Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
Mataifa ya Ulaya na Marekani hayawezi kuja na msimamo wenye kauli ya kuitaka Israel kuacha mashambulizi wala mataifa ya Waarabu hayawezi kukiambia kikundi cha Hamas kuja na kauli ya kutaka wafanye mazungumzo ya amani kwa kuwa hata wao wangeguswa kama ilivyoguswa Israel na Gaza wangefanya kitu hichohicho walichofanya Israel na Gaza.

Kama ilivyoshambuliwa Marekani kipindi kile, halafu aje mtu awaambie wakae meza moja kufanya mazungumzo ya amani na Al qaeda au kama Tanzania ilipovamiwa na Nduli Iddi Amini, halafu angekuja mtu kutwambia tukae na Iddi Amini tufanye mazungumzo ya kutafuta amani.

Kwa asili Wapalestina ni watu wazuri sana, binafsi nawakubali katika asili yao, naamini Israel na Palestina wakiachwa wenyewe, bila Waarabu na Wamarekani kuingilia wana uwezo mkubwa wa kukubaliana na kuja na suluhu, ila akili na maamuzi ya kufundishwa ndiyo yanayowagharimu.

Sasa je hadi tuipoteze Gaza mazima na hapo ndiyo amani itarudi au hadi tuipoteze Israel ndio amani itarudi?

Enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, msimamo wake ulikuwa wazi, aliita nyekundu ni nyekundu na nyeupe aliita nyeupe, msimamo wa Mwalimu Julius Nyerere ndio ulikuwa msimamo wa kiitikadi wa Tanzania kutoshirikiana na mataifa yanayokandamiza jamii fulani ya watu na kukiuka haki zao za binadamu.

Mwalimu Nyerere alikuwa wazi kabisa kiitikadi aliunga mkono jitihada za Wapalestina kuwa huru katika eneo lao, sambamba na azimio la Umoja wa Mataifa la kuwa na mataifa mawili katika lile eneo (two states solution).

Jambo hili lilikuwa wazi kwamba linalofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina ni sawa na ilichofanya serikali ya makaburu dhidi ya wazalendo wa Afrika Kusini, na hivyo kama hatukukubali kuwa na uhusiano na serikali ya makaburu hatupaswi kuwa na uhusiano na serikali ya Israel ili kuwashinikiza kuwatendea haki Wapalestina.

Mwalimu Julius Nyerere hakujali wakishirika wa Israel kama Marekani na Uingereza mataifa ambayo yangeweza kukataa kutupa misaada mbalimbali, ni dhahiri Mwalimu Julius Nyerere alisimama kwenye haki, hakupumbazwa na vibaraka wa wazungu waliokuwa wanafurahia misaada, na Mwalimu Julius Nyerere akafungua Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania.

Hayati Rais John Magufuli alifungua ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa faida mbili ya kiroho na ya kimwili, Faida ya kiroho alirejea Mwanzo 12:3 Anayekubariki, nitambariki; anayekulaani, nitamlaani, kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”

Hii ni ahadi ya Mungu kwa Ibrahim, Isaka, na Yakobo aliyebeba jina la Israel baada ya kupewa na Malaika, faida ya kimwili tukirejea uhusiano wetu na Israel, walitujengea Nkrumah Hall, baadhi ya majengo ya UDSM, Ubungo Plaza na JWTZ imara, lakini zaidi ya yote kuvunja uhusiano na Israel au Palestina kuwafurahisha watu fulani ni upuuzi.

Tufanye uamuzi kwa kuzingatia faida na hasara za kiuchumi na kijamii ndipo tuamue kipi kina faida kwetu, zaidi ya yote Jamii zote duniani zinastahili haki, usawa na usalama.

Ukitaka Tanzania ipoteze kabisa uhusiano, tufute uhusiano wa Tanzania na Saudia au nchi zote za kiarabu, tulipofuta uhusiano wa Tanzania na Israel wahujani walipata shida sana kuitembelea Israel, ilikuwa hadi kuchukua visa Nairobi, na pamoja na figisu zote bado wahujani walikwenda kokote kule kupata visa ya Israel kwenda kuhiju kwasababu tu Mungu tunaemwabudu ni Mungu wa Israel, hivi ndivyo ilivyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu.

Nini msimamo wetu kwa sasa, kutokana na niliyoyaeleza hapo juu Tanzania kwa sasa ipo kwa wote kwa sababu ifuatayo, pale si Israel wala Palestina anayetakiwa kuondoka, wote pale ni kwao kabisa pasipo na shaka.

Wapalestina hawakuwahi kufukuzwa pale, miaka yote Wapalestina na Wayahudi wamekuwa pamoja kwenye ardhi ile pamoja na kuwa na tofauti zao, kulikuwa na Wapalestina Wakristo, Wapagani pia wengi tu walioabudu katika Uyahudi.

Hata ulipokuja Uislam na Wapalestina wakaamua kuupokea Uislam, bado maisha yalikuwa ya kawaida,t ofauti na mikwaruzano miongoni mwao haikuwahi kuisha ila maisha yaliendelea.

Pressure kubwa iliyoleta chuki haikuwa sababu ya Wapalestina kuwa Waislam, bali fitna na gilba za wageni walioingia Israel, Palestina na Jordan, hao ndiyo walipelekea pressure na kujenga chuki kwa waamini na wasioamini. Maneno yao ndio yaliyoharibu haki, usawa na usalama wa watu wa Israel na ukanda wa Gaza.

Nimalizie kwa tafakuri jadidi, je, suluhu imeshindwa ukanda wa Gaza? Je, neno la Mungu ni kweli juu ya taifa la Israel kama Waisrael wanavyoichukulia mipaka ya Biblia kuwa ndiyo mipaka yao hata sasa? Je, Mkataba wa Oslo unaheshimiwa kwa mataifa yote mawili Israel na Palestina?

Tunafahamu vita ilipelekea nchi ya Palestina igawanyike katika sehemu tatu, Taifa la Israel, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan (West Bank) na Ukanda wa Gaza, sasa je, vita itakwenda kurudisha sehemu hizo tatu kuwa nchi moja!?

Nikiishia hapa, mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
  • Bachelor of business administration in International business.
  • Master of Leadership and Management.
Recent Publications;
- Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Misimamo yetu haina tija yoyote kwenye eneo lile. Wale watu hawataweza kuelewana milele daima, na tatizo lao ni madhehebu yao na imani zao.

Cha msingi waachwe watwangane, mpaka kizazi kimoja kipotee kabisa ama Israel au Palestina. hapo ndio itakuwa mwisho wa vita na mizozo baina ya hao mahasimu wawili.

Dunia hii haina ardhi isiyo namwenyewe, tungewapa wakaishi huko. Hatuja pata sayari inayoweza kukalika tungewapeleka huko.

Kwasasa solution ni kuwaacha waangamizane wenyewe, kizazi kimoja kiishe kabisa hatutaki masalia sijui watoto, maliza hadi mifupa ibaki historia kama dinosor duniani, huo ndio muafaka wa kudumu.
 
Hii imeandikwa kwenye Biblia kuwa hili ni taifa Mungu. Tunatakiwa kulipenda na kulibariki na kuwa pamoja nalo kwa kila jambo. Mwanzo 12:3.

Mwalimu Nyerere alikosea sana kumkumbatia Arafat na kuacha kuwa pamoja na taifa la Israel.

Ndio maana aliaacha taifa letu masikini kwa kila kitu.

image_search_1697063292247.jpg

Hii imeandikwa kwenye Biblia kuwa hili ni taifa Mungu. Tunatakiwa kulipenda na kulibariki na kuwa pamoja nalo kwa kila jambo. Mwanzo 12:3.

Mwalimu Nyerere alikosea sana kumkumbatia Arafat na kuacha kuwa pamoja na taifa la Israel. Ndio maana aliaacha taifa letu masikini kwa kila kitu.View attachment 2779428
Utumbo mtupu. Waarabu hawa wawili wanatuhusu nini. Wale ni dugu moja dugu yangu hapana poteza mida yako bure
 
Hakuna upande, tuangalie kama movie tukisubiria mshindi mwisho. Hapa Mungu asihusishwe, hawa ni mahasimu wawili waliokataa suluhu, msuluhishi na hawataki kupatana. Waachwe tuwaangalie wazipige kisawasawa mpaka mwisho.
 
Wewe ni mpumbavu kiasi hakuna haja ya kukujibu zaidi ya kukuita pumbavu....
Eti mungu wa israeli...pumbavu kabisa
Hakuna nchi inayoitwa Palestina. Palestina ni nchi feki iliyoanzishwa na Warumi mwaka 133 AD. Warumi waliwapiga Israel na kuwatawanya, wakarudi 1948 na kuwakuta Wapalestina. Mtu anarudi kwake umwite mvamizi? Quran 5:21 inasema wazi nchi hiyo ni ya Waisraeli, huwezi kupata Palestina kwenye Quran na Biblia Bali utapata Israel.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mataifa ya Ulaya na Marekani hayawezi kuja na msimamo wenye kauli ya kuitaka Israel kuacha mashambulizi wala mataifa ya Waarabu hayawezi kukiambia kikundi cha Hamas kuja na kauli ya kutaka wafanye mazungumzo ya amani kwa kuwa hata wao wangeguswa kama ilivyoguswa Israel na Gaza wangefanya kitu hichohicho walichofanya Israel na Gaza.

Kama ilivyoshambuliwa Marekani kipindi kile, halafu aje mtu awaambie wakae meza moja kufanya mazungumzo ya amani na Al qaeda au kama Tanzania ilipovamiwa na Nduli Iddi Amini, halafu angekuja mtu kutwambia tukae na Iddi Amini tufanye mazungumzo ya kutafuta amani.

Kwa asili Wapalestina ni watu wazuri sana, binafsi nawakubali katika asili yao, naamini Israel na Palestina wakiachwa wenyewe, bila Waarabu na Wamarekani kuingilia wana uwezo mkubwa wa kukubaliana na kuja na suluhu, ila akili na maamuzi ya kufundishwa ndiyo yanayowagharimu.

