Haya mambo ya kuarifiana yameanza miaka hii ya teknolojia mpya (simu na mitandao), huko nyuma hata mtu akitoa taarifa kabla ilikuwa ya salamu za mdomo au barua. Lakini ukweli wapo ambao hawatoi taarifa hata wangekuwa na simu ngapi. Kuhusu chakula, "wanachokula watatu wanaweza kula sita, lakini kuna mengine yanaudhi na hayavumiliki.
Mfano ni hilo la wageni kutoka mikoani au vijijini, wanakuja kikundi na watoto wao. Wamekuja na tiketi za kuja, za kurudi utoe wewe. Ukisema uwakomoe usiwape nauli, watabakia hapo miezi; ukitoa nauli, wakirejea walikotoka wataenda kusifia kuwa pesa unazo. Nyumba uliyojenga vyumba vitatu (chako, cha watoto na cha wageni) unashitukia imejaa kama nyumba ya ndege mpaka wengine wanalala sitting. Chooni foleni, wasojua matumizi ya choo wanapakaza vinyesi kila kona; nguo zimezagaa kila pembe...Bujibuji, baraka ya aina hii ninaitilia mashaka.