Wadau,
Nipo mwanjelwa njia ya mfikemo, vijana wanapita kwenye maduka na kuwaagiza wafanyabiashara wa maduka kufunga maduka yao ili waanze kufanya fujo kupinga agizo la kuwaondoa wasifanye biashara barabarani.
Nitawajuza zaidi maana tayari makelele yameshaanza.
----------------------------------------------------
Yaani, Dunia nzima inaendeshwa kwa Kodi. Hata huo mtambo unaondikia hapo umetengenezwa kwa kodi watu wenye akili na kufirikia. Ukiwa mjina na m.pumbuvu huwezi kulipa kodi hata siku moja. Kilichotakiwa hapo ni kuungana kwa wafanyabiashara na wenzao wote kutafuta namna nzuri ya kupia kodi na si kugoma au kufanya fujo. Hiyo ndo naita u-pumbafu mkubwa sana. Na Mbeya kama Mbeya pekee haiwezekani ikagoma isikilizwe wakati wengine hata habari hawana. Ukigoma kwa mtindo huo ni u-upumbavu. Umenipata? Naamini nawewe si mpumbafu mwenzao au kama ulikuwa sasa utaacha upu-mbafu wako
JK na serikali ya ccm walipoambiwa wasipokuwa makini nchi haitatawalika walisema CDM wachochezi. Nchi inawaka moto kila kona, watu wamechoka kuonewa na serikali 'sikivu' isiyojali watu wake. Hii iwe changamoto ya kufanya maamuzi 2015. Mungu Ibariki Tanzania!
Utauliza wabunge hadi mwisho wa dunia na hutopata majibu, tushukuru Mungu kuwa pamoja na maeneo mengine machache hapa Tanzania wananchi wa Mbeya wanaonekana wazi kuwa wako tayari kwa lolote mradi haki na ukweli vipatikane na kweli inaonekana hata kwa wenye uelewa mdogo kama magamba.wafanyabiashara wamefunga maduka na kukusanyika viwanja vya Mwanjelwa huko mbeya kupinga mashine za Tra.
my take. hizi mashine bei yake ni ml 1.5 ila lap top mpya sh laki nne huu si ufisadi huu?
Wabunge wapo wapi?
Laptop mpya ni laki nne ila
Microsoft Windows 7 ni $220
Microsoft Windows 8 ni $120
Microsoft Office 2013 Proffessional ni $400
Antivirus ni $50
Hapo bado hujaweka softwares nyingine kulingana na mahitaji unayoyataka. Lakini pia fahamu kuwa laptop ya shilingi laki nne haiwezi dumu kwa muda mrefu kama inatumika muda wote. Ndio maana laptop zilizo imara bei yake si chini ya 1.3M.
My take: Usipende kulinganisha vitu usivyovijua. Kama hizo mashine ni gharama basi toa uthibitisho wa kwa nini hazipaswi kuwa bei hiyo na siyo kulinganisha na kitu ambacho haviendani. Fahamu kuwa kompyuta ni mashine tu ambayo inafanya kazi kulingana na programs ulizoweka kwa maksudi ya kazi ulizokusudia. Waweza nunua laptop kwa lakini nne lakini program ya kukuwesha ufanye kazi yako ukanunua kwa dola $100,000.00
Mbona kama hujui unachoongea? Lazima siyo mtu wa Mbeya wewe. Mbeya wana akili sana za kufikiria
Ni kweli hawa wamekaririshwa wanadhani watanzania wa leo ni wale wakuburuzwa kama walivyozoea na bdo huu ni mwanzo tu wakuwango'a kabisa hawa mafisadi.Usiendeshe mambo kwa kukariri, kuna namna nyingi za kuifikia haki kutegemeana na anayekudhulumu. Kama mdhulumaji ana angalao chembe ya hekima, utu na akili, njia unayofikiria wewe itafanya kazi. Lakini kama mdhulumaji mwenyewe ni kama hii serikali yetu, mazungumzo hayafanyi kazi. Watakusikiliza lakini mwisho wa yote, hakuna kitakachobadilika. Angalia kodi ya line za simu, watu mbalimbali walilalamika, wakapitia njia ya mazungumzo, na serikali ikakiri kuwa italifanyia kazi, baada ya mambo kupoa, kodi imerudi.
Yale masuala ya malipo ya mafao ya kijamii (NSSF, PPF, n.k.), wafanyakazi wa mgodi wa Barrick waligoma kufanya kazi kwaajili ya kushinikiza serikali ifute sheria gandamizi na ya kipumba.vu kuzuia fao la kujitoa, wakafanikiwa, mpaka leo watu wanapokea mafao yao. Serikali yetu haisikii sauti za raia kwa njia ya kawaida kwa sababu inaendeshwa na falsafa yao ile kuwa, 'baada ya muda watasahau'. Serikali ya Tanzania ina uwezo wa kuona tu, mkifanya kitu ndiyo wanaona na kujua kuwa mmedhamiria kudai.
Njia waliotumia wanaMbeya, kwa kuzingatia utendaji wa serikali yetu, ndiyo njia pekee inayoweza kuleta mabadiliko. Hapa cha muhimu ni kuhamasisha na mikoa mingine, wafanyabiashara wafanye hivyo hivyo. Ifahamike kuwa wafanyabiashara hawagomei kulipa kodi, wanagomea bei ya wizi wa mashine za kodi. Na pesa ya mauzo ya mashine hizo siyo ya TRA bali inaenda kwenye mifuko ya mafisadi ambao siku zote hufanya kazi kwa kushirikiana na watendaji mafisadi ndani ya serikali. Hapa wananchi wanapinga ufisadi, ni lazima waungwe mkono.
Nikwel kabisa asee,
nko hapa Ilomba nmejifungia ndan, ni mabomu kwelkwel
Mbeya hakufai, why kila siku nyinyi tu?
Wadau waliopo mbeya watupe Updates ya kile kinachojiri huko mbeya!
Halmashauri imetoka wapi kwenye Machine za TRA? fikiri kabla ya kuandika, au hujui tofauti ya TRA na municipal?
Ni vizuri kuelewa hii kitu ili wafanyabiashara wajue wanasimama wapi? Hofu yangu ni TRA kutenda haki kwa mujibu wa maelezo haya hapa chini ili wasisumbue wafanyabiashara wadogo.Badala ya kufuata misingi ya sheria unakuwa mwanya wa rushwa.Haya maelezo hapa chini ndio msingi wa hiyo operation wawaambie maafisa wao wasionee mtu wakaleta bifu na umma bila sababu.
Na bado tutaendelea kuwachagua haohao wasio na akili na wavutabangi wasio wezi wa mali ya umma.Unaongea kama wewe na siyo ..."sisi". Jifunze lugha kwanza. Alafu, ukiwa huna akili sawa sawa lazima kila kitu ukifanya utajiona huna woga. Lakini ukiwa na akili, unakuwa timamu, hata vitu vidogo vidogo huwezi tumia nguvu ya kukuumiza. Utafanya busara tu. Kukosekana akili za kutosha ndizo zinakufanya ujiite SISI wana Mbeya wakati ni wewe unayeongea na kukosekana akili huko huko kunakufanya uumie kwa kitu ambacho ungetumia akili ndogo tu ungekuwa na raha.
serikali inatambua gharama za uendeshaji wa biashara.uliyoyasema yanakubalika yote tatizo wengi hatunauthibitisho wa risiti ama au mikataba.pia lengo la hizi mashine ni kuondokana na mfumo wa ukadiriaji wa kodi.lakini siyo kila mtu anatakiwa awe na mashine ni mwenye mauzo ya tsh 38700 kwa siku ambayo ni sawa na 1.1m kwa mwezi au 14m kwa mwaka.wafanyabiashara wamepewa miezi sita yaani may hadi november kununua kwa hiari.wamepewa pia uhuru wa kununua kutoka kwa wasambazaji kumi na moja.Kupitia majesho ya kodi watarudisha gharama za kununulia mashine.tunapenda kusukumwa badala ya kujituma.Mtaki Milion 1 ,Frem unalipia kwa mwezi laki 4 hd 8...alafu kwa siku unauza laki 2 kwa mwaka utakuwa umepata faida km milioni 2 hv na hapo hapo unalazimishwa kununua kimachine chaooo......pumbavuu zaooo
Mbona kama hujui unachoongea? Lazima siyo mtu wa Mbeya wewe. Mbeya wana akili sana za kufikiria
Serikali sikivu lakini kiziwi lol
Dah,Ndugu yangu uyu jamaa haelewi kitu ata umuelimishe vipi nadhani ata mwalimu wake darasani alikuwa anapata shida sana.Muacheni ameshalipwa buku7 lumumba.Anataka kueneza nidhamu ya woga kwa watanzania wakati wananchi tayari wameshaamka.Usiendeshe mambo kwa kukariri, kuna namna nyingi za kuifikia haki kutegemeana na anayekudhulumu. Kama mdhulumaji ana angalao chembe ya hekima, utu na akili, njia unayofikiria wewe itafanya kazi. Lakini kama mdhulumaji mwenyewe ni kama hii serikali yetu, mazungumzo hayafanyi kazi. Watakusikiliza lakini mwisho wa yote, hakuna kitakachobadilika. Angalia kodi ya line za simu, watu mbalimbali walilalamika, wakapitia njia ya mazungumzo, na serikali ikakiri kuwa italifanyia kazi, baada ya mambo kupoa, kodi imerudi.
Yale masuala ya malipo ya mafao ya kijamii (NSSF, PPF, n.k.), wafanyakazi wa mgodi wa Barrick waligoma kufanya kazi kwaajili ya kushinikiza serikali ifute sheria gandamizi na ya kipumba.vu kuzuia fao la kujitoa, wakafanikiwa, mpaka leo watu wanapokea mafao yao. Serikali yetu haisikii sauti za raia kwa njia ya kawaida kwa sababu inaendeshwa na falsafa yao ile kuwa, 'baada ya muda watasahau'. Serikali ya Tanzania ina uwezo wa kuona tu, mkifanya kitu ndiyo wanaona na kujua kuwa mmedhamiria kudai.
Njia waliotumia wanaMbeya, kwa kuzingatia utendaji wa serikali yetu, ndiyo njia pekee inayoweza kuleta mabadiliko. Hapa cha muhimu ni kuhamasisha na mikoa mingine, wafanyabiashara wafanye hivyo hivyo. Ifahamike kuwa wafanyabiashara hawagomei kulipa kodi, wanagomea bei ya wizi wa mashine za kodi. Na pesa ya mauzo ya mashine hizo siyo ya TRA bali inaenda kwenye mifuko ya mafisadi ambao siku zote hufanya kazi kwa kushirikiana na watendaji mafisadi ndani ya serikali. Hapa wananchi wanapinga ufisadi, ni lazima waungwe mkono.