Mwenye haki kufungisha ndoa sahii huyu hapa msome umuone

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,389
672
NDUGU JAMAM NA MARAFIKI NIMEONA WATU WENGI WANAULIZA NANI ANAHAKI KUFUNGISHA NDOA NA NDOA IPI INAYO TAMBULIKA KISHERIA NA NANI ANAYR RUHUSIWA KUFANYA HAHYO???

NIMEONA NIWASAIDIE KUWA MWONGOZO MZIMA WA MAMBO NDOA INGAWA NI MREFU SANA LAKINI WAWEZA KUUKOPI NA KUU SAVE KWA COMP YAKO UKAUSOMA KWA MDA WAKO



SEHEMU YA KWANZA

MAANA YA NDOA
Kufuatana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, Ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao.

AINA ZA NDOA;
Kuna aina mbili za ndoa ;
i) ndoa ya mke mmoja, hii ni ndoa ambapo mwanaume ana mke mmoja tu.
ii] ndoa ya wake wengi, hii ni ndoa ambayo mwanaume ana wake zaidi ya mmoja.
Ndoa itokanayo na dhana ya ndoa; hii ni ndoa ambayo mwanamke na mwanaume wamekaa pamoja ndani ya nyumba kama mke na mme kwa muda wa miaka miwili na kuendelea na wote wakapata hadhi ya kuwa wanandoa.
Je ni vipengele gani vya kuzingatia ili wanaotaka kufunga ndoa wakubaliwe kisheria kufunga ndoa yao?

(a) NI LAZIMA MUUNGANO UWE WA HIARI:
Mume na mke wawe wameamua kuishi pamoja kwa ridhaa yao wenyewe. Hii inamaanisha kusiwe na kulazimishwa, kuhadaiwa kwa aina yoyote kwani muungano kama huo utakuwa batili kisheria. Ni kosa la jinai kushiriki katika shughuli ya ndoa ambayo mmoja wapo au wote wamelazimishwa kufunga ndoa.

(b) MUUNGANO UWE NI KATI YA MWANAMKE NA MWANAMUME:
Muungano wa watu wa jinsia moja hata kama ni wa hiari muungano huo hautambuliki kisheria. Pia mtu huhesabika mwanamke au mwanaume kutokana na sehemu za siri alizozaliwa nazo na siyo alizozipata baadaye. Jamii inachukulia kuwa ndoa ni njia pekee ya kujipanua. Upanukaji huku ni kwa kuzaa watoto. Kwa hali hiyo ili kupata watoto ni lazima ndoa iwe kati ya mwanaume na mwanamke.

(c) MUUNGANO HUO UWE UNAKUSUDIWA KUWA WA KUDUMU:
Pamoja na kuwa mwanamke na mwanaume wameamua kuishi pamoja kwa hiari yao lakini siyo
kwa kudumu muungano huo hautambuliki kisheria kama ndoa. Muungano ni lazima uwe wa kudumu maisha yote au kama mmoja wao amefariki au kama ndoa imekumbwa na matatizo na mahakama ikaona ni bora kutoa talaka kwa yeyote aliyefika kulalamika.

(d) WAFUNGA NDOA WASIWE MAHARIMU:
Maharimu ni watu walio na mahusiano ya karibu ya damu au kindugu.
Wawili wanaoamua kufunga ndoa wasiwe na uhusiano wa karibu kindugu. Inakatazwa katika kifungu cha 14 cha Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 mtu kuoa au kuolewa na mzazi wake, mtoto au mjukuu wake, kama ni dada yake, mama au shangazi au baba wa mjomba wake, baba au mama wa kambo na mwanaye aliyemfanya kuwa mtoto wake (adopted child).

