Wageni wa 'ghafla' majumbani mwetu.....

Wageni wa 'ghafla' majumbani mwetu.....

Theboss, baada ya yule mwenye jina la kiume kukuzimia,
umeanza ubahili, embu acha hizo kwanza.
hata mkulima hali mwenyewe, umesikia eeh.
 
LOL! ntakuachia nguo na sefuria za kusugua na mchanga ndo utatia akili hahaha
well,issue yangu mie sio kwenye mchele kwa kweli. ni kuhusu ratiba,ukizingatia maisha yalivyo fasta. unakuta tumetaftana mwaka mzima afu leo ndo tumekubaliana tuonane afu anaingilia mgeni. japokua come to think of it, kama tulikua tunatoka wenyewe tu na sio issue kiviile, basi ugeni wenyewe mjini ni mara moja kwa miaka, nikimuona ndugu wa mwenzangu ama wangu kaingia ghafla tutaangalia upepo. ila kukuachia nyumba wala usishangae, nakupa abc's tu afu huyoo. na kurudi kwangu majaaliwa ujue!
Kumbe ndivyo unavyofanya eh? Next time nikija halafu ukadanganya hivyo nitakujibu poa hamna noma niachie tuu funguo, ukirudi utanikuta. Kwishaney.
 
hahahaha....bujibuji bana wewe ni funga kazi....wakija hivyo poa...kero hapa ni pale ulipojiwekea mazingira ya kupumzika
vp wakija na bia zao na za kwenu? Halafu wawe wamebeba grill na nyama tamu kuliko zote duniani na masala zake pamoja na mapochopocho mengine kwa ajili ya BBQ?
 
Unakuwa mpole tu Boss; utamaduni wetu bado unaruhusu hili bana........................lakini unawapiga vijembe vya utani MARUFUKU kuwakasirikia wageni! Hujui ni Baraka?
 
yaani bosi ni kama umeniona apa ndo yamenikuta saa ivi jamani sina hamu.lakini lazima nitoke nimepanga ngoma kumi ma nusu nawaaga mi nasepa zangu

ukifanya hivyo unadhani watajisikiaje..? yani wataweka vimaneno kinyama na vinaweza kua na impact kubwa yani mpaka ukajuta yani
 
Dah, yalinikuta hayo last sunday nilikuwa njiani natoka kanisani ghafla nikapigiwa cm eti tuko njiani tunakuja kutembea. Kwa vile walinifanyia sapraiz na mm nikawatoa kimasomaso nikawaambia mm na wife tuko kwenye mfungo. Waliondoka wamenununa usipime.

hahaaaa hii ni balaa aseee yani hapa kwaa kuondoka wako hivyo umeshajua kua ni lipi walikua wanafuata dah asee hii ni kali...!
 
Hiyo ni baraka, maana sehemu za outing ziko nyingi sana, ukiona watu wamekuja kwako kufanya outing ya sikukuu yao umshukuru Mungu.
Pia kwenye sikukuu kuna mabalaa mengi sana, kama kuibiwa, ajali na kadhalika, huenda Mungu amekuepusha.

ila hapa kunaukweli mzee wangu.....!
 
halafu wawe wamekuja na One way ticket, wakitegemea ya kurudia utawapa wewe. Mimi huwa nawafukuza mkuu huwezi kuja nyumbani kwangu bila ya kunitaarifu hata chooni ukiingia unapiga hodi sasa inakuwaje wanakuja moja kwa moja kama wanakwenda Muhimbili au kituo cha polisi.
Ndugu zangu na marafiki zangu wananijua huwa simuonei haya mtu hata akiwa Maza lazima ukweli umfikie na mimi huwa siendagi kwa mtu bila ya kumtaarifu

mpaka maza mzee wewe ni nnoumer
 
Mgeni akija nyumbani kwangu bila ya nitaarifu hata kama nipo ndani sifungui mlango na akipiga simu akiniambia nipo nje ndio namwambia sina appointment ya kukutana na wewe na wala sipo nyumbani nimetoka nitarudi kesho. Kama hana Nauli atajua pakuipatia

nigger u seems to be very serious kwenye matumizi mabovu ya hela..? vipi limeshawahi kukutokea hili nini manake mzee unatoa kama vile limeshakupata na uliexecute namna hii....?
 
I am taking my life serious not as a Joke. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi, sasa lazima wakubaliane na matakwa yangu sio unakuja kama unakuja kwako, heshimu nyumba ya mtu kama mimi ninavyoheshimu nyumba zao.
Sitaki Ujinga mimi sio Fisadi Kikwete kuchecheka na Mafisadi, Huwa natoa maamuzi mazito wengi wenu hapa JF hamuwezi

baba wewe ni balaa ninapenda sana nipate misimamo yako kwenye kazi zangu.....!
 
Ukiona wageni wengi kwako ujue unafahamu kuishi vizuri na watu
 
Inaboa kiukweli. Lakini inabidi uvumilivu. Au unatoka na simu yako kwenda sehemu husika
 
theboss hata humu jf una-tongo-zwa ina maana una bahati,
so usishangae ukiona wageni hapo home kwako,
tena mwambie huyo mywife wako awe na moyo mkuu,
hali halisi ndiyo hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom