Ushauri wangu, Wananchi wasipojitokeza kuandamana 29th October

Ushauri wangu, Wananchi wasipojitokeza kuandamana 29th October

Ipo shida ya watu kupenda kusikia kile masikio yao yanataka kusikia, lkn mleta mada kaongea hali halisi..wewe unaishi Tanzania ipi kuamini kuwa watanzania wanaweza kuandamana? Ukipita mitaani na kutazama sura za wananchi unaona Kuna mwenye dalili ya kuandamana? Maandamano Yako mtandaoni na yataishia humu humu....Kwa kusema hivyo haimaanishi mimi sitamani maandamano..nchi bado imejaa watu wajinga na waoga
Unataka watanzania wakuonyeshe dalili gani za kuandamana? Wewe binafsi ukisema tu kwamba hautaandamna shida gani? Kwanini unalazimisha kuwasemea wengine?
 
Siku hiyo mimi siendi kupiga kura ndio maana ya NRNE lakini sitoandamana mpaka nitakaposikia msimamo wa chama.
Lissu alisema watazuia uchaguzi kwa kufanya maandamano siku ya uchaguzi mkuu. Wengi wanafikiri organizer wa maandamano ni Mange Kimambi, lakini yule dada anachokifanya ni kukuza tu yale aliyokua anayaongea Lissu kabla hajakamatwa kwa mashtaka ya uhaini
 
Tunaye makamu mwenyekiti mbona yuko kimya.
 
ishu hasa ndiyo hiyo ya kujitokeza, huu umati mkubwa unaojitokeza kujaza mikutano ya kampeni nchi nzima kama watajitokeza kupiga kura basi CCM haina haja ya kuhimiza wananchi wajitokeze kupiga kura maana tayari ina kura milioni 13 za wanachama wake, ukichanganya na hawa wanaojaza viwanja watasogea mpaka milioni 20. Milioni 40 hata wasipopiga kura CCM itatangazwa kushinda.
Ashukuriwe aliyeleta idea ya mabasi na malori 😂
 
Kama uliona wakati wa uandikishaji wa daftari la mpiga kura watu walikuwa hawajitokezi, walikuwa wanaingia nyumba kwa nyumba kutafuta watu wajiandikishe... Kwenye upigaji kura inaweza ikawa mara mbili yake au zaidi. Kuna hatari vituo kukaa bila watu.
 
Mkuu samahani, haya unayaelezea umeyagundua lini? Mana ulikua shabiki mkubwa wa chadema na Lissu uchaguzi uliopita
Baada ya Dr Slaa kujiunga na kambi moja ya watu nilikuwa nawaamini sana na baya zaidi baada ya uchaguzi kuisha wengi wakawa wananunulika kujiunga hapo ndio nikagundua hakuna upinzani wa kweli ila kuna ile na mimi nitapata lini. Ile kambi ya upinzani ya 2015 wangesimama pamoja pamoja na yote yaliyotokea wangepiga hatua moja mbele. Baada ya 2015 wapinzani walipoteza dira kabisa ikawa wanaibuka na matukio tu.... wapinzani waliteswa sana wakati wa JPM lakini leo wanamuimbia mapambio hawa ndio wapinzani wa leo.
 
Watanzania wengi wamelizika na maisha yao.
Ili mradi mtu anapata pesa ya kula, na kiakiba kidogo.
Akishashabikia simba na yanga, au bongofleva,
Mwingine akishaenda kwenye nyumba za ibada akapewa matumaini
Maisha ndio yameisha hapo.

Hawa watu kushituka usingizini ni mpka hali iwe mbaya sana.
Inasikitisha sana.
 
Kusema kuboresha maisha hiyo ni kauli ya kijumla haina mashiko, lazima useme utafanya nini sababu iko mifano mingi imetokea nchi nyingi sana lakini leo ukienda kuwauliza wanasema bora zamani. Nchi nyingi za mashariki ya kati zilipita huko kabla ya sisi lakini leo hii Iraq, Egypt, Libya sijui Tunis wanakiri walikuwa bora kuliko leo. Hapa Africa nchi nyingi zimepita huko lakini hata Congo na uhakika wansema bora enzi za Mobutu walikuwa na heshima na utulivu.

Nasema hivi tusikimbilie jambo hatujui tunataka nini kwenye mabadiliko, kubadili serikali tu bila mikakati ni sawa kubadilisha daladala tu lakini unakoenda ni kulekule. Wapinzani wanatakiwa kuweka nini watafanya bora kuliko hawa CCM.
Kwani mara ngapi CCM imekuambia itafanya nini na haijafanya??
Maisha bora kwa kila Mtanzania ya JK yako wapi?
Uchumi wa viwanda wa jiwe uko wapi?
Unafikiri utaupata utu chini ya utawala wa mama yenu??
Kusema ni jambo moja tu, utashi na utayari kutenda ni jambo lingine kabisa.
 
Hii ni mjadala mwingine, system zote hazina shida maana ziko nchi nyingine hawana hata vyama vya siasa lakini watu wake wanaishi vizuri sana, tuchukulie nchi za Mashariki ya kati hawana hata vyama vya siasa na wananchi wao wanaishi vizuri na kuna China chama kimoja na wako mbali sana na ziko nchi multi party wako mbali. Hapo ni wewe mfano gani unataka kutumia.
Sasa kwa nini CCM wanahangaika na uchaguzi wa maigizo wakipoteza mabilioni ya pesa za walipa kodi? Kwa nini wasifute vyama vingine rasmi tubaki na chama kimoja tu??
 
Kwani mara ngapi CCM imekuambia itafanya nini na haijafanya??
Maisha bora kwa kila Mtanzania ya JK yako wapi?
Uchumi wa viwanda wa jiwe uko wapi?
Unafikiri utaupata utu chini ya utawala wa mama yenu??
Kusema ni jambo moja tu, utashi na utayari kutenda ni jambo lingine kabisa.
Sasa achana na uwongo wa CCM wewe una nini chaku offer tofauti. Hii ndio shida tenu mnakosoa tu lakini sijawahi kusikia sera za kiuchumi zaidi tu ya People Power na siku No reform no election na ile 2015 zungusha zungusha....
 
Wewe kwa akili yako mpaka sasa bado unafikiria shida ya Tanzania na Africa kwa ujumla ni sera za uchumi ??
 
Kama uliona wakati wa uandikishaji wa daftari la mpiga kura watu walikuwa hawajitokezi, walikuwa wanaingia nyumba kwa nyumba kutafuta watu wajiandikishe... Kwenye upigaji kura inaweza ikawa mara mbili yake au zaidi. Kuna hatari vituo kukaa bila watu.
hili lipo wazi, kutakuwa na gap/interval kubwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupiga kura. Walipata kazi hiyo ya usimamizi wa kupiga kura ni bora wajaze mabando ya kuperuzi mitandaoni tu wakati wanasubiri watu waje kupiga kura, upigaji kura wa mwaka huu utadorora sana. Wapiga kura wa mwaka huu wengi watakuwa ni wanachama na machawa tu, the rest hawataenda kupoteza muda bure!
 
Hili lipo wazi, usishangae vyombo vya habari vikazuiliwa kuripoti habari mbalimbali kutoka vituo vya kupigia kura. Maana watu watakuwa hamna.
 
Hili lipo wazi, usishangae vyombo vya habari vikazuiliwa kuripoti habari mbalimbali kutoka vituo vya kupigia kura. Maana watu watakuwa hamna.
kama media zitazuiliwa kuripoti uchache wa watu kujitokeza kupiga kura basi mitandao iripoti. Huu uchaguzi hauna hamasa kwa wananchi. ni wanaccm wenyewe kwa wenyewe ndio wanahamasishana wakapige kura. Hawa kina coaster. mwajuma, kinje, busungu, mwalimu na wenzao wanaogombea hawana ushawishi na mvuto, wapo kama hawapo. wanafanya abrakadabra tu!
 
Kuna kila dalili huenda wakajitokeza wachache wakakamatwa au wasijitokeze kabisa.

Baada ya 29th October itakuwa wakati mzuri wa wanaharakati wa Tanzania kukata tamaa.

Watanzania inabidi waachwe kwenye mateso na changamoto ambazo zitaamsha akili zao bila kuwepo yeyote wa kuwasemea.

Idadi ya watanzania wajinga bado ni kubwa sana, hata wale wanaoelewa mambo ni waoga, hii inarudisha nyuma jitihada zozote za kuikomboa nchi.
Kama hatutafanikiwa kuung'oa huu utawala dhalimu kipindi hiki,

WATANGANYIKA tutarajie miaka mitano migumu na MICHUNGU! maradufu zaidi ya sasa!

Mwanadamu hasa mwanamke ana asili ya kisasi!

Huyu mama atalipa kisasi kwa kutukomoa na tozo za kila aina!...tusijisahaulishe kuwa hasomi mitandao kuhusu asivyopendeka....

Anasubiria the right time ATUNYOOSHE! KI-SAWA SAWA!!
 
kama media zitazuiliwa kuripoti uchache wa watu kujitokeza kupiga kura basi mitandao iripoti. Huu uchaguzi hauna hamasa kwa wananchi. ni wanaccm wenyewe kwa wenyewe ndio wanahamasishana wakapige kura. Hawa kina coaster. mwajuma, kinje, busungu, mwalimu na wenzao wanaogombea hawana ushawishi na mvuto, wapo kama hawapo. wanafanya abrakadabra tu!
La mitandao haitazuilika, labda wazime na wakizima wao nao wanakosa Mawasiliano
 
Back
Top Bottom