Mavazi ya mwanamke Mcha Mungu kwa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani pamoja na Kwaresma

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
810
Habari Ya Asubuhi JF njooni hapa mjue Mavazi Ya Mwanamke Mcha Mungu kama mada ilivyoelezwa

MAVAZI YA MWANAMKE MCHA MUNGU


1. JE, MUNGU HAANGALII MAVAZI?

Nyakati hizi za mwisho tulizonazo, kumekuwepo na wimbi kubwa la mafundisho potofu la waalimu wa uongo, manabii wa uongo na wanaojiita watumishi wa Mungu lakini wa uongo, kuhusiana na hoja ya Mkristo na mavazi.Wapo watu wengi wanaosema na kufundisha kwamba Mungu haangalii mavazi. Maana yake uko huru unaweza kuvaa vyovyote tu utakavyo wewe. Haina shida kabisa!Na wapo wengine wanaosema kwamba binadamu aliumbwa uchi kwenye shamba la Edeni, hivyo hakuna shida hata akivaa nguo za kuanika nyeti zake,ilmradi moyo wake unamuogopa Mungu!Sasa swali ni moyo gani unamuogopa Mungu alafu unakusukuma utembee uchi?

Ndivyo wanavyoamini wao, ndivyo wanavyosema na ndivyo wanavyofundisha watu. Lakini Biblia inasema nasi katika kitabu cha 1 Timotheo 4 1-2, "Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza ROHO ZIDANGANYAZO , na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe." Kisha katika Wakolosai 2:4-8, "Nasema neno hili, mtu asije akawadanganya kwa maneno ya kuwashawishi. Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na MADANGANYO MATUPU, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo."

Mafundisho ya namna yoyote yanayosema kuwa Mungu haangalii mavazi, yaani maana yake, uko huru kuvaa vyovyote tu utakavyo. Hayo ni mafundisho ya uongo ya roho zidanganyazo ambayo hayatokani wala hayalingani na ukweli wa neno la Mungu, Kama Biblia inavyotufundisha.

Ni muhimu kuelewa ukweli huu. MUNGU ANAANGALIA NA KUJALI SANA MAVAZI YETU. Na ndiye mwanzilishi aliyetufanyia sisi mavazi wanadamu(Mwanzo 3:21). Na kama Mungu angekuwa hajali wala haangalii issue ya mavazi, basi kwanini asingewaacha Adamu na wakaeendelea tu kuwa uchi?Lakini Mungu aliwafanyia mavazi yake yaliyokuwa bora zaidi tofauti na yao yaliyokuwa hayawasitiri vizuri uchi wao(Mwanzo 3:7,21).Swali ni kwanini binadam alitengenezewa vazi wakati siku zote aliishi humo shambani akiwa uchi?Ni kwa sababu aligundua uuchi wake baada ya kukaribisha dhambi,na akawa na ufahamu na utashi wa chema na baya!

Binadamu anajitambua,anajua ubaya wa kuona utupu wa mwenzie,ndo maana Mungu akaonyesha kwa vitendo,kwa kuwapa vazi la kuwasitiri. Kisha akaonya kwa maandishi kabisa,katika kitabu cha Kumbukumbu 22:5," Mwanamke asivae MAVAZI YAMPASAYO mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo NI MACHUKIZO KWA BWANA, Mungu wako." Sijui kama Biblia ilibadilika lini!

Tena bado hata katika Agano jipya kwa kukazia issue hiyo hiyo ya mavazi vilevile akaendeleaa kusema mwanamke na ajipambe kwa mavazi ya kujisitiri(1 Timotheo 2:9). Sasa kama Mungu angekuwa haangalii wala hajali kuvaa kwetu,basi asingesema tukivaa hivi au vile ni MACHUKIZO KWAKE YEYE MUNGU. Kumbe Kama anasema ni machukizo tukivaa tofauti na jinsi anavyopenda Yeye,basi hii ni waziwazi inathibitisha ukweli huu kwamba kumbe bado Mungu anajali sana jinsi ya kuvaa kwetu wanadamu.

Na si hilo tu,utaona pia Biblia inaelekeza hata watumishi wake namna ya kuvaa(Kutoka 39:1).
Kwa ufafanuzi wa andiko hilo, kama Mungu angekuwa haaangalii mavazi wala hajali mavazi,asingeagiza chochote kuhusu mavazi tena yawe yapi na yatengenezwe vipi?

Hata mbinguni bado Mungu anaendelea kulitazama suala la mavazi yetu vilevile likoje.Kule mbinguni watakatifu tutavikwa mavazi meupe. Mungu mwenyewe amevaa mavazi meupe Kama theluji. Malaika nao wamevikwa mavazi meupe (Ufunuo 3:4-6; Danieli 7:9; Yohana 20:12).Sasa wewe vaa litaiti lako na T-sheti likubane eti unamtumikia Mungu,siyo huyu Yehova,labda mungu wako mwingine!

Mungu amekwenda mbali zaidi na kutuwekea MPAKA. Na anasema kuna vazi LIMPASALO mwanaume na kuna vazi LIMPASALO mwanamke. Na tukiingiliana kimavazi inakuwa ni dhambi kwa Mungu.

Sasa tunawezaje kujua kanuni kwamba vazi hili ni vazi LIMPASALO mwanamke au mwanaume?Biblia imetupa jibu katika 1Wakorintho 11:14, "Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na........" Ebu isome yote!

Jinsi Mungu alivyotuumba kati ya kike na kiume ni tofauti. MAUMBILE ndiyo yanayoweza kufanya hata tofauti ya matengezo ya mavazi yetu. Mavazi pia yametengenezwa kulingana na maumbile. Kwa mfano;Vazi la sindiria limebuniwa kwa mwanamke kwa sababu ana matiti. Na vile vile sketi, gauni, blauzi n.k. inampa urahisi mwanamke hata wakati wa dharura ya kujisaidia haja ndogo au kubwa. Na vilevile ni vazi ambalo halichori mwonekano wa utupu wa mwili wake.Tambua ukweli kwamba vazi linaloonyesha umbile lako mwanamke ni CHUKIZO kwa Mungu!

Simumunyi maneno,suruali sio mtindo wa vazi limpasalo mwanamke kwa sababu za kimaumbile. Na pia vilevile hata akilivaa halimstiri vizuri ipasavyo LINAMCHORA umbile kama makalio, hipsi, mapaja, na sehemu za siri. Kumbuka kwa asili jinsi mwanamke alivyoumbwa maumbile yake ni ya kutamanisha tamanisha kwa mwanaume. Na hivyo itazalisha dhambi ya matamanio kwa watu wa Mungu (Mwanzo 3:16; 2 Samweli 11:2-4; Mathayo 5:27-28).Yaani mwanamke ukiamua kuvaa kitu kinachofanana na suruali,basi liwe la wazi,halibani,lifanane na sketi!

SURUALI SIO VAZI LA KIMAADILI kwa wanawake wanaomcha Mungu na kujiheshimu kisawasawa.Na wazo hilo linaungwa mkono na Biblia ikisema katika 1Wathesalonike 4:1-2,"Kila mmoja wenu AJUE KUUWEZA MWILI WAKE KATIKA UTAKATIFU na HESHIMA; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu." Ukiamua kuvaa vibaya, juwa ukweli kwamba wewe ni wa mataifa, duniani, siyo wa Yehova!

1Timotheo 2:9, "Vivyo hivyo wanawake na wajipambe KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na adabu nzuri........" Hakika mwanamke asiyejisitiri hana adabu!

Suruali ni mojawapo ya mavazi yasiyo na adabu kwa wanawake. Na kama nilivyosema mwanamke anayemcha Mungu na kujiheshimu kisawasawa hawezi kamwe kuvaa vazi hili Kama fashion.

2. WANAWAKE WA KWANZA DUNIANI KUVAA SURUALI:
Kulingana na mtandao wa Wakipedia vazi hilo limechambuliwa sana kwa undani tokea lilipoanzia mpaka sasa lilipofikia.

Na vazi hili la suruali limeanza kuvaliwa na wanawake katikati mwa karne hii ya 20 na sio kabla ya hapo. Lakini vazi hili tokea mwanzo lilipobuniwa lilikuwa likivaliwa na wanaume tu.

Ingawa vazi hili lilipoanzia kuvaliwa na jinsia ya wanawake ilikuwa ni ngumu sana kukubalika au kupokelewa na jamii nyingi, ilionekana kama ni kitu kigeni. Tofauti na Sasa ambapo vazi hili limeshakuwa rasmi kuvaliwa na wanawake walio wengi duniani.

Wanawake waliokuwa wa kwanza kabisa kuvaa suruali duniani ni hawa wafuatao:

(1) ANDRE COURREGES-sachi jina umjue,mwaka 1960 ilikuwa.
(2) CHARLOTTE REID-mgoogle umjue,mwanasiasa wa chama cha Republican,mwaka 1969.
(3) PAT NIXON-Mke wa kwanza wa rais kuvaa suruali mbele za umma!
(4) REBECCA MORGAN,mwaka 1989,seneta wa kwanza mwanamke kuvaa suruali ndani ya seneti huko Marekani.
(5) HILLARY CLINTON,mke wa rais wa kwanza kuvaa suruali na kupigwa picha nalo rasmi.

Utaona hawa wote wanawake wa mwanzoni mwanzoni kabisa kuvaa suruali duniani,walikuwa wa kiduniani, walikuwa ni wanawake ambao sio wa hekaluni kabisa, sio wanawake wa ki-kristo halisi waliomcha Mungu. Walikuwa wapagani tu na wanasiasa wa kawaida.

Angalia vazi la watumishi sasa,Kutoka 28:3,42-43," Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, NILIOWAJAZA NA ROHO YA HEKIMA wamfanyie Haruni mavazi. Nawe wafanyie SURUALI ZA NGUO ya kitani, ILI KUFUNIKA TUPU YA MIILI yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani; na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania "Naamini mnaona!

Narudia tena kitu hiki,binadamu asingekengeuka pale Edeni,angekuwa huru sana,angetembea uchi kote duniani,kwa sababu hakujua kutofautisha chema na baya, hakujua dhambi. Lakini kwa kuwa dhambi ilishaingia duniani,kutembea na nguo za kubana,au nusu uchi ni chukizo mbele za Mungu kwa sababu unalazimisha binadam wengine waingie kwenye dhambi ya uzinifu, ambayo ni moja kati ya dhambi mbaya kuliko zote kwa Mungu!

Tujiulize,mwanamke anayevaa nguo za kikahaba anawezaje kusema siyo kahaba?Ndivyo hivyo kwa mwanamke anayevaa vizuri kiheshima,atatambulika kuwa ni mcha Mungu bila hata ya kusema neno moja!

Yehova atuongoze,AMINA!
 
Mtu haijalishi atakavyovaa ila nafsini mwake anawaza nini? Hilo ndio la msingi,maana hakuna sababu ya kuvaa magauni marefu wakati nafsini mwako umebeba husda,tamaa,wivu,kiburi,hasira,kisasi,uchoyo na mengine mengi yasiyoonekana Kwa macho ya nyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vigezo vya kuiona mbingu ni vingi jamani.Kwenye mavazi hapa nahisi ntaiona nchi ya ahadi ileee,af sitoingia
 
Vigezo vya kuiona mbingu ni vingi jamani.Kwenye mavazi hapa nahisi ntaiona nchi ya ahadi ileee,af sitoingia
Roho yako ndiyo inatakiwa iwe safi ndio kigezo kikubwa zaidi Cha kuiona mbingu..

Mambo ya mwilini ni mwilini na rohoni ni rohoni...
 
Back
Top Bottom