Wakristo kimavazi tunazidi kupotea, Mavazi yaliyoshauriwa kwenye maandiko yamepuuzwa, Pongezi kwa Waislam kuendela kuvaa mavazi yanayositiri

vishati vya kufanya Vifua kuachwa wazi kuonyesha matiti ishakuwa fashen

Suruali za za kubana kuchoresha makalio, hips na mapaja

Magauni nayo pia yamekuwa ya kubana kuchoresha makalio na hips
 
Hakika hujui historia ya dini yako.

Tambua hakuna dini yenye vazi lake. Yesu alivaa kanzu (robe) sababu yale ndio ayalikuwa mavazi ya zamani. Mabadiliko yakatokea kipindi cha industrialization.

Watu wakahama na fashion. Ila Uislam wao waliendelea na mavazi yale ila ukiangalia kila siku yanakuwa modified sio kama yale ya kipindi cha yesu.
 
1 Timotheo 2 :9
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani.
 
1 Timotheo 2 :9
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani.
KUSUKA NYWELE hapo watakwambia wanavaa MAWIGI
 
Yaani mavazi ya Mashariki ya kati ndiyo kujisitiri? Wayahudi na Waarabu walivaa kanzu sababu ya joto. Walifunika nywele wanawake kwa waume sababu ya vumbi kali. Si mchezo kudeal na vumbi kama una nywele ndefu. Turudie asili yetu waafrika kuvaa nusu uchi.
 
Kama kweli kumtamani mwanamke nisawa na kuzini nae, basi 80% ya wanaume ambao huenda kanisani huzini kwasababu ya mavazi ya wanawake wa kileo makanisani. Poleni sana wanaume wa kikristo kwa majaribu mnayopitia huko makanisani

Hongereni waislamu kwa kuamua kutenganisha wanaume na wanawake wakati wa kuswali na kuabudu misikitini na hata majumbani, hakika mliona mbali sana.
 
Kwa tamaa zao wangebanduana hata misikitini, hvy wakaona yanini.! ni bora kuwatenganisha
 
Mwanamke wa Kikristo wa kweli vs Wanawake wa Kikristo bandia
 
Attachments

  • Screenshot_20230419-183907.jpg
    Screenshot_20230419-183907.jpg
    59.4 KB · Views: 1
Kuvaa nguo ndefu ni utamaduni wa waarabu... Utamaduni wa kiafrika ni kuficha papuchi tu.. Utamaduni wa nchi za ulaya.. Ambazo ndiyo walileta ukristo africa ni upi?
 
Sisi wa kristo asilia hatuna maneno na mavazi, ata wasipovaa nguo kabisa, tuko kiroho sana, tunaenda na kurudi mbinguni kama posta mpya. Muulize Mwakasege
 
Wameibuka mapasta vijana ndio wanapenda waumini wao wavae mavazi ya kishua, hawataki kuona mavazi ya kizamani wanaona ni ya kizee na yamepitwa na wakati
 
vishati vya kufanya Vifua kuachwa wazi kuonyesha matiti ishakuwa fashen

Suruali za za kubana kuchoresha makalio, hips na mapaja

Magauni nayo pia yamekuwa ya kubana kuchoresha makalio na hips
Hayo ni ya Dunia.

Wakati mababu na mabibi zetu walipokuwa wanavaa matawi ya miti ilikuwaje?
 
vishati vya kufanya Vifua kuachwa wazi kuonyesha matiti ishakuwa fashen

Suruali za za kubana kuchoresha makalio, hips na mapaja

Magauni nayo pia yamekuwa ya kubana kuchoresha makalio na hips
Kama umeona watawa wanavyovaa, basi pengine ndio jinsi wanawake wanavyopaswa kuvaa.

Kumb ya Torati 22:5

Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.

1 Korin 11:3

Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.

5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.

6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.

7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.

8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.

9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.

10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.

11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.

12 Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.

13 Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?

14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?

15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.
 
vishati vya kufanya Vifua kuachwa wazi kuonyesha matiti ishakuwa fashen

Suruali za za kubana kuchoresha makalio, hips na mapaja

Magauni nayo pia yamekuwa ya kubana kuchoresha makalio na hips
Mkuu tofautisha mkristo na mkristo mshika dini hata upande wa pili wapo wenye sifa ulizotaja lakini nao ni wa huko, ukimkuta mkristo mshika dini huwezi kumkuta amevaa nguo isiyo na stara hata siku moja ukimkuta mtu wa upande wa pili hajashika dini utashangaa alivyovaa hivyo usimjaji mtu kutokana na mavazi kuwa upande huu hauna maadili never
 
Unategemea dini hadi kwenye suala la kujisitiri??!! WTF vipi kama dini ikikuelekeza utembee uchi?? Dont be dumb.
 
Back
Top Bottom