Wafanyabiashara wa Tanzania wachekelea baada ya kuzinduliwa njia mpya ya meli kati ya China na Dar es Salaam

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
1710917148027.png

Hivi karibuni Tanzania ilizindua njia mpya ya meli ya moja kwa moja kati ya China na Bandari ya Dar es Salaam. Huduma hii mpya ambayo inatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa mizigo kusafiri kutoka China na kuwasili Tanzania, kutoka wiki sita (siku 42) hadi wiki tatu (siku 21), inaonekana ni habari njema zaidi waliyoipokea wafanyabiashara wa nchi hiyo, ambayo bilashaka itaongeza ufanisi wa biashara za Tanzania.

Kusafirisha bidhaa kutoka China kwenda Tanzania ni mchakato muhimu sana kwa wafanyabiashara wanaotaka kuuza bidhaa za China kwenye soko la Tanzania.

Ili kufanikisha mchakato huu, hasa wale wafanyabishara wakubwa wanaonunua bidhaa nyingi kwa pamoja njia pekee inayokidhi mahitaji yao ni njia ya meli.

Hii ni njia nzuri kwa ajili ya bidhaa kubwa na zenye uzito mkubwa, pia ni njia nafuu zaidi kuliko njia nyingine za usafirishaji lakini ina changamoto yake ambayo sasa imepatiwa mwarobaini.

Sasa hivi kumekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabishara wa Tanzania wanaonunua bidhaa zao kutoka China, lakini wengi wa wafanya biashara hawa hulalamikia huduma ya usafirishaji wa meli ambayo kwa kweli inachukua muda mrefu sana, na baaadhi ya wakati kuchelewesha bidhaa zenye uharaka.

Kabla ya msimu wa sikukuu, yaani kuanzia mwezi Disemba hadi Januari, wafanyabiashara wengi wanaonekana kuwa na pilikapilika nyingi za kuja China huku wengine wakiagiza bidhaa wanazohitaji kwenye mitandao mbalimbali ya China.

Lakini ijulikane kwamba kutokana na umbali mrefu sana kutoka China hadi Tanzania, kusafirisha bidhaa kwa njia ya meli hasa kwa wale wanaosafirisha kwenye makontena, kawaida inachukua kuanzia miezi miwili na nusu hadi mitatu.

Waswahili wanasema “safari hatua”, baadhi ya wakati mizigo hii huchukua zaidi ya miezi mitatu na kupelekea machungu makubwa kwa wafanyabishara, hasa wale niliowataja hapo awali ambao wananunua bidhaa zao kwa ajili ya kuuza katika msimu wa sikukuu.

Ucheleweshaji huu wakati mwingine hufanya mzigo kufika baada ya sikukuu kumalizika, na kupelekea bidhaa kudoda madukani huku wafanyabishara wakipata hasara kubwa jambo ambalo linafanya baadhi yao kukata tamaa ya kuendelea kufanya biashara.

Kwa maana hiyo kuanzishwa kwa njia hii ambayo itapunguza muda wa kusafirisha makontena, itakuwa ni faraja kubwa kwa wafanyabishara wa Tanzania, na pia itaongeza zaidi bidhaa za China kwenye soko la Tanzania.

Akitoa maoni yake katika hafla ya uzinduzi wa njia hii mpya ya meli ya moja kwa moja kati ya China na Bandari ya Dar es Salaa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof Godius Kahyarara, alisisitiza umuhimu wa kuvutia shughuli za usafirishaji wa pande hizi mbili, akibainisha kuwa njia hiyo ni hatua kubwa kwa bandari ya Dar es Salaam na ni fursa kubwa ya ustawi wa biashara kati ya Tanzania na nchi za Asia.

Katika uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa Rais Meli Services Tanzania (RSS), Neelakandan naye pia alisema kuwepo kwa meli za moja kwa moja kutoka bandari kubwa za China hadi bandari ya Dar es Salaam kutasaidia kupunguza muda wa kusafirisha mizigo pamoja na kuwahudumia wateja kwa wakati.

Akizungumzia kuhusu ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Tanzania Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, alisema ukuaji wa biashara kati ya nchi hizi mbili kuanzia mwaka 2022 hadi Juni, 2023, umefikia Dola za Marekani bilioni 8.31 sawa na shilingi trilioni 20 za Kitanzania, ikiwa ni zaidi ya mara tatu na nusu ya muongo uliopita, jambo ambalo linaboresha ushirikiano.

Kuongezeka kwa uwekezaji na biashara ya pande mbili kati ya China na Tanzania kumesaidia sana kujenga uchumi wa nchi hizi mbili, kutoa fursa zaidi kwa biashara mpya, na kupambana na ukosefu wa ajira nchini Tanzania.

Hivyo basi bila shaka tunatarajia kwamba uzinduzi huu wa njia ya baharini kutoka China hadi bandari ya Dar es Salaam, utakuwa ni mwanzo tu wa kurahisisha ufanyaji biashara wa nchi hizi mbili.
 
MSAADA:Kuna mtu anaulizia mara namna gani anaweza agiza machine ya kufyatua na kufungasha pipi toka China au kutuma mtu
 
MSAADA:Kuna mtu anaulizia mara namna gani anaweza agiza machine ya kufyatua na kufungasha pipi toka China au kutuma mtu
Ongea na muuzaji alieko China,then nenda kwa kampuni ya usafirishaji wao unaweza wapatia pesa wakakununualia huko,kwa sharti la kusafirisha hio machine kwa kampuni yao.
 
Na sisi tunawauzia nini wao, au ndo tumekuwa dampo la bidhaa zao, wao wanakuza thamani ya pesa yao sisi maviongozi yetu yanachekelea bila kuchukua hatua za kuwezesha na sisi tuwauzie chochote ili iwe win win situation.
 
Back
Top Bottom