wewe husemi kweli kabisaa, at least ungesema umepata michango ya harusi milioni 20, ingeingia akilini. lakini milioni 42 unatudanganya tuu hapa na kutupotezea muda.
lakini kwa nini watu ukiwaambia nichangie nijenge wanakuwa wagumu sana, lakini ukiwaambia nichangieni nifanye sherehe inakuwa sio ngumu? nalo neno hilo.
akili zetu zimedumaa kwa mambo yasiyo na tija na kuleta maendeleo.
mfano,
ndugu anaumwa tatizo sio kubwa sana lakini kuchangiwa akatibiwa mtu hawezi kuuza kishamba chake ili amtibu ndugu yake, lakini tatizo likiwa kubwa na ishara ya kuwa haponi tena au kufa watu wanaanza kutapatapa huku na kule, michango ya mazishi hutolewa hapa na ghrama kubwa tuu, ambazo zingeweza kumsaidia kutibiwa wakati alipokuwa hai.
au
Mtoto wa ndugu anahitaji hela ili aendelee na masomo hatutaki kumchangia kabisaa, ikiwa wakike akizurura mitaani kuhangaika huenda akapata mimba ohoooo kelele nyingi sana kwa mama mzazi wa mtoto na mtoto mwenyewe, au kama wa kiume akija kuharibikiwa wakati alikufuata umsaidie au unamuona ana akili sana lakini mazingira anayokaa ni mibaya sana na una uwezo wa kumtoa pale na kumpeleka boarding school ili apate elimu zaidi na utulivu wa akili, hutaki kumsaidia unaona hela yako itapungua kwa kumsaidia yeye huwezi kumpa kabisaa kwa roho mbaya tuu.
Hayo yawe kwenye familia au nje ya familia, kusaidiana kuleta maendeleo zaidi tupo wagumu sana. Mfano mwengine unakaa katika mtaa watu wanahangaika kutafuta maji, wewe una uwezo wa kujenga kusima ili watu wapate maji, hutaki kutoa hela, utadhani hilo hila utazikwa nazo ukifa zoote au unasahau kuwa yule alokupa alikwambia pia uwe unatoa, ila wewe unajitoa fahamu kabisa.
ni mengi tuu