Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

ni sawa ,ulishawahi ona wapi polisi haogopewi na raia??hii ndo njia sahihi,lazima polisi waogopewe
 
Ivi wanainchi tukiamua kua wakakamavu kidogo tunashindwa kukomaa na hawa mgambo?maana kupenda amani wakati wa vita ni ufala wa hali ya juu na ikibidi tukomae nao hata uku uswahilini maana hawa jamaa tunaishi nao.
 
Achana na machinga, kuna siku nilikuwa zangu pale posta cone tower, kulikuwa kuna askari polisi wakitimuana na bodaboda, ile staili aliyetumia yule polisi ya kumuonya yule boda boda si sawa. Baaba ya kufukuzwa na askari kule chini ferry bodaboda akawa anakimbilia juu kumbe huku juu kuna askari alikuwa amepaki na bonge rungu ilekukatiza tu pale usawa na jengo la ardhi jamaa alikula bonge rungu likalia kabisa tiii!! kwenye mgongo jamaa akayumba akayumba akayumba tena na kusepa na pikipiki yake huku akiwa ameshikilia mgongo wake kwa maumivu.
 
HIVI WALE MAKABURU WEUSI ALIOSEMA HAYATI MWL. NYERERE. TOFAUTI NI RANGI TU. KWANI UTAWALA WA BHOTA NA MAGU TOFAUTI IPO WAPI? UBAGUZI WAKE NA UKANDAMIZAJI WAKE KILA CHA OVYO OVYO KAMA PACHA NA HAYATI NDULI IDD AMIN DADA.
 
Source; ITV.
Walioshuhudia mapigo ya wamachinga jijini Mwanza kwa macho or through ITV habari jioni wamesema hayo mambo yalikuwa yanatokea before 1994 kule South Africa na ni nadra sana kuyaona katika nchi huru.
Hivi si ni Rais aliyewaruhusu hawa Watanzania wenzetu wafanye biashara?
Tuna serikali yenye midomo miwili?
Machozi yamenitoka kuona mtu amepiga magoti kujisalimisha akipigwa teke usoni.
Usanii unapoanzia kichwani hata miguuni na mkiani ni lazima ujitokeze
 
Uko mwanza si ndio tulipata kura nyingi? Kweli tunaisoma nba
 
Source; ITV.
Walioshuhudia mapigo ya wamachinga jijini Mwanza kwa macho or through ITV habari jioni wamesema hayo mambo yalikuwa yanatokea before 1994 kule South Africa na ni nadra sana kuyaona katika nchi huru.
Hivi si ni Rais aliyewaruhusu hawa Watanzania wenzetu wafanye biashara?
Tuna serikali yenye midomo miwili?
Machozi yamenitoka kuona mtu amepiga magoti kujisalimisha akipigwa teke usoni.
Aisee nimeiona hiyo kitu imeniuma sana ndio maana nimejua kwanini serikali haiwajibiki juu ya unyama wanaofanyiwa watanzania huko msumbiji
 
Watanzania tumezidi unyonge ngoja wapigwe tu! Kila siku vilio vya mtandaoni
Words without actions ni upumbavu!!
 
Source; ITV.
Walioshuhudia mapigo ya wamachinga jijini Mwanza kwa macho or through ITV habari jioni wamesema hayo mambo yalikuwa yanatokea before 1994 kule South Africa na ni nadra sana kuyaona katika nchi huru.
Hivi si ni Rais aliyewaruhusu hawa Watanzania wenzetu wafanye biashara?
Tuna serikali yenye midomo miwili?
Machozi yamenitoka kuona mtu amepiga magoti kujisalimisha akipigwa teke usoni.
CCM ni chama kikatili sana , hata hivyo mateso ya watu wa Mwanza ni sawa na kutimizwa kwa utukufu wa Mungu , ukabila umewamaliza na wala hawana wa kumlaumu .

Binafsi nilitumia muda mrefu sana ikiwa ni pamoja na pesa zangu kuwaelimisha , lakini wakaamua kuchagua kifo badala ya uhai , majuto ni mjukuu .
 
Daaaah nimeangalia hiyo clip, ngoja nikae kimya tu mana wanasema ukiwa na hasira njia pekee ya kufanya maamuzi ni kukaa kimya
 
Sijaelewa kabisa ni kwanini wamempiga yule kijana aliyebeba nguo..

Huu ni ukatili na unyama wa hali ya aina yake!

Mgambo wenyewe wachovu wanapiga wachovu wenzao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom