Skylar
JF-Expert Member
- Nov 10, 2021
- 2,206
- 5,198
Pole sanaWadau,
Nimekuja kugundua nilikosea kuoa baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 15 na kupata watoto wanne. Dah nilijichanganya nikaoa a Corporate lady ambaye alikuwa mwanasheria kule Arusha, alikuwa ana vihela flani na connections za watu wazito ndani ya bongo....duh acha kabisa!!!
Nilikuja kujuta sana manake kazi zoote na mambo yooote ya nyumbani yalikuwa yanafanywa na mabeki tatu kuanzia Kufua nguo zangu, maji ya kuoga, kupika nk alikuwa hana time kabisa na nyumba yake. Hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake kila kitu anabishana na kushindana.
Mtu wa vikao vya dinner karibu kila siku. Miaka ya mwanzoni nilikuwa namdunda sana sana baadaye nikapataga kesi, wakati mwingine ilibidi niingie hasara ya kumpeleka hospitali na kumhudumia manake alikuwa na watoto wadogo.
Nikaamua kuingia kwenye pombe na michepuko ili nimpuuzie. Nikawa nampuuzia kama vile hayupo na yeye akanikazia, akazidisha kiburi na jeuri nikaanza tena kumdunda nikapata tena kesi kubwa manake ilikuwa nimuulie mbali.
Sasa baadaye nikafikiria sana watoto wangu tukafikia hatua ya kuachana na kukubaliana jinsi ya kuwalea watoto. Sasa tumeweka nguvu zoote katika kuwalea watoto na hali imekuwa shwari kabisa kila mtu anaishi kivyake baada ya talaka.
Najua kuna wale watakaosema tuishi nao kwa akili. Nilijitahidi kufanya hivyo kwa miaka 15 lakini ikashindikana manake ningeishia jela baada ya kumtoa uhai na watoto wangeteseka.
Bora iwe hivi hivi wote tupo wazima wa afya.
ALAMSIKI, DUH USIOMBE KUKOSEA KUOA BORA UKOSEE KUZALIWA
KARIBU NI WADAU WENZANGU MLIOKOSEA KUOA.
Kuna namna ambavyo ulishindwa kusimamia mamlaka yako au nafasi yako kama mume ndani ya nyumba.
Ukiona mpaka mwanamke anafikia hatua ya kujiamulia kuishi anavyotaka ndani ya nyumba na ku deligate majukumu yake kwa beki 3 basi kuna shimo mahali ambalo hukuliziba tangu mwanzo wa ndoa yenu na sasa limekua sugu halizibiki
Umeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye suala zima la ku handle issue kwenye ndoa, huwezi kutatua changamoto au tofauti kwa kumpiga mke
Mwisho wa yote you knew her better na ulikua inajua anapenda nini, priorities zake ni zipi na carreer goals zake ni zipi, badala ya kumpiga mngekaa pamoja mkubaliane namna ambavyo anaweza kubalance her career onjectives pamoja na majukumu ya kifamilia bila kuathiri kimoja wapo