NGOMEKONGWE2021

JF-Expert Member
Dec 6, 2021
543
1,064
Wadau,

Nimekuja kugundua nilikosea kuoa baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 15 na kupata watoto wanne. Dah nilijichanganya nikaoa a Corporate lady ambaye alikuwa mwanasheria kule Arusha, alikuwa ana vihela flani na connections za watu wazito ndani ya bongo....duh acha kabisa!

Nilikuja kujuta sana manake kazi zoote na mambo yooote ya nyumbani yalikuwa yanafanywa na mabeki tatu kuanzia Kufua nguo zangu, maji ya kuoga, kupika nk alikuwa hana time kabisa na nyumba yake. Hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake kila kitu anabishana na kushindana.

Mtu wa vikao vya dinner karibu kila siku. Miaka ya mwanzoni nilikuwa namdunda sana sana baadaye nikapataga kesi, wakati mwingine ilibidi niingie hasara ya kumpeleka hospitali na kumhudumia manake alikuwa na watoto wadogo.

Nikaamua kuingia kwenye pombe na michepuko ili nimpuuzie. Nikawa nampuuzia kama vile hayupo na yeye akanikazia, akazidisha kiburi na jeuri nikaanza tena kumdunda nikapata tena kesi kubwa manake ilikuwa nimuulie mbali.

Sasa baadaye nikafikiria sana watoto wangu tukafikia hatua ya kuachana na kukubaliana jinsi ya kuwalea watoto. Sasa tumeweka nguvu zoote katika kuwalea watoto na hali imekuwa shwari kabisa kila mtu anaishi kivyake baada ya talaka.

Najua kuna wale watakaosema tuishi nao kwa akili. Nilijitahidi kufanya hivyo kwa miaka 15 lakini ikashindikana manake ningeishia jela baada ya kumtoa uhai na watoto wangeteseka.

Bora iwe hivi hivi wote tupo wazima wa afya.

ALAMSIKI, DUH USIOMBE KUKOSEA KUOA BORA UKOSEE KUZALIWA

KARIBU NI WADAU WENZANGU MLIOKOSEA KUOA.
 
Wadau,

Nimekuja kugundua nilikosea kuoa baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 15 na kupata watoto wanne. Dah nilijichanganya nikaoa a Corporate lady ambaye alikuwa mwanasheria kule Arusha, alikuwa ana vihela flani na connections za watu wazito ndani ya bongo....duh acha kabisa!!!

Nilikuja kujuta sana manake kazi zoote na mambo yooote ya nyumbani yalikuwa yanafanywa na mabeki tatu kuanzia Kufua nguo zangu, maji ya kuoga,

Mkuu hao watoto wa 4 nakushauri uwapime DNA.
 
Hukumpenda kweli toka moyoni ulimpendea hela na connection baada ya kuingia ndoani ukajua kuwa ndoa ni zaidi ya hela, ikiwemo bond and chemistry hapo ndio ukachaganyikiwa.

Pole na move on with life maana inferiority ilikuwa inakusumbua
 
Wanawake wasomi kama huyo huwa hawaolewi, wao ndio wanaoa.

Ila kama uliweza kuishi nae kwa miaka yote hiyo ningekushauri ungeishi nae tu hivyohivyo kama skrepa lako kwa maslahi mapana ya watoto.

Kwakuwa tayari Mahakama imeshabariki Talaka hapo hamna suluhisho lingine, Pole mkuu
 
Hukumpenda kweli toka moyoni ulimpendea hela na connection baada ya kuingia ndoani ukajua kuwa ndoa ni zaidi ya hela, ikiwemo bond and chemistry hapo ndio ukachaganyikiwa.

Pole na move on with life maana inferiority ilikuwa inakusumbua
Very funny...kwanza nilimsomesha mwenyewe, anikamtafutia kazi alikuwa akilipwa mshahara chini ya laki 1,...nikaendelea kumpa maisha ,akaota mapembe... hajanizidi kwa chochote financially
 
Wanawake wasomi kama huyo huwa hawaolewi, wao ndio wanaoa.

Ila kama uliweza kuishi nae kwa miaka yote hiyo na kupata nae watoto wanne, ningekushauri ungeishi nae tu hivyohivyo kama skrepa lako kwa maslahi mapana ya watoto.

Pole mkuu. Kwakuwa tayari Mahakama imeshabariki Talaka hapo hamna suluhisho lingine.
Nilimkuta akiwa hana ishu mkuu.....kuanzia shule mpaka kuanza kazi ...ila akaja kuota mapembe baadaye
 
Yaani unampiga mkeo kisa hajapika au hajafua! Hivi sijui kwanini mnafananisha mwanamke anayetafuta pesa na anayeshinda nyumbani, mkae mkijua hawa ni wanawake wa aina mbili tofauti yaani hawatakaa wawe sawa, kama ambavyo mwanaume tajiri na mwanaume masikini hawako sawa kwenye hii dunia!

Mwanamke anayekusaidia wewe kutafuta pesa usitegemee ataweza kutimiza majukumu yake kikamilifu kama anavyofanya mama wa nyumbani, ninyi wenyewe si ndiyo mmetaka haya mambo ya kusaidiana maisha, kwa kukimbia majukumu yenu! Basi kama vipi oeni wanawake wasiosoma muwahudumie tu!
 
Nilimkuta akiwa hana ishu mkuu.....kuanzia shule mpaka kuanza kazi ...ila akaja kuota mapembe baadaye
Aisee. Pole sana, Hali ya kuota mapembe huwa inatokea kwa wanawake wachepukaji na kupelekea kuanza dharau kwa waume zao na kupelekea kuangusha ndoa zao.

Msingefikia hatua ya Talaka nina hakika mke wako angekuja kujirudi na kubadilika baada ya kufikia umri fulani. Maana Watoto ndio wanaathirika sana mnapotengana
 
NGOMEKONGWE2021 - Tupo wengi, kiongozi. Mie pia watoto 4 kama wewe. Miaka 12 ya ndoa. Mama wa nyumbani. Tatizo hawezi kujifunza kitu.

Kila siku ni shida tupu ndani ya nyumba. Mfano, hawezi kutoa magamba ya samaki yakaisha yote kabla ya kumpika samaki. Chakula anavyonunua kwenye supermarket, ndivyo anavyokipika!

Anaweza kupika nyama ya kuku na kinyeo chake ama bado kuna kiasi fulani cha vinyoya!! Hata nikimweleza vipi, akili yake haishiki!! Hataki niwafundishe watoto. Nikiwakosoa watoto kwa namna ya kuwafundisha, anakuja juu.

Watoto wananiona mimi shetani na yeye malaika. Amejenga chuki kati yangu na watoto ambao bado ni wadogo tu. Sijawahi kumpiga ama kuchepuka lakini nilikwisha mwambia kuwa tungekuwa tunaoa mara ya 2, nisingemuoa tena. Sina hamu tena hata ya kulala naye.
 
Back
Top Bottom