kanganyoro
Senior Member
- Jun 22, 2011
- 127
- 33
Wadau,
Nipo mwanjelwa njia ya mfikemo, vijana wanapita kwenye maduka na kuwaagiza wafanyabiashara wa maduka kufunga maduka yao ili waanze kufanya fujo kupinga agizo la kuwaondoa wasifanye biashara barabarani.
Nitawajuza zaidi maana tayari makelele yameshaanza.
----------------------------------------------------

wafanyabiashara wamefunga maduka na kukusanyika viwanja vya Mwanjelwa huko mbeya kupinga mashine za Tra.
my take. hizi mashine bei yake ni ml 1.5 ila lap top mpya sh laki nne huu si ufisadi huu?
Wabunge wapo wapi?
Kuna ufisadi mkubwa sana unafanywa na TRA.
Bei ya hizi machine ni juu sana kwa sababu TRA wametoa tender kwa watu wao hivyo huwezi kukwepa ulanguzi wao. Ni kwanini TRA wasiseme aina za machine zinazotakiwa, halafu mtu anakuwa huru kununua anakoweza na baadae unapeleka TRA ili wai-set hiyo machine? Ni kwanini WANAHODHI hizi machine? Bei ya machine haizidi laki 5, lakini hawa TRA kupitia kwa walanguzi wao wanauza machine kwa 1.5 million na kuendelea! Wizi mtupu.
Pili, huu umahiri wa TRA kuwafungia machine wafanyabishara kwa nini hatuuoni kwa makampuni ya simu? Wafanyabiashara wanaweza kabisa kukataa kuweka hizi machine hadi pale makampuni ya simu yatakapofunga machine. Unyonyaji huu ndio tunaona sasa wanataka kutoza kodi Mama ntilie line simu huku makampuni yenyewe yakiachwa. Unyonyaji.