Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

Magufuli huu ndio wakati wake wakupata kiki na kujijenga kisiasa
Naimani atatumia fursa hiyo kwa kutoa matamko makali ya kukemea tena inawezekana akawatoa kafara ao mgambo waliofanya hilo tukio

Na baada ya kufanya hayo watanzania tutakuja na mapambio ya kumsifu kuwa ni shujaa na anatupenda sie masikini.

Naamini lazima atumie hiyo fursa
Hawa watu wamehamishia biashara kubwa kubwa barabarani kodi ya mapato hazilipiki tena! Lazima serekali iweke control ili watu warudi kwenye maeneo yao ya biashara na walipishwe kodi!
 
...... tunaipenda wenyewe, chaguo letu milele......
 
Mkuu sidhani kama nitakosea nikisema aliye waruhusu kuingia barabarani alikuwa anatafuta "political mileage" na sasa anahisi kama wananchi hawamuelewi, so ni bora atengeneze hofu ili hata vijiweni muogope kupiga story za kukosoa au kushangaa madudu yanayofanyika. Kila mwenye akili alishangaa wakati alipotoa kauli ya kwamba wasibugudhiwe ilhali ni yeye ndiye aliesema mwanzo sheria na tataratibu zizingatiwe.hakuna asiyejua chaos wanayosababisha wamachinga mabarabarani ila tulivumilia kwakuwa mwenye nguvu aliwaruhusu wafanye biashara kandokando mwa barabara kwakuwa wao ndio wapiga kura.Ghafla waziri mmoja nae akaibuka na kutoa agizo wafurushwe maramoja, sasa tuelewe nani ni bosi wa nani na kauli ya nani ndio ya mwisho katika serikali? Maana nilitarajia aliewaruhusu ndio atoe tamko lingine la kuwaambia waende katika maeneo rasmi kama tayari wameshatengewa.Kiufupi nimelaani na kushtushwa na hatua zilizochukuliwa kwa kutumia excessive power kuwaondosha, hakika hii sio tanzania tunayoitaka.Wamachinga wanazo haki katika inchi hii kama raia wengine wowote.Unapowaahidi kitu na wakakushangilia halafu kimyakimya tena utoe maagizo nguvu itumike ni uzandiki mkubwa sana.
Ni kweli wamachinga wanaresist kwa sababu order ya kuwarudisha ilitoka juu kabisa Ila na wao wajue nchi ina taratibu na sheria mheshimiwa aliwaruhusu kipindi cha mpito na sio permanent! Pita ubungo pale wamejenga mavibanda ya hovyo hadi aibu
 
Mbunge wetu (kipenzi) Mabulla, kwenye zoezi la awali lililositishwa na rais alisema atawasaidia machinga kufungua kesi ili wamshitaki mkuu wa wilaya na mkutugenzi wa jiji ili walipwe fidia ya mali zao zilizoharibiwa na wagambo, sasa siku hizi simsikii sijui kaishia wapi!?
 
Ni kweli wamachinga wanaresist kwa sababu order ya kuwatudidha ilitoka juu kabisa Ila na wao wajue nchi ina taratibu na sheria mhedhimiwa aliwaruhusu kipindi cha mpito na sio permanent! Pita ubungo pale wamejenga mavibanda ya hovyo hadi aibu

mkuu mheshimiwa hakusema wakae kwa muda gani, ila alitoa maagizo wasibugudhiwe na mtu kwakuwa wao ndio wapiga kura. Haya ndio madhara ya kila jambo kufanywa kutokana na mihemko ya kisiasa.
 
Kitendo cha askari mgambo kumpiga yule mmachinga vile mpaka watu wengine wakawa wanawasihi kwa maneno ya watamuua kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote.. Kinachonisikitisha ni kwamba hakuna askari yeyote ambae atachukuliwa hatua na maisha yataendelea kama kawaida, kwa hao askari kuendelea kutembeza kipigo kwa raia wengine..

Very sad aiseee..
Mmesahau kuwa askari walishaua mwandishi tena mbele ya camera na maisha yakaendelea?
-rip Mwangosi
 
Muda sio mrefu utasikia ITV wakipewa onyo kali na serikali kwa kufanya uchochezi. AU
Repota wa ITV wa Mwanza (Mabere Makubi) ajiandae kukamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya na kuswekwa ndani.

Hii ni serikali ya awamu ya tano, hakuna mchezo.
Hapa kazi tu.
Hatutaki fyoko fyoko........
 

Hivi leo hawa machinga wa Mwanza waliokuwa wakimshangilia mtukufu miezi miwili
iliyopita leo wanajisikiaje wakiuguza majeraha kwa kipigo walichotembezewa?
Kweli wajinga ndio waliwao...!​

Hawa watu ukiwaona leo wamefimba midomo
 
Mliambiwa na bado mnaambiwa kwamba MAGUGU ni boya na hafai kuendesha gari hili.
 
Kweli inatakiwa watu kuoneana huruma mtu hela anaitafuta kwa shida jua limewaka biashara yenyewe inatembezwa hujui utapata sh. ngapi maisha yamekuwa magumu vitu vinapanda bei sasa mtu anatumia uwezo wake wakuzungusha ujasiliamali wake bado unamwadhibu vibaya ikumbukwe pia hawa nao ni watu nao wanahitaji maisha mazuri, pia hebu hata serikali ijaribu ikae iwasikilize wanachotaka na iwajengee mazingira rafiki kutokana na hicho wanachofanya tuone kama haya yatatokea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom