TPA: Hakuna Mgomo katika Bandari ya Dar es Salaam

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Jumapili Machi 03, 2024 kupitia mitandao ya kijamii na makundi sogozi, zilisambaa taarifa za kudorora kwa utendaji kazi ya kuhudumia Meli na Shehena katika Bandari ya Dar es Salaam kunakohusishwa na mgomo wa wafanyakazi wenye madai mbalimbali likiwemo kufutiwa mikataba yao ya kazi.

Kufuatia taarifa hiyo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao, Kwanza, hakuna mgomo wala hujuma zozote katika Bandari ya Dar es Salaam na badala yake kazi za uhudumiaji Meli na Shehena zinaendelea kutekelezwa ipasavyo katika Magati yote kwa mujibu wa taratibu za shughuli za Bandari.

Pili, hakuna Mtumishi yeyote wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). (Mtumishi wa ajira ya kudumu au Mtunishi wa ajira za muda maalum) aliyesitishiwa mkataba wake kwa sababu zozote zile. Watumishi wote Wanatimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuzingatia ratiba za sehemu zao za kazi.

Tatu, Menejimenti ya TPA inatimiza ipasavyo jukumu lake la kusimamia kikamilifu utendaji wa ldara na Vitengo vyote vya operesheni za kibandari katika Bandari ya Dar es Salaam kwa saa 24 ili kuhakikisha kuwa, huduma zinatolewa kwa Weledi, kasi na ufanisi wa hali ya juu wakati wote huku Mkurugenzi wa Bandari na Wakuu wa ldara na Vitengo wakipatikana muda wote katika sehemu zao za kazi na kupitia Mawasiliano ya Simu.

Nne, Mamlaka imejiwekea utaratibu wa kuchapisha taarifa za mwenendo wa uhudumiaji Meli Bandarini ili kuwapa Wateja na Wadau taarifa sahihi wakati wote. Taarifa hizi zinaeleza idadi ya Meli zinazohudumiwa gatini, Meli zilizo nje zikisubiri kuingia (Outer Anchorage) na Meli zilizokwisha hudumiwa na kuondoka. Hakuna Meli zinazohudumiwa kinyume na utaratibu huu.

Tano, kutokana na tabia iliyojengeka siku za hivi karibuni ya Watu wasio na nia njema kuzua taharuki kwa kusambaza Habari za uongo zinazochafua taswira njema ya TPA mbele ya Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla, Mamlaka imejjpanga kuanza kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaobainika kuhusika na upotoshaji huu.

TPA inawasihi Wateja na Wadau wake wote kuendelea kutumia huduma za Bandari ya Dar es Salaam na Bandari zote za TPA bila shaka yoyote kwa kuwa Mamlaka imejipanga vyema kuendelea kutoa huduma bora wakati Wote na kutatua kwa haraka changamoto zote zinazojitokeza kwa kushirikiana na Wadau wote wanaohusika na uondoshaji wa Shehena Bandarini.

Aidha, TPA inaendelea kukaribisha taarifa zote kuhusiana na huduma zake kupitia njia rasmi za Mawasiliano za Mamlaka ambazoni Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo ghorofa ya 6 katika Jengo la Makao Makuu ya TPA (One Stop Centre). Mawasiliano pia yanapokelewa kupitia simu ya bure kwa namba 0800-110032, Barua pepe kwa anuani ya customercare@ports.go.tz, Tovuti www.ports.go.tz na kurasa rasmi za Mitandao ya kijamii ya Instagram, X (Twitter) na facebook kwa jina @tpa_tz, kwa saa 24.

Imetolewa na; Kurugenzi ya Masoko na Uhusiano; TPA-Makao Makuu.

IMG-20240304-WA0004.jpg
IMG-20240304-WA0002.jpg
IMG-20240304-WA0003.jpg


Pia, woma; Tetesi: - Kuna mashaka Bandarini. Serikali itoe tamko ya kinachoendelea ili kama yanayoripotiwa ni tetesi yasilete taharuki
 
Sawa, sisi yetu macho mwisho wa siku ukweli huwa una tabia ya kushinda. Kwa hiyo acha iendelee kuvuja panapovuja ni rahisi sana kupaona
 
Jamii imepewa wito wa kupuuza taarifa zinazoenea hivi karibuni zikieleza kuwa shughuli za uendeshaji katika Bandari ya Dar es Salaam zimesimama badala yake inapaswa kufahamu kuwa Bandari hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa saa 24 tena ikitumia teknolojia ya kisasa katika kurahisisha zoezi la utoaji wa huduma.

Akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia leo, Jumatatu, Machi 04.2024 akiwa Bandarini hapo Afisa utekelezaji Bandari ya Dar es Salaam kutoka idara ya Kichere Agapi Kasebele amesema Bandari hiyo haijawahi kusimamisha shughuli zake kwa sababu yoyote ile badala yake imekuwa ikiongeza wigo wa utoaji huduma kwa kutumia teknolojia ambazo zinasaidia wateja na wadau wa Bandari kwa ujumla wake kuhudumiwa kwa haraka tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Amesema idara hiyo ya Kichere ambayo kwa kawaida inahusika na ushushaji wa mizigo kama vile Ngano, Sulphur, Mbolea nk kwa usiku huo pekee imekuwa ikishusha shehena ya Ngano ya tani 46,000 (Elfu Arobaini na Sita), ambayo kwa shifti moja (1) inashusha tani 3,000 (Elfu Tatu), huku kwa siku moja ambayo inahusisha shifti tatu (3) inaweza kushusha tani kati ya 9,000 (Elfu Tisa) hadi 10,000 (Elfu Kumi) huku akibainisha kuwa meli hiyo ya tani 46,000 inamaliza kushusha mzigo kati ya siku nne (4) hadi tano (5).

Kwa upande wake Mahmoud Ramadhan Makanyaga ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Shipping line (Chinese - Tanzania Shipping Company) ameupongeza uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kufanikisha urahisishaji wa kazi kwenye eneo hilo kwa kuwa kwa sasa meli zao zimekuwa zikimaliza kushusha mzigo kwa haraka pindi zinapotia nanga Bandarini hapo.

Ametolea mfano kuwa moja ya meli wanayoifanyia kazi iliyoingia Februari 28 mwaka huu ikiwa imebeba mizigo mchanganyiko, kwa sasa inamalizia kushusha mzigo kisha iondoke kurejea nchini China.

Baadhi ya wadau na watumiaji wa Bandari hiyo wakiwemo Mzee Bure Abdallah na Alexander Bukuku ambao ni madereva wamewaeleza wanahabari kuwa kwa sasa hawapati usumbufu katika kutoa mizigo yao badala yake wamekuwa wakihudumiwa kwa haraka, huku wakitumia fursa hiyo kupongeza uwekezaji uliofanyika kwenye mifumo ya kiutendaji (teknolojia) ambapo afisa wa eneo moja anaweza kuwasiliana na wa eneo jingine kwa haraka hasa kwenye masuala ya uhakiki na ukaguzi.

Naye, Juma Abdrehman Juma ambaye ni Afisa Mwandamizi kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini (TPA) kitengo cha General Cargo inayohusisha mizigo mchanganyiko amesema kwa usiku huo pekee Bandari ya Dar es Salaam inahudumia meli nne (4) kwa pamoja zikiwa zimebeba mizigo tofauti ikiwemo Magari, vyuma vya Reli, Mabomba, Makontena nk.
 
Wazee wa DP worlddddddddd wanasema mambo ni shwariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii meli zinatoka ndani ya siku moja hahahahahahahahahaha
 

Attachments

  • IMG_2061.jpeg
    IMG_2061.jpeg
    657.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom