Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Soma thread za wenzako ujue majibu yake na sio unafungua thread mpya kama juha! Mbona unakuwa kiazi kama huyo Che Nkapa!

Majibu yako sawa na Vicent, unaonekana una PhD ya matusi na ndio maana mna mispoint, kwa sababu media zimecapitalize tuhuma alizotoa si ufafanuzi kuhusu ubini wake.
 
Kwani alishawahi kujitangaza yeye ni mtoto wa Julius Nyerere? Kwani hili jina amejibambika? Yeye ni mtoto wa Mzee Josephat (Kiboko) Nyerere ambaye ni mtu na kaka yake na Julius Nyerere. Hivyo jina la Nyerere kwake ni sawa. Che Nkapa alitaka kumbomoa Vincent na CHADEMA kisiasa kwa kupakazia kuwa jina la Nyerere limetumiwa kujitafutia umaharufu- Sasa amejikaangia sumu na wanafamilia hao. Haya sasa....
 
Duniani kote wanajua maradhi yaliyokuwa yanamsumbua baba wa Taifa mwalimu Nyerere sasa watu wanapotosha Kizazi cha taifa letu ,huyu Mkirua kwenye jamii Forum si mtu mzuri anawafundisha nini kizazi chetu kuwa taifa letu ni taifa la Wauaji Mungu akusaidie na serikari ukusaidie pia kwa njia yoyote hata kupimwa kichwa
 
Kuna jamaa aliwahi kuniambia Mwl aliwekewa toilet paper za kimafia na TISS aliokuwa akiwaamini sana baada ya muda mfupi Kapt Komba akaambiwa aandae nyimbo za maombolezo masikini Nyerere wangu daima nitakukumbuka.

Mkapa mshahara wa dhambi ni mauti angalia sasa unavyoumbuka wengi walikuwa hawajui hii maneno umeingia kichwa kichwa vijana wanakupa za uso bila soni.


1995 Nyerere aliingizwa mkenge na wajanja kuwa Mkapa anafaa wakati chaguo lake lilikuwa Salimu. Lakini JKN alikuja kugundua Mkapa kawa siye yule aliyembeba. Baada ya Mkapa kuingia tu Ikulu akaanza kuuza mashirika ya umma kwa mgongo wa ubinafsishaji kwa rafiki zake hasa wa SA akijua JKN hawezi mfanya lolote. Nyerere alikasirika sana akamwambia kwanini lakini? Mkapa akamjibu hatuwezi kukwepa impact ya globalization. Well but don't touch (MY) NBC. Baada ya Mkapa kuona mchonga kakasirika wenzake ABSA wakamshauri aigawe NBC, by 1997 zikawa NBC 3. Nyerere aliijua hiyo mbinu ila hakuwa na uwezo tena wa kuzuia akawa anasema pembeni kama kunung'unika vile, wakaona isiwe tabu ndipo walipoanza kutafuta alternatives kwa kushirikiana na TISS. Baada ya kifo chake 1999 haukupita hata mwaka NBC(1997) ikauzwa SA. Watu wana connect dots. Kama mtakumbuka Mwakyusa aliyekuwa dokta wake siku chache kabla ya kifo familia ya Nyerere ilimpiga marufuku kwenda hosptali alikolazwa London.
 
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.

Huna weredi wewe! Mwanaasha mkubwa wewe
 
Kuanzia chaguzi kuu hadi hizi ndogo wanachofanya CCM ni kama kumtupia mbwa mfupa anabaki anahangaika nao kuula wakati mwizi anapita getini. hilo ni moja tu mengine yanakuja, matokeo yake kampeni za CDM zinakuwa za kujibu mapigo badala ya sera
 
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.

Mbona kasema yeye ni mtoto wa Josephat wewe ulitaka asemeje? Au ulikuwa na shauku kusikia yeye ni mtoto wa Julius?
 
mkuu umesema ukweli kabisa,
aseme tu walichomfanyika baba wa taifa hili.
 
Mwl. Nyerere ni kiongozi bora aliyekuwa mbele kutetea maslahi ya wanyonge. Hii habari kwamba kuna huyu mtu kahusika kumuua kisa tu aliingilia ajenda yake ya kuuza nchi inasikitisha sana. Mnaweza kulindana kwa hili lakini Kwa kadri ya neno la Mungu aliye hai laana itamwandama pamoja na kizazi chake mtu yoyote atakayemwaga damu isiyo na hatia.

Mbona CCM wamemwaga damu nyingi tu za wasio na hatia lakini bado wanapeta? au nikutajie uwakumbuke? DR. Juma, Kolimba, Sokoine,
 
Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!

Uko sawa mkuu lakini tunahitaji wananchi wa Tanzania washikwe na hasira. Wakishikwa na hasira wataachana na hawa watumia sumu wasitumalize. Hebu fikiria ni nusu tu ya wananchi wa Arusha mjini ndio walikataa madiwani wa CCm na nusu nyingine ikawachagua leo Arusha haitawaliki tofauti na kama wananchi wote wangeikataa CCM. Ngoja kwanza tuanike siri za hawa wauaji!
 
Piga nikupige eti Ben kambip Vincent
Jana katika hotuba yake ametumia muda mwingi sana kuisema CHADEMA na akanisema mimi kwa jina moja kwa moja, sasa ‘kanibipu' na mimi nimeamua kumpigia,alisema Vincent Nyerere
 
Ndio maana CCM wanamwita Mkapa kwenye uchaguzi mgumu kwao wakiamini ni jabali kwakuwa ndie pekee aliweza kumuua Mwalimu kwakuwa CCM ya sasa ya kina Mkapa ilikuwa ikipingana na sera za mwalimu,sasa tunaona Mkapa ana wine kuendesha sera za kifisadi kwa hali ya juu baada ya mwalimu kufariki anaziendesha kibabe na kwanguvu aridhi na madini vinauzwa kwa fujo mbuga za wanyama hata maziwa kama victoria vinauzwa hasa maeneo ambayo samaki sangara wanapopatikana ni huyu bwana Benn.
 
Siku zote nimekuwa nikijiuliza huyu Ben tatizo lake lipi kwanini asiachane na siasa? Kitendo cha kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa kwenye kampeni za ccm ni kosa kubwa la kujutiwa katika siku zake za uhai zilizo salia, ana mengi ya kujibu kwa wananchi badala ya kutoa matusi na kebehi, ingekuwa bora kwake leo akakaa kimya na kutojiingiza kwenye siasa za maji taka.

Ninachoweza kusema ni kwamba hakuna siri chini ya mbingu inayoweza kusitirika, mabaya yake yote yanafahamika na ukizingatia teknolojia ya habari na mawasiliano ndio usiseme kabisa, vijana wana kila taarifa, nzuri na mbaya hivyo ni bora kujua madhara yanayoweza kutokea kabla ya kukurupuka.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nasikia kuwa Prof. David mwakyusa ndo Alikuwa Dr. Wa mwalimu? So huenda anajua kuna uzi unaendelea, lkn huu ni tofauti kidogo, maneno yamezuka arumeru, kazusha v.nyerere kuwa mwl. Aliuliwa na yeye kupoozwa na uwaziri. Nadhan Dr. Wake anautaalamu Zaidi na anaweza kutupa ABCs,


Mimi nadhani Dr.hawezi kueleza lolote maana amekuwa kimya mno toka tukio hadi sasa ni muda mrefu zaidi atatudanganya kufuatia upepo wa kisiasa ulivyo.
 
Kuna jamaa aliwahi kuniambia Mwl aliwekewa toilet paper za kimafia na TISS aliokuwa akiwaamini sana baada ya muda mfupi Kapt Komba akaambiwa aandae nyimbo za maombolezo masikini Nyerere wangu daima nitakukumbuka.

Mkapa mshahara wa dhambi ni mauti angalia sasa unavyoumbuka wengi walikuwa hawajui hii maneno umeingia kichwa kichwa vijana wanakupa za uso bila soni.



aina ya sumu iliyowekwa ni arsenic....na mwalimu aliwekewewa huko South africa
 
Duniani kote wanajua maradhi yaliyokuwa yanamsumbua baba wa Taifa mwalimu Nyerere sasa watu wanapotosha Kizazi cha taifa letu ,huyu Mkirua kwenye jamii Forum si mtu mzuri anawafundisha nini kizazi chetu kuwa taifa letu ni taifa la Wauaji Mungu akusaidie na serikari ukusaidie pia kwa njia yoyote hata kupimwa kichwa

Duniani kote waliambiwa na Mkapa.......au wewe bado unaamini Osama alizikwa baharini just because duniani kote tuliamabiwa hivyo na Obama?
 
Mkuu Pasco,

Makongoro aliwahi kuwa mbunge wa Arusha 1995 kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.


asco;3493390]Tena wadai genes za kina Nyerere zina chembechembe za CCM, hivyo kitendo cha Vincent kujiuunga Chadema ni uthibitisho dili ilichezwa hivyo kudai anayepinga DNA ifanyike kuthibitisha not only ni mtoto wa nje bali pia wa kusingiziwa!.[/QUOTE]
 
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.
Vicent Nyerere hajawahi sema yeye ni mtoto wa Mwl. Nyerere. Wakati wa kampeni 2010 huyu VN ametangazwa sana ktk vyombo vya habari,ikiwemo JF kama mtoto wa Josephat Kiboko Nyerere sasa hizi habari za kipuuzi wewe na Mkapa mmezitoa wapi?
 
Vincent Nyerere ni mtoto wa nje wa mdogo wake Nyerere, Familia ya Nyerere hawamtambui kabisa mdogo wake Nyerere alizaa na mwanamke mmoja pale Makoko.
 
Back
Top Bottom