(e) WAFUNGA NDOA WAWE WAMETIMIZA UMRI UNAOKUBALIKA KISHERIA:
Mwanamke na mwanaume wawe wametimiza miaka 18 ili kufunga ndoa. Hata hivyo mwanamke anaweza kuolewa akiwa na umri wa chini ya miaka
18 lakini sio chini ya miaka 15 kama atapata idhini ambayo hutolewa na baba na kama hayupo ni mama au kama wote wamefariki idhini itatolewa na mlezi wa binti huyo. Kama wote wamefariki basi hatahitaji idhini. Kuna wakati katika mazingira fulani mahakama inaweza kutoa idhini kwa binti kuolewa akiwa na miaka 14 lakini si chini ya hapa ikiwa ataonekana kwa mfano ana mimba. Pia mwanaume anaweza kuruhusiwa na mahakama kuoa akiwa na umri wa miaka chini ya 18 lakini lakini si chini ya 16 kama ataonyesha kuelewa jukumu lake kama mtu mzima. Lakini hii ni pale ambapo kuna tatizo kama la kumpa msichana mimba ndipo mahakama inaweza ikatoa idhini. Katika ombi la kuoa la SHABIRI A. M. VIRJI (1971) HCD NO. 407 la Mahakama Kuu ya Tanzania, mwombaji alikuwa na miaka 16 lakini alimpa mimba binti wa miaka 18. Mahakama katika kuchunguza ombi la mvulana la kuoa ilitoa kibali kwa sababu wote wawili walipendana sana na wazazi wao hawakuwa na kipingamizi cha wao kuoana.

(f) KUSIWE NA NDOA INAYOENDELEA:
Kama mwanamke ana ndoa inayoendelea na inatambulika kisheria haruhusiwi kufunga ndoa nyingine (Polyandry). Kadhalika kama mwanaume ana ndoa ya mke mmoja au kama ni mwislamu ana wake wanne tayari hataruhusiwa kufunga tena ndoa.

(g) KUSIWE NA KIPNGAMIZI:
Kama ndoa imezuiwa na Mahakama au halmashauri ya usuluhishi kutokana na uwezo zilizopewa na ndoa ikaendelea kufungwa kabla ya wenye kupeleka kipingamizi hawajasikilizwa au Mahakama imeshaamua ndoa hiyo isifungwe basi ndoa hiyo itakuwa ni batili.
(h) MFUNGISHAJI NDOA KUTOKUWA NA MAMLAKA:
Kama wanaofunga ndoa wanajua wazi kuwa anayewafungisha ndoa hana mamlaka hayo na kwa makusudu wakakubali awafungishe ndoa basi ndoa hiyo itakuwa ni batili. Mfungishaji ndoa ili kuwa na mamlaka anapaswa kusajiliwa na Msajili Mkuu wa Ndoa na kupewa leseni ya kufungisha ndoa.

(i) KUTOKUWEPO KWA WAFUNGA NDOA:
Kama ndoa imefungwa bila ya wafunga ndoa wote kuwepo basi ndoa hiyo haitambukuliki kisheria. Hata hivyo sheria inaruhusu ndoa kufungwa ikiwa mmoja wa wafunga ndoa hayupo, Kama mfunga ndoa ambaye hayupo amewakilishwa na mtu ambaye alikuwepo wakati mfunga ndoa hayupo, alipotoa ridhaa yake ya kuoa au kuolewa.

(j) MASHAHIDI WA NDOA:
Ili ndoa itambulike kisheria ni lazima ishuhudiwe na mashahidi wasiopungua wawili ambao wanaruhusiwa kisheria yaani umri wao usipungue miaka 18 na wafahamu kinachosemwa na kutendeka wakati wa kufunga ndoa.

(k) KUWA KATIKA EDA:
Eda ni kipindi cha kukaa ndani kinachotolewa kwa mwanamke wa kiislamu aliyeachika katika ndoa au aliyefiwa na mumewe, ili taratibu fulani za kidini zifanyike.
Kama mwanamke ambaye ndoa ilifungwa Kiislamu anaolewa wakati wa kipindi cha Eda hakijaisha basi
ndoa hiyo ni batili. Lakini mfaruku au mtalikiwa awe anafuata dini ya Kiislamu. Kama atabadili dini baada ya kufiwa au kupewa talaka masharti ya Eda hayatambana.

