Mkurugenzi wa Bandari ya Dar asema "Hali ni shwari Bandari ya Dar es Salaam, operesheni zinaendelea"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
4a2a9cf6-1153-4bf5-b046-629e4ad43f33.jpeg
Shughuli za kiuendeshaji katika Bandari ya Dar es Salaam zinaendelea vyema huku gati zote ndani ya bandari hiyo zikiendelea na shughuli za kupakia na kupakua mizigo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho wakati akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya uwepo wa msongamano bandarini kutokana na kutofanya kazi kwa baadhi ya gati, Jumapili Januari 28, 2024
aa859ca5-a97c-42fc-aa3b-8b1134520a6f.jpeg

c992110c-c289-4ea3-94a0-5d43a9a7e6f8.jpeg
Mrisho amethibitisha kuwa, gati zote zinafanya kazi na kwa sasa meli zinaendelea kuhudumiwa katika gati zote.

Akitoa mfano kwa kusema kwa leo pekee (Januari 28, 2024) kuna meli 13 kwenye gati zote kuanzia gati namba 0 hadi gati 11 zikiendelea kuhudumiwa na meli 31 zikiwa zinasubiri kuhudumiwa.

Mrisho ameongeza kuwa, kwa upande wa gati za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Terminal l kuna meli zipatazo 10 zikiendelea kuhudumiwa ambazo zimebeba shehena mbalimbali.

"Pale gati namba 0 kuna meli ya MV Yangze 32 inapakua, gati namba 1 kuna meli ya MV Loa Fortune inahudumiwa, gati namba 2 kuna MV African Macaw, huku gati namba 3 kukiwa kuna meli ya MV Tong Da na meli zote hizi zinapakua mizigo mchanganyiko," amesema Mrisho na kuongeza:

"Gati namba 4 hivi sasa kuna meli ya MV Fearless, gati namba 5 kuna MV Anassa, gati namba 6 na 7 kuna MV MSC Nora III, pale KOJ I kuna meli ya MT NCC Abha, KOJ II kuna meli ya MT Lubersac na mwisho pale SPM kuna meli ya MT Torm Hannah ikiendelea kupakua"

"Upande wa gati za TPA Terminal ll, ambazo ni gati namba 8, 9 10 na 11.

"Katika gati za TPA Terminal ll, ambazo ni gati namba 8, 9, 10 na 11 hivi sasa Kuna meli tatu (03) zikiendelea kuhudumiwa," amesema Mrisho.

Ufafanuzi huo umetolewa, kufuatia taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa, ni gati mbili pekee ndio zinazofanya kazi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, ameongeza kuwa kukamilika kwa sehemu ya miradi ya maboresho ya miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam kumeanza kuleta matokeo chanya kwani kupitia maboresho hayo kumekuwa na ongezeko la idadi ya shehena inayohudumiwa kwa mwezi bandarini hapo.

Maboresho makubwa yaliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam yamehusisha ujenzi wa gati na uongezaji wa kina katika lango la kuingilia bandarini ambapo kumeiwezesha bandari ya Dar es Salaam kuongeza idadi ya mizigo na magari inayohudumiwa kwa wakati mmoja.


Pia soma
= Bandari ya Dar es Salaam sasa inafanya kazi 24/7
= Bandari ya Dar kuna Urasimu, mizigo inatoka taratibu sana. Serikali, nini kinaendelea?=
 
Back
Top Bottom