Sasa je hadi tuipoteze Gaza mazima na hapo ndiyo amani itarudi au hadi tuipoteze Israel ndio amani itarudi?

Enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, msimamo wake ulikuwa wazi, aliita nyekundu ni nyekundu na nyeupe aliita nyeupe, msimamo wa Mwalimu Julius Nyerere ndio ulikuwa msimamo wa kiitikadi wa Tanzania kutoshirikiana na mataifa yanayokandamiza jamii fulani ya watu na kukiuka haki zao za binadamu.

Mwalimu Nyerere alikuwa wazi kabisa kiitikadi aliunga mkono jitihada za Wapalestina kuwa huru katika eneo lao, sambamba na azimio la Umoja wa Mataifa la kuwa na mataifa mawili katika lile eneo (two states solution).

Jambo hili lilikuwa wazi kwamba linalofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina ni sawa na ilichofanya serikali ya makaburu dhidi ya wazalendo wa Afrika Kusini, na hivyo kama hatukukubali kuwa na uhusiano na serikali ya makaburu hatupaswi kuwa na uhusiano na serikali ya Israel ili kuwashinikiza kuwatendea haki Wapalestina.

Mwalimu Julius Nyerere hakujali wakishirika wa Israel kama Marekani na Uingereza mataifa ambayo yangeweza kukataa kutupa misaada mbalimbali, ni dhahiri Mwalimu Julius Nyerere alisimama kwenye haki, hakupumbazwa na vibaraka wa wazungu waliokuwa wanafurahia misaada, na Mwalimu Julius Nyerere akafungua Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania.

Hayati Rais John Magufuli alifungua ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa faida mbili ya kiroho na ya kimwili, Faida ya kiroho alirejea Mwanzo 12:3 Anayekubariki, nitambariki; anayekulaani, nitamlaani, kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”

Hii ni ahadi ya Mungu kwa Ibrahim, Isaka, na Yakobo aliyebeba jina la Israel baada ya kupewa na Malaika, faida ya kimwili tukirejea uhusiano wetu na Israel, walitujengea Nkrumah Hall, baadhi ya majengo ya UDSM, Ubungo Plaza na JWTZ imara, lakini zaidi ya yote kuvunja uhusiano na Israel au Palestina kuwafurahisha watu fulani ni upuuzi.

Tufanye uamuzi kwa kuzingatia faida na hasara za kiuchumi na kijamii ndipo tuamue kipi kina faida kwetu, zaidi ya yote Jamii zote duniani zinastahili haki, usawa na usalama.

Ukitaka Tanzania ipoteze kabisa uhusiano, tufute uhusiano wa Tanzania na Saudia au nchi zote za kiarabu, tulipofuta uhusiano wa Tanzania na Israel wahujani walipata shida sana kuitembelea Israel, ilikuwa hadi kuchukua visa Nairobi, na pamoja na figisu zote bado wahujani walikwenda kokote kule kupata visa ya Israel kwenda kuhiju kwasababu tu Mungu tunaemwabudu ni Mungu wa Israel, hivi ndivyo ilivyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu.

Nini msimamo wetu kwa sasa, kutokana na niliyoyaeleza hapo juu Tanzania kwa sasa ipo kwa wote kwa sababu ifuatayo, pale si Israel wala Palestina anayetakiwa kuondoka, wote pale ni kwao kabisa pasipo na shaka.

Wapalestina hawakuwahi kufukuzwa pale, miaka yote Wapalestina na Wayahudi wamekuwa pamoja kwenye ardhi ile pamoja na kuwa na tofauti zao, kulikuwa na Wapalestina Wakristo, Wapagani pia wengi tu walioabudu katika Uyahudi.

Hata ulipokuja Uislam na Wapalestina wakaamua kuupokea Uislam, bado maisha yalikuwa ya kawaida,t ofauti na mikwaruzano miongoni mwao haikuwahi kuisha ila maisha yaliendelea.

Pressure kubwa iliyoleta chuki haikuwa sababu ya Wapalestina kuwa Waislam, bali fitna na gilba za wageni walioingia Israel, Palestina na Jordan, hao ndiyo walipelekea pressure na kujenga chuki kwa waamini na wasioamini. Maneno yao ndio yaliyoharibu haki, usawa na usalama wa watu wa Israel na ukanda wa Gaza.

Nimalizie kwa tafakuri jadidi, je, suluhu imeshindwa ukanda wa Gaza? Je, neno la Mungu ni kweli juu ya taifa la Israel kama Waisrael wanavyoichukulia mipaka ya Biblia kuwa ndiyo mipaka yao hata sasa? Je, Mkataba wa Oslo unaheshimiwa kwa mataifa yote mawili Israel na Palestina?

Tunafahamu vita ilipelekea nchi ya Palestina igawanyike katika sehemu tatu, Taifa la Israel, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan (West Bank) na Ukanda wa Gaza, sasa je, vita itakwenda kurudisha sehemu hizo tatu kuwa nchi moja!?

Nikiishia hapa, mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
  • Bachelor of business administration in International business.
  • Master of Leadership and Management.
Recent Publications;
- Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
Kila zama na kitabu chake.
 
Back
Top Bottom