Ndio maana serikali inapenda kugonga mihuri ya SIRI hata documents ambazo hazipaswi kuwa siri.
 
Sijalaumu,

Unajaza progressive report.. na unaweka percentage za performance, mkuu ana approve.. unaona progression zinapanda na tulijaza mpaka 100.

Ila mfumo umeweka 88 kama progressive percentage na 62 kama total score. Sasa ilitakiwa nifanye nini ambacho sijafanya?

Na pia elewa idadi ya walimu na level zao za uelewa., huwezi linganisha na kada zenye watu wachache wanaoweza kujifunza Kwa manual guide.

Hivi unayajua mazingira ya walimu wote tz.. nasemea wengi pia
Sasa Wewe hata mwaka haujaisha ushafika 100% labda kwa baadhi ya Task ,pale unajzaa hata 3 kwa kila wiki inategemea na uzito wa kazi yako...ikitokea uko chini ya hapo unaweza ku'appeal.
 
Ripoti ni ya mwaka Jana ndio inatumika
 
Hlo n suala dogo tu wewe komaa uwajazie PePmis yao isome 100 arf wanafunzi watajijua
 
Nafikir pia tunahitaji elimu ya namna pepmis invyo calculate score
Progress percentage Ikiwa 100 = Total score ya 70.
Supervisor wako ana 30 kama Qualitative.
Hivyo kwenye assesment anakuongezea 30 ili ufikishe score ya 100.
 
Vip mnapata communication allowance ili mnunue vocha mpate mb za kutosha kujaza hizi taarifa kila wiki/siku/mwezi?? Kingine huu mfumo si mgumu sana kama mazingira na seminar za mara kwa mara zingefanyika kuwajengea watumishi uelewa wa hii mifumo..NB watumishi wengi hasa waalimu mifumo mingi ya computer mfano mdogo microsoft Excell kwao ni kipengele
 
Umenielewa vizuri Sanaa

Ndio lengo la kuweka huu Uzi angalau watu wasihukumiwe Kwa muda huu..

Maana mfumo ni rahisi kutolea taarifa ila ufinyu wa semina na mabadiliko ya kiutawala wa shule na huleta changamoto.

Hasa mwaka Jana mfumo ulipoanza rasmi wengi walikuwa hawajui baadhi ya vitu hasa Hawa supervisor.
 
Back
Top Bottom