Lissu kuachiwa Agosti 21?

Lissu kuachiwa Agosti 21?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,122
Reaction score
17,405
LISSU KUACHIWA AGOSTI 21? MAJAJI KUAMUWA KAMA ANA KESI YA KUJIBU AU LA SIKU YA IJUMAA

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam leo Agosti 17, 2026 kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 21, 2026 siku ya Ijumaa ambapo Majaji watatu wataamuwa kama Tundu Lissu ana kesi ya kujibu au la.

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu imeahirishwa hadi Ijumaa ya Agosti 21 ambapo mahakama itaamua kama Mwenyekiti huyo wa upinzani nchini ana kesi ya kujibu au la!

Kesi hiyo Na.19605/2025 ilianza kwa upande wa Jamhuri kufunga mashahidi wake 17 kati ya 30 ambao walitoa ushahidi wao.

Baada ya kufunga mashahidi hao, upande wa mashtakiwa Tundu Lissu alitoa Submission (Majumuisho) ya ushahidi wote uliotolewa Mbele ya Mahakama huku akisema baada ya kusikiliza mashahidi wote 17 wa upande wa mashtaka,upande huo umeshindwa kabisa kuthibitisha kwamba (Prima-facaie case/Evidence )ni "ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka usipojibiwa na upande wa mteteze, Mahakama inaweza kumhukumu mtumhumiwa.

Mshitakiwa amesema kuwa prima facie evidence kimsingi ni ushahidi wa upande wa mashtaka peke yake na kama haujafikia kiwango au kujibiwa hakuna kesi.

Amesema kifungu Cha 312(1) kinasema kuwa, kama haujafikia ushahidi uliotolewa,Mahakama utasema hakuna hatia.

Akiendelea kutoa utetezi wake, Lissu amesema hicho kifungu Cha 312(1) kimefanyaiwa maamzi mengi ya nchi yetu kwa kutengeneza misingi mikubwa ya Kisheria juu ya kitu gani Mahakama inatakiwa kujibu kuhusu hakuna kesi ya kujibu(No case to answer).

Amesema msingi mkuu Wa Kisheria juu ya kwamba hakuna hoja ya kujibu iliwekewa tangu miaka 70 iliyopita na mahakama ya Rufani Afrika Mashariki.

Amesema kesi hii si ya kwanza kufanyika nchini Tanzania,bali ni kesi ya tatu,iwewemo ya Khatibu Gandi na wenzake dhidi ya Jamhuri.

Amesema katika kesi ya kwanza kati ya Gray Nkunku Matata na wenzake iliweka vigezo vitatu kuthibitisha kama kesi ni ya uhaini,akitaja vipo ukurasa wa 406.

Utiifu wa Jamhuri,Je, ulikuwa na nia ya kutenda kosa la uhaini?,hiyo nia lazima uthibitishwe kwa maandishi au kwa matendo ya wazi. 39(2d) kwa mujibu wa kifungu Cha makosa ya adhabu.

Aidha Lissu ameendelea kuisisitiza Mahakama kuturuhusu kujitetea kwasababu hana kesi ya kujibu

Hata hivyo mshitakiwa amesema bado Mahakama inaweza kutoa fidia kwa hizo siku zote 496 kutokana na kifungu Cha 367.
 
Bado wanatafuta Kesi? Sasa mwaka mzima walikuwa wanatafuta nini?
 
LISSU KUACHIWA AGOSTI 21? MAJAJI KUAMUWA KAMA ANA KESI YA KUJIBU AU LA SIKU YA IJUMAA

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam leo Agosti 17, 2026 kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 21, 2026 siku ya Ijumaa ambapo Majaji watatu wataamuwa kama Tundu Lissu ana kesi ya kujibu au la.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 248

Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji ni muhimu kukumbuka kuwa, mimi ni mshtakiwa pekee katika kesi hii na ikumbukwe katika kesi ya Khatibu Gandi inasema maneno ya mtu mmoja, hayatengenezi uhaini, kwa ushahidi uliotolewa haujathibisha nia ya kutenda kosa la uhaini then on the basis kuwa kusipokuwa na primafacie case nitaitwa nijitetee kwa kipi?

Ni ushahidi gani nisipojitetea utanitia hatiani? Ushihidi ukoje kuhusu publication ya reasonable act?

Lazima kuwe na ushahidi wa machapisho au matendo ya wazi wakati wa pre trial Upande wa Mashtaka wanasema mimi nilichapisha maneno kwenye mtandao wa Jambo TV, hivyo uthibitisho wa haya maneno ulitakiwa uwepo Jambo Tv.

Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwaelekeze ukurasa wa 185 wa record za Mahakama, upande wa mashtaka ulionyesha ushahidi wa nyaraka 9 na aina 2 za vielelezo ikiwemo Video clips, hawajaleta hata moja.

Shahidi PW 17 ni shahidi pekee wa eye witness aliyenishuhudia kwenye mkutano, testimony ya mashahidi, shahidi PW 17 ndiyo shahidi mwenye ushahidi mzito, alisema yeye na wenzake watano ndiyo waliorecord na kurusha, amesema kwa maneno yake na kwa maandishi kupitia kielelezo D16 na ni shahidi wao, Kwahiyo kama ni tuhuma ya publication siyo yak wangu, aliyepublish ni PW 17 na amesema mpaka leo vipo kwao.

Ushahidi wa nani aliyechapisha hawajaujibu.
Waheshimiwa Majaji, walidai ooh wewe ndiye uliyeitisha Mkutano, shahidi wao PW 17 amesema mwaliko waliupata kwa afisa habari wa Chadema anaitwa Brenda Rupia, na nikamuuliza uliniona mimi nikifanya maandalizi nikipanga viti akasema, hakuna.

Kwenye hili suala la tatu hawajathibitisha kabisa kosa la kuchapisha maneno.

Naomba nimalizie,

Kama hakuna proof ya kucommint treason act, hakuna intention maana yake ni kuwa hakuna primafacie case, na kama hakuna primafacie case mkiruhusu nijitetee mtakuwa mnafanya makosa ya kisheria.

Sasa Waheshimiwa majaji msipokubali mnafanyaje? Mnafanya kile ambacho sheria imewataka mfanye kwa mujibu wa kifungu cha 312 (1) kufanya finding ya kuwa hakuna case ya kujibu.

Waheshimiwa Majaji naomba kama mtatoa huo uamuzi muutoe leo, kama mnaridhika na hoja hii, reason ruling mtatupa baadae, hakuna haja ya mimi kurudishwa Ukonga leo. Hili ni la pili;

La 3 lipo kwenye kifungu cha 367 cha CPA (Sheria ya Makosa ya Mwenendo wa Jina), kama mashtaka ni ya uonevu ya kusingizia mnaweza kuamuru mtuhumiwa alipwe fidia, haya maumivu yangu na familia yangu nani atafidia?? mashahidi wote 17 mmewasikia.
Hivyo naomba iamriwe kuwa sina kosa la kujibu pia ipangwe tarehe nije kuthibitisha madai/ fidia yangu.

Naomba niwape Waraka wa kikosi kazi wa Umoja wa Mataifa, uamuzi wa tarehe 23/2/2026 unaosema niachiwe mara moja na kulipwa fidia. Hivyo Waheshimiwa Majaji msimamo ni kuwa hakuna primafacie case na kwakuwa hakuna Primafacie case, sheria inawataka muandike findings ya NO CASE TO ANSWER

Waheshimiwa majaji ya kwangu ni hayo tu.

Mhe. Lissu anamaliza na kuketi.

Jaji Ndunguru : Ehee Jamhuri ?

Wakili wa serikali Katuga anasimama anasema Upande wetu kwanini tunaona mshatikiwa ana kesi ya kujibu ni kutokana na makosa aliyoshtakiwa nayo kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) (d)

Anasoma kosa kama lilivyoainishwa katika hati ya mashtaka na anaainsha maneno ya uhaini...

"WANASEMA KITU KIMOJA SAHIHI HAPA, WANASEMA TUTAHAMASISHA UASI, NI KWELI TUTAHAMASISHA UASI, TUTAKINUKISHA VIBAYA......"

Waheshimiwa DPP Vs Philipo Joseph Mtonda, 217 Rufaa ya jinai, Tanzlii 2021.... case hii ili cite case Tambaklal na ikarudia maneno ya hiyo Landmark cases ya Tambklal case.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba Mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.

Akiwasilisha hoja zake leo Agosti 17, 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru Lissu akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha ile aliyoiita Prima facie case (kutokuwa na kesi ya kujibu).

Lissu ameieleza Mahakama kuwa kuwa Prima facie evidence/case ni ushahidi wa upande wa mashtaka pekee yake kama haujafikia kiwango cha kumtia mtuhumiwa hatiani usipojibiwa hakuna hatia na Mahakama inatakiwa kurekodi mtuhumiwa kutokua na hatia.

Akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na maamuzi ya Mahakama katika kesi kadhaa ikiwemo ya kesi ya Rambaklal Trambaklal Bhatt dhidi ya Jamhuri amesema zimetengeneza misingi ya kisheria juu ya kitu gani mahakama inatakiwa kufanya kuhusiana na hoja ya kutokuwa na kesi ya kujibu.

Sababu ziliaoainishwa na mahakama hizo ni kuwa ni utiifu wa Jamhuri ya Muungano, lazima kuwe na uthibitisho wa nia ya kufanya kitendo cha uhaini na hiyo nia lazima ithibitishwe kwa maandishi au matendo ya wazi.

Anaeleza kuwa suala la utiifu kwa Jamhuri ya Muungano halina mjadala na suala lenye shida ni je kulikuwa na nia ya dhati ya kufanya uhaini akieleza kuwa katika maneno yaliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka ambayo aliyatoa April 3, 2025 na pia kupitia ushahidi wa mashahidi 17 wa jamhuri hakuna sehemu alipoonyesha nia ya kuitisha serikali kwani hakuna sehemu ilipotamkwa.

Lissu anasema kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani ya mwaka 2023, Sheria ya Kanuni ya Adhabu na sheria zingine hazithibitishi kosa la uhaini analodaiwa kulifanya.

1786970696361.png
 
Kwa tunacho weza kuita jeuri , wanaweza kumkuta na hatia ili isionekane walikosea, kisha mkuta na hatia namna ya kumaliza labda isha andaliwa ili mradi tu asikose jinai, nawanavyo sema jinai haifi.

Ila kama kuna mtu wa kumchukulia mfano wa mapambano yoyote ni lisu! Ni mpambanaji haswa.
 
LISSU KUACHIWA AGOSTI 21? MAJAJI KUAMUWA KAMA ANA KESI YA KUJIBU AU LA SIKU YA IJUMAA

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam leo Agosti 17, 2026 kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 21, 2026 siku ya Ijumaa ambapo Majaji watatu wataamuwa kama Tundu Lissu ana kesi ya kujibu au la.
View attachment 3651931

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu imeahirishwa hadi Ijumaa ya Agosti 21 ambapo mahakama itaamua kama Mwenyekiti huyo wa upinzani nchini ana kesi ya kujibu au la!

Kesi hiyo Na.19605/2025 ilianza kwa upande wa Jamhuri kufunga mashahidi wake 17 kati ya 30 ambao walitoa ushahidi wao.

Baada ya kufunga mashahidi hao, upande wa mashtakiwa Tundu Lissu alitoa Submission (Majumuisho) ya ushahidi wote uliotolewa Mbele ya Mahakama huku akisema baada ya kusikiliza mashahidi wote 17 wa upande wa mashtaka,upande huo umeshindwa kabisa kuthibitisha kwamba (Prima-facaie case/Evidence )ni "ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka usipojibiwa na upande wa mteteze, Mahakama inaweza kumhukumu mtumhumiwa.

Mshitakiwa amesema kuwa prima facie evidence kimsingi ni ushahidi wa upande wa mashtaka peke yake na kama haujafikia kiwango au kujibiwa hakuna kesi.

Amesema kifungu Cha 312(1) kinasema kuwa, kama haujafikia ushahidi uliotolewa,Mahakama utasema hakuna hatia.

Akiendelea kutoa utetezi wake, Lissu amesema hicho kifungu Cha 312(1) kimefanyaiwa maamzi mengi ya nchi yetu kwa kutengeneza misingi mikubwa ya Kisheria juu ya kitu gani Mahakama inatakiwa kujibu kuhusu hakuna kesi ya kujibu(No case to answer).

Amesema msingi mkuu Wa Kisheria juu ya kwamba hakuna hoja ya kujibu iliwekewa tangu miaka 70 iliyopita na mahakama ya Rufani Afrika Mashariki.

Amesema kesi hii si ya kwanza kufanyika nchini Tanzania,bali ni kesi ya tatu,iwewemo ya Khatibu Gandi na wenzake dhidi ya Jamhuri.

Amesema katika kesi ya kwanza kati ya Gray Nkunku Matata na wenzake iliweka vigezo vitatu kuthibitisha kama kesi ni ya uhaini,akitaja vipo ukurasa wa 406.

Utiifu wa Jamhuri,Je, ulikuwa na nia ya kutenda kosa la uhaini?,hiyo nia lazima uthibitishwe kwa maandishi au kwa matendo ya wazi. 39(2d) kwa mujibu wa kifungu Cha makosa ya adhabu.

Aidha Lissu ameendelea kuisisitiza Mahakama kuturuhusu kujitetea kwasababu hana kesi ya kujibu

Hata hivyo mshitakiwa amesema bado Mahakama inaweza kutoa fidia kwa hizo siku zote 496 kutokana na kifungu Cha 367.
Natangaza kreti 5 za bia kwa Wana mabadiliko woteeeeeee watakao kua viunga vya mahakama kujipongeza..

NB. TUNDU LISU AKIACHIWA INABIDI AWE MPOLE KWA SASA

AKIANZA KUWABAGAZA NA KUSEMA AMEWAGALAGAZA KINA LUCAS NA THLAATLAA WATA NUNA SANAA HAKUNA NAMNA

Cc. min -me
 
Lissu anajitia janja janja ila akinusurika hapa goma linaanza upya, tunadaka brenda rupia ambaye kakaangwa na Lissu mwenyewe kuwa ndiye aliyealika kikao cha kupanga uhaini na shahidi pw17 alimshuhudia katika mandalizi ya kikao hicho cha kupanga uhaini.
Upande wa mashtaka ukimbana brenda rupia tuambie ni nani alikuwa ndo mwenye kikao, automatically atamtaja tundu lissu na hapo sasa ngoma ndo inarindima vizuri dadadeki!!
 
Back
Top Bottom