Wageni wa 'ghafla' majumbani mwetu.....

Nilikuwa zamani wakija wageni wa ghafla kwetu hata kama age zangu, ikifika time za misere yangu nawaaga natoka kidogo kidogo. Nachukulia kuwa hawajanijia mie :]]

ha haa haa hiyo easy ukiwa kwenu
but kwako ni ngumu....labda ujifanye 'umeitwa kazini ghafla'
uwe na kazi ya aina hizo lol
 
vp wakija na bia zao na za kwenu? Halafu wawe wamebeba grill na nyama tamu kuliko zote duniani na masala zake pamoja na mapochopocho mengine kwa ajili ya BBQ?

Hata waje na Nyama za mbinguni nitawafukuza, huwezi kuja bila ya nitaarifu. Niache Shughuli zangu kwa ajili ya wageni wamekuja na Chakula chao? Kwanini wasikae makwao na kula hizo nyama choma zao? au wasiende ufukweli na kuchoma hizo nyama zao?
 
Upo nyumbani kwako umepumzika,ni wikiendi au sikukuu
kama leo.una mipango yako binafsi
labda unataka kulala tu siku nzima
au kutoka na mkeo/mumeo bf/gf so mnavuta vuta mda hivi....

ghafla bin vuu wanaibuka 'wageni ' pengine ndugu zako au wa mwenzio
au tu marafiki na jamaa, wamekuja 'kukutembelea' au
'kusheherekea sikukuu' labda wamekuja na 'watoto wao'
na muelekeo wao ni kushinda hadi jioni ndo warudi makwao.....

dah jamani mimi hili huwa linanikera mno....
siku hizi si kuna simu????inakuwaje jamani??????

nyinyi ikiwatokea mnafanya nini?????????

Alaa rahisi,nakufukuza sina cha swalia mtume mimi. Nimepanga na dume langu la mbegu kutoka wewe unaniletea gozi gozi zako kuja kunitembelea bila taarifa. Nahisi wanaofanya hivyo ni wale wasiojua. Unakwendaje kumtembelea mtu bila taarifa. Usipomkut?
 
Mgeni akija nyumbani kwangu bila ya nitaarifu hata kama nipo ndani sifungui mlango na akipiga simu akiniambia nipo nje ndio namwambia sina appointment ya kukutana na wewe na wala sipo nyumbani nimetoka nitarudi kesho. Kama hana Nauli atajua pakuipatia
 
Hiyo ni baraka, maana sehemu za outing ziko nyingi sana, ukiona watu wamekuja kwako kufanya outing ya sikukuu yao umshukuru Mungu.
Pia kwenye sikukuu kuna mabalaa mengi sana, kama kuibiwa, ajali na kadhalika, huenda Mungu amekuepusha.

Katika hili, ukarimu wa kisukuma umechukua nafasi.safi sana shemejiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, hapa nilipo dada yako anakupigia makofi
 
Ila akija demu bila taarifa, aaaaaaaaaah, hakuna noma kaja kakako unaona noma, mweeeeeeeee! Mi nkiwa sina kitu ndo presha huwa inapanda lakini kama ni fresh, hata ukoo ukija sina noma, mbona mie nimelelewa ktk makuzi ya kuwathamini wageni, waje kwa taarifa au la, haina kwere!
 
Mbona mi napenda sana? Itakuwaje siku ya IDI wewe unapanga kwenda out wakati uwezo wa kupokea watu unao? acha watu waje mchangie kile mlicho nacho, watoto wanakula kwa sinia, wanawake mnapika sufuria kubwa ya pilaw na wanaume wana catch-up sebuleni au garden about mambo yao ya kazini etc. Tena mnakokotana from mskitini tu, straight home kusonga bokoboko! hahahahaha
Natamani Afrodenzi aje asome hapa....
 
watu tupo tofauti
mimi huwa napenda kujua nani na nani wanakuja kwangu
'sio ghafla' ulipanga bajeti ya watu wanne,ghafla una watu kumi na mbili
na wameingia 'lunch time' hadi 'wageni wako' hawa enjoy...
 
Mie huwa kwa kweli wananishangaza wale wanaosombwa kutoka msikitini wakenda majumbani mwa mwengine wakapiga soga mpaka mchana unafika hawajarudi kwa wake zao. Sijui hata wake zao huwa wanafikiria nini! lol
 
watu tupo tofauti
mimi huwa napenda kujua nani na nani wanakuja kwangu
'sio ghafla' ulipanga bajeti ya watu wanne,ghafla una watu kumi na mbili
na wameingia 'lunch time' hadi 'wageni wako' hawa enjoy...
Wacha kujifanya western bwana, siku ya idi ni siku ya familia at large! alafu jioni ukisha wapa nauli ya bus na wakaondoka ndio upange vya rafiki. Itakuaje unajali rafikizako kuliko familia siku ya idi? lol
 
Duh!

Mzalendo unatishaaaaaaa!!

I am taking my life serious not as a Joke. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi, sasa lazima wakubaliane na matakwa yangu sio unakuja kama unakuja kwako, heshimu nyumba ya mtu kama mimi ninavyoheshimu nyumba zao.
Sitaki Ujinga mimi sio Fisadi Kikwete kuchecheka na Mafisadi, Huwa natoa maamuzi mazito wengi wenu hapa JF hamuwezi
 
Mbona mi napenda sana? Itakuwaje siku ya IDI wewe unapanga kwenda out wakati uwezo wa kupokea watu unao? acha watu waje mchangie kile mlicho nacho, watoto wanakula kwa sinia, wanawake mnapika sufuria kubwa ya pilaw na wanaume wana catch-up sebuleni au garden about mambo yao ya kazini etc. Tena mnakokotana from mskitini tu, straight home kusonga bokoboko! hahahahaha
Natamani Afrodenzi aje asome hapa....

RR hii ya kukokotana toka msikitini ni nzuri kwa vile mnafika wote kuwasha majiko ,mnajua mpike nini cha kuwatosha kuliko ile ya ghafla bin vuuu...
Ila long time nilikuwa naona home tunapika chakula kiiingi ili hata akija mgeni wa ghafla inakuwa sio tabu tena labda tuendelee na hiyo fomula1
 
mi nilivyonasura ya mbuzi watasoma tu sura yangu na kujua kama hapo wameniboa, itakuwa juu yao waage au wabaki kiugumu
 
Kama vipi siku ambayo hamtaki wageni mmwe mnaweka bango la kwamba mmehama au kapeti la mlangoni limeandikwa karibu tena wakati mtu anaingia akikutana na ujumbe kama huo na halmashaur ya kichwa chake inafanya kazi ataelewa umemaanisha nini
 
I am taking my life serious not as a Joke. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mdogo, sasa lazima wakubaliane na matakwa yangu sio unakuja kama unakuja kwako, heshimu nyumba ya mtu kama mimi ninavyoheshimu nyumba zao.
Sitaki Ujinga mimi sio Fisadi Kikwete kuchecheka na Mafisadi, Huwa natoa maamuzi mazito wengi wenu hapa JF hamuwezi

hahahaha loooool .......wewe mkareeee!

Hata huko kwako dini, mila na tamaduni zinasema utoe taarifa kuwa unarudi siku fulani :]] (kama ulikuwa mbali kipindi kidogo)

So taarifa kutolewa muhimu
 
RR hii ya kukokotana toka msikitini ni nzuri kwa vile mnafika wote kuwasha majiko ,mnajua mpike nini cha kuwatosha kuliko ile ya ghafla bin vuuu...
Ila long time nilikuwa naona home tunapika chakula kiiingi ili hata akija mgeni wa ghafla inakuwa sio tabu tena labda tuendelee na hiyo fomula1
Ndio hivo. Kuna ambao wamesalia mskiti wa mbali ila watakuja tu. Hakuna mgeni wa ghafla siku ya shughuli kama IDI bwana. Siku hiyo nyumba iko wazi kwa family gathering na watu mnakumbukana, mnajuliana hali na kukumbushana vya zamani. Kuna watu huwaoni zaidi ya siku hiyo sababu ya time schedule. Very nice surprise wakija unexpected!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom