IGP Sirro: Niwasisitize tu, wakati wa uchaguzi mtu asithubutu kuandamana, nitakushughulikia pale pale, kama ni suruali yako itachanikia pale pale

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,184
IGP SIRRO ATOA ONYO KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

"Niwasisitize tu, wakati wa uchaguzi mtu asithubutu kuandamana, nitakushughulikia pale pale, kama ni suruali yako itachanikia pale pale kabla hujafika mbali na kwenda kuleta madhara kwa watu wasio na hatia,- Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro.

=====

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefunguka kuhusu utendaji wa jeshi hilo katika miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, akimmwagia sifa kwa kuliimarisha, hali iliyolisaidia kudhibiti uhalifu nchini.

Mbali ya hilo, ameeleza kuhusu anavyonyimwa usingizi na suala la ugaidi nchini Msumbiji, lakini pia alizungumzia mauaji ya mifugo wilayani Tarime mkoani Mara.

Pia, amezungumzia suala la aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema) kurejea nyumbani, kauli yake kuhusu vifo vya Akwilina Akwiline na David Mwangosi na madai kuwa hatoshi katika wadhifa huo.

IGP Sirro amefanya mahojiano maalumu na gazeti hili na kutumia dakika 45 kuzungumza mambo hayo na mengine, akimpongeza Rais Magufuli kwa kipindi cha miaka minne kuwa ameweza kuliimarisha jeshi hilo.

Alisema pamoja na changamoto ikiwemo matukio ya ugaidi yanayoendelea nchini Msumbiji kumnyima usingizi, Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli amekuwa bega kwa bega na jeshi hilo.

Alisema katika kipindi cha miaka minne, Jeshi la Polisi limekuwa imara zaidi, kuna mambo ambayo Rais Magufuli ameyafanya ambayo hayajawahi kufanywa kwa muda mrefu.

“Sisi hatujawahi kununuliwa helikopta tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, lakini Rais Magufuli ameweza kutoa shilingi bilioni 5.3 za kununua helikopta mpya inayotusaidia katika operesheni zetu,” alisema IGP Sirro.

Alisema pia jeshi hilo lilikuwa na changamoto ya sare kwa askari wake na ilifikia kipindi askari wanaazimana sare na wengine kuuziana, lakini Rais Magufuli amelipatia jeshi hilo Sh bilioni 10 kwa ajili ya sare.

Alisema Chuo cha Polisi Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam ni cha muda mrefu na kwamba awali kilikuwa chini ya jeshi baadaye wakapewa Polisi.

Alisema chuo hicho kilikuwa cha mbao na kimechoka, lakini sasa wamejenga majengo mawili ya ghorofa mbili baada ya Rais Magufuli kuwapatia Sh milioni 700.

“Vitu vingi sana ametuboreshea na kuhakikisha jeshi linafanya kazi kwa weledi, mkitaka kujua jeshi letu lipoje angalia matokeo ya Kibiti na Rufiji, mpaka Mtwara,” alisema mkuu huyo wa Jeshi la Polisi.

“Hali ingekuwa mbaya si unaona Msumbiji wamepeleka mpaka Warusi kwenda kusaidia, kwa hiyo unaweza kutofautisha jeshi letu la Polisi na majeshi mengine, kwa sababu ya mkono wa Amiri Jeshi Mkuu na maelekezo yake, hakupenda kuona watu wake wapate matatizo, imesaidia kwa kiasi kikubwa” alisema.

Alisema pia Rais Magufuli alilipatia jeshi hilo Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba za Polisi nchi nzima.

Ugaidi Msumbiji wamnyima usingizi IGP Sirro alisema mauaji yanayoendelea nchini Msumbiji na utekaji wa vijiji nchini humo, vinamnyima usingizi, kwani wanaofanya vile wengi wanatoka Tanzania.

“Mashaka yangu ni kuwa wale walioenda Msumbiji watakuja kutusumbua, intelijensia yetu na wale tuliowakamata wanasema wanaenda Msumbiji kujiimarisha kisha warudi,” alisema IGP.

Alisema jeshi lake limeshawakamata watu 104 wanaoshukiwa kuwa waasi, wanaopanga kuanzisha ngome yao katika taifa jirani la Msumbiji.

Aidha, alifafanua kuwa jeshi la polisi limeanzisha operesheni dhidi ya wahalifu Mashariki na Kusini mwa nchi na baadhi ya washukiwa walikamatwa, wengine walikufa na wenginewalitoroka.

“Washukiwa waliokamatwa walipohojiwa wamesema walikuwa wanakwenda Msumbiji kujiunga na makundi ya wapiganaji wenye misimamo mikali.

“Mashambulizi takriban 40 yamefanyika tangu Oktoba mwaka jana katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji ambalo liko mpakani na Tanzania. Zaidi ya watu 100 wameuawa katika mashambulizi hayo, wasiwasi wangu kule wanajenga ‘base’, watarudi, inabidi tujizatiti hasa na hilo ndilo linalonikosesha amani,” anasisitiza.

Wizi wa mifugo Tarime Alisema matukio mengine yanayomnyima usingizi ni wizi wa mifugo wilayani Tarime Mkoa wa Mara, ambayo mingi inaenda Kenya.

IGP Sirro anasema jeshi hilo ni lazima wafanye mkakati kudhibiti, kwani mtu anapoibiwa ng’ombe watano ni kumuingiza kwenye umaskini.

Aonya maandamano wakati wa uchaguzi Alisema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24, mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2020, wameimarisha jeshi vizuri. Alisema hawatapuuza uchaguzi uwe mdogo au mkubwa na kwamba wamejipanga vizuri.

Alisema kila mkoa wameweka madawati ya uchaguzi, ambayo yanatoa elimu na pili wale wachache watakaovunja sheria watawashugulikia.

“Sasa tunakwenda katika uchaguzi, hatuwezi kupuuza, ili tuweze kwenda vizuri lazima kuwa na mpango mkakati wa kuzuia na kupambana na wale watakaoleta uhalifu wa kuvuruga,” alisema IGP Sirro.

Aliongeza, “Angalizo kuna watu bila kufanya fujo, bila kuleta ujanja ujanja hawawi na amani, tutawashugulikia na askari wameshajipanga na wana vifaa vya kisasa.

“Tumejiimarisha vizuri na sisi hatupuuzi uchaguzi uwe mdogo au mkubwa, tumejipanga vizuri na kila mkoa tumeweka madawati ya uchaguzi; kwanza kutoa elimu na pili wale wachache watakaovunja sharia tutawashughulikia.

“Angalizo kuna watu bila kufanya fujo, bila kuleta ujanja ujanja hawawi na amani, tutawashughulikia na askari wameshajipanga na wana vifaa vya kisasa, atakayefanya fyoko tutamshughulikia kikamilifu.”

Maandamano “Kuna wale wanaopenda kuandamana na mawe yanarushwa, nashangaa wanaosemaga polisi wanatumia nguvu kubwa huwa siwaelewi, semeni tunatumia nguvu ya kadri, mnapoandamana bila kibali ni makosa, maana yanakuwa sio ya amani, ni maandamano mabaya.

“Niwasisitize tu, wakati wa uchaguzi mtu asithubutu kuandamana, nitakushughulikia pale pale, kama ni suruali yako itachanikia pale pale kabla hujafika mbali na kwenda kuleta madhara kwa watu wasio na hatia,” alisisitiza.

Fitna, chuki majungu

IGP Sirro alisema ili jeshi lifanye kazi vizuri, lazima wawe kitu kimoja, kwani kukiwa na chuki na majungu, kazi haziwezi kwenda vizuri.

“Sitoi nafasi kwa mtu au kikundi cha watu kuwa na chuki na majungu, kazi yetu kama jeshi inahitaji upendo ili mambo yaende, mimi ni kiongozi na watu ninaowaongoza ni wengi, najua sio mkamilifu na siwezi kupendwa na watu wote.

“Nilipoongea pale Bwalo la Polisi nilikuwa natoa angalizo, hata nilipomtaja RPC wa Kinondoni, sikumanisha yeye ndio analeta majungu, nilipitisha tu ujumbe kwake.

“Kuna watu wana tabia za majungu majungu, ndio nilikuwa nawapa tahadhari na kuwakumbusha kaulimbiu yetu; ‘Umoja wetu ndio Nguvu yetu. Kama hatuna umoja na upendo, kazi itakuwa ngumu.

Akijibu swali kuwa kupitisha ujumbe kwa mwingine ndio majungu kwa nini asiwe wazi, IGP Sirro alisema, “Mimi ni kiongozi, na kiongozi lazima uongee kwa mifano, pale nilikuwa natoa mifano tu, jeshi letu tunapendana sana.” A

jigamba anatosha

u-IGP “Ninapojitathmini naona natosha tena sana, kama wapo wanaodai sitoshi ni kwa chini chini tu, lakini kazi yetu hatufanyi ndani ya chumba, hatujifungii ukiteuliwa IGP hujapitia vitengo vyote ndio utaambiwa hutoshi.

“Lakini mimi nimepita sehemu mbali mbali kabla ya kuteuliwa IGP, binafsinajiona natosha sana, kama kuna binadamu wachache wanafikiria hivyo, nawaambia tu mimi nipo vizuri na naamini Watanzania wanajua,” anasema Sirro aliyeteuliwa kushika wadhifa huo Mei 28, 2017 akimbadili Ernest Mangu, ambaye ilielezwa kuwa atapangiwa kazi nyingine.

Mangu sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Kabla ya uteuzi wa kuwa IGP, Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akiwa na cheo cha Kamishna wa Polisi.

Asema amedhibiti ujambazi, mauaji, ajali “Nilipoingia ujambazi ulikuwa juu hasa kwenye mitandao ya simu, na uvamizi wa vituo vya polisi na kutekwa silaha na watu kuuawa lakini matukio hayo yamepungua.

“Changamoto nyingine niliyokutana nayo ni watu wa Kibiti, watu walikuwa wanakufa sana, lakini sasa Kibiti hata viwanja vimepanda bei, naona kuna kitu kimefanyika. “Sasa jeshi letu si legelege na kila mtu anaona umoja wetu ndio nguvu yetu na umoja ndio umetusaidia.

“Ajali barabarani tumepunguza asilimia 47, haya ni mafanikio, lakini bado tunaendelea kupambana kuhakikisha tunazipunguza kwa asilimia ndogo zaidi.

“Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo nikijitathmini naona natosha kwa asilimia zote, ingawa watu wa nje ndio wataweza kunitathmini vizuri zaidi,” alisema IGP.

Amwita nyumbani Tundu Lissu Akizungumzia suala la aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ambaye anaishi ughaibuni kwa sasa tangu alipojeruhiwa kwa risasi jijini Dodoma mwaka 2017, IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi linafahamika kazi zake ni kulinda watu na mali zao, hivyo Lissu ni Mtanzania na akishakuja ni wajibu wao kama Jeshi la Polisi, kumlinda na kuhakikisha anakuwa salama.

“Lissu na dereva wake tunawahakikisha usalama watakaporejea nchini, na pia itakuwa vizuri tukapata maelezo yao ya kina kwa aliyotendewa Lissu. Bila kupata maelezo kwa kina tunashindwa kupata mahali pa kuanzia, na pia dereva wake bila kumhoji kwa kina tunashindwa kupata pa kuanzia.

“Kesi yoyote ya jinai inahitaji ushirikiano, kama hatujapata tutaanzia wapi?” alihoji.

Aliongeza, “Bahati nzuri kesi ya jinai huwa haifi, siku akirudi na bahati nzuri ameshakuwa mzima na anatembea, naamini atatusaidia na tutapata majibu, na haki itatendeka.”

Kigoma kinara wa uhalifu IGP Sirro alisema operesheni ambayo rais aliagiza ifanyike kukabiliana na uhalifu hasa kambi za wakimbizi, imezaa matunda kwani usiku wa kuamkia Oktoba 31, mwaka huu kwenye misitu ya Biharamulo waliua majambazi wanne, na kupata silaha aina ya AK47 na risasi nane.

Alisisitiza kuwa operesheni inaendelea Kagera na Kigoma.

Alisema Mkoa wa Kigoma bado unasumbua kwa uhalifu, hasa wa kutumia silaha sababu ya kambi za wakimbizi, ingawa alieleza kuwa matukio yamepungua kwa asilimia kadhaa, ukilinganisha na siku za nyuma ambako yalikuwa mengi.

Hata hivyo, alisema lazima waongeze nguvu, na tayari wamepeleka askari wa kutosha na wanaendelea kufanya hivyo. Matukio ya ubakaji IGP Sirro alisema matukio ya ubakaji na kulawiti, yamekithiri na ndiyo yanayoshika kasi sana kwa sasa nchini.

Alisema hiyo inatokana na uelewa wa watu, kwani wakifanyiwa vitendo hivyo wanaripoti polisi, tofauti na siku za nyuma ambako watu walikuwa wanaona aibu.

Matukio ya ubakaji yameongezeka Tanzania katika kipindi cha Desemba 2015 kutoka 394 hadi kufikia 2,984 kwa Desemba 2017 ambalo ni ongezeko la matukio 2,590.

Alisema jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wengine, limechukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kuanzishwa kwa kamati za 10,988 ulinzi wa wanawake na watoto, na vikundi vya malezi 1,184 ikiwa ni pamoja na kuweka madawati ya jinsia kwenye vituo vya Polisi.

“Pamoja na adhabu kali ambazo zimekuwa zikitolewa ingefaa watu waogope kujihusisha na vitendo vya ubakaji na ulawiti, lakini vitendo hivyo vimeendelea kuongezeka,” alisema Sirro.

Kwa mujibu wake, wanaofanya matukio hayo wengi huwa wanatoka karibu na familia au ni ndugu wa watoto.

Alisema uhalifu mwingine uliongezeka ni mauaji yanayotokana na ulevi, na mapenzi, “Viongozi wa dini watusaidie kama unamkuta mwanamke wako anaenda na mwanamume mwingine ni bora kuachana naye sio kumuua, ni mauaji ambayo Jeshi la Polisi peke yake haliwezi, viongozi wa dini, wanasiasa watusaidie,” alisema.

Takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka 2016 hadi Mei 2018 zinaonesha wanandoa 341 wameua wenza wao.

Mikoa ya Geita, Singida, Mbeya, Mwanza, Tabora, Kagera, Songwe, Dodoma na Njombe, ndio iliyongoza kwa wanaume kuua wake zao wakati kwa upande wa wanawake kuua waume zao katika kipindi hicho mikoa iliyoongoza ni Tabora, Shinyanga, Kagera, Mwanza na Singida.

Uvamizi benki

Sirro anasema uvamizi na kuvunja kwenye mabenki umeisha, na hiyo inatokana na Jeshi la Polisi kuimarishwa zaidi pamoja na kushirikiana na wadau wengine wa ulinzi na usalama, wananchi pia wamekuwa wakitoa taarifa nyingi.

“Wengi tumewakamata na wengine wametangulia mbele za haki wakati wa kuwakamata,na imefanikuwa kutokana na ushirikiano wa wananchi wamekuwa wakitupa taarifa nyingi sana za uhalifu,” alisema.

Wizi wa mtandaoni Alisema uhalifu wa mitandao bado unasumbua kwani ni makosa ambayo ni mageni, na makosa yake yanavuka mipaka.

Anasema ndio maana wamewapeleka askari nje ya nchi kupata mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu wa Interpol, ambao wanakuja kuwapa mafunzo maalumu. Azory yupo?

Akijibu swali kuhusu alipo mwandishi huyo aliyekuwa akiripoti kutoka Rufiji mkoani Pwani, IGP Sirro alisema “Ni suala gumu kusema yupo au hayupo, maana tunasema ametekwa, nani aliyemteka, au ameenda kusaka maisha yake. Kama kuna mtu ana ushahidi atupe, jalada tumeshafungua.

“Sina jibu moja kwa moja, tupo tayari kupokea ushahidi wowote kusaidia jambo lolote,” alifafanua IGP Sirro.

Chanzo: Habari leo

1573708038738.jpeg
 
View attachment 1262709
Huyu na muroto wanawaza kuwachakaza wananchi tu, hawana mawazo ya maana hata kidogo
 
Aibu sana kwa IGP kutoa kauli kama hizi siasa ina masharti yake na sheria zake. Jee kufanya maandamano ni kinyume na sheria? Kama serikali haitoi haki kwa wananchi wake kuna ubaya wananchi kuonesha hasira zao juu ya serikali yao?.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Tanzania usipokuwa mwanachama wa CCM wewe ni 2nd class citizen.
 
Hela anazotoa Mh Rais ni hizozo ambazo jeshi la polisi limekusanya, utakuta kwa mwaka linakusanya pesa nyingi ambazo Mh huzirusisha kwao na wao huona kama wanasaidiwa lkn in fact ni haki yao ile kupata sare, majengo mazuri ila kwenye helicopter 5 bil ni nyingi sana.

Hizo hela zingetosha kusaidia wananch kule mtama wanaoteseka na adha ya maji wakiamka asubuhi na mapema. Magari yana tosha, na sidhani kama Kuna taasisi ya serikali inayoongoza kuwa na magari mengi kama polisi haswa kwa upande wa kanda maalum ya Dar.
 
Suala la mauwaji yanayoendelea sasa hivi (Hususani ambayo yametokea wiki hii) ameongelea?

Kuna mauwaji yanaendelea Huko Tandahimba na Serikali inafanya siri, hali ya kuwa watu wanapoteza ndugu zao.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom