Video: Uhaini wa Lissu uko hapa

Video: Uhaini wa Lissu uko hapa

Sehemu ya kwanza kwa tafsiri ya kizungu kupitia chatgpt

1787399547979.png

1787399598711.png
 
Kuzuia uchaguzi ndio uhaini?

Halafu Lissu alizuia vipi mnaoita uchaguzi uliofanyika October na yeye alishikiliwa tangu April ?
 
Hiyo ulitakiwa iwe kesi ya uchochezi unajua maana ya uhaini?
Na kesi za uchochezi ni takataka zinazotumika kuwakandimiza wapinzani.

Angalia nchi zenye sheria za kesi za uchochezi ni nchi zile zile takataka.

UK na Australia walishafuta hii sheria ya kikandamizaji 2009/2010, sisi huku gizani tunaendelea kuzikumbatia sababu zinatumika kama tool dhidi ya wapinzani.
 
Kama Nyerere alimaanisha unachotaka, mbona hakuwavumilia akina Kambona, Bibi Titi, Kasangatumbo, Mapalala, Seif Shariff Hamad, Horace Kolimba?
Kusema mtu hawezi kuwa mhaini kwa sababu ameshtakiwa peke yake ni kuchanganya uhaini na conspiracy. Section 39(2) haidai lazima kuwe na washirika; inahusu hata mtu mmoja anayefanya nia yake ionekane kwa maandishi au kitendo cha wazi. Mfano, mtu mmoja akipanga kumpindua Rais au kuzuia Serikali kwa nguvu na akadhihirisha nia hiyo, anaweza kuwajibika chini ya 39(2).

Mfano wa wazi ni William O. Meighan, aliyeshtakiwa Uingereza katika kesi ya treason-felony mwaka 1868. Mashtaka yalihusu nia ya kumpindua Malkia na vitendo vya wazi (overt acts); baadhi ya mashtaka yalikuwa yakimlenga yeye binafsi, si lazima kuwe na mshtakiwa mwenza
 
Boss, hadi hapa nakushauri ufanye ustaarabu na kukubali kuwa hoja hii imefeli. Bora uzingatie ushauri uliotolewa na wadau hapa uwaambie wakuu wako huko government wabadili mashtaka kuwa uchochezi. Halafu waipunguze ile patoon ya maninja wanaomsonga Lissu all the time na hali yake ile huko mahakamani. Wanatia aibu.

Usiwe kama Trump aliyebaki kuropoka ropoka vitisho kila siku na kulidhalilisha jeshi la Marekani huko mashariki ya kati badala ya kufanya ustaarabu wa kumalizana na kina ayatollah kwa makubaliano muafaka. Yaani anashindwa kuona kuwa hakuna cha Venezuela pale.

Nilikuelewa hoja zako kali kuhusu JPM enzi zile lakini sasa naona umeamua kushuka na kuungana na watu duni (big show, mwashambwa na tlaatlaa) kwa kulazimisha hoja duni bila sababu zinazoeleweka. Ni kama vile una kero binafsi na watu fulani hivi. Umeshindwa kabisa kuona moral context anayopambania Lissu nchini kwa muda mrefu sasa? Yaani umeamua kushusha brand ghafla sana. Why?
Tusipangiane cha kuandika. Hawa akina Tundu walimkimbia Magufuli, na alipokufa Mama kawarudisha na kuwafutia kesi zao. Walimdharau ngoja wacheze ngondoigwa
 
Hochomoi hiyo huyo mwendawazimu

Amesababisha umwagaji damu na uharibifu mkubwa sana ndani ya Taifa hili

Ale kitanzi tuh fala huyo
Mama yenu alitwambia waandamanaji walilipwa fedha ili waandamane, ni nani aliwalipa?? na ni nani alitoa order to kill?? na je uchaguzi ulifanyikaau haukufanyika?? kama ulifanyika maanake uchaguzi haukuzuiwa. na kama haukufanyika kwa sababu ya kauli ya Lissu je kura 32M alizopata mama yenu zilipatikanaje?
 
Kwa wale wasioridhika na maamuzi ya jana ya jopo la majaji wa Mahakama kuu chini ya Jaji Ndunguru, wasikilize tena clip hiyo. Tundu lazima aeleze hiyo kauli ilikuwa ina maana gani?

Tundu alete mashahidi watakaomtoa kwenye hiyo kauli, na siyo drama za kumleta Rais, kitu ambacho kwa Katiba yetu hakiwezekani.
Bila shaka mnausaka "uhaini" kwenye haya maneno:

1. "Tutahamasisha uasi"

2. "Tutauvuruga vuruga kweli huu uchaguzi"

3. "Tutakinukisha kwelikweli"

Ufafanuzi wa kukujengea ufahamu

#TUTAHAMASISHA UASI:

Maana yake ni rahisi tu ni kujenga awareness kwa watu ili kuzikataa na kuzipinga taratibu na sheria mbaya za jambo fulani linalofanyika au linalotarajiwa kufanyika, bila shaka HUO NI UASI MTAKATIFU, UNAOFAA

#TUTAVURUGA VURUGA KWELI UCHAGUZI HUU:

Maana yake ni moja na rahisi tu, watu hawataenda kupiga kura kwa kuwa wanakuwa wameelewa kuwa wanachokwenda kukifanya hakuna maana yoyote kwao kwa kuwa matokeo ya kupikwa yameshaandaliwa tayari. Kwa kitendo hiki taratibu zote za kupiga kura zilizoandaliwa na wezi wa uchaguzi zinakuwa zimevurugika vurugika kwelikweli!

#TUTAKINUKISHA KWELIKWELI:

Maana yake ni rahisi tu, kuwa hii ni lugha ya picha ikiwa na maana ya kuvuma na kuenea kwa jambo au tukio fulani kwa mfano wa harufu inayotokana na kitu fulani kunuka. Watu kutojitokeza kupiga kura kulishitua waanadaa uchaguzi na wezi wa chaguzi (CCM na serikali yake).

Kwa ujinga wao wakajiingiza wenyewe kwenye mtego wa maneno haya ya Tundu Lissu.

Wakafungua maghala ya silaha, wakawapa Polisi na wanajeshi na kuagiza kuua kila wanayekutana naye mitaani na wengine kufuatwa majumbni, vijiweni na maeneo ya starehe bar, mabanda umiza ya mpira, vijiwe vya kahawa nk..

BTW, subiri. Hili somo ni zuri sana. Utaendelea kulipata tokea mahakamani. Lilianza jana Ijumaa, litaendelea J3 na siku zinazofuata mpaka muelewe na yaingie kwenye akili zenu..
 
Jaji kasema japo ushahidi ni dhaifu sana lkn yeye haawaangalii ushahidi wanaangalia maneno. Hawajui kwamga kesi hii ni ya KIFO?
 
Hiyo maana uneotoa kwenye kamusi gani?
 
Hochomoi hiyo huyo mwendawazimu

Amesababisha umwagaji damu na uharibifu mkubwa sana ndani ya Taifa hili

Ale kitanzi tuh fala huyo
Ni kweli alitoka jela nakwrenda kuwapiga watu risasi, magereza wanapaswa kihojoea ilikuwaje aruhusiwe kutoka kwenye mikono yao
 
Kwa wale wasioridhika na maamuzi ya jana ya jopo la majaji wa Mahakama kuu chini ya Jaji Ndunguru, wasikilize tena clip hiyo. Tundu lazima aeleze hiyo kauli ilikuwa ina maana gani?

Tundu alete mashahidi watakaomtoa kwenye hiyo kauli, na siyo drama za kumleta Rais, kitu ambacho kwa Katiba yetu hakiwezekani.
Hakuna uhaini hapo. Uhaini ni conspiracy na matendo, sio public statements. Na duniani hakunaga conspiracy ya mtu mmoja, kwasababu, by definition, a conspiracy requires an agreement between two or more people!

Kama angekuwa anakabiliwa na mashitaka ya uchochezi angalau kungekuwa na hoja ya kujadili.
 
Kwa wale wasioridhika na maamuzi ya jana ya jopo la majaji wa Mahakama kuu chini ya Jaji Ndunguru, wasikilize tena clip hiyo. Tundu lazima aeleze hiyo kauli ilikuwa ina maana gani?

Tundu alete mashahidi watakaomtoa kwenye hiyo kauli, na siyo drama za kumleta Rais, kitu ambacho kwa Katiba yetu hakiwezekani.
Ungeipeleka mahakamani ingesaidia sana,Jaji asingesema kuwa mahakama haiangalii uzito wa ushahidi wala kuaminika kwake'.
 
Swali kuu ni hili.

Kama mnakiri uchaguzi ulizuiliwa kwa kukinukisha je Samuya alipataje uhalali wa kuitwa rais ilhali uchaguzi haukufanyika?
 
Kusema nitakuibia haitoshi kumshtaki mtu kwa kosa la wizi,anyway CCM na mapunga yenu mnajua mnachofanya,msitupotezee muda katafuteni wauaji na watekaji kwanza
 
Back
Top Bottom