Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!

Kampeni manager amefanya kazi yake ya kutuliza pepo za kusi zisije kuharibu flow ya mgombea wa Chadema kueleza atawafanyia nini wana Arumeru. Vicent hatawafanyia kitu wana Arumeru bali mgombea mwenyewe hayo mambo ya maji, umeme nk.

Mkapa tangu mwanzo amepotea njia anatafuta sehemu ya kujitokezea ili ajisafishe. Ni aibu kwa rais mstaafu kujikita kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo moja ambalo mmelishikilia kwa miaka yote. Amekwenda kuongeza yale tusiyoyafahamu kwenye CV yake. Kama wanavyotaka Chadema arudi kule wapambane. Aibuuuuu mzee mzima. Pumzika vizuri
 
Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!
Mkuu Keil, asante sana kwa hii, nawashauri wanaChadema wenye mapenzi ya kweli, waikate hii post, waipaste, waiprint na kuitumia kama msahafu wa kampeni!.

Kwa vile Vincent ni mtoto wa baba mdogo, CCM watamtumia mtoto halisi wa Nyerere preferably Madaraka au Makongoro ku caunter attack hii kauli ya Vincent huku CCM wakiwachagiza wazee wa familia ya Nyerere kina Chifu Wanzagi kutoa karipio kali la kutaka Nyerere aachwe apumzike kwa amani hivyo kuutumia kisingizio hicho kum disown Vincent na kum ex-communicate asizingumze lolote kumhusu Nyerere na hayo aliyozungumza ni ya kwake binafsi na sio ya kina Nyerere.

Nashauri concetration ya Chadema iachane na siasa za maji taka, ijikite kwenye issues!. Siasa hizi za maji taka na vijembe, zina hold water maeneo yenye uswahili kama ukanda wa pwani, Kanda ya Kaskazini ni issues tuu sio mipasho wala uswahili!.

Ule msimamo wangu uchaguzi Arumeru ilishaisha, bado uko pale pale!. Na kwamba kinachoendelea sasa ni kutimiza tuu matakwa ya katiba na kufiatwa tuu kwa taratibu, sheria na kanuni za uchaguzi ili kuhalalisha matokeo!.
 
Hizi ndio zinaitwa siasa za maji taka, wakati mwingine nadhani CCM wanazianzisha makusudi maana inaelekea kwa namna moja au nyingine zina wasaidia. CDM wananchi wa Arumeru Mashariki wanahitaji kujua sera zenu. Mkapa ni huyu huyu na lifanya hivi hivi Igunga.........ina maana tumesahau
 
Halali yake kabisa! Manake siku hizi amekuwa baba wa mipasho! Jitu zima na akili zako unakalia kutukana hovyo hovyo na kuleta mijadala isiyosaidia! What happened to u Ben! Think with your head ben! Not your balls!
 
Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!

Mkuu hapa umenena lakini mara nyingine kama CDM walivyosema kampeni hizi zina sura ya kitaifa so zinapokuja hoja kama alizoziibua Mkapa tena zingine zikimgusa Vincent Nyerere moja kwa moja lazima zijibiwe hapo hapo. Naamini majibu haya ya Bw. Nyerere siyo pekee yaliyotawala mkutano huo wa kampeni bali kulikuwa na muda wa kunadi sera pia
 
Na mtaona jinsi serikali ya CCM itakavyojiingiza katika kauli hii ya Vincent. Itamfungulia mashitaka ya jinai dhidi yake eti kwa kutoa kashfa.
kama ni kashfa (libel) ni haki ya Mkapa kumfungulia kesi VN. Nyie ngojeni tu mapolisi wa magamba watakavyofanya kama kawaida yao!
TBC wataandaa vipindi maalumu wakiwahoji wanafamilia wa Mwl Nyerere kukanusha hizi habari za VN. Siyo ajabu tutasikia Vicent si mtoto wa nje wa Josephat Kiboko Nyerere!
 
Kitaalamu watu wa kazi ambao wako busy kama mwalimu huwa sio watu wa kuugua hovyohovyo kwanza hawapo kwenye risk,predisposing factor za kupata maradhi hovyo tulishangaa mwalimu kupata maradhi yale na kukibizwa uingereza,hapa kuna jambo kina benny walilifanya na baada ya kufariki mwalimu walianza kugawiana ma kiwira kama njungu na huyu mkewe anaporomosha majumba tu huku tizama lile jengo la kitega uchumi la kibiashara analoporomosha pale Tegeta new bagamoyo road mama huyu alitumia ikulu ya mume wake kama mgongo wa kujinufaisha sasa wana mpango kabambe hawa CCM wa kuweka madarakani watoto wao iliwawalinde wakiustaafu ndio haya ya kina Sioyi.
 
siasa za bongo ni za kuchafuana tu ni style ya mwaga mboga nimwage ugali wote tulale na njaa but all in all watuonyeshe utekelezaji wa ahadi zao hapo baadaye
 
hata mi nilijua tu kuwa kuna mkono wa mkapa kwenye kifo cha jk ila sikuwa tu na ushahidi. Natamani hii ingekuwa ni ndoto tu kwa mkapa maana sasa amejipeleka kwenye kona na hana pakutokea
 
Na mzee wenu aliyeanza matusi je?
Mkapa alisema ukweli, hajawahi kutambulishwa na JKN huyo mtu anayeitwa Vicent...
Sasa kushare tu sir name na Nyerere huyo Vincent tayari anajiona ni wa familia ya JNK!
BTW huyo Josepahat ndio nimemskia leo...nyerere sidhani kama alishawahi kumtambulisha popote as well!
 
Maswali ya kujiuliza ni haya:

kwa nini mkapa alimpiga marufuku daktari wake Mtanzania asimsogelee mwalimu wakati akiwa hosptali?

Pili, ni kwa nini serikali iliamua kumpeleka London wakati walijua kuwa Uingereza haikuwa na uwezo wakati huo kutibu leukemia, kama kweli leukemia ndio uliomsumbua Mwalimu?

Kwa nini daktari wake hakushauri apelekwe New York kwa yule daktari aliyempima Mwalimu 1998?

kwa nini walipomfikisha london hawakumpeleka hosp moja kwa moja bada yake wakamuweka mwalimu hotelini hadi alipozimia ndo wakampeleka hosp?

Kwa nini alipelekwa hospitali ya St. Thomas ambayo ni general hospital isiyo specialize na magonjwa maalumu?

kwa nini hakuwekwa chumba maalumu akawekwa tu eneo wazi la wagonjwa wote?

napenda kuhitimsha hivi mkapa anahusika na kifo cha mwalimu Nyerere
 
Kwa habari ya siasa chafu nahakika CCM wakiamua kulikomalia victim atakuwa Vincent, maana anaweza kukanwa hadi na ukoo wake mwenyewe
 
Maneno ya mwalimu wakati anakwenda kutibiwa alisema anakwenda kufanyiwa uchunguzi tu wa afya yangu kwa maana hiyo hakuwa anaumwa kivile tukashangaa inarudi maiti yake baba huyu Mkapa naroho yake ya kishetani hakutangaza kifo cha mwalimu mapema iliafanye maandalizi alikuwa anajua anachokifanya leo yako wapi Benny.
Nyerere alikwenda London na nguvu zake akitembea airport na kupungia watu mkono kumbe ndio alikuwa anatuaga.
 
Nasubiri kimbunga atakacho shuka nacho!!!Dah!kujibu hoja!!Nakampeni itaishia hapo!
 
TBC wataandaa vipindi maalumu wakiwahoji wanafamilia wa Mwl Nyerere kukanusha hizi habari za VN. Siyo ajabu tutasikia Vicent ni mtoto wa nje wa Josephat Kiboko Nyerere!
Tena wadai genes za kina Nyerere zina chembechembe za CCM, hivyo kitendo cha Vincent kujiuunga Chadema ni uthibitisho dili ilichezwa hivyo kudai anayepinga DNA ifanyike kuthibitisha not only ni mtoto wa nje bali pia wa kusingiziwa!.
 
Ni daktari gani huyo aliyenyamazishwa kwa kupewa uwaziri?
Bila shaka daktari anayezungumzwa hapa ni Prof. David Mwakyusa ambaye ndiye aliyekuwa dkt wa Mwalimu mpaka mauti yake. Lakini hapa ndio napata mashaka na ukweli wa tuhuma hizo maana ukweli ni kwamba Prof.Mwakyusa aliteuliwa kuwa Waziri wa Afya 2006 tena na JK wala sio Mkapa. Kipindi cha utawala wa Mkapa huyu daktari alikuwa mbunge wa kawaida tu. Sasa wakati mwingine mtu unaweza ukawa unajichanganya mwenyewe kwenye maelezo kwa kutoa taarifa zisizo za kweli na mwisho wa siku tuhuma zako zikahusishwa moja kwa moja siasa za majitaka.
 
khhaaaa haya maneno ni mazito sijawahi kuyadhania...mhhh kumbe mkapa ndo ulivyo hivo!!!.....
 
Back
Top Bottom