Wageni wa 'ghafla' majumbani mwetu.....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Upo nyumbani kwako umepumzika,ni wikiendi au sikukuu
kama leo.una mipango yako binafsi
labda unataka kulala tu siku nzima
au kutoka na mkeo/mumeo bf/gf so mnavuta vuta mda hivi....

ghafla bin vuu wanaibuka 'wageni ' pengine ndugu zako au wa mwenzio
au tu marafiki na jamaa, wamekuja 'kukutembelea' au
'kusheherekea sikukuu' labda wamekuja na 'watoto wao'
na muelekeo wao ni kushinda hadi jioni ndo warudi makwao.....

dah jamani mimi hili huwa linanikera mno....
siku hizi si kuna simu????inakuwaje jamani??????

nyinyi ikiwatokea mnafanya nini?????????
 
yaani bosi ni kama umeniona apa ndo yamenikuta saa ivi jamani sina hamu.lakini lazima nitoke nimepanga ngoma kumi ma nusu nawaaga mi nasepa zangu
 
Kinachonikera zaidi wamekuja kupiga tu stori, hakuna suala la maana wanaloongea.
 
Duh! poleni sana

Ila walipofika tu ulikuwa uwaambia kuwa "mlikuwa na safari ya kutoka"

Kama wao walivyokuja kuwatembelea na nyingi kuna sehemu/watu mnataka kwenda kuwatembelea
 
ha ha ha hiyi inaitwa 'uso wa mbuzi'
umewahi fanyia mtu hivyo?
 
Upo nyumbani kwako umepumzika,ni wikiendi au sikukuu
kama leo.una mipango yako binafsi
labda unataka kulala tu siku nzima
au kutoka na mkeo/mumeo bf/gf so mnavuta vuta mda hivi....

ghafla bin vuu wanaibuka 'wageni ' pengine ndugu zako au wa mwenzio
au tu marafiki na jamaa, wamekuja 'kukutembelea' au
'kusheherekea sikukuu' labda wamekuja na 'watoto wao'
na muelekeo wao ni kushinda hadi jioni ndo warudi makwao.....

dah jamani mimi hili huwa linanikera mno....
siku hizi si kuna simu????inakuwaje jamani??????

nyinyi ikiwatokea mnafanya nini?????????

Hiyo ni baraka, maana sehemu za outing ziko nyingi sana, ukiona watu wamekuja kwako kufanya outing ya sikukuu yao umshukuru Mungu.
Pia kwenye sikukuu kuna mabalaa mengi sana, kama kuibiwa, ajali na kadhalika, huenda Mungu amekuepusha.
 
Dah, yalinikuta hayo last sunday nilikuwa njiani natoka kanisani ghafla nikapigiwa cm eti tuko njiani tunakuja kutembea. Kwa vile walinifanyia sapraiz na mm nikawatoa kimasomaso nikawaambia mm na wife tuko kwenye mfungo. Waliondoka wamenununa usipime.
 
Mwenzio Juzi kati nimeandaa menu ya watu watatu ghafla bin vuu mida ya saa moja na nusu usiku wageni wanne wanaingia lol tunapiga story hata sioni dalili za wageni kuaga ngoja nikomee hapa The Boss
 
umeona tatizo ni kubwa hili,tulizungumze lol
 
Upo nyumbani kwako umepumzika,ni wikiendi au sikukuu
kama leo.una mipango yako binafsi
labda unataka kulala tu siku nzima
au kutoka na mkeo/mumeo bf/gf so mnavuta vuta mda hivi....

ghafla bin vuu wanaibuka 'wageni ' pengine ndugu zako au wa mwenzio
au tu marafiki na jamaa, wamekuja 'kukutembelea' au
'kusheherekea sikukuu' labda wamekuja na 'watoto wao'
na muelekeo wao ni kushinda hadi jioni ndo warudi makwao.....

dah jamani mimi hili huwa linanikera mno....
siku hizi si kuna simu????inakuwaje jamani??????

nyinyi ikiwatokea mnafanya nini?????????

halafu wawe wamekuja na One way ticket, wakitegemea ya kurudia utawapa wewe. Mimi huwa nawafukuza mkuu huwezi kuja nyumbani kwangu bila ya kunitaarifu hata chooni ukiingia unapiga hodi sasa inakuwaje wanakuja moja kwa moja kama wanakwenda Muhimbili au kituo cha polisi.
Ndugu zangu na marafiki zangu wananijua huwa simuonei haya mtu hata akiwa Maza lazima ukweli umfikie na mimi huwa siendagi kwa mtu bila ya kumtaarifu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom