Nimeamini kuwa watanzania wengi tuko nyuma kwenye "fasihi" mnataka nini tena Deus Mallya aseme? mbona mwenye akili tayari anajua ebu angalia nukta zifuatazo:
-Kwamba hatojibu wa vile anapokea matusi, kejeli na kutishiwa kuvamiwa,
-Kwamba ameambiwa akae kimya,
-Kwamba hata wakimtisha na hata akifa ukweli utabaki kuwa ukweli na utaishi hata kwa vizazi vijavyo,
-Kwamba wanaomtisha na kumwambia akae kimya ni wafuasi wa chadema,
-Kwamba tujiulize kwa nini wanamtisha na wanamwambia akae kimya?
-Kwamba wanamwambia akae kimya ili asiseme nini?
-Kwamba kwa nini chadema wana hofu asiseme?
Tukijiuliza na tukichambua nukta hizi tutapata jibu, na kwa mwenye akili jibu liko wazi na kuwa Deus Mallya kwa maana nyingine tayari ameshasema.