By Deus F Mallya:
Majibu mengine:
"Inadaiwa kuwa kuna watu waliokuwa 'Nyuma ya pazia' kwenye kesi ile (Ndiyo maana ilifunguliwa wilaya ya Dodoma Mjini badaya ya Kongwa)."
Binafsi sina majibu hapa Duniani. Mimi ni Binaadamu kama walivyo wengine. Pia mimi ni mgumu sana kuzungumza nisichokuwa na uhakuka nacho. Ikiwa wapo waliokuwa 'Nyuma ya pazia' kuzuia lengo langu 2010 (Japokuwa halikuwepo kiukweli) Nilishamwambia Mungu Ashughulike nao.
Kuna mdau hapo juu amesema kuwa 'Atapitishwa' Komu 2015. Naomba kumhakikishia kuwa CHADEMA na CCM ni tofauti kama ilivyo Jehanum na Mbinguni. Maamuzi ya CHADEMA huwa hayafanywi kama ya CCM!.. CHADEMA kuna viongozi, CCM kuna Watawala. Kuna taratibu za kumpata mgombea kwa mujibu wa katiba kwa maana hiyo hata kama nisipogombea/kutokupitishwa kwenye kura ya maoni bado nitakuwa na imani na Kiongozi atakayepitishwa. By the way bado tupo kwenye main road kuelekea M4C nadhani haya si vyema sana kujadili kiundani kwa sasa.
Sote ni ndugu, tatizo ni CCM!.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Mallya huyohuyo akikirarua ccm ambacho ni chama alicho na mahaba ya dhati kwa sasa!