Usikubali kufanywa mdogo na yeyote

Usikubali kufanywa mdogo na yeyote

Kutokukubali kudharauliwa na Confidence ni vitu muhimu, lakini pia inahitajika kuambatana na unyenyekevu pia.

Hakuna mtu anayejua kila kitu, kila mmoja wetu ana nguvu zake, uwezo, ujuzi na maarifa yake lakini bado kuna maeneo ya kujifunza. Vilevile Kujithamini hakumaanishi kujiona juu ya wengine, bali kujua thamani yako bila kupunguza thamanj ya mwingine

YNWA
 
Naunga mkono hoja yako mkuu 🤝
 
Ila ukinyenyekea maana yake si ni kwamba umekubali kushuka au !
Unyenyekevu haufanyi usijione hauwezi. Ni kukubaliana na ukweli kwamba kuna eneo linahitaji kuboreshwa na uchukue hatua stahiki.

Mleta uzi anaposema usikubali kufanywa duni, ni ile mtu anakufanyia vitu vinavyoathiri nafsi yako kiasi cha kuona hauna uwezo wa kufanya chochote, unakosa ujasiri kabisa.

Mara nyingine inaweza asiwe mtu, unapitia hali ngumu hadi wewe unajiona duni na hauwezi chochote, inafika mahali unahisi hata wengine wanakuchukulia hivyo, inaathiri sana unavyoishi na watu au kujieleza kwao, tayari ndani yako umeshaweka kuwa wewe ni duni.

Kwa ufupi, ni kuwa mtu wa matumaini na kutokata tamaa kutokana na mazingira, hali, nyakati au watu.
 
Kutokukubali kudharauliwa na Confidence ni vitu muhimu, lakini pia inahitajika kuambatana na unyenyekevu pia.

Hakuna mtu anayejua kila kitu, kila mmoja wetu ana nguvu zake, uwezo, ujuzi na maarifa yake lakini bado kuna maeneo ya kujifunza. Vilevile Kujithamini hakumaanishi kujiona juu ya wengine, bali kujua thamani yako bila kupunguza thamanj ya mwingine

YNWA

Mtego wa kiburi: Kujiona duni ndiko kunakomfanya mtu atumie kiburi au dharau kama ngao ya kuficha aibu ya kutokujua.

Unyenyekevu ni Fursa: Ili ujazwe maarifa, lazima ukubali kwanza kuwa "hauwezi kujua vitu vyote." Mwanafunzi mpole pekee ndiye anayeweza kukua hadi kufikia au kuvuka kiwango cha mwalimu wake.

Ukuaji Halisi: Unapoweka aibu pembeni na kuikumbatia shauku ya kujifunza, unainua uwezo wako badala ya kuuangamiza.

Mtazamo wako wa unyenyekevu na nia ya kujifunza ndiyo nguzo kuu ya kufikia mafanikio yoyote.
 
Unyenyekevu haufanyi usijione hauwezi. Ni kukubaliana na ukweli kwamba kuna eneo linahitaji kuboreshwa na uchukue hatua stahiki.

Mleta uzi anaposema usikubali kufanywa duni, ni ile mtu anakufanyia vitu vinavyoathiri nafsi yako kiasi cha kuona hauna uwezo wa kufanya chochote, unakosa ujasiri kabisa.

Mara nyingine inaweza asiwe mtu, unapitia hali ngumu hadi wewe unajiona duni na hauwezi chochote, inafika mahali unahisi hata wengine wanakuchukulia hivyo, inaathiri sana unavyoishi na watu au kujieleza kwao, tayari ndani yako umeshaweka kuwa wewe ni duni.

Kwa ufupi, ni kuwa mtu wa matumaini na kutokata tamaa kutokana na mazingira, hali, nyakati au watu.
Exactly 💯
Umenielewa vyema maana yangu ilikua ni hii
 
Ila tu kwa namna ya kukuny'ong'onyeza
Inabidi unyenyekee ki vipi?
Clearly hiyo ni dharau, unaweza usikubaliane nae ila uka-ignore tu ili maisha yandelee japo wewe unajua uwezo wako ni nini!

Hoja yangu ni kwamba kuna muda unatakiwa ukubali kuwa mdogo (sio mnyonge) ili kuepusha kelele zisizo na ulazima, ukishindwa kutambua hilo matokeo yake unakuwa kam kijana flani humu jukwaani sitomtaja jina ila ana shida ya kujiona mkuu sana/mkubwa/muhimu/mjuaji nk nafikiri ni kwasababu hiyo
 
Mwanzo nilijihisi mdog hata kama kwenye kikao au watu wengi nisigeweza kuogea hata kama nigeogea ugesikia watu wanasema na wewe unataka kusema nin hii ilinitesa sana nikakoswa ujasiri nikawa mnyonge sababu sijui kuogea haraka haraka naogea taratibu
Ila now naujasiri zaid ya simba siwez kuruhusu mtu anifanye mdog/ mnyonge
 
Kwa dunia ya sasa, nadhani si mwanaume wala mwanamke asiyeweza kujua ni kitu gani anachohitaji
Nadhani kila mtu anajua thamani yake

Huwa nashangaa sana ninapoona mtu akitumia nguvu kubwa kumfanya mtu mwingine ajihisi au ajione mdogo

Na kisha huyo mtu anakubali kabisa na kuanza kujiona mdogo na kujishusha thamani

Mbinu hii ya kutaka kuwafanya wengine wajihisi wadogo hutumiwa na watu wadogo wanapotaka kuweka mizani sawa

Huna haja ya kukubali hizi mbinu zisizo na maana yeyote

Ni ukweli usiopingika kwamba duniani tupo katika viwango tofauti sana
Kuna watu walio kwenye high level, kuna walio kwenye low level, na kuna walio kwenye average level

Lakini licha ya yote hayo, confidence inaweza kumbeba sana mtu

Yes hata ukiwa mtu wa kiwango cha chini kiasi gani
Ukiwa na confidence unaweza kufanya vingi na vitu postitive
Unaweza kuitwa kwenye interview, ukaweza kujieleza vizuri bila hofu na ukafaulu

Unaweza kuanzisha biashara ndogo na ukafanikiwa

Watu wanasema bila pesa huwezi kuwa na confidence
Mimi hilo sioni kuwa ni kweli, au kama kuna ukweli ndani yake, basi ni mdogo sana

Ukiwa na confidence, uwezekano wa kuzipata pesa unakuwa mkubwa pia

Watu waoga waoga huwa wanachukua muda mrefu sana kufikia malengo au wasifikie kabisa matamanio yao

Ujumbe wangu wa leo ni huu:
No matter what, huna haja ya kukubali kufanywa mdogo na yeyote

Hasa sisi wanawake, huna haja ya kujiona wa kawaida
Na hii si kiburi wala jeuri ni moja ya njia za kujiwekea kiwango na mipaka ambayo si kila mtu anaweza kuvuka

Mimi : ShesRise_1
hupendelea kusema:👇

Mimi si wa kawaida, ila wewe unaponitazama mimi na ukaniona wakawaida
wewe ndiyo wa kawaida sana kiasi kwamba huwezi kuona viwango vyangu.

Wewe mdau umewahi kujihisi mdogo?
Nini kili rudisha confidence yako?

ShesRise_1 🤚

Safi, nzuri sana hii.

"Na hii si kiburi wala jeuri ni moja ya njia za kujiwekea kiwango na mipaka ambayo si kila mtu anaweza kuvuka"

Watu wengi huwa wanadhani mtu anayejitambua na kusimamia thamani yake ana kiburi au jeuri.
 
Kwani kuna namna ya kufanya usiumie ?
Au kuna jinsi ya kukabiliana na maumivu bila kukuachia athari kubwa ?

Ngoja wajuzi waje
Ila unaweza kujiepusha na maumivu kwa kujitenga na sababu zinazoweza kupelekea maumivu
Ni kweli. Ila pia mara nyingi ni ngumu kujiepusha na changamoto ya kusemwa vibaya (kufanywa uonekane mdogo). Na sometimes ni haiwezekani kabisa. Tunatofautiana tunavyozipokea changamoto za maisha. Kuna watu kwa asili tu ni wagumu kuumia. Na kuna wale wanaumia kirahisi sana na ni wagumu kusahau na kusamehe.
 
Clearly hiyo ni dharau, unaweza usikubaliane nae ila uka-ignore tu ili maisha yandelee japo wewe unajua uwezo wako ni nini!
Sasa hapa kuna utofauti sana kuna mtu anaweza ku ignore dharau na kuamini uwezo wake na akaendelea vizuri

Lakini pia kuna mwingine akiambiwa wewe huwezi kabisa hata iweje
Hasa akiambiwa kwa njia ya dharau anayabeba kama yalivyo
Na kujikuta akishindwa kabisa kufanya hata kwa udogo tu
Yaani anashindwa mazima
Hoja yangu ni kwamba kuna muda unatakiwa ukubali kuwa mdogo (sio mnyonge) ili kuepusha kelele zisizo na ulazima, ukishindwa kutambua hilo matokeo yake unakuwa kam kijana flani humu jukwaani sitomtaja jina ila ana shida ya kujiona mkuu sana/mkubwa/muhimu/mjuaji nk nafikiri ni kwasababu hiyo

Kukubali kunyenyekea na kujifunza ni nzuri sana kwa sababu hakuna namna mtu anaweza kujua kila kitu
 
  • Nzuri
Reactions: ---
Upo sahihi kabisa
Kwa mkutadha huo ni sawa

Hivi hujawahi kukutana na watu wanaopenda kudogosha wengine kwa njia ya kuwanyong'onyeza ?
Karibu kila siku.

Hao wanapanguliwa kwa logic tu.

It is not a matter of nani mkubwa na nani mdogo, it is a matter of what it true.

Mara nyingi wanatumia logical fallacies kama ad hominem, non sequitur, strawman argument.

You just point out the logical fallacies.

I do that everyday here.
 
Na hii si kiburi wala jeuri ni moja ya njia za kujiwekea kiwango na mipaka ambayo si kila mtu anaweza kuvuka

Safi, nzuri sana hii.

"Na hii si kiburi wala jeuri ni moja ya njia za kujiwekea kiwango na mipaka ambayo si kila mtu anaweza kuvuka"

Watu wengi huwa wanadhani mtu anayejitambua na kusimamia thamani yake ana kiburi au jeuri.
Ni kweli watu tunashindwa kutofautisha mtu kujua thamani yake
Na mtu kua na mipaka yake

Na kuyaona hayo kama kiburi au jeuri
Hivi vitu vipo tofauti ni vile vinawekwa kapu moja
 
Karibu kila siku.

Hao wanapanguliwa kwa logic tu.

It is not a matter of nani mkubwa na nani ndogo, it is a matter of what it true.

Mara nyingi wanatumia logical fallacies kama ad hominem, non sequitur, strawman argument.

You just point out the logical fallacies.

I do that everyday here.
Hakika kaka nimeona hapa jukwaani ukijikita kwenye hoja inayokua mezani badala ya kum shambulia mtu binafsi

Hapa sasa ndiyo naelewa maana ya kusema watu wa namna hiyo wanapanguliwa kwa logic

Maana yake unapo jadiliana na mtu kwa logic tu hakuna namna ataona amedharauliwa unless ni mtu asietaka kujifunza au kupata uzoefu mpya

Badala yake atagundua kua uwezo wake bado ni mdogo na akipenda atachukua point

Shukran bro na karibu tena 🙏🙏
 
Ni kweli. Ila pia mara nyingi ni ngumu kujiepusha na changamoto ya kusemwa vibaya (kufanywa uonekane mdogo). Na sometimes ni haiwezekani kabisa. Tunatofautiana tunavyozipokea changamoto za maisha. Kuna watu kwa asili tu ni wagumu kuumia. Na kuna wale wanaumia kirahisi sana na ni wagumu kusahau na kusamehe.
Kusemwa vibaya inauma lakini ukiangalia anaekusema ni nani hii inaweza kupunguza maumivu yako au kuisha kabisa

Kuna mtu akikusema unajua kabisa hii sio kawaida ikibidi unajitathmini
Kwa sababu lazima kutakua na namna tu umeharibu

Ila sasa kuna mwingine kwa Title yake tu hupaswi kabisa kuhisi hata dalili za kuumia kama ukisikia anakusema vibaya
 
Mwanzo nilijihisi mdog hata kama kwenye kikao au watu wengi nisigeweza kuogea hata kama nigeogea ugesikia watu wanasema na wewe unataka kusema nin hii ilinitesa sana nikakoswa ujasiri nikawa mnyonge sababu sijui kuogea haraka haraka naogea taratibu
Ila now naujasiri zaid ya simba siwez kuruhusu mtu anifanye mdog/ mnyonge
Pole kwa hiyo changamoto uliyopitia
Na hongera kwa kuishinda

Hii ya kushindwa kuongea mbele ya watu wengi inawakumba watu wengi sana

Mtu anawaza nikiongea watanielewa kweli?
 
Mtego wa kiburi: Kujiona duni ndiko kunakomfanya mtu atumie kiburi au dharau kama ngao ya kuficha aibu ya kutokujua.

Unyenyekevu ni Fursa: Ili ujazwe maarifa, lazima ukubali kwanza kuwa "hauwezi kujua vitu vyote." Mwanafunzi mpole pekee ndiye anayeweza kukua hadi kufikia au kuvuka kiwango cha mwalimu wake.

Ukuaji Halisi: Unapoweka aibu pembeni na kuikumbatia shauku ya kujifunza, unainua uwezo wako badala ya kuuangamiza.

Mtazamo wako wa unyenyekevu na nia ya kujifunza ndiyo nguzo kuu ya kufikia mafanikio yoyote.
safi kabisa kumbe unajielewa
 
Pole kwa hiyo changamoto uliyopitia
Na hongera kwa kuishinda

Hii ya kushindwa kuongea mbele ya watu wengi inawakumba watu wengi sana

Mtu anawaza nikiongea watanielewa kweli?
nilivyofanya mim nilianza kuogea na watu wawili baadaye watano, kumi, ishirin, mpak wat mia nikapata ujasiri na unapotaka kuzugumza kwa watu kama mia chagua mtu mmoja uwe kama unazungumza naye watakuelewa wote
HAKIKISHA WATU HAWAKUCHUKULII KAWAIDA
 
Wow hongera sana
Jazia nyama hapo kwenye kuchagua mtu mmoja wa kuzungumza nae
Hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom