Wakati wa mimi kusema umefika

Wakati wa mimi kusema umefika

kwanini ameibuka katika kipindi hiki wakati CDM inataka kufanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa?
 
Usimtishe mwache aseme hawa wote waliwahi kifanya kazi cdm makao makuu wanasiri kuwa za mauaji
Mkuu Gwanco, kwanza asante kwa kudhani namtisha!, no!, nampa tuu ukweli halisi wa kitu kinachoitwa "criminal responsibility" na "criminal liability", mtu ukiijua criminal activities yoyote usipoiripoti kwenye vyombo husika, then wewe pia ni mhusika as "an accessory before the fact" kama uliijua kabla haijatendeka or "an accessory after the fact", kama uliijua baada ya kutendeka, na akistakiwa mtendaji uhalifu huo, wewe uliojua ukanyamaza, unaunganishwa kwenye kesi husika!.

Hata hivyo sheria imetoa kinga kwa watu wenye kitu kinachoitwa "fiduciary relationship" hata wakiujua ukweli wa jinai, wasiporipo, hawashitakiwi!, hawa ni "mke na mume", "mzazi na mtoto", "mwalimu na mwanafunzi", daktari na mgonjwa", na "wakili na mteja wake", kundi hilo, hata wakijua au kushuhudia jinai ya wahusika hao, hawapaswi kuripoti jinai hiyo, na hata wakijulikana walijua, hawawajiki kuitwa kutoa ushahidi dhidi ya watu wao, unless wenyewe kwa ridhaa yao bila shinikizo lolote wakiamua kuripoti, then taarifa yao itachukuliwa bila wao kuwajibika kuja kutoa ushahidi!. Hivyo hicho alichokisema humu Mwampamba ni jinai by now alipaswa kuanza kuny.. debe long time!.

Thanks.

Pasco
 
Deus Mallya umenifanya kukumbuka utata wa kifo cha Wangwe, ulikuwa naye kwenye gari;
1. Toka nyumbani wewe ulikuwa ukiendesha gari, ukalipeleka gereji.
2. Baada ya ajali mwili wa Chacha Wangwe umekutwa katika siti ya abiria ya mbele, ikiwa imefungwa seat belt bila kuwepo ndani ya gari wewe dereva uliyekuwa unaendesha gari ile.
3. Wenyeji wa Pandambili namkumbuka Mzee Mwigune aliyekuwa wa kwanza kufika eneo la ajali na kukuta gari ikiwa na abiria tu Chacha Wangwe bila dereva.
4. Baada ya dakika kadhaa mashuhuda wanakuona ukitokea ilikotoke gari kabla ya ajali ukiwa na damu katika shati lako mkononi ukiwa na laptop ya marehemu.
5. Hapa ndipo tunapoanzia kujiuliza process ya kifo chake ilikuwa huko ulikotokea?
6. Nini kilikupeleka pale ukiwa na laptop ya marehemu wakati hukuwemo kipindi gari inapinduka.
7. Ikiwa nyumbani ulionekana ukiendesha gari ile wewe je nani alikupokea usukani?
8. Kama ni Wangwe mwenyewe alikuwa akiendesha,, alihameje kiti toka cha dereva hadi cha abiria akajifunga mkanda kisha akafariki?
9. Laptop ulikuwa nayo tokea wapi, uliichukua wakati gani na kwanini.
10.USHAURI WANGU KWAKO DEUS MALLYA;
Tafuta mwanasheria akushauri kwa kuwa ulishatumikia kifungo chako kidogo huku ukiwa umeacha kovu ambalo kamwe halitafutia kwa wanafamilia, bora ungekaa kimya kwasababu kisheria suala hili lilishaisha vinginevyo ukweli utakao utoa leo utai-provoke mahakama lazima kila kitu kianze upya.
Umeonyesha facts zako vizuri lakini hapo kwenye red sikubaliani na wewe kuna shida gani kesi ikianza tena lakini haki ikapatikana?

Salaam!

Kwa muda Mrefu nimekuwa nikipata msukumo unaonitaka kuzungumzia maneno yaliyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kutoka kwa ndugu ma makundi mbali mbali.

Kimsingi sintajibu wanayotaka kwa sababu nimeendelea kupokea jumbe za Matusi na kejeli hata kuvamiwa na wanaodai ni wafuasi wa CHADEMA wakitaka niendelee kuwa Kimya!. Wapo walioamua kujitaja majina yao ili nijue ni kiasi gani wako 'Serious' kwenye kile wasemacho!.

Japo nilishatoa taarifa Polisi, kwa sasa nimechoka kuishi maisha ya kuwindwa ndani ya Nchi yangu. Nimechoka. Nitakachofanya ni KUONGEA na si KUJIBU kilichosemwa na yeyote kuhusu Mimi na 'Ajali ya Pandambili'

Naamini kwa Mungu siku zote
Naamini nikifa ni kwa Mpango wake
Nikifa ukweli Utaishi hadi vizazi vijavyo.

