Achana na machinga, kuna siku nilikuwa zangu pale posta cone tower, kulikuwa kuna askari polisi wakitimuana na bodaboda, ile staili aliyetumia yule polisi ya kumuonya yule boda boda si sawa. Baaba ya kufukuzwa na askari kule chini ferry bodaboda akawa anakimbilia juu kumbe huku juu kuna askari alikuwa amepaki na bonge rungu ilekukatiza tu pale usawa na jengo la ardhi jamaa alikula bonge rungu likalia kabisa tiii!! kwenye mgongo jamaa akayumba akayumba akayumba tena na kusepa na pikipiki yake huku akiwa ameshikilia mgongo wake kwa maumivu.