Wafanyabiashara Mbeya wafunga maduka kupinga mashine za TRA

Wafanyabiashara Mbeya wafunga maduka kupinga mashine za TRA

watu kulipa kodi hawataki lakini bado wanahitaji huduma muhimu, sasa sijui hiyo serikali itatoa wapi fedha kama si kwenye makusanyo ya kodi..

Laiti kama hiyo sh 800,000 ingekuwa inaingia serekalini,hiyo ni dili la watu.mbona nyie waafrica wagumu kuelewa?
 
alafu kwa turnover ya milioni 14 ni biashara ya kawaida sana hata stationary inafikisha hyo,je faida ni sh ngapi?maana turnover kubwa haimaanishi faida kubwa.naona bora wange base kwenye faida.

Faida wanasema 45,000 kwa siku!!
 
Hayo yanatokea kwa kuwa wale agents waliopewa tenda ya kuuza hizo machine wanachukua pande fulani kubwa cha juu ... natumaini ufuatiliaji ukifanyika itagundulila tatizo liko wapi ... yaani hap ni kuwa mmiliki wa hizo EFD anawauzia agents wake mikoa yote then wale agents wanauza kwa bei ya juu ...
 
kanga [/QUOTE said:
hivi kwanini TRA wasinunua hizi machine kisha wakawapatia wafanyabiashara bure? kwani lengo ni kuuza machine ama kukusanya kodi? Jamani seriakli yetu ndio maana inapoteza mapato ... ndio maana watu wanaamua kutumia njia za panya ni sababu ya usumbufu kama huu ... ni sawa tu na hawa tanesco kucharge gharama kubwa ya nguzo na pia gharama kubwa za installation ya umeme ili hali lengo ni kuuza umeme ... kuna sababu nyingi za kijinga zinazowafanya serikali ikose mapato ... ni frustration kama hizi ... naona wananchi wameshaanza kuamka usingizini ... taratiibu somo litaeleweka...
 
Wadau,

Nipo mwanjelwa njia ya mfikemo, vijana wanapita kwenye maduka na kuwaagiza wafanyabiashara wa maduka kufunga maduka yao ili waanze kufanya fujo kupinga agizo la kuwaondoa wasifanye biashara barabarani.

Nitawajuza zaidi maana tayari makelele yameshaanza.

----------------------------------------------------
hivi kwanini TRA wasinunue hizi machine kisha wakawapatia wafanyabiashara bure? kwani lengo ni kuuza machine ama kukusanya kodi? Jamani serikali yetu ndio maana inapoteza mapato ... ndio maana watu wanaamua kutumia njia za panya kujipatia huduma na kukwepa kodi ni sababu ya usumbufu kama huu ... ni sawa tu na hawa tanesco kucharge gharama kubwa ya nguzo na pia gharama kubwa za installation ya umeme ili hali lengo ni kuuza umeme ... kuna sababu nyingi za kijinga zinazowafanya serikali ikose mapato ... ni frustration kama hizi ... naona wananchi wameshaanza kuamka usingizini ... taratiibu somo litaeleweka...
 
Vita vimepamba moto kati ya polisiccm na wapigania haki wa Mbeya, Landcruser nyingi FFUccm kutoka nje ya Mbeya zinaingia kuunajisi mji wa Mbeya kwa mabomu ya machozi. Sasa hivi mabomu ya machozi yanapigwa mfurulizo ni hatari tupu lakini wanambeya wanaendelea kupambana kupigania haki yoa ya kutoporwa mitaji yao midogo walioikopa kutoka mabenki yenye kutoza liba kubwa hapa tz.
 
Bado Arusha tuna wasubili, huu ni wizi yaani hivyo vidude vyao hapo kenya unaweza kuvipata kwa 150000 lakini hapa kwetu unaambiwa lakini nane halafu lazima ununue kutoka kwa watu wao...yaani ni kama biashara ya vizibiti mwendo..
wananikumbusha enzi za vizititi mwendo - madili ya watu kupeana pasi.
 
Inafikia hawa watunga kodi inabidi waangalie, athari za kodi zao. Maana sidhani kama kuna mtu anaeuza bidhaa barabarani na kuishi maisha ambayo yapo comfortable yeye na familia yake. Ni lini mtanzania wa chini atapewa haueni ya kodi kila kukicha kodi kodi kodi, hivi hawa jamaa hawana mbinu zingine za kuongeza pato la taifa zaidi ya kodi hata zenye kwenda kuongeza maumivi ya maisha kwa muuzaji, mnunuaji na hiyo sector yote.

Hii ministry imezidi kwakweli seriously it's time we demand watu wanao elewa kazi zao na namna ya kutunga kodi kila kukicha wao ni walala hoi tu ndio waminye, safi sana vijana wa mbeya kwa kuonyesha it is enough, akuna mtu anaepata chakula kutoka mbinguni ni kuchakarika tu lakini hawa wenzetu wa serikalini kila kukicha kutaka kuwaongezea watu ugumu, jamaa wanachosha kwakweli.
 
hata mimi nina biashara yangu,lakini sina mpango kabisa wa kununua hiyo mashine kama kweli wanashida ya kukusanya kodi kutoka kwangu basi wanipe hicho kifaa bure,or waiuze kwa reasonable price otherwise HAKATWI MTU HAPA...
 
Wakati sasa umefika wa wananchi kutambua kuwa KULIPA KODI ni wajibu wa kila raia mwenye stahiki hiyo, na kwamba wanaokwepa kulipa kodi wanapaswa kukaripiwa na kusutwa kama 'mbeya'. Kodi ndiyo chanzo cha mapato ya serikali mapato yanayo gharimia huduma za jamii na ujenzi wa miundombinu, kwa kutaja machache. Kelele za kuitaka serikali ipanue wigo wa walipa kodi na kuhakikisha kodi inakusanywa, ni za muda mrefu. Utekelezaji unapofanyika tupongeze na si kupinga kwa maandamano.
 
Bila kukusanya watapataje maendeleo;
Tukisema upinzani ni janga la kitaifa
mnarusha mawe.

Kama ni issue ya mashine za tra ifanyiwe ufumbuzi;
Na kwanini lianzie mbeya.

why Mbeya? kila ukombozi una kitovu chake!
 
Hali ni mbaya sana,watu wawili niliowashuhudia wamepigwa risasi,haijulikani kama wamekufa au wamepona,hali ni tete sana,
 
Hali ni mbaya sana,watu wawili niliowashuhudia wamepigwa risasi,haijulikani kama wamekufa au wamepona,hali ni tete sana,

Agizo la pinda linafanya kazi vizuri hapo.
Mbeya msikubali kuburuzwa!!
 
Wewe nafikiri una tatizo kubwa ambalo hata mwenyewe hujalielewa. Watu wanaongelea ufisadi katika uuzaji wa mashine za TRA zinazouzwa na watu binafsi kwa kupitia mgongo wa TRA, wewe unakuja na umuhimu wa kodi. Umuhimu wa kodi kila mmoja anaujua, na hakuna mtu anayepinga kulipa kodi. Wananchi wa Mbeya wanapinga ufisadi wa biashara ya mashine za kutolea risiti ambao ni mradi wa watu binafsi na siyo TRA.

Kakae na kufikiria uje na mchango kuhusiana na ufisadi wa makampuni binafsi yanayoitumia TRA kujitajirisha kupitia uuzaji wa mashine za kutolea risiti. Kwa nini mashine hizo ziwe na bei karibu mara 10 ya bei ya mashine hizo hizo katika nchi nyingine?.

Wakati sasa umefika wa wananchi kutambua kuwa KULIPA KODI ni wajibu wa kila raia mwenye stahiki hiyo, na kwamba wanaokwepa kulipa kodi wanapaswa kukaripiwa na kusutwa kama 'mbeya'. Kodi ndiyo chanzo cha mapato ya serikali mapato yanayo gharimia huduma za jamii na ujenzi wa miundombinu, kwa kutaja machache. Kelele za kuitaka serikali ipanue wigo wa walipa kodi na kuhakikisha kodi inakusanywa, ni za muda mrefu. Utekelezaji unapofanyika tupongeze na si kupinga kwa maandamano.
 
Wakati sasa umefika wa wananchi kutambua kuwa KULIPA KODI ni wajibu wa kila raia mwenye stahiki hiyo, na kwamba wanaokwepa kulipa kodi wanapaswa kukaripiwa na kusutwa kama 'mbeya'. Kodi ndiyo chanzo cha mapato ya serikali mapato yanayo gharimia huduma za jamii na ujenzi wa miundombinu, kwa kutaja machache. Kelele za kuitaka serikali ipanue wigo wa walipa kodi na kuhakikisha kodi inakusanywa, ni za muda mrefu. Utekelezaji unapofanyika tupongeze na si kupinga kwa maandamano.
Kulipa kodi sio tatizo, lakini kodi lazima imwangalie na mlengwa, kuna sababu gani ya kwenda kumwekea kodi mtu ambae biashara yenyewe aiwezi kumpa hata sustainable life yeye na familia yake, baada ya kazi bado maisha yake yanasua sua na yana ugumu halafu wewe tena unamwekea na kodi juu duuh uungwana gani huo.

Kila mtu anataka maisha bora wengi wetu bado hatuna kipato cha hivyo, hapo hapo serikali inayotakiwa kututengenezea njia safi zenye kuwezesha hilo la maisha bora imeshindwa kufanya hivyo kwa kukuza ajira, kuwekeza kwenye sector za maendeleo. Leo watu wameamua kuchukua risk na savings zao hili kuweza kupata mlo tu serikali inaona kodi, kama vipi wapunguze matumizi ya serikali yamezidi sana.

Lakini kwakweli wengi wetu tumechoka kuona ndugu na jamaa wakitanzania wanavyo nyanyaswa na serikali yao kupitia fees ambazo hawawezi mudu kwenye services zao na kodi ambazo zinalenga kumwongezea ugumu wa maisha mfanyabiashara mdogo safi sana vijana wa mbeya unyanysaji umezidi.
 
Serikali kupitia wizara ya fedha na TRA wana wajibu wa kukaa na wananchi wawaeleze kwanini wanauza hizo devices kwa bei kubwa hivyo while wangeweza kuuza kwa bei elekezi ambayo kila mfanyabiashara angeimudu. Kupiga raia wako kwa mabomu na risasi ni kuongeza chuki dhidi ya serikali halali iliyoko madarakani.

Serikali ya CCM imeonesha udhaifu mkubwa sana katika kushughukia matatizo ya lazima 'basic needs' za wananchi wake na sasa wanalazimisha wanunue devices ghali wakati inawezekana kutumia njia mbadala kama ya kuagiza vifaa rahisi. Matokeo ya kupiga raia hovyo na kulazimisha mwenye nchi anunue kitu kilichoko nje ya uwezo wake ndio kitu kiitwacho udikteta.

Kwani hakuna wazee wanaoheshimiwa watakaoishauri serikali jinsi ya kuwaweka wananchi wake karibu nayo? Ieleweke wananchi hawakatai kulipa kodi ila mazingira wanayowekewa ana serikali ndiyo yanawafanya wataharuki. Siku zote serikali haiweza kutatua migogoro baina yake na wananchi walioiweka madarakani endapo haitajipa muda wa kuongea na kuwajulisha wahusika A to Z kuhusu mustakabali wa uchumi bila ya kodi.

Ni mategemeo yangu kuwa viongozi na wahusika watasoma na kuufanyia kazi ujumbe wangu huu.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
 
Wakati ni ukuta. Wakati wa kila Mfanyabiashara kuwajibika na kulipa Kodi halali kwa mfumo unaopunguza fursa za ubadhirifu, umefika. Ninashangaa ni kwa nini wagomee Mfumo/teknolojia na wasigomee viwango vya Kodi vinavyotozwa na kufuatilia/kuhoji matumizi ya Kodi hiyo!
 
Back
Top Bottom