Deus Mallya
Dar es Salaam.
Hivi utaendelea hadi lini kutumika kama gogo la chooni!? Hivi unajua athari za hayo uliyotumwa kusema? Hebu jaribu uone utakavyoishia gizani you damn traitor mchumia tumbo!! Hayo ndiyo uliyofuata kwa bosi wa star tv!!???Cheza na MUNGU usijelaumu kwa njaa zako zinavyokutuma!!
 
Pasco,
Ndio maana mimi ntasema mpaka kesho ZZK ana watu vilaza sana ambao hawawezi kumsaidia. Ni wepesi mno vichwani, wana fikira kiduuchu (short term) sana. At least wewe Pasco ni mjanja mjanja kidogo ingawa bado.....Sometimes you can get back to your senses...

Watu wa design hii hawamfikishi ZZK kokote. Hivi kweli mtu unasema hadharani fulani kamuua fulani na bado vyombo husika vinakuchekea tu? Kweli....?

Hii nchi imekuwa ni ya ajabu sana, Njaa ni kitu kibaya sana...Mungu atusaidie...
Ni kweli kabisa!! Huyu atajionyesha alivyotenda jinai kwenye mahakama na ataishia jela ya maisha!! kama siyo kunyongwa!!
 
Mkuu BMO, asante kwa ushauri huu kwa huyu dogo, wasiwasi wangu sio ukweli kujulikana, bali hii dilly dallying ya nseme nsiseme!, isije akawa silenced jumla!.

Thanks.

Pasco

Wewe Pasco sometimes una akili sana wewe...sasa issue ni nani ataem-silence jumla?
 
hivi vituko ni kawaida kujitokeza kila uchaguzi mkuu unapokaribia na kuna watu watatumika sana lakini uchaguzi ukipita watatelekezwa kama misukule.

unamkumbuka yule chizi aliyekuwa akizungushwa majukwaani na mwigulu? yuko wapi sasa? kwishney---katupwa kama ganda la mua la jana. mtatumika sana safari hii.
 
Duh "Benazir" !

Sasa mimi naingiaje hapa? Povu ulilotoa hapa linatosha.Niongeze lingine la nini?

Dogo wa sumu na wewe bado yako yanawekwa sawa waje wafunguke?!

Ha ha haaaaaaaaaa mbona unataka kukimbia?!@Ben Saanane
 
Umeonyesha facts zako vizuri lakini hapo kwenye red sikubaliani na wewe kuna shida gani kesi ikianza tena lakini haki ikapatikana?

Naungana nawe, wakati natoa ushauri sijui nilikuwa nawaza nini, lakini nimshauri kuwa aseme ukweli ili kweli umweke huru.
 
Kinachowasumbua hawa vilaza makuwadi wa zitto ni kuona uchaguzi wa cdm ukiendelea tena kwa mafanikio makubwa tofauti na mikakati yao miovu waliyopanga kwa ushirikiano na ccm.wamebaki kutapatapa wakidhani wanaweza kuzuia mafuriko kwa mikono! Cdm ni kisiki cha mpingo wala hakiwezi kutetereshwa na kelele za vyura!
 
Mkuu Gwanco, kwanza asante kwa kudhani namtisha!, no!, nampa tuu ukweli halisi wa kitu kinachoitwa "criminal responsibility" na "criminal liability", mtu ukiijua criminal activities yoyote usipoiripoti kwenye vyombo husika, then wewe pia ni mhusika as "an accessory before the fact" kama uliijua kabla haijatendeka or "an accessory after the fact", kama uliijua baada ya kutendeka, na akistakiwa mtendaji uhalifu huo, wewe uliojua ukanyamaza, unaunganishwa kwenye kesi husika!.

Hata hivyo sheria imetoa kinga kwa watu wenye kitu kinachoitwa "fiduciary relationship" hata wakiujua ukweli wa jinai, wasiporipo, hawashitakiwi!, hawa ni "mke na mume", "mzazi na mtoto", "mwalimu na mwanafunzi", daktari na mgonjwa", na "wakili na mteja wake", kundi hilo, hata wakijua au kushuhudia jinai ya wahusika hao, hawapaswi kuripoti jinai hiyo, na hata wakijulikana walijua.
***KAMANDA LEO UMEMEZAMAWE YA HATARI N YENYE KILO ZISIZO PIMIKA KIMZANI!
='SHERIA NI MAISHA NA MAISHA NI KWA SHERIA DHIDI YA DHULUMA'.
 
Ni kweli kabisa!! Huyu atajionyesha alivyotenda jinai kwenye mahakama na ataishia jela ya maisha!! kama siyo kunyongwa!!

Mkuu huyu anatumika na wanaomtuma wapo juu ya sheria na lengo mahususi la hiki anachokichokonoa na kuihusisha CHADEMA na kifo cha Chacha Wangwe lakini ikumbukwe wakati Chacha Wangwe anafariki alikuwa na hoja Binafsi aliyotaka kuiwasilisha Bungeni na ilihusu kifo cha Balali kwani yeye Marehemu iliaminika alikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa Balali hajafa na ni wapi yupo na ilikuwa iwasilishe hoja hiyo baada ya Kurudi safari yake ya DSM lakini ndio mauti yakamkuta kabla ya kutimiza lengo lake.
- Pia ni vema tukajikumbusha matukio baada ya kifo chake, Familia ilitafuta wataalamu kutoka nje ya nchi(Kenya) kwa ajili ya kufanya Postmoterm huku serikali ikiweka wataalam wake kwa ajili ya kazi hiyo matokeo ya Postmoterm yalileta utata na ikabidi Serikali izuie majibu ya wale wataalam wa kigeni na kutamka wazi kuwa majibu ya wataalam wa Serikali ndio yatakayokubalika na suala zima la upindishaji wa Taarifa hizi lilisimamiwa kwa nguvu zote na kaka wa Marehemu Ndugu Wangwe ambaye ni kada wa CCM na kama sikosei anakacheo ndani ya CCM.
- Ninachojiuliza kama ni kweli kuna mkono wa CHADEMA na kifo kile na kwa jinsi CCM wasivyoipenda CHADEMA na kutaka ipotee kabisa hususani hawa viongozi wake Mbowe na Dr. Slaa ni kweli katika chunguzi zote zile walishindwa kuyagundua haya anayoyataka kuyasema huyu Mchumia tumbo Deus?
 
Wala hawaambui lolote!! wale wataalam wa Kenya wanayoripoti! na sababu za serikali kuificha na kutengeneza yake zitajulikana!! Huyu Mallya haponi!! hebu subiri watamfanya mbuzi wa kafara!!
 
Mkuu BMO, asante kwa ushauri huu kwa huyu dogo, wasiwasi wangu sio ukweli kujulikana, bali hii dilly dallying ya nseme nsiseme!, isije akawa silenced jumla!.

Thanks.

Pasco

Mkuu ebu naomba tujikumbushe CHADEMA walifanya nini baada ya Tukio lile na hii ni Barua ya Mnyika kama inavyojieleza hapa chini, na kwenye kipengere No. 6 na 7 je polisi walitoa majibu stahiki kama ilivyoombwa?

C/HQ/ADM/SG/02/185 30 Julai, 2008

MKUU WA JESHI LA POLISI,
P.O.BOX DAR ES SALAAM ,
TANZANIA.

YAH; KIFO CHA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE MBUNGE WA TARIME.

Kutokana na ajali iliyotokea tarehe 28 Julai 2008 katika eneo la Pandambili Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, ninalazimika kukuandikia rasmi kuhusiana na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini juu ya utata ambao umekighubika kifo hicho na haswa mazingira ya ajali yenyewe. Katibu Mkuu wa CHADEMA, katika mahojiano yake na TBC1 katika mahojiano yake kwenye kipindi cha Jambo Tanzania alielezea pia utata huo na kutaka Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina.

Maelezo ya Ndugu Deus Mallya ameyatoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na jinsi ajali hiyo ilivyotokea na eneo ambalo yeye alikuwa amekaa wakati ajali inatokea , pamoja na kusema kuwa yeye alikuwa amekaa kiti cha nyuma huku Dereva wa Gari akiwa ni Marehemu Chacha Wangwe yameongezea kwenye utata huo.

Taarifa ambazo zimetolewa na watoto wa Marehemu kama walivyohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuripotiwa na vyombo hivyo na haswa maelezo yaliyorushwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), na vituo vingine vya Television, pamoja na Habari za Magazeti mbalimbali ya tarehe 30-07-2008 ,kama vile Magazeti ya The Guardian, Nipashe, Tanzania Daima ,Mwananchi na mengineyo ambayo yaliandika kuhusiana na maelezo aliyotoa Ndugu Deus Mallya pamoja na watoto wa Marehemu yakilinganishwa na maelezo ya Deus Mallya yanahitaji kupatiwa majibu ya kina, jambo ambalo CHADEMA kama mwathirika wa ajali hiyo isingeliweza kulifumbia macho.

CHADEMA , tumefuatilia kwa kina sana kuhusiana na maelezo hayo ambayo yametolewa kwa nyakati tofauti na watu tofauti kuhusiana na ajali hiyo na hatimaye msiba huo.

Hivyo basi , Chadema kama Chama kilichoathirika kwa kumpoteza Mbunge wake, Mwenyekiti wake wa Mkoa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti na hivyo kuwa na maslahi ya karibu sana katika uchunguzi huu, tunalitaka Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vingine vya Usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na mambo yafuatayo;

1. Kujua huyu ambaye alikuwa (Deus Mallya) na Marehemu kwenye gari lake wakati anafariki ni nani na anafanya shughuli gani.
2. Deus Mallya alienda Dodoma kufanya shughuli gani na ana uhusiano gani na Marehemu na au Familia ya Marehemu.
3. Ndugu Deus Mallya alikuwa amekaa kwenye kiti gani wakati ajali inatokea.
4. Ni nani alikuwa anaendesha Gari wakati ajali na hatimaye umauti unamkuta Mheshimiwa Chacha Wangwe.
5. Ni mazingira gani yaliyopelekea na au kusababisha ajali hiyo kutokea .
6. Tunataka Polisi wachukue hatua stahiki za kisheria ili Deus Mallya akaisaidie Polisi na kuhojiwa kwa kina juu ya suala hili kwani maelezo yake yana utata mkubwa sana.
7. Jeshi la polisi liitoe ripoti ya uchunguzi huo mapema na kuiweka ripoti hiyo hadharani.

Tunapendekeza hatua hizo zichukuliwe mara moja kwani tunaamini kuwa kifo hiki kimeghubikwa na utata mkubwa sana na haswa kutokana na maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyeshuhudia ajali (Deus Mallya) pamoja na watoto wa marehemu.

Tunaamini kuwa utatupatia ushirikiano wa kina ili kuhakikisha kuwa hatua za haraka na za dharura zinachukuliwa mara moja kwa ajili ya kuujua ukweli wa kifo hiki tata.

Pamoja na hayo, hivi karibuni wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakipata taarifa za vitisho pamoja na kuzushiwa vifo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi na ujumbe huo kusambazwa sana kama ilivyoripotiwa kwako na Mheshimiwa Zitto Kabwe (MB).

Tunaomba wabunge wetu wapatiwe Ulinzi na pia taarifa hizo zifanyiwe kazi kwa kina.

Nakutakia kazi njema.

Wako katika ujenzi wa Demokrasia na Utawala Bora.

……………………
John Mnyika - 0754694553,
Kaimu Katibu Mkuu,
Na Mkurugenzi wa Vijana Taifa ,

Nakala:
1. Mhe.Lawrence Masha – Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
2. Mhe.Dr. Willbrod Slaa (MB) - Katibu Mkuu CHADEMA .
3. Robert Manumba -Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mhe-chacha-wangwe-na-uchunguzi-wake-24.html
 
kaka ni bora kufa maskini wa roho kuliko kuuza utu wako wa vipande vichache vya fedha - tena mbaya zaidi za umma!!

kajamaa kameshatangaziwa dili - hapo lazima kaite press ndani ya wiki hii ili kujaribu kuvuruga uchaguzi wa kitaifa - CDM

FUSO
Mbona mnatia huruma, huyo jamaa si ndio chama kilitoa tamko la kutokumtambua?" sasa iweje leo mnahofu na atakayoyazungumza mtu msiyemtambua?

mnatia shaka
 
Naungana nawe, wakati natoa ushauri sijui nilikuwa nawaza nini, lakini nimshauri kuwa aseme ukweli ili kweli umweke huru.
Ukizingatia sheria ya ushahidi inavyosema "hawezi kushitikiwa tena kwa kosa lile na ushahidi uleule" hivyo yeye aseme atakuwa huru zaidi.

hivi vituko ni kawaida kujitokeza kila uchaguzi mkuu unapokaribia na kuna watu watatumika sana lakini uchaguzi ukipita watatelekezwa kama misukule.

unamkumbuka yule chizi aliyekuwa akizungushwa majukwaani na mwigulu? yuko wapi sasa? kwishney---katupwa kama ganda la mua la jana. mtatumika sana safari hii.

- Wacheni aseme mnaogopa nini na hamuhusiki na kumuuaaa Wangwe mpaka mnatia huruma, kule UKAWA Lissu kaulizwa na Rais sio wewe uliyelilia Rais asiwe na mamlaka ya kuvunja bunge sasa unalilia nini hana jibu here you are muwacheni aseme sisi wananchi tutaamua kama ana hoja au hana mambo ya UKAWA kupigana ngumi kwenye vikao vyenu msituletee kwenye Taifa!!

Le Mutuz
 
Mkuu BMO, asante kwa ushauri huu kwa huyu dogo, wasiwasi wangu sio ukweli kujulikana, bali hii dilly dallying ya nseme nsiseme!, isije akawa silenced jumla!.

Thanks.

Pasco

We jamaa fitna unazimaster aisee...

167706_490908615387_6184476_n.jpg
 
Back
Top Bottom