Mallya wa Wangwe afungwa miaka 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mallya wa Wangwe afungwa miaka 3

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtanzania, Mar 18, 2009.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mallya wa Wangwe afungwa miaka 3
  Martha Mtangoo, Dodoma
  Daily News; Wednesday,March 18, 2009 @18:36

  Kijana Deus Mallya (27) aliyekuwamo kwenye gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha gari kwa mwendo kasi.

  Hukumu hiyo iliyotolewa leo, ilimfanya wakili aliyekuwa akimtetea, Godfrey Wasonga, kulia mahakamani hapo na kusababisha shughuli za mahakama kusimama kwa sekunde kadhaa.

  Wakili huyo alilia baada ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, Thomas Simba, kusoma vifungu vya kumtia hatiani mteja wake ambaye licha ya kuendesha kwa mwendo kasi, alihukumiwa kwa kuendesha gari bila leseni.

  Hata baada ya hakimu kumaliza kusoma vifungu na kumtaka wakili atoe utetezi kabla ya hukumu, Wasonga alifanya hivyo huku akilia. Katika hukumu yake, Hakimu Simba alisema ameridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka ambao ulitolewa mahakamani hapo.

  Hakimu alisema makosa aliyobainika kuyafanya Mallya, yana adhabu kali, lakini alimpunguzia kutokana na ombi la mshitakiwa. Katika kosa la kuendesha gari kwa mwendo kasi na kusababisha kifo, alisema kwa mujibu wa sheria namba 63 kifungu cha pili (A) adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu jela.

  Alimhukumu pia kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kuendesha gari bila leseni na kusema kwamba adhabu zote zinakwenda pamoja. Kwa mujibu wa hakimu, kifo cha Wangwe kilisababishwa na kubanwa mlango wa gari wakati wa ajali na kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na shahidi upande wa mashitaka namba nne, tano na sita, inaonyesha dhahiri mshitakiwa huyo aliendesha gari licha ya yeye kukana mashitaka hayo.

  Hata hivyo, kabla ya hukumu kutolewa, Wakili Wasonga aliiomba mahakama itoe adhabu ya faini kwa mteja wake ombi ambalo lilitupiliwa mbali na mahakama. Awali, akijitetea kabla ya hukumu, Mallya aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kile alichodai kuwa ana wazazi wanaomtegemea.

  Vilevile alidai kwamba anasomesha yatima na kwamba wapo vijana anaowasaidia kutokana na biashara zake na anamsomesha mdogo wake pia. Akizungumza baada ya hukumu nje ya mahakama, Wakili Wasonga alisema hajawa na uamuzi wa kukata rufaa hadi hapo atakapokaa na mteja wake (Mallya).

  Ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Wangwe na hatimaye kusababisha kijana huyo afungwe, ilitokea Julai 28 mwaka jana saa 2.30 usiku katika eneo la Pandambili, wilayani Kongwa takribani umbali wa kilometa 120 kutoka Dodoma.

  Wangwe alikuwa akitoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ambako pamoja na masuala mengine, alikuwa akienda kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe, Bhoke Munanka. Ajali hiyo ilizusha utata mkubwa baada ya familia ya Wangwe kudai kwamba ndugu yao aliuawa na hivyo kulazimu waite madaktari kufanya uchunguzi kabla ya kuzikwa nyumbani kwake, Kemakorere, Tarime mkoani Mara. Mbunge aliyechukua nafasi yake ni Charles Mwera.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo teknikale amefungwa miaka minne, si mitatu
   
 3. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Imekwisha!!!!!!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama jamaa bado alikuwa anakana kuendesha gari, nani alikuwa anaendesha. Kilichosababisha gari kupata ajali ni nini? Kwenda kasi tu hakusababishi ajali!
   
 5. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na hili ndilo nilikuwa nasema kwamba sio miaka 3 ni 4 ingawa still bado naona kama haitoshi maana hukumu hiyo sidhani kama hata ina chembe ya kuziba pengo la Mh. Wangwe
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,667
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuendesha gari kwa mwendo kasi ni kosa na kuendesha gari bila leseni ni kosa pia. Hivyo malya anastahili kufungwa kma mazingira yote yanaonyesha kuwa alifanya hivyo.
  Lakini hata marehemu Wangwe kama angelikuwa hai alistahili kifungo pia kwa kumpa mtu asiye na leseni gari yake kuendesha na pia kumruhusu kuendesha gari kwa mwendo kasi.
  Na dhani askari wa usalama barabarani wapate fundisho kwamba wabunge wanapofanya makosa ya barabarani wasiachiwe tu bali wachukuliwe hatua. Mimi naamini mara nyingi askari wetu waonapo bendera zinapepea kwenye magari ya hawa waheshimiwa huwa hawana ubavu wa kuwasimamisha hata kama wameona wanatenda makosa. Na hapa ndio chanzo cha ajali za wakubwa wetu walio wengi.
   
 7. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Maiti haulizwi swali, hata akiulizwa haki yake ya kukaa kimya lazima ataitekeleza..

  Kama wange angalalikuwa hai labda angalisema kwamba hakuja kama Mallya alikuwa ana leseni au pia angalisema kwamba hakujua tofouti kati ya learner na full driving license... Hatuwezi kujua ni nini mawazo ya mtunga sheria makini kama marehumu wange alipo mkabidhi ufunguo mtu asiye na leseni...

  Sijui ni Bima gani itawafidia maana Mallya hakuwa na leseni ukiachilia mbali mwendo wa kasi, pia kwamba inaonesha Wangwe alikuwa either reckless kumkabidhi huyo kijana gari... Hii ni contributory death ambayo alijitakia mwenyewe ingawaje ajali ni ajali hata uwe makini vipi itakuja tu...

  Mwisho ni kwamba mallya atatoka gerezani ndani ya miezi Tisa hasa ukizingatia kwamba alikuwepo lupango tangu Julai mwaka jana, na akiwa na tabia nzuri gerezani, na parole bodi ikahesabu siku zake, tutamuona mtaani kabla ya mwisho wa December 2009...Pia ni kweli kifungo chake ni miaka minne technically kwani kosa moja kapewa mvua tatu na lingine mvua moja lakini adhabu yote ina run concurrently..

  Ni hayo tuu wakuu
   
 8. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #8
  Mar 19, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda alisinzia, au walisinzia wote wawili kumbuka ilikuwa usiku. Isitoshe ilisikika Wangwe alikuwa amekunywa dawa na akidai ana malaria. Now we wont know. Weve lost a good opportunity. Wangwe ambaye anajua kuendesha gari na anayelipia bima ya hilo gari kumkabidhi mtu aliendeshe bila kujua kama ana leseni au la ni kutokuwajibika.

  Nafikiri ingekwenda vizuri kama Wakili angemtetea kwa kusema wangwe alikuwa ana hofu ya kuuliwa na hivyo kulazimisha polisi kutetea kwamba ilikuwa ajali. Wangeingia kwa undani kuelezea hasa nini kilisababisha ajali kwa kuwa mwendo tu haitoshi. Mengi zaidi yangewekwa in public. Wakili angejijengea umaarufu kwa njia inayoeleweka sio kwa kutumia chozi-la-Pinda style.

  Mallya ilikuwa afungwe tu. Angekuwa mjanja tangu awali angesema ndio anayo leseni na ilipotea eneo la ajali pamoja na wallet yake. Ni watu wachache sana wanafahamu namba za leseni zao, haingeshangaza akisema haikumbuki hiyo namba. Aliogopa kukamatwa akiendesha gari iliyoua bila leseni ndio maana akasema alikuwa haendeshi. Udhaifu wa polisi wetu upo hapo katika kuweka kumbukumbu za leseni na sio katika ku-prove ulikuwa umekaa kiti gani kwenye gari katika mazingira kama yale.

  Mwandishi wetu wa Daily news naye ameonyesha udhaifu. Alitakiwa aihoji familia ya wangwe kama wameridhika na uamuzi huo. Kuna mjadala mkubwa sana uliubuka mwaka jana kwamba wangwe ameuliwa, na kwa wengine jibu bado halijapatikana. je hii litamaliza mjadala?
   
 9. M

  Mzee wa Kale Member

  #9
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamanda wangu Mallya pole sana kwa yote sheria imechukua mkondo wake na yote hayo ni mambo ya Mungu yameandikwa ni mitihani ambayo tukiwa dunia kama binadamu tuapaswa kuipitia, umeanza maisha mengine gerezani, nakukumbuka hasa tulipokua pamoja kule Libya vituko vyako na hasa tulipokua pamoja ukasahau tiketi yako na pasport yako ndani ya ndege pale Zurich ukamfanya hata Mufti ahangaike kwa ajili yako,

  Ndugu yangu nakupa pole kwa yote na sisi wengine tumejifunza kupitia kwako inabidi tuwe makini sana katika dunia hii,
   
 10. Ntaramuka

  Ntaramuka Senior Member

  #10
  Mar 19, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haya maamuzi ya mahakama bado siyaelewi vizuri! Kama Mallya aliendesha gari kwa mwendo wa kasi na aliendesha bila leseni na hatimaye kusababisha kifo alitakiwa ahukumiwe kwa kosa la kuua, lakini kwa vile hakuua kwa kukusudia moja kwa moja yaani ''without direct intent'' then hii ni manslaughter ambayo kwa kwa mujibu wa sheria yetu ya makosa ya jinai angehukumiwa kifungo cha maisha.
   
Loading...