waacheni wabunge wafanye shughuli zingine muhimu msiwaongezee mzigo usio wa lazima. jambo la kufanya vikao vya chama Ikulu ya nchi siyo sawa na hata alieitisha anaelewa hivyo ila kaamua kujitoa ufahamu tu.
 
Raisi haungwi mkono kwenye chama wala kwenye jeshi kwahiyo sehemu pekee salama kwake ni ikulu / anahisi.
Ulishawahi kuona wapi huko nyuma raisi akiongozana na mkuu wa usalama wa taifa kwenye ziara zake? Unajua kwanini?
Tukiwa arusha raisi alilazimika kwenda monduli usiku kwenda kuwapigia magoti wanajeshi baada ya kutaka kumgomea.
 
24E7071A-9180-44A9-B987-C2707700F984.jpeg


Moja kati ya matamanio yangu ya muda mrefu sasa ni kuona vikao vya CCM kufanyika Ikulu vikikoma kabisa.

Sina uhakika sana huu mtindo ulianza lini lakini nakumbuka kipindi cha utawala wa Rais Kikwete, ulishamiri sana.

Ikulu ni mahali pa shughuli za kiserikali. Siyo mahala pa shughuli za chama cha kisiasa.

Itapendeza endapo huyu Rais wetu mpya hataendelea na huo mtindo.

Akiuendeleza, tutamkosoa tu. Haogopwi mtu. Hapendwi mtu.

Tanzania kwanza.
 
Waking'ang'ania kuendelea kukutania Ikulu basi akina TADEA na wengine wote waruhusiwe kutumia Ikulu kwa mikutano yao ya kisiasa. Iwe Ikulu vurugu.
 
Afanye tu kikubwa tuwe na Amani, Hamna kutekana, kuuana, kupigana risasi, kupotezana kama enzi za Magufuli.

Enzi za JK tulikuwa na Amani, hela ilikuwepo hatukuwahi kusikia vyuma vimekaza hata kama alifanya hayo usiyoyataka.

Mama pia achia hela kitaa wewe uendelee na mambo yako
 
Back
Top Bottom