Usikubali kufanywa mdogo na yeyote

Usikubali kufanywa mdogo na yeyote

Kuna sehemu unaenda kumsikiliza mtu anajua quantum physics kwa kiwango ambacho wewe unatakiwa kujiona si lolote.

Hilo halimaanishi wewe si lolote.

Hilo linamaanisha wewe si lolote kwenye fani hiyo.

Na labda kuelewa kuwa wewe si lolote katika fani hiyo ndiyo chachu ya kukufanya ujifunze zaidi.
Upo sahihi kabisa
Kwa mkutadha huo ni sawa

Hivi hujawahi kukutana na watu wanaopenda kudogosha wengine kwa njia ya kuwanyong'onyeza ?
 
Kujiona mdogo ukimaanisha nini? Kujiona dhaifu? Ni hali ya kawaida ya asili kujiona mdogo mara kadhaa. Na kuna wakati ni kweli unakua mdogo. Siyo vibaya kuukubali uhalisia. Cha msingi ni kujitahidi kuwa positive hata kipindi unapokuwa dhaifu kwasababu mbalimbali za kibinadamu.
Wewe unataka mtu ajione mdogo kwa namna gani ?

Mimi namaanisha mtu kutokubali kubagazwa na watu wengine kwa kusema hana uwezo
Na kuishia kushindwa kabisa
Kwa ku athiriwa na maneno yao
 
Yani mtu anayejua fizikia kuliko wewe anakwambia hapa juu sana huwezi kuruka ukabaki salama, halafu wewe ambaye hujui fizikia vizuri umbishie ukatae kujifunza ukweli kwa sababu hutaki kuwa mdogo?

Kuna sehemu unatakiwa kukubali kuwa mdogo, ujifunze.

Na kukataa kuwa mdogo kwa confidence tu hata kama hauko sawa, kunaweza kukuua.

Kiongozi uko sahihi kabisa, unatembea sambamba na maandiko...

Luka 6:40: "Mwanafunzi hawezi kuwa mkubwa kuliko mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi aliyekamilika atakuwa kama mwalimu wake."

Kuukataa ukweli au uhalisia ni kiburi na upumbavu, hata sio ujinga ( not even foolishness Sir).

Kwa mtizamo wangu, hapa tatizo kubwa ni ile hali ya unyonge na kujiona duni.

Kwenye mfano wako, ntakua zaidi ya juha kugoma kuelekezwa na mtu kitu ambacho sikijui kwa ukaidi kwamba naelewa. Natakiwa kuwa mpole ili niweze kujifunza.

Hapa ni ile kuifanya potential yako kuwa haiwezi, unaniambia bwana mdogo Monk njoo nikupe kipindi hapa uelewe mambo ya stock na uwekezaji yanavyoenda, mue hapo ndani najiona siwezi na aibu kwamba kwanini sifahamu kama wewe, napoteza ujasiri hata wa kuwa na shauku ya kujifunza, naanza dharau au kupingana na ukweli kwamba nikiwa mtulivu ukanipiga kipindi, ntaelimika na kuongeza kitu.

Mwalimu ana mchango mkubwa katika kuumba mtazamo na maisha ya mwanafunzi, hivyo kujifunza kunahitaji unyenyekevu na utii.

Mfano hai ni mimi ambavyo nimekua nikisema mara kwa mara kwamba, kuna vitu vingi nimejifunza kwako.
 
Wewe unataka mtu ajione mdogo kwa namna gani ?

Mimi namaanisha mtu kutokubali kubagazwa na watu wengine kwa kusema hana uwezo
Na kuishia kushindwa kabisa
Kwa ku athiriwa na maneno yao
Afanyeje mtu yule ambaye hapendi kuumia akiumizwa ila bado anajikuta tu kaumia akisemwa vibaya? Kumshauri tu kwamba asijali au asikubali kufanywa mdogo inatosha kumsaidia mtu wa namna hiyo?
 
Afanyeje mtu yule ambaye hapendi kuumia akiumizwa ila bado anajikuta tu kaumia akisemwa vibaya? Kumshauri tu kwamba asijali au asikubali kufanywa mdogo inatosha kumsaidia mtu wa namna hiyo?
Kwani kuna namna ya kufanya usiumie ?
Au kuna jinsi ya kukabiliana na maumivu bila kukuachia athari kubwa ?

Ngoja wajuzi waje
Ila unaweza kujiepusha na maumivu kwa kujitenga na sababu zinazoweza kupelekea maumivu
 
Ila ukinyenyekea maana yake si ni kwamba umekubali kushuka au !
Kwahiyo ukiambiwa kwa dharau kua wewe hata iweje hutokaa ufaulu mtihani na huambiwi hivi kwa kua wewe labda ni mkaidi hutaki kujifunza

Ila tu kwa namna ya kukuny'ong'onyeza
Inabidi unyenyekee ki vipi?
 
Back
Top Bottom