Wanawake wasomi kama huyo huwa hawaolewi, wao ndio wanaoa.

Ila kama uliweza kuishi nae kwa miaka yote hiyo na kupata nae watoto wanne, ningekushauri ungeishi nae tu hivyohivyo kama skrepa lako kwa maslahi mapana ya watoto.

Pole mkuu. Kwakuwa tayari Mahakama imeshabariki Talaka hapo hamna suluhisho lingine.
Hivi mkuu mahakama wakishatoa taraka mkakubaliana mrudiane inawezekana?
 
Mkuu ni kwamba umeangukia kwa mwanamke mwenye upumbavu wake kichwani.

Kuna wanawake wasomi au wenye uwezo kifedha wenye kujielewa na wenye heshima.

Mwanamke mpumbavu ni mpumbavu tu. Elimu na uwezo wa kifedha ndio vinakuja kuthibitisha upumbavu wake maana ndo wakati ambao anaanza kuuonesha.

Nawajua wanawake wengi sana wenye nidhamu na adabu kwenye ndoa. Kikubwa wanachohitaji ni upendo na kuheshimiana. Vikikosekana hivi ndio utaona reaction zao.

Kupiga sio suluhisho hata kidogo na omba sana Mungu watoto wasiwe wameliweka akilini.

Kikubwa angalieni tofauti zenu zisiathiri maendeleo ya watoto wenu. They are innocent and they deserve care from you parents. Waleeni bila kuhusisha tofauti zenu wala kutafuta kuwaweka upande wa mmoja kati yenu
 
NGOMEKONGWE2021 - Tupo wengi, kiongozi. Mie pia watoto 4 kama wewe. Miaka 12 ya ndoa. Mama wa nyumbani. Tatizo hawezi kujifunza kitu.

Kila siku ni shida tupu ndani ya nyumba. Mfano, hawezi kutoa magamba ya samaki yakaisha yote kabla ya kumpika samaki. Chakula anavyonunua kwenye supermarket, ndivyo navyokipika!

Anaweza kupika nyama ya kuku na kinyeo chake ama bado kuna kiasi fulani cha vinyoya!! Hata nikimweleza vipi, akili yake haishiki!! Hataki niwafundishe watoto. Nikiwakosoa watoto kwa namna ya kuwafundisha, anakuja juu.

Watoto wananiona mimi shetani na yeye malaika. Amejenga chuki kati yangu na watoto ambao bado ni wadogo tu. Sijawahi kumpiga ama kuchepuka lakini nilikwisha mwambia kuwa tungekuwa tunaoa mara ya 2, nisingemuoa tena. Sina hamu tena hata ya kulala naye.
Dah nimejikuta nacheka aise pole sn,..anapika kuku na kinyeo?
 
Tena kwa miaka 12! Ndio napambana kwa ajili ya watoto lakini ananionyesha kwa watoto kuwa mi ni katili! Na watoto wananichukia.
Duh something for the kids uwe unatafta mda wa kukaa nao nakutoka out, pia uwe una wa spoil na vitu wanavopenda, huyo mkeo sorry to this ana akili ndogo na Ali grow mazingira ya ajabu hivi mama wa nyumbani anashindwaje kuandaa hata chakula kizuri au kuparua samaki si aibu tupu.
Na hizo sumu anazowalisha watoto waeleze a, b, c, d isije ku ku cost wewe ka provider siku ukiwa mtu mzima utengwe bure iwe ka hujazaa
 
Inferiority complex Ni ugonjwa sugu kwa wanaume tulio wengi..! Tunahitaji kunyeyekewa na kuheshimiwa hvi vitu vikikosekana ndani tuna Anza unganisha dot..!
Ni kweli hili ni janga na hyo inferiority complex huwafanya muanze kuwanyanyasa wanawake zenu kihisia na kuwa control too much, kiasi mkifikiri mnajenga kumbe mnaharibu na hizo gubu zenu.
 
Huo ndio ukweli uliopo kuna wanawake wa aina mbili mama wa nyumbani na mfanyakazi ambaye naye anasukuma gurudumu la kiuchumi kwenye familia na hii imenikumbusha ushauri wa mwalimu wangu nikiwa chuo alisema kuna mambo ambayo anayafanya mke wako kama hayana madhara kwako achana nayo usiyatilie maanani sana kitu kama kufuliwa nguo na yeye, kukupikia au kukuwekea maji ya kuoga bafuni yaani anaweza kukuchotea maji yeye au binti wa kazi wewe ukabeba na kwenda nayo bafuni, kufuliwa nguo na binti wa kazi isipokuwa boxa zako is not an issue ninachomaanisha sio kila kitu ukichukulie maanani sababu unajua kabisa mnatoka wote asubuhi kwenda kazini mnarudi jioni wote kama ataweza kuingia jikoni sawa lakini kama dada kafanya kila kitu whats the problem, mimi nachozingatia kikubwa papuchi sikosi na heshima yangu kama mume na baba wa familia ipo pale pale na kweli sijawahi mpiga hata kibao sababu maudhi mengine najitahidi kuyakwepa mapema.
Sure mkuu wanaume wote mngekuwaga kama hivi ndoa nyingi zingekuwa na maelewano mno
 
pole sana ingawa nimecheka hapo kupika kinyeo Cha kuku huwa ni kitamu sana, I understand you hivo vitu vidogo dogo huua ladha ya mahusiano kabisa imagine kumuelekeza mtu mzima huwa inachosha, angalia asiwaambukize watoto ujinga maana wataalamu husema watoto hurithi akili za mama
Si kweli. Acheni kudanganyana.
 
Nataka kusema kitu kimoja

Wadogo zangu mlioolewa na msioolewa ndoa ni sacrifice kwa mwanamke!
Mwanaume ni kiongozi wa mwanamke,tunafeli kutaka kua sawa na wanaume.Hiko kitu hakipo na hakitakaa kiwepo hata usome mpk wapi au uwe na mshahara billions of cash...!!!Labda uolewe na wazungu hukoo au mukubaliane kimkataba b4 hamjaona kua mtaishi kizungu zungu ila hawa wa kitanzania utaenda kazini,utarudi na utamhudumia yeye binafsi uchoke usichoke utajiju.
Ukihisi huwezi kumtake care mwanaume au unapretend ukiolewa unaonesha makucha yako mtashindwana mwisho kutafutiana lawama kuzungushana mahakamani Bure.
Kingine hakuna mwanaume anapenda mkewe amzidi kipato ikitokea ndo hvyo atakubali lakini wengi inakua shida plus mawivu na maugomvi.
So choose wisely mwenza wako,na Mungu awasimamie sana.
Ndoa ni changamoto sana,siku hizi sihukumu wanandoa mmegundua wake na waume wotee vimeo Siku hizi.
Umeandika tu haya huwajui wanaume kinachowatesa sio wanawake wafanya kazi ni inferiority complex ndio huleta hayo yote, mwanaume asiye jiamini huwa hana jema hata ukikosea ka binadamu atakyshambulia kuwa unaringa una elimu na umemuzidi mshahara kumbe wala mtu umevurugwa tu, so kuna wanawake Wana vyeo na wanaheshimu waume zenu, ila Ile inferiority wengi inawafanya wajione less wanaume, pia mahusiano na kugombana kupo tu uwe na shule kubws au ndogo daily kina mwajuma ndala ndefu huolewa na kuachika, so relationship ikishindikana inabidi kujiuliza ni wapi tulikwama na sio ku blame one side of the story, and from my experience saa nyingine wanaume kutokusimama ka familia na kujisahau na kufanya vitu huwafanya wanawake na wao wawe wakorofi waanze kushindana, na vile ni ngumu mwanamke mwenye kipato kuvumilia mateso ya mtu anaondoka.
So I'm sure wanawake wakiwa na kipato Cha uhakika ni nadra kuvumilia ndoa chungu umaskini hufanya watu wavumilie hata visivo vumilika
 
Back
Top Bottom