Nini ambacho uliwahi fanya/kutofanya katika mapenzi/mahusiano, na huwa unatamani muda urudi nyuma ili ukirekebishe?

Mogadishuu

Member
Jun 22, 2019
32
63
Wakuu hii story yangu ambayo niliandika kama kisa ambacho siwezi kukisahau na huwa kinanitesa mpaka leo kwenye maisha yangu, na nilikiandika kama mchango katika uzi wa ndugu yetu

laskaboza , lakini kwa mapendekezo ya wadau ni bora kuwepo na uzi wa visa vya nyuma wenye mlengo wa mapenzi au mahusiano, na mimi nimeitikia wito huo, karibuni tupeane moyo ama ushauri juu ya matukio haya ambayo yalipita lakini tunajutia kuyafanya au kutoyafanya katika maisha yetu huko nyuma na huwa tukiyakumbuka yanatutesa/kutugharimu mpaka leo. Kilichofanya niandike ni maneno haya niliyoyaona katika uzi ule ya ndugu The Garang ,''

Nlichojifunza ukimuelewa mtu usikawie kusema, mwambie akatae mwenyewe na kujifanya unaogopa tongoza kuhofia utapoteza urafiki wenu nimejua ni ujinga.'' Ni ukweli kabisa, yaani ni swala la kuzingatia sana mimi mpaka leo nina kazi nzuri namshukuru Mungu lakini sina furaha upande wa familia japo nilioa.

ANGALIZO
Najua wapo watakaoniona mjinga au zuzu lakini kiukweli unaweza kuona jambo ni dogo kwako lakini kwa mwenzako ni kubwa na linamsumbua

Ipo hivi, kulikuwa na binti nampenda sana, tulikuwa tunaishi nae mtaa mmoja,(kutokana na mambo ya shule mimi sikuishi sana nyumbani) ila nikirudi tulikuwa tunaonana japo hatukuwahi kuongea. Basi bwana ile kutokujiamini sababu kuna kitu fulani nilikuwa napitia(ugonjwa) changanya na ugumu wa maisha home basi mzee nikawa sina comfidence ya kumface na kumwambia kama nampenda kutokana na jinsi alivyo japo nilimzidi kiumri lakini nilijiona kabisa sitaweza kumhudumia au angenikataa kutokana nilivyokuwa kipindi hicho(ugonjwa wa ngozi), miaka ikaenda, nikawa vizuri tu na michongo ikatiki hatimaye ukafika muda wa kutaka kuoa.

Nishakua kwenye mahusiano kadhaa lakini ulipofika muda wa kuoa nikakumbuka kuna mwanamke huwa nampenda na kwa sababu nipo vizuri basi sasa ndio muda muafaka wa kuongea nae. (Kitu ninachojuta sikutaka kumtuma mtu nilitaka kwenda kuongea nae face to mimi mwenyewe na bahati mbaya sikuwa na connection kwao). Basi kila nikirudi kitaa kutaka tuongee simpati, mara tunapishana muda nao ukaenda sana, mwisho nikakata tamaa, nikajisemea kwanza mtu mwenyewe kwa jinsi alivyo (mzuri na anatakwa na wengi, pengine malaya tu na mpenda pesa) na sijawahi kuongea nae pengine ashapata bwana na kuolewa au ana mahusiano yake.

Basi me nikaendelea na maisha yangu, muda ukafika nikaoa(japo sikumpenda sana mke wangu kama B, nilifanya kama formality tu) maisha yakaendelea, japo sijawahi kuacha kumfuatilia B, iwe nipo mtaani au sipo. Basi siku moja nikiwa kikazi huko mikoa ya kaskazini, ghafla namuona dada ambaye nahisi namjua, kumsogelea hivi nikaita jina B, kageuka nikajitambulisha pale mpaka akanikumbuka tukabadilishana namba kisha baadaye tukawasiliana na kukubaliana siku ya pili tukutane kwa ajili ya kupiga story zaidi.

Siku imefika mzee, nikamtoa out B wangu(nilikuwa najisemea hivyo toka kitaa sababu niliamini yeye ni wangu), katika kupiga story nikamchana live mimi nilikuwa nakukubali toka kitambo B ila niliogopa kukwambia kutokana na hivi na hivi, .....alicheka sana akajibu uoga wako tu mimi sipo kama ulivyodhani (ni kweli nilikuja kujua baadaye) nikapiga mistari pale mtoto mzuri kaelewa bila shida kabisa japo hakusema lakini indirect nikaona tayari, sikuona ajabu sababu ya ile trust ya kujuana toka kitaa.

Kwa huo mji alikuwa anakaa kwa ndugu yake basi ikawa nikimhitaji tunakutana na penzi likashamiri, wakati huo mambo ya kama nimeoa sijamwambia ila nilimwambia kuwa kuna mwanamke nilizaa nae tu hivyo tunalea mtoto, na yeye pia aliniambia kwamba alikuwa na mtoto tayari(moja moja hapo japo roho iliumia hapa kusikia kazalishwa).Kazi ikaisha nikarudi nilikotoka

Baada ya muda kule kaskazini kulitokea nafasi na kwa sababu mimi nilikuwa naenda mara kwa mara boss akapendekeza mimi ndio nihamie kule(Nilifurahi sana kwenda kuungana na B wangu) , basi ikawa kama nimemuoa B wangu, pika na kupakua, kahama kwa ndugu yake kahamia kwangu tunaishi. Maisha yameendelea, mtoto wake alimuacha kule hometown tulipokua tunakaa kwa wazee wake. Sababu nampenda niliishi na B wangu vizuri sana mpaka akawa ananilaumu kwa nini sikumwambia/sikumtongoza mapema kipindi kile maana kapitia mengi sana.Nikamwambia B wangu, mipango ya Mungu huwezi jua maana yeye ndio mpangaji wa kila kitu.
SIRI YA KUOA INAFICHUKA

Njia ya muongo fupi, siku ya siku ikawadia na katika makosa nilyofanya ni kumruhusu B kuwa anapekua simu yangu nikiwepo (nilitaka asiwe na wasiwasi na mimi japo nilipanga kuja kumuelezea ukweli baadaye kidogo). Kuna namna nillisave namba ya wife ili asishtuke lakini kumbe alishaanza kuchunguza kuhusu ile namba maana aliona mawasiliano ni mara kwa mara, haipiti siku lazima tuongee. Basi kumbe ile simu yangu huwa nikifuta meseji za kawaida zinakaa recycle bin kwanza mpaka uki clear ndio zinaondoka.

Kumbe kupekua pekua kwake kaenda mpaka recycle bin na kaona kila kitu. Nakumbuka siku hiyo nimetoka kuoga nakuta mtu analia kwa uchungu namuuliza nini, anasema kwa nini hukuniambia kama umeoa? Kwa nini mimi maisha yangu ya mapenzi ni mikosi tu, kwa nini.... alilia kwa uchungu sana B wangu mpaka na mimi nikalia, tulilia sana siku hiyo kwa uchungu.

Tulibembelezana, maumivu yakapungua kidogo lakini tukaapa kutoachana kwa namna yoyote ile. To be honest sikuwa nampenda mke wangu kama ninavyompenda B (Mungu anajua na anisamehe). Na hilo swala la kutompenda hata yeye huwa ananiambia toka mwanzo. Imebidi niishi na wanawake wawili bila kupenda japo sikuwahi kuwaza au kupanga hivyo. Mke mmoja na mchepuko mmoja wa kudumu, B wangu. Nilijitahidi kuachana na B lakini ilishindikana, na yeye ndio huwa anasema tuachane tu kila mtu aendelee na maisha yake lakini nimeshindwa (hajaniroga ni mapenzi yangu tu kwake) kuona anaishi na mwanaume mwingine.

Kinachonisumbua sijui wanaooa wanawake wengi wanaweza vipi, mimi nimeshindwa kubalance upendo. Nimeelemea kwa B zaidi kuliko mke wangu(shame on me). Mke wangu kanizalia watoto wawili wazuri lakini nawapenda wanangu sio yeye, roho huwa inanisuta sana, yaani Binti wa watu anajitahidi kutimiza majukumu kama mke lakini wapi. Mahitaji namtimizia pamoja na watoto hakuna malalamiko, malalamiko yapo kwenye upendo tu. Mbaya zaidi ilibidi nimueleze tu kwamba naishi na mwanamke mwingine huku nilipo maana sikuhamia na familia, alilia sana na huwa anaumia sana.

Sistahili kuwa na huyu dada kwa ninayomfanyia kiukweli, angekuwa mwingine angeshaniacha lakini yupo na mimi tu, saa zingine mpaka huwa nahisi atakuja kuniua maana uvumilivu huu sio wa kawaida. Huwa nawaza labda tuachane halafu nimuachie kila kitu na watoto mimi nianze maisha upya ili asisononeke sana?

Nimejilazimsha kumpenda nimeshindwa mimi ninampenda B kuliko yeye (Mungu anajua)
B, yeye huwa simlaumu maana alishanipa option kwamba tuachane lakini kwa ajili ya amani yangu ya moyo nilimwambia siwezi kuishi bila yeye, na ukweli kabisa maana alivyonipa background yake tu maumivu niliyoyapata mpaka nilitafuta watu wa kunishauri hao wakubwa wa mitandaoni, na nimeshindwa kuachana nae.

Hilo swala tu la kusikia yupo na mwanaume mwingine au aliwahi kuwa na mwanaume mwingine huwa linaniumiza sana yaani kumuacha aende naumia(sipo tayari kumuona na mwanaume mwingine) na akibaki pia sometimes huwa naumia(ananikumbusha mambo ya nyuma, jinsi nilivyoshinwa kujiamini na kumtongoza). Mbaya zaidi yeye pia huwa ananiambia anajihisi kupata dhambi kuishi na mume wa mtu, na anahisi anashindwa kushea mapenzi, huwa nambembeleza anatulia lakini huwa anajikaza tu najua.

Huwa nipo njia panda kwa kweli, nina kazi nzuri lakini likija swala la familia huwa napata shida, yaani kuna muda mpaka nashindwa kufanya kazi vizuri.

MAJUTO KUHUSU B WANGU

Nachoweza kusisitiza hapa, mwanamke ukimpenda saa zingine bora usimuulize background yake, hicho ndio kinachonifanya niumie mpaka nitaingia kaburini.
Basi katika kuulizana ulizana akanitajia mwanaume wake wa kwanza (namjua), na anasema hakumpenda sana ila ni ushawishi tu wa ndugu zake jamaa aliutumia na ndio maana hata hawakudumu nae, akaja jamaa mwingine alikuja kuwa msanii na ndiye alimzalisha mtoto. Mwingine ni boda boda (alitake advantage baada ya B kuzalishwa na msanii na hakuwa anamjali)..........

MAUMIVU YANGU
Kinachoniuma mpaka leo, B nilikuwa namchukulia labda ni malaya sababu ya uzuri wake na kutakwa na wengi lakini aliweza kujitunza (kutunza usichana wake) mpaka miaka hiyo mimi namuona mkubwa, means ningempata ningekuwa ndio mwanaume wake wa kwanza. Hapa maumivu ambayo huwa nayapata hayaelezeki, huwa natamani siku zirudi nyuma mpaka ule mwaka tu kisha nimtongoze (Na huo mwaka huwa sipendi kuusikia, yaani kama kuna tukio lilifanyika huo mwaka au kuna kitu cha kukumbuka huo mwaka huwa sitaki kukumbuka wala kusikia).

Yaani boda boda(inauma japo ni binadamu mwenzangu, mnisamehe) alinizidi ujasiri mimi wa kuongea na mwanamke ninayempenda mpaka akatembea nae(yaani mara nyingine nikionaga boda boda huwa wananikumbusha jamaa aliyetembea na B wangu, imagine kuna bodaboda wangapi)

Nashindwa kumruhusu B aendelee na maisha yake sababu nampenda lakini pia kubaki kwake mara nyingine ananikumbusha nyuma hivyo naumia pia.
Siwezi kabisa kusikiliza nyimbo za huyo msanii, hata iwe nzuri vipi sababu tu alizaa na B wangu, kuna memory huwa zinanijia mbaya sababu namjua kitambo.

Nimejikuta siwezi kabisa kurudi mtaani kwetu tena au hometown sababu nahisi kuna vitu nitavikumbuka vitaniumiza
Ubaya kila ninachopitia ni uzembe wangu mwenyewe, sina wa kumlaumu, nilishaongea na watu mbali mbali lakini nimeshindwa kupona maumivu ya B wangu, mara nyingine nahisi bora nisingemuona au kuishi nae mtaa mmoja.

JUTO KUU ni kwa nini sikumtongoza mapema B wangu, pengine ningeepusha mengi.

KARIBUNI
 
We jamaa hujachapa mbusus nyingi na hilo ndilo tatizo lako.

Hapo ilibidi uwe ushapitia mahusiano kama 20+, uwe ushakula madada poa kwa kiwango cha chini 100 tu maana ni wengi sana.

Ila bahati mbaya sana ushapenda mara moja tu, na umedate na wanawake wasiozidi 10 tu.

Tafuta expirience kijana la sivyo maumivu hayatakuacha salama.
 
Nakumbuka siku hiyo nimetoka kuoga nakuta mtu analia kwa uchungu namuuliza nini, anasema kwa nini hukuniambia kama umeoa? Kwa nini mimi maisha yangu ya mapenzi ni mikosi tu, kwa nini.... alilia kwa uchungu sana B wangu mpaka na mimi nikalia, tulilia sana siku hiyo kwa uchungu.

Ndugu Wasomaji...
Hii ni summary ya uzi wote...

Kijana wa kiume anayeweza fanya hayo mpeni jina wenyewe...
 
Katika kitu ambacho huwa sifanyi ni kumuuliza mwanamke mahusiano yake ya nyuma wala mimi kumwambia yangu ,hii imenisaidia kutomuumiza au yeye kuniumiza ,kama anasikia asikie tu kwa watu ila sio kumthibitishia kwa kinywa changu ,
Kumwambia mwanamke /mwanamme idadi ya ya ulokuwa nayo ,ni kuhalalisha maovu atayokutendea siku za usoni ,maana hakutokuwa na geni
 
Wakuu hii story yangu ambayo niliandika kama kisa ambacho siwezi kukisahau na huwa kinanitesa mpaka leo kwenye maisha yangu, na nilikiandika kama mchango katika uzi wa ndugu yetu
Kwahio unafikiri kipindi kile ambacho huyo B alikuwa kwenye kilele cha urembo na mitongozo angemkatalia Mr.Blue kisha akukubalie wewe kapuku mwenye ngozi ya kobe?

Amini kwamba huyo B angekutosa vibaya sana usingeamini jombaa. Mtoto wa kike akiwa mzuri ndani ya miaka 18-24 huwa hashikiki na anachagua chagua sana wanaume. Lazma uwe na uspesho flani ndio atakukubalia.Huyo anakupa moyo sahizi sababu tayari kashafanya overhaul😂 hana jipya.

Acha mkeo umuoe B ili huyo boda boda wake akiendelea kumkaza uendelee kufurahia show.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom