one by one
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 5,835
- 9,330
Kusema kuboresha maisha hiyo ni kauli ya kijumla haina mashiko, lazima useme utafanya nini sababu iko mifano mingi imetokea nchi nyingi sana lakini leo ukienda kuwauliza wanasema bora zamani. Nchi nyingi za mashariki ya kati zilipita huko kabla ya sisi lakini leo hii Iraq, Egypt, Libya sijui Tunis wanakiri walikuwa bora kuliko leo. Hapa Africa nchi nyingi zimepita huko lakini hata Congo na uhakika wansema bora enzi za Mobutu walikuwa na heshima na utulivu.waandamanaji wangepata mlinzi wa uhakika nafikiri watanzania
kwamba hakuna huwezekano wa watu kuboreshewa maisha uko serious kweli na akili timamu?
Nasema hivi tusikimbilie jambo hatujui tunataka nini kwenye mabadiliko, kubadili serikali tu bila mikakati ni sawa kubadilisha daladala tu lakini unakoenda ni kulekule. Wapinzani wanatakiwa kuweka nini watafanya bora kuliko hawa CCM.