SEHEMU YA PILI
AINA ZA UFUNGAJI WA NDOA NA TARATIBU ZA KUFUATA:
TAARIFA YA NIA YA KUOANA:
Kwanza kama mwanamke na mwanaume wanataka kufunga ndoa ni wajibu taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe kwa mfungishaji ndoa siku 21 kabla ya siku ya kufunga ndoa. Taarifa hiyo ionyeshe mambo yafuatayo:-
(i) Majina kamili na umri wa hao wanaotaka kuoana.
(ii) Uthibitisho kwamba hakuna kipingamizi dhidi ya hiyo ndoa wanayotarajia kufunga.
(iii) Majina kamili ya wazazi wao na sehemu
wanakoishi.
(iv) Hadhi ya wafunga ndoa. Yaani kama ni
mwanamke ifahamike kama hajaolewa,
ametalakiwa au ni mjane na mwanaume pia anapaswa kama hajaoa, au ana mke
/ wake wengine (Hii ni kwa ndoa za kiserikali na Kiislamuu) au kama ametaliki.
(v) Kama muolewaji ana umri chini ya miaka 18, jina la mtu aliyetoa idhini ya yeye kuolewa kama yupo ionyeshwe.
(vi) Kama ni ndoa ya Kiserikali au Kiislamuu
hapana budi kueleza kama ndoa ni ya wake wengi au inatazamiwa kuwa ya wake wengi, majina ya wake waliopo yatajwe. Pia katika fungu hili kama mtu anataka ndoa iwe ya mke mmoja anapaswa kueleza. Baada ya taarifa yenye maelezo haya kufikishwa kwa mfungishaji ndoa yeye anawajibika kutangaza hii nia ya kufunga ndoa. Sababu ya kufanya hivyo ni ili kama kuna mwenye kipinganizi na ndoa hiyo atoe taarifa. Matangazo haya hutolewa kama ndoa inatarajiwa kufungwa kidini, sehemu za ibada. Kama ni ndoa ya Kiserikali tangazo litabandikwa nje ya ofisi ya msajili wa Ndoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya. Vipingamizi vya ndoa viko vya aina mbili, cha kwanza ni kile cha kisheria yaani kama ndoa itakayofungwa itakuwa batili. Kipingamizi cha pili ni kama muoaji ana mke au wake wengine tayari, hivyo mke au wake wanaweza kutoa kipingamizi kama uwezo
10
wa muoaji kifedha ni mdogo kiasi kwamba kuongeza mke mwingine kutazidisha taabu.
Mfungishaji ndoa anapopokea taarifa ya kupinga ndoa isifungwe, ataipeleka taarifa hiyo kwenye Baraza la Usuluhishi la Ndoa. Huko aliyewekewa kipingamizi na aliyeweka wataitwa na kila mmoja atajieleza. Baada ya kusikiliza pande zote Baraza lina uwezo wa kuamua ndoa hiyo ifungwe au isifungwe na mfungishaji ndoa atafuata uamuzi wa baraza. Kama mtu atatoa kipingamizi cha uongo na ikithibitika hivyo, adhabu yake anaweza kufungwa kifungo kisichozidi miaka mitatu. Baada ya kipengele hiki kutimizwa ndoa inaweza kufungwa.
AINA ZA NDOA:
Kuna aina mbili za ndoa:
(a) NDOA YA MKE MMOJA:
Huu ni muungano unaoruhusu mwanaume kuoa si zaidi ya mke mmoja. Mfano: Ndoa ya Kikristo.
(b) NDOA ZA ZAIDI YA MKE MMOJA:
Huu ni muungano unaoruhusu mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja. Mfano, ndoa za Kiislamu na ndoa za kimila.
11
Sheria ya ndoa inatambua aina 3 za ufungaji wa ndoa yaani kiserikali, kidini na kimila.
Ndoa hizo zaweza kufungwa kwa kufuata taratibu za kidini au za kiserikali. Utaratibu huo utafuata au kuzingatia kama wanandoa ni waumini wa dhehebu Fulani au la.
(a) NDOA YA KIDINI:
Ndoa hii hufungwa kwa mujibu wa taratibu ya dini husika. Ni lazima masharti yote yatimizwe kisheria na taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe na ndoa ifungiwe mahali pa wazi panapokubalika kisheria na mfungishaji awe na mamlaka hayo kisheria.
(b) NDOA YA KISERIKALI:
Ndoa hii hufungwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye Msajili wa Ndoa. Ndoa itafungiwa katika ofisi ya Msajili au mahali pengine popote palipotajwa katika leseni yake ya kufungisha ndoa.
(c ) NDOA YA KIMILA:
Ndoa inaweza kufungwa kimila iwapo mmoja wa wafunga ndoa au wote wawili wanafuata sheria za mila za kabila fulani. Mwandishi wa ndoa za kimila
12
ni Katibu Tarafa. Ndoa ya kimila hufungishwa na mtu anayetambulika kimila kuwa ana uwezo huo. Ni muhimu sana Katibu Tarafa kuhudhuria kwenye ufungishaji huo wa ndoa kwani ndiye atakayehusika na kuleta vyeti vya ndoa kutoka kwa msajili.
13

SEHEMU YA TATU
UFUNGAJI NDOA NJE YA NCHI:
Kifungu cha 8 cha sheria kinampa mamlaka Waziri wa Sheria kuteua baadhi ya maofisa ubalozi kuwa wasajili wa ndoa. Ni lazima msajili aridhike kuwa masharti yote yametimizwa ndipo afungishe ndoa. Kuna masharti ya nyongeza kama angalau mmoja wa wafunga ndoa awe ni Mtanzania. Pia kama mmoja wa wafunga ndoa si mtanzania ni lazima Msajili aridhike kuwa ndoa inayokusudiwa kufungwa itatambulika kisheria katika nchi ambayo huyo mmoja wa wafunga ndoa ni mkazi. Utaratibu unaotumika kufungisha ndoa hizi ni sawa na ule unaotumika katika kufungisha ndoa za kiserikali.

DHANA YA KUCHUKULIA NDOA:
Kuna dhana inayokanushika (rebuttable
presumption) kuwa mwanaume na mwanamke wakiishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi huchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa. Dhana hii imeelezwa katika kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa.
14
Ili dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe.
(i) Lazima ithibitike kwamba mwanamke na
mwanamume wameishi pamoja kwa muda wa miaka 2 au zaidi kwa mfululizo.
(ii) Lazima pia ithibitike kuwa umma
unaowazunguka unawachukulia na
kuwapa heshima kama mke na mume.
(iii) Lazima ithibitishwe kuwa watu hao
walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume
wakati walipoanza kuishi pamoja kama umri ulikubalika kisheria.
(iv) Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao
wawili au wote hakuna aliye na ndoa
inayoendelea.

NDOA BATILIFU NA SABABU ZINAZOWEZA KUIFANYA NDOA KUWA BATILIFU:
Ndoa batilifu ni ndoa ambayo itachukuliwa kisheria kuwa ni ndoa halali hadi hapo amri ya kuivunja itakapotolewa. Ndoa batilifu ni halali kama ndoa nyingine isipokuwa ina kasoro fulani. Wanandoa katika ndoa hii wana haki na wajibu sawa kama ilivyo katika ndoa nyingine zisizo na kasoro. Kadhalika watoto waliozaliwa katika ndoa ya namna hii ni halali na wana haki zote kisheria.
15
NI VITU GANI VINAFANYA NDOA KUWA BATILIFU:

1. MARADHI YA ZINAA:
Kama wakati wa kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa alikuwa na maradhi ya zinaa na yule asiye na Ugonjwa kama wakati wa kufunga ndoa alikuwa hajui lolote anaweza kulalamika mahakamani na ndoa ikavunjwa.

2. KUKATAA KWA MAKUSUDI KUITIMILIZA NDOA:
Kama baada ya kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa atakataa kuitimiliza ndoa anayekataliwa ana haki ya kuiomba mahakama kuvunja ndoa hiyo. Maingiliano yanayotambulika kisheria ni yale yanayofanyika siku ya ndoa na kuendelea na siyo kabla ya ndoa. Kukataa kuitimiliza ndoa kunakuwa sababu ya kubatilisha ndoa ikiwa mwenye kukataa hana sababu yoyote ya msingi na mwenye kukataliwa ametumia kila mbinu kumshawishi aliyekataa lakini ikashindikana kufanya tendo la ndoa.

3. MIMBA YA MWANAUME MWINGINE:
Kama wakati wa kufunga ndoa mke atathibitika ana mimba aliyopata kwa mwanamume mwingine, mume
16
anaweza kuiomba mahakama ivunje ndoa hiyo. Kama itathibitika kuwa mume alijua hivyo hali wakati wa kufunga ndoa, lalamiko lake halitasikilizwa.

4. WAZIMU AU KIFAFA CHA VIPINDI:
Mmoja wa wafunga ndoa kama ana wazimu au kifafa cha kurudia rudia na mwenzake alikuwa hajui hilo hali wakati wa kufunga ndoa, atakuwa na haki ya kuiomba mahakama kuivunja ndoa hiyo. Ieleweke kuwa Ugonjwa ni lazima uwe unarudia rudia na siyo mtu awe aliugua na akapona.

5. KUSHINDWA KUITIMILIZA NDOA:
Kama mmoja wa wafunga ndoa atashindwa kuitimiliza ndoa basi ndoa hiyo inaweza kubatilishwa. Kwa mwanaume kama anashindwa kuitimiliza ndoa kwa sababu ya kukosa nguvu za kiume basi ana haki ya kuiomba mahakama kuibatilisha ndoa. Ili kukosa nguvu za kiume kuwe sababu ya kubatilisha ndoa ni lazima ithibitike kuwa hali hiyo ilitokea kabla au wakati wa kufunga ndoa na siyo baada ya kufunga ndoa wakati kitendo cha kuitimiliza ndoa kilishafanyika. Ili ndoa iweze kubatilika ni lazima kukosa nguvu huko kuthibitishwe na daktari kuwa hakuponi au kunapona lakini mwanaume hataki matibabu.

17Mwanamke
anaweza kuwa na maumbile ambayo yanaweza kufanya ndoa ishindwe kutimilizika. Ikithibitika hali hii inathibika lakini mwanamke hataki tiba mwanamume anaweza kuomba mahakamani ndoa kubatilishwa. Ili mahakama iweze kusikiliza shauri la kuomba kubatilisha ndoa ni lazima shauri hilo lipelekwe haraka. Kama shauri litakwenda mahakamani baada ya mwaka mmoja tangu tarehe ya ndoa Mahakama haitalipokea. Pia ni lazima ithibitike kuwa mlalamikaji alikuwa hajui kasoro hiyo wakati wa kufunga ndoa na baada ya kuigundua hiyo kasoro hajawahi kuingiliana na mwenzie mwenye kasoro hiyo.
Ndoa batilifu huvunjwa na mahakama pekee baada ya kupokea malalamiko toka kwa mmoja wa wanandoa. Kama hakutakuwa na malalamiko yatakayopelekwa mahakamani na anayedhurika na kasoro hizo, ndoa hiyo itadumu ama labda mmoja afariki au kama kuna talaka itatolewa na mahakama.
Watu waliooana wana uhuru wa kugeuza ndoa yao kuwa ya mke mmoja au ya wake wengi pale wanapofuata taratibu zinazokubalika kisheria. Kabla ya kufanya uamuzi wa kugeuza ndoa ni budi wanandoa wakubaliane kuhusu uamuzi huo.

18Kitendo
cha kugeuza ndoa hufanywa mbele ya Hakimu wa Wilaya au Jaji ambapo wanandoa watatoa tamko la maandishi lenye sahihi zao na Hakimu au Jaji aliyeshuhudia naye hutia sahihi yake.
Katika kugeuza ndoa, ndoa ya kiserikali ya kienyeji au ya Kiislamu inaweza kugeuzwa kuwa ya mke mmoja kama kabla ya kugeuza hizi zinaweza kugeuzwa kuwa ya wake wengi.
Ikumbukwe kuwa kubadilisha dini pekee hakubadilishi hadhi ya ndoa.
19Vilevile ndoa ya kikristo haiweza kugeuzwa kuwa ya wake wengi wala ndoa ya wake wengi inayodumu kuwa ya mke mmoja.

SEHEMU YA NNE
TALAKA NA TARATIBU ZA KE
Talaka ni ruhusa au amri ya mahakama ya kisheria ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha mwenzake.
Chombo chenye mamlaka ya kutoa talaka ni mahakama tu. Mahakama hiyo itatoa talaka kwa ndoa ambayo imedumu kwa muda wa miaka miwili au zaidi. Mahakama inaweza kutoa talaka kwa ndoa ambayo haijafikisha muda huo endapo mlalalmikaji atatoa sababu za msingi mahakamani.

KUTENGANA
Kutengana si talaka. Kutengana maana yake ni hali ambayo mke na mume hukaa mbalimbali. Kukaa mbalimbali au kutengana kwaweza kuwa kwa mapatano kati ya wanandoa hao au kutengana kwaweza kuwa kwa amri ya mahakama. Mahakama itatoa amri hiyo endapo mmoja wao atapeleka maombi mahakamani. Faida ya kutengana wote au mmoja wao waweza au aweza kutambua makosa na baadaye kukata shauri kurudiana au kuishi tena.
Kutengana kwa mapatano, ni kutengana kwa hiari yao wenyewe bila shuruti.
20Mapatano hayo yaweza
kuwa ya maandishi au ya mdomo. Mambo kadha yaweza kuzingatiwa wakati wa makubaliano kama; heshima kwa kila mmoja, matumizi / matunzo,watoto kama wapo watakaa na nani, mali ya pamoja je itatunzwa namna gani na kutobughudhiana.
Kutengana kwa amri ya mahakama, hii ni hali ya mume na mke kutengana kwa amri ya mahakama na mahakama imeridhika kuwa ndoa imevunjika. Ushahidi wa kuwa ndoa imevunjika ni ushahidi ambao unaweza kutolewa mbele ya mahakama kunapokuwepo na maombi au shauri la talaka.

SABABU YA KUTOA TALAKA MAHAKAMANI
Kabla ya kupeleka shauri au maombi mahakamani ya talaka, mwanandoa husika hana budi kufuata au kuzingatia hatua zifuatazo;
a) kufungua au kupeleka malalamiko kwenye
Baraza la Usuluhishi la Ndoa kwa mfano
Bakwata, kanisani,Utawi wa Jamii au
Baraza la Kata.
b) Baraza litasikiliza, na endapo litashindwa
mapatano au muafaka kati ya wanandoa hao,
21
basi baraza litatoa cheti ambacho kitaeleza kuwa limeshindwa kusuluhisha mgogoro wa ndoa na kuomba
mahakama kuendelea kutoa talaka.
c) Baada ya mwanadoa mmoja kupata cheti hicho basi atatakiwa atayarishe madai ya talaka akionyesha kuwa kulikuwa na ;-
ndoa halali,
kuna mgogoro kati yao,
watoto,
mali walizochuma wakati wa ndoa yao,.
Muombaji huyo ataiomba mahakama hiyo itoe amri ya
talaka,
mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa nguvu za pamoja,mamlaka ya kukaa na watoto na matunzo yao,
gharama za madai / shauri.
Ili mahakama itoe talaka sababu kadha huangaliwa na mahakama. Sababu hizo ni mambo ambayo yatakayofanya ndoa ionekane kuwa imevunjika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena, mambo hayo ni kama ifuatavyo;
•
•
•
•
•
•
•
22
a) Ugoni; hii ni zinaa ambayo hufanywa na mwanaume na mwanamke ambao hawajaoana.
Hii hutokea ambapo mwanaume ana mke wake au mwanamke ana mume wake, hivyo mmoja wapo anamwacha mke/mume na kufanya zinaa na mtu mwingine.
b) Ukatili; ukatili ni kuumiza nafsi nyingine, kuharibu mwili au kuwa na hofu ya kuumizwa.
c) Kulawiti; kulawiti ni kumwingilia mtu kinyume na maumbile,
d) Kichaa; ni kutokuwa na akili timamu, na hali hii lazima iwe imethibitishwa na madaktari bingwa wa akili.
e) Kuzembea wajibu kwa makusudi; haya ni majukumu ya mume, majukumu hayo ni kama haya; kumtunza mke kwa kumpa chakula, malazi na mavazi.
f) Uasi Ni hali ya mke au mume kuhama nyumba ya ndoa na kwenda kuishi mahala pengine bila sababu yoyote ya msingi,
g) Kutengana; kukaa mbalimbali kwa mume na mke kwa muda wa miaka isiyo pungua mitatu, kutengana kwao ni sababu tosha ya talaka.
23
h) Dhana ya kifo; hii ni hali ambayo mmoja wa wana ndoa amekufa, na hii hutokea iwapo mojawapo hataonekana / ametoroka kwa muda mrefu, kama miaka 5. Hapo mahakama hutoa tangazo kuwa fulani amekufa.
i) Kifungo; hii ni hali ambayo mume au mke ametenda kosa la jinai na ametiwa hatiani na mahakama imemfunga miaka 5 au maisha basi mahakama inaweza kutoa talaka kwa mwombaji.
j) Tofauti za imani za kidini, endapo mwanandoa mmoja atabadili dini basi ni sababu tosha ya kuomba mahakama ivunje ndoa na kutoa talaka.
HAKI NA WAJIBU KATIKA NDOA
Baada ya kufunga ndoa na ikaonekana haina kasoro yoyote, mke ana haki mbalimbali kisheria anazostahili kuzipata kisheria. Haki hizi ni kama;
- Matunzo; mke au wake wana haki ya kutunzwa na mume wao kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama chakula, malazi, mavazi, matibabu, n.k kulingana na uwezo alionao mume.
- Kumiliki mali; mke ana haki ya kumiliki mali aliyoipata kabla na baada ya ndoa kama aliipata kwa
24
fedha yake mwenyewe. Mke ana haki ya kuingia mikataba, kushitaki na kushitakiwa. Makubaliano yaweza kufanywa na wanandoa hiyo jinsi ya kumiliki mali iliyopatikana kabla ya ndoa yao jinsi gani waimiliki. Kwa mali iliyopatikana wakati wa ndoa, mali hiyo ni mali ya wanandoa wote, kwa sababu imepatikana kwa mchango wa nguvu za pamoja. Hii haijalishi kuwa mmoja wa wanandoa (mke) hachangii pesa tasilimu au anakaa nyumbani na kufanya shughuli za nyumbani tu. Kufanya shughuli za nyumbani ni mchango mkubwa na ameokoa fedha nyingi. Umiliki wa mali kwa wanandoa haujalishi kuwa mmoja wapo amemiliki mali hiyo kwa jina lake au la. Sheria ya Ardhi inatamka wazi kuwa kama mwanandoa mmoja anamiliki mali kwa jina lake, na mwanandoa mwingine akachangia nguvu zake katika kuendeleza, kuboresha au kuzalisha mali hiyo basi anapata haki ya kumiliki mali hiyo.
- Haki ya kukopa kwa dhamana ya mume; jukumu la kutunza mke na watoto ni jukumu la mume au baba. Kwa msingi huo, endapo baba amesafiri, au ametoroka na baadaye matatizo yakajitokeza yanayohitaji fedha, basi mke ana haki ya kukopa fedha kwa jina la mume au kuweka rehani mali ya
25
mumewe.
- Haki ya kuishi katika nyumba ya Ndoa;
Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mke na mume wanaishi wakati wa ndoa. Hata kama wanandoa wana nyumba nyingi, basi wanayoishi au kutumia kama makazi ndiyo nyumba ya wanandoa. Nyumba hii haiwezi kuuzwa, kuweka rehani au kuchukuliwa na mtu mwingine kama zawadi bila ya makubaliano ya wanandoa wote.(bila ridhaa ya wanandoa). Mwanandoa ana haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka amri ya mahakama ya kuvunja ndoa, au kutengana itakapotolewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom