Kwanini Barabara mpya kwa Jiji la Dar es Salaam zinajengwa kwa njia 4?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Kipimo cha uwezo wa mwanadamu kama anafikiri sawasawa ni namna anavyofanya mambo yake kulingana na wakati husika.

Dar es Salaam ndo Jiji Kuu la Biashara la Tanzania. Sio hivyo tu, ndo Jiji lenye watu wengi zaidi Tanzania na kadri siku zinavyozidi kwenda idadi ya watu inazidi kuongezeka.

Kwa binadamu ansyefikiri sawasawa, sikutegemea kama katika karne hii ya 21 tena mwaka 2023 kwenye Jiji hili barabara kuu zingeendelea kujengwa kwa njia 4.

Nipo Dar es Salaam na nimesikitishwa sana maana imejengwa barabara mpya kabisa kutoka mbagala hadi posta ila bado imejengwa kwa njia 4( mbili kwenda na mbili kurudi na katikati mwendokasi). Nimetembea pia njia ya kutoka Posta hadi Uwanja wa ndege nimeona ujenzi unaendelea na hali ni hiyo hiyo.

Swali langu kwenu Viongozi wa Tanzania. Je uwezo wenu wa kufikiri ndo umeishia hapo?

Kwa namna Jiji hili lilivyo na linavyotakiwa kuwa yaaani kama Jiji bora na la mfano Afrika Mashariki na Kati, nilitegemea barabara hizi kujengwa kwa Njia 6 hadi 8 pamoja na mwendokasi.

Kiufupi barabara zote kubwa za Dar zinazoingia Posta kuelekea Kibaha, Pugu, Mbagala, Bunju na inayotoka Morroco hadi Keko bila kusahau ya Mwenge- Ubungo hadi Bandarini zinatakiwa kuwa za njia 3 mpaka 4 kila upande na njia ya mwendokasi/ treni ya umeme katikati.

Ifike wakati nchi hii watu tufikiri kama tunaishi katika dunia wanayoishi wenzetu warabu na nchi za ulaya. Inasikitisha sana kuwa na mipango ya mwaka 1950/ 60 katika karne hii ya 21.

Naomba Viongozi wa Tanzania mbadilike kwa kweli.
 
Utaambiwa bajeti
Hakuna na bajeti ni uvivu wa kufikiri. Miradi hii inajengwa kwa fedha za mikopo sasa kwa nini tusikope fedha za kutosha na tukafanya jambo kwa kumaliza kabisa? Unaweza kuta baada ya miaka 4-5 unasikia wanaongeza ukubwa tena wa barabara ile ile waliyojenga.
 
Kiufupi barabara zote kubwa za Dar zinazoingia Posta kuelekea Kibaha, Pugu, Mbagala, Bunju na inayotoka Morroco hadi Keko bila kusahau ya Mwenge- Ubungo hadi Bandarini zinatakiwa kuwa za njia 3 mpaka 4 kila upande na njia ya mwendokasi/ treni ya umeme katikati.
Umeangalia kama kuna nafasi ya kutosha pembeni kuwezesha huo upanuzi wa njia 8?
 
Ile barabara ya Kimara-Kibaha imejengwa njia 6 na katikati 2 za mwendokasi, jumla 8

Siku hizi ukitoka Kimara kwenda Kibaha hakuna foreni kabisa ukiwa na private kusimama ni kwenye mataa tu

Ilitakiwa barabara zote kuu za jiji zinazoingia city centre angalau ziwe kama hiyo ya Kimara-Kibaha
 
hizo fedha za kujenga barabara sijui 10 dargiza, kwa nini wasijenge kwingine mikoani ambako hata barabara hakuna? watu kama wewe ndiyo mnaoibakiza hii nyuma, sasa mji umezidiwa kwa sababu kila kitu kinafanyika dar, wangewekeza mikoani na wilayani wengi wangeishi huko na maisha hangekuwa bora zaidi kwa kila mtu …
 
Kiuchumi unaweza fananisha mchango wa Dar es Salaam na hiyo mikoa mingine?
 
Kipimo cha uwezo wa mwanadamu kama anafikiri sawasawa ni namna anavyofanya mambo yake kulingana na wakati husika.

Dar es Salaam ndo Jiji Kuu la Biashara la Tanzania. Sio hivyo tu, ndo Jiji lenye watu wengi zaidi Tanzania na kadri siku zinavyozidi kwenda idadi ya watu inazidi kuongezeka.

Kwa binadamu ansyefikiri sawasawa, sikutegemea kama katika karne hii ya 21 tena mwaka 2023 kwenye Jiji hili barabara kuu zingeendelea kujengwa kwa njia 4.

Nipo Dar es Salaam na nimesikitishwa sana maana imejengwa barabara mpya kabisa kutoka mbagala hadi posta ila bado imejengwa kwa njia 4( mbili kwenda na mbili kurudi na katikati mwendokasi). Nimetembea pia njia ya kutoka Posta hadi Uwanja wa ndege nimeona ujenzi unaendelea na hali ni hiyo hiyo.

Swali langu kwenu Viongozi wa Tanzania. Je uwezo wenu wa kufikiri ndo umeishia hapo?

Kwa namna Jiji hili lilivyo na linavyotakiwa kuwa yaaani kama Jiji bora na la mfano Afrika Mashariki na Kati, nilitegemea barabara hizi kujengwa kwa Njia 6 hadi 8 pamoja na mwendokasi.

Kiufupi barabara zote kubwa za Dar zinazoingia Posta kuelekea Kibaha, Pugu, Mbagala, Bunju na inayotoka Morroco hadi Keko bila kusahau ya Mwenge- Ubungo hadi Bandarini zinatakiwa kuwa za njia 3 mpaka 4 kila upande na njia ya mwendokasi/ treni ya umeme katikati.

Ifike wakati nchi hii watu tufikiri kama tunaishi katika dunia wanayoishi wenzetu warabu na nchi za ulaya. Inasikitisha sana kuwa na mipango ya mwaka 1950/ 60 katika karne hii ya 21.

Naomba Viongozi wa Tanzania mbadilike kwa kweli.
Peleka watoto Ibiza,nunua gari Kali achana na hao watu wnaitwa wanasiasa watakuua
 
Ibiza wataenda tu ila siku ya mwisho Tanzania ndo nyumbani. Hawa watu akili zao zinatupa mashaka sana tunaotembea duniani huko! Wanafanya vitu kama hawana akili kusema kweli
 
Kiuchumi unaweza fananisha mchango wa Dar es Salaam na hiyo mikoa mingine?

unafikiri ni kwa nini iwe hivyo labda? >60% ya wakazi wa dargiza hawajazaliwa dar wametokea mikoani na kila siku wanamiminika, wataishi wapi? watatibiwa wapi? maji safi ya kunywa hakuna, mwendo kasi imezidiwa tatizo hili likitatuliwa kesho wanaingia watu laki moja na wanakuja kimoja mnarudi palepale, zima moto ni moja kwa mji mzima na tangia ukoloni mtu anaishi tegeta km 20 ktk city nyumba ikiwaka moto zimamoto isafiri km 20 kwenda kuzima moto uliona wapi hili? hivyo hata wajenge br njia 20
zitajaa pia maadamu huko kwingine hakuna fursa yoyote …
 
Ile barabara ya Kimara-Kibaha imejengwa njia 6 na katikati 2 za mwendokasi, jumla 8

Siku hizi ukitoka Kimara kwenda Kibaha hakuna foreni kabisa ukiwa na private kusimama ni kwenye mataa tu

Ilitakiwa barabara zote kuu za jiji zinazoingia city centre angalau ziwe kama hiyo ya Kimara-Kibaha
Pamoja na mapungufu ya Magufuli ila alijaribu sana kutupa akili ya kuwaza tofauti ili kupata matokeo mazuri.

Barabara ya Kimara- Kibaha ni mfano tosha namna alivyotaka tuanze kufanya vitu kwa muono wa kitofauti ila shida hakuna anayetaka kufanya hivyo.

Kwa sasa barabara zote kubwa za Dar hazipaswi kabisa kuwa za njia 4. Ni matumizi mabaya ya fedha za umma na kuitia hasara serikali kujenga barabara kuu kwa njia 4 jijini Dar es Salaam.
 
Kipimo cha uwezo wa mwanadamu kama anafikiri sawasawa ni namna anavyofanya mambo yake kulingana na wakati husika.

Dar es Salaam ndo Jiji Kuu la Biashara la Tanzania. Sio hivyo tu, ndo Jiji lenye watu wengi zaidi Tanzania na kadri siku zinavyozidi kwenda idadi ya watu inazidi kuongezeka.

Kwa binadamu ansyefikiri sawasawa, sikutegemea kama katika karne hii ya 21 tena mwaka 2023 kwenye Jiji hili barabara kuu zingeendelea kujengwa kwa njia 4.

Nipo Dar es Salaam na nimesikitishwa sana maana imejengwa barabara mpya kabisa kutoka mbagala hadi posta ila bado imejengwa kwa njia 4( mbili kwenda na mbili kurudi na katikati mwendokasi). Nimetembea pia njia ya kutoka Posta hadi Uwanja wa ndege nimeona ujenzi unaendelea na hali ni hiyo hiyo.

Swali langu kwenu Viongozi wa Tanzania. Je uwezo wenu wa kufikiri ndo umeishia hapo?

Kwa namna Jiji hili lilivyo na linavyotakiwa kuwa yaaani kama Jiji bora na la mfano Afrika Mashariki na Kati, nilitegemea barabara hizi kujengwa kwa Njia 6 hadi 8 pamoja na mwendokasi.

Kiufupi barabara zote kubwa za Dar zinazoingia Posta kuelekea Kibaha, Pugu, Mbagala, Bunju na inayotoka Morroco hadi Keko bila kusahau ya Mwenge- Ubungo hadi Bandarini zinatakiwa kuwa za njia 3 mpaka 4 kila upande na njia ya mwendokasi/ treni ya umeme katikati.

Ifike wakati nchi hii watu tufikiri kama tunaishi katika dunia wanayoishi wenzetu warabu na nchi za ulaya. Inasikitisha sana kuwa na mipango ya mwaka 1950/ 60 katika karne hii ya 21.

Naomba Viongozi wa Tanzania mbadilike kwa kweli.
Mtanikumbuka ndio angekuwa na uwezo wa kufanya
 
unafikiri ni kwa nini iwe hivyo labda? >60% ya wakazi wa dargiza hawajazaliwa dar wametokea mikoani na kila siku wanamiminika, wataishi wapi? watatibiwa wapi? maji safi ya kunywa hakuna, mwendo kasi imezidiwa tatizo hili likitatuliwa kesho wanaingia watu laki moja na wanakuja kimoja mnarudi palepale, zima moto ni moja kwa mji mzima na tangia ukoloni mtu anaishi tegeta km 20 ktk city nyumba ikiwaka moto zimamoto isafiri km 20 kwenda kuzima moto uliona wapi hili? hivyo hata wajenge br njia 20
zitajaa pia maadamu huko kwingine hakuna fursa yoyote …
Haya uliyoyasema ndo yanaunga mkono hoja yangu kuwa jiji hili ni vizuri kuwa na miondombinu sahihi mfano hizo barabara za njia 6 hadi 8.

Kwa kurahisisha shughuli kwenda vizuri na uchumi kwenda sawia hakuna budi kujenga barabara kubwa zaidi kwa njia kuu ili kurahisisha shughuli za uchumi ambapo mapato yataongezeka zaidi na kwenda kuhudumia sehemu nyinginezo.
 
Pamoja na mapungufu ya Magufuli ila alijaribu sana kutupa akili ya kuwaza tofauti ili kupata matokeo mazuri.

Barabara ya Kimara- Kibaha ni mfano tosha namna alivyotaka tuanze kufanya vitu kwa muono wa kitofauti ila shida hakuna anayetaka kufanya hivyo.

Kwa sasa barabara zote kubwa za Dar hazipaswi kabisa kuwa za njia 4. Ni matumizi mabaya ya fedha za umma na kuitia hasara serikali kujenga barabara kuu kwa njia 4 jijini Dar es Salaam.
Ni kweli, barabara kuu za jiji kuweka njia 4 ni kosa kubwa sana na matumizi mabaya ya pesa na akili
 
Wanafanya hivyo mikaka michache ijayo wapige tena.

Kwani world bank si watu kama watu wengine? Unafikiri hakuna wapigaji mule?
 
Back
Top